Kanisa la TAG mbona kama limepoa?

Kanisa la TAG mbona kama limepoa?

TAG ilikuwa na nguvu tangu 19970's mpaka miaka ya kati ya 1980. Waliposhindwa kusolve tatizo mpaka ikapelekea kanisa kupasuka na ikazaliwa EAGT mwaka 1989....likawa anguko la TAG. Limebaki kanisa la wachungaji kushinda kusoma falsafa za dini yao ya assemblies tu na kupelekana marekani kusoma. Kuhubiri injili si issue tena kwao.....Hiyo miaka ya 2000 unayoisema sijui ni TAG gani unayoizungumzia.
Ninachofahamu ni kuwa kikwazo kikubwa kwa matapeli wanaojinadi kuwa ni ministry za kipentekoste ni kanisa LA TAG! Mafundisho ya uongo ya mitume na manabii hasa yalengayo utajirisho bila kusisitiza utakatifu na toba huumbuliwa na mafundisho safi ya neno LA Mungu huko TAG.
 
Ubaguzi ni kitu kibaya sana. TAG wanaona wao tu ndio wenye tiketi ya Mbinguni. Wameshindwa kusimamisha makanisa vijijini. Makanisa yao yako mjini. Yaani ukiwa na pesa pale TAG utaheshimika sana na pastor atakuombea kweli,maskini TAG si kwao maana huishia kudharauliwa. Mahubiri yao ni kutoa fungu la kumi tu. Hii imepelekea kutohubiri watu kuacha dhambi. Cha ajabu kabisa,mashemasi na wazee wa kanisa ni wakorofi balaa. Ukienda kusali utasukumwasukumwa kama nini. TAG labda watubu kwanza ndio watarudi kwenye mstari.
Si kweli! Kanisa LA TAG lina watu wa aina zote maskini na matajiri, wasomi na wasiosoma! Inaelekea una chuki binafsi na TAG! Je umeokoka?
 
dhambi ya kuwakebehi EAGT na wale wapentekoste wenzao inawala.Ilifikia hatua mpaka wakatenga wanafunzi wao mashuleni CASFETA .Wale waluotengwa akina EAGT,FPCT and like wise ndiyo ukawa mwanzo wa kuanzishwa Umoja wao mashuleni wa TAYOMI.Hawa ndugu ni bora wakaona dhambi zao na kuzitubu ili kuleta neema na uwepo wa nguvu za Mungu kwenye Taasisi yao Mungu atawarehemu
Usiseme mambo usiyoyajua! Utajipatia hatia bure! Sioni haja ya kukuelezea mgogoro wa casfeta maana hauko tayari kuelewa wala kusaidika! Unachokisema wewe ndio uongo ulivyoenezwa kwa lengo LA kujipatia huruma kwa mwasisi wa casfeta tayomi ambaye kwa sasa no marehemu!
 
Hayo makanisa ni Mali ya mtu mmoja! Huwezi kumwengua hata kama akitumia bapa!

Mkuu ahsante kwa kumrekebisha mtoa mada hapo juu ila tuwe makini na mijadala ya dini katika majukwaa kama haya, ni bora na hekima wakati mwingine tuwaendee inbox na kuwachapa neno au kuwa fact huko huko.
 
Nashukuru kwa Hoja zako nzuri, hata hivyo kuna mambao mengi niliyoyaongea ya msingi ambayo hukuyagusa kabisa. Ni kweli kwa miaka michache iliyopita sijaabudu TAG hapa nilipo ingawa huko nyuma nimekuwa mshirika mzuri katika Ibada za TAG. Sikuwahi kuwa kiongozi katika TAG katika kipindi hiki cha miaka kama nane hivi kwahiyo basi kuna uwezekano kukawepo taratibu mpya za kikanisa (kiuongozi) ambazo yamkini sizijui. Lakini niseme kwamba ni vizuri jukwaa kama hili likatumika sio kwa kutetea tu udhehebu bali kupokea mawazo ya watu halafu baadaye ikafanyika tafakuri (reflection) ya wapi TAG ilipofanya vizuri ili kuendeleza au wapi haijafanya vizuri sana ili kufanya maboresho.


Ahsante

Na wewe si mshirika wa TAG. Na kama ni mshirika basi hujihusishi kabisa kulifahamu kanisa lako. TAG ni kanisa lililojikita katika falsafa ya kanisa LA mahali pamoja linalojiongoza lenyewe na kujiendesha lenyewe na kujitegemeza lenyewe kwa kufuata miongozo, taratibu na sheria kutoka uongozi wa juu. Mchungaji hapewi posho wala msaada wowote toka makao makuu ya kanisa kama unavyodai! Wachungaji hawana mishahara wanayoweza kuidai! Kila kanisa humtegemeza mchungaji wao kwa kadri wanavyoweza kwa kufuata miongozo.
Wachungaji wa TAG acha Mungu awabariki! Wengi wanaona mafanikio yao ya leo lakini hawajui walikotoka! Wamelala njaa Mara nyingi! Watoto wao wamefukuzwa shule Mara nyingi huko nyuma! Leo wakijenga majumba ya kifahari ni ushahidi wa uaminifu wa Mungu kwa watu wake!
Miaka ile ya themanini na tisini wasichana wengi walikuwa hawakubali hata kuolewa na mchungaji! Wazazi wengi hawakupenda watoto wao wawe wachungaji! Leo mambo ni tofauti hasa kwa wachungaji wa mijini walioanza zamani. Ndiyo maana wachungaji vijana leo wanaobanana kuchunga mjini wito wao hutiliwa mashaka!
Wachungaji wa vijijini wengi bado wana changamoto lakini huko mbele ya safari lazima Mungu atawakumbuka tu!
 
Uchaguzi mkuu TAG ni mwaka 2019. Cha kusikititisha tayari kampeni zimeanza. Askofu wa jimbo fulani la mwanza keshaanza kumpigia kampeni anayemtaka ili naye aje apewe cheo cha kitaifa. Kwa kweli inasikitisha sana kwa hapo TAG ilipofika
Je umeokoka? Kwa nini unapoteza muda kufuatilia mambo ya wengine wakati mambo ya roho yako huyaangalii! Hivi inakupa faida gani kiroho kuamua kuchafua kanisa kwa mambo usiyoweza kuyaainisha! Je kwa kufanya hivyo utajiepusha na hukumu ya Mungu?
 
Hii imeshakuwa dini ndg yangu kama dini nyingine yyt unayoijua! Mahubiri yao makubwa now ni kuponda makanisa mengine ya kipentecoste na kusisitiza hakuna nabii wala mtume ila ni Yesu tuu! Sasa najiuliza can you make the entire TZ become TAG members??? Falsafa yao ya kujiona bora kuliko wapentecoste wengine ndio kichefuchefu kikubwa haijalishi kuongezeka kiidadi mbona roman wako dunia nzima issue ni what au doing!
Hizo ni tuhuma za miaka nenda rudi toka kwa maadui wa msalaba!
 
Mke wa mchungaji ana nafasi yake kikatiba. Ni mshauri wa idara ya wanawake yaani WWK.
Ila kuna wake za wachungaji ambao pia wana huduma na wito. Hivyo wamekuwa no wachungaji wasaidizi na hufanya huduma nzuri tu na hupewa heshima kubwa kanisani. Ni haki yao. Ila kwenye uongozi wa kanisa hawamo, nafasi yao ni ushauri, hawako juu ya wazee wa kanisa. Kama kuna kanisa LA TAG ambalo mama mchungaji anajiona kuwa na madaraka na mamlaka ya kikanisa zaidi ya wazee wa kanisa hilo ni kosa sawa na kosa lolote lingine maana katiba haielekezi hivyo. Japokuwa mama mchungaji kutokuwa sehemu ya uongozi wa kanisa kikatiba siyo tiketi ya wazee wa kanisa "kumkanyaga"! Aheshimiwe kama anavyoheshimiwa mchungaji!
In red! Ndivyo ilivyo kanisani kwetu! Amekuwa mvurugaji badala ya kuwa mshauri. Yeye ndiye anayepanga nini kifanywe na idara pamoja na baraza. Ukihoji anajibu "nimeshapanga"! Kwa kweli amepoteza kibali alichokuwa nacho mioyoni mwa washirika walio wengi.
 
Na wewe si mshirika wa TAG. Na kama ni mshirika basi hujihusishi kabisa kulifahamu kanisa lako. TAG ni kanisa lililojikita katika falsafa ya kanisa LA mahali pamoja linalojiongoza lenyewe na kujiendesha lenyewe na kujitegemeza lenyewe kwa kufuata miongozo, taratibu na sheria kutoka uongozi wa juu. Mchungaji hapewi posho wala msaada wowote toka makao makuu ya kanisa kama unavyodai! Wachungaji hawana mishahara wanayoweza kuidai! Kila kanisa humtegemeza mchungaji wao kwa kadri wanavyoweza kwa kufuata miongozo.
Wachungaji wa TAG acha Mungu awabariki! Wengi wanaona mafanikio yao ya leo lakini hawajui walikotoka! Wamelala njaa Mara nyingi! Watoto wao wamefukuzwa shule Mara nyingi huko nyuma! Leo wakijenga majumba ya kifahari ni ushahidi wa uaminifu wa Mungu kwa watu wake!
Miaka ile ya themanini na tisini wasichana wengi walikuwa hawakubali hata kuolewa na mchungaji! Wazazi wengi hawakupenda watoto wao wawe wachungaji! Leo mambo ni tofauti hasa kwa wachungaji wa mijini walioanza zamani. Ndiyo maana wachungaji vijana leo wanaobanana kuchunga mjini wito wao hutiliwa mashaka!
Wachungaji wa vijijini wengi bado wana changamoto lakini huko mbele ya safari lazima Mungu atawakumbuka tu!

Hakika unalijua vema kanisa la TAG lakini pia utambue kwamba kuna baadhi ya mapungufu yanayotajwa hapa ni ya kweli kabisa. Kumbuka baadhi yetu ni washirika na yumkini ni viongozi ndani ya kanisa. Baadhi ya makanisa ya TAG yanaendeshwa wakati mwingine pasipo kufuata katiba, kanuni na miongozo kutoka juu. Wamefanya makanisa yao kuwa family property!
 
Ninachofahamu ni kuwa kikwazo kikubwa kwa matapeli wanaojinadi kuwa ni ministry za kipentekoste ni kanisa LA TAG! Mafundisho ya uongo ya mitume na manabii hasa yalengayo utajirisho bila kusisitiza utakatifu na toba huumbuliwa na mafundisho safi ya neno LA Mungu huko TAG.
Siyo makanisa yote ya TAG yanayosisitiza utakatifu na toba! Kuna kanisa moja la TAG wana mzee wa kanisa ambaye amemwacha mke wa ndoa na kuoa mke wa pili. Huyo baba na mke wa pili wanaimba kwaya kanisani humo. Mke wa kwanza ameshitaki kwenye section lakini mchungaji wa huyo baba amemkingia kifua kwa kuwa ni kiongozi huko kwenye section.
 
Dr. Huruma Nkone, PhD wa Victory Christian Church Tebarnacle (VCCT) akabidhiwe chombo hicho uone vijana watakavyokimbilia hilo kanisa TAG
Kule ambapo Vimini, kujichubua, usister Du na ubraza men ulipokolea?
Hayo si Ndo Baazi ya mambo yaliyoifanya TAG kupoa?
 
MIAKA HIYO T.A.G ILIPIGA MARUFUKU KUVAA VIMINI NA MAVAZI YOTE YASIYO YA STAHA, KUJICHUBUA, KUVAA MAWIGI NA KUWEKA KALKITI, KUNYOA DENGE/VIDUKU, KUPAKA RANGI KUCHA , KUWEKA KUCHA ZA BANDIA, KITCHEN PARTY, KUNYWA GRAND MALTER, RED BULL, WINE(NON-ALCOHOLIC),N.K ILA LEO WAMERUHUSU YOTE HAYO KIMYA KIMYA TENA WATOTO WA WACHUNGAJI NA MAMA WACHUNGAJI NDIO WANOONGOZA KWA KUJICHUBUA, KUVAA MAWIGI NA VIMINI..... JAMANI MLIOMBE MSAMAHA KANISA KAMA MLIKUWA MMELIPOTOSHA.
 
Habari za muda huu waungwana?
Natumai mnaendelea vizuri hasa baada ya mihangaiko ya siku.

Niende moja kwa moja kwenye mada niliyokusudia kuianzisha leo.

Kwa wale wakristo mtakua mpo aware zaidi kuhusu ukristo ulivyo na ulivyo hapa nchini.

Miaka ya nyuma kidogo ukristo ulikua imeenea zaidi kwa makanisa ya Romani Catholic, Lutheran na Pentecoste. Miaka ilivyokwenda zaidi ndipo tulipo shuhudia idadi kubwa ya makanisa hapa nchini.

Nakumbuka miaka ya 2000 kanisa la TAG lilianza kuja kwa kasi sana. Kufikia miaka ya '03-0'5 walikua wanasikika sana kutokana na makongamano makubwa na mahubiri yao.
Hawa watu walikua wanaponda sana makanisa mengine hususan wakatoliki.Hapa ndipo walipopata waumini wengi kutoka makanisa kongwe niliyotaja hapo juu kutokana na miujiza waliyokua wanafanya makanisani mwao kama kutoa pepo na kuombea wagonjwa just little to mention.

Walikua kwa kasi sana na hapa matajiri wengi pia walihamia huko wakajenga makanisa nchi nzima na kukua kwa kasi kutokana na styl yao mpya ya kuabudu na mahubiri.

Ilikua changamoto sana kuoa binti wa kilokole enzi hizo.Ilifika mahali mtu akitoka katoliki,lutheran au pentecoste akajiunga TAG alikua anatengwa na familia na ndugu na aliitwa muasi.Ikafika mahali kukawa na kama ka uadui fulani kati madhehebu hayo.
Enzi hizo karibu kila mlokole alikua anaweza kutoa pepo na kuongea zile lugha zao.

Miaka ilivyo anza kwenda sasa;taratiiibu ile power yao ya ku preach na kufanya miujiza ikaanza kupotea na kufifia.
Hivi sasa wameshazoeleka na wapo very normal sana.
Hivi sasa wana intergrate na wakristo wengine vizuri sana tofauti na zamani.

Maswali yangu:

1:Kwanini TAG wamepoa sana na hawapo hot kama zamani?
2:Je mi kwa sababu waumini wamesha jaa hivyo basi hawana nia ya ku expand zaidi?
3:Au ni utandawazi unachangia?

Karibuni kwa mawazo
Kwa sababu shetani hujihudhurisha na watu wa Mungu, roho ya Jezebel ipo makanisani kuanzia kwa wachungaji mpaka waumini
 
Wapo sana tu mkuu,isije kuwa wewe ndio umebanwa na mambo ya kidunia ndio maana unaona kama wamepotea...
 
Jmani naombeni mwenye katiba ya wwk (umoja was wanawake was kristo)
 
Back
Top Bottom