Kanisa la TAG mbona kama limepoa?

Kanisa la TAG mbona kama limepoa?

Dr. Huruma Nkone, PhD wa Victory Christian Church Tebarnacle (VCCT) akabidhiwe chombo hicho uone vijana watakavyokimbilia hilo kanisa TAG
 
Dr. Huruma Nkone, PhD wa Victory Christian Church Tebarnacle (VCCT) akabidhiwe chombo hicho uone vijana watakavyokimbilia hilo kanisa TAG
Atakae sababisha wakimbilie ni nani?kwa nini umelenga vijana pekee?wakisha kimbilia then what next?......
 
Vijana ndio chachu na nguvu ya mabadiliko. Tena wao wametajwa bayana kwenye maandiko matakatifu
 
Dr. Huruma Nkone, PhD wa Victory Christian Church Tebarnacle (VCCT) akabidhiwe chombo hicho uone vijana watakavyokimbilia hilo kanisa TAG
Mimi ni MTAG lakini hapa umeongea pumba rafiki.Watu hawatakiwi wajekanisani kwa ajili ya mtu ili kwa ajili ya Yesu na uzima wao.
 
Sasa mkuu hayo uliyosema yanahusiana vipi na hali ya kupoa kwa kanisa!
Unaweza ukawa na mipango mingi tu ikiwa hakuna nguvu ya Mungu mtaishia kujenga taasisi za ulaji tu
Mtoa mada aneongelea juu ya kwamba hawana elimu na mipango ya kufanya kanisa lisonge ndio maana nikampa fact hiyo.
 
Mimi ni MTAG lakini hapa umeongea pumba rafiki.Watu hawatakiwi wajekanisani kwa ajili ya mtu ili kwa ajili ya Yesu na uzima wao.
hata mimi nimeona niliongea Pumba kabisa. lakini lengo ilikuwa kufurahiusha baraza tu (Samahani MtAG kindakindaki) by the way Askofu Mkuu Mbeba Maono Dr. Mchungaji (PhD) Mheshimiwa Pangalile Rwakatare, MP, wa Mlima wa Moto, bado yupo TAG?
 
Sijasema hivyo nimetaja makanisa ya wokovu hapo chini pls nenda huko uokoke.
unafikiri kanisa litakupeleka mbinguni??
kwamba makanisa fulani tuu waumini wake ndio wenye guarantee ya kwenda mbinguni ilihali mengine wote mtachomwa si ndo unacho maanisha???

Kuna makanisa wamejiaminisha kwamba wao tayari wameshaokaka na watakwenda kwa MUNGU siku ya mwisho huku wakiwahukumu na kuwasema vibaya makanisa mengine.
Yaani wao kazi yao ni kuhuburi watu wahamie kwenye makanisa yao na sio kububiri matendo mema kama kusaidia yatima nk.

Sasa kifupi mgoja nikuambie,iko hivi;

1:Siku ya hukumu ya mwisho watakao enda mbinguni watakuwepo TAG,Anglicana,Lutheran,Roman Catholic,wasabato,waislam na wote wanaomuamini Mungu wa kweli

2:watakao chomwa moto pia watakuwepo wa imani zote ikiwemo hizo nilizo taja hapo bila kusahau hata hao TAG .

Tutahukumiwa kwa matendo yetu na sio bendera au majina ya makanisa
 
Habari za muda huu waungwana?
Natumai mnaendelea vizuri hasa baada ya mihangaiko ya siku.

Niende moja kwa moja kwenye mada niliyokusudia kuianzisha leo.

Kwa wale wakristo mtakua mpo aware zaidi kuhusu ukristo ulivyo na ulivyo hapa nchini.

Miaka ya nyuma kidogo ukristo ulikua imeenea zaidi kwa makanisa ya Romani Catholic, Lutheran na Pentecoste. Miaka ilivyokwenda zaidi ndipo tulipo shuhudia idadi kubwa ya makanisa hapa nchini.

Nakumbuka miaka ya 2000 kanisa la TAG lilianza kuja kwa kasi sana. Kufikia miaka ya '03-0'5 walikua wanasikika sana kutokana na makongamano makubwa na mahubiri yao.
Hawa watu walikua wanaponda sana makanisa mengine hususan wakatoliki.Hapa ndipo walipopata waumini wengi kutoka makanisa kongwe niliyotaja hapo juu kutokana na miujiza waliyokua wanafanya makanisani mwao kama kutoa pepo na kuombea wagonjwa just little to mention.

Walikua kwa kasi sana na hapa matajiri wengi pia walihamia huko wakajenga makanisa nchi nzima na kukua kwa kasi kutokana na styl yao mpya ya kuabudu na mahubiri.

Ilikua changamoto sana kuoa binti wa kilokole enzi hizo.Ilifika mahali mtu akitoka katoliki,lutheran au pentecoste akajiunga TAG alikua anatengwa na familia na ndugu na aliitwa muasi.Ikafika mahali kukawa na kama ka uadui fulani kati madhehebu hayo.
Enzi hizo karibu kila mlokole alikua anaweza kutoa pepo na kuongea zile lugha zao.

Miaka ilivyo anza kwenda sasa;taratiiibu ile power yao ya ku preach na kufanya miujiza ikaanza kupotea na kufifia.
Hivi sasa wameshazoeleka na wapo very normal sana.
Hivi sasa wana intergrate na wakristo wengine vizuri sana tofauti na zamani.

Maswali yangu:

1:Kwanini TAG wamepoa sana na hawapo hot kama zamani?
2:Je mi kwa sababu waumini wamesha jaa hivyo basi hawana nia ya ku expand zaidi?
3:Au ni utandawazi unachangia?

Karibuni kwa mawazo
Your observation is 100% correct.Satan is busy at work,anajua siku zake zimebaki chache.Ila kupoa sio TAG tu,ni makanisa yote ya Kipentekosti,sasa ni madhehebu tu kama Waroma,Wasabato,Presbyterian, African Inland Church nk. Ila naomba nikurekebishe kidogo,TAG, yaani Tanzania Assemblies of God, ni dhehebu la Kipentekosti pia.
 
Your observation is 100% correct.Satan is busy at work,anajua siku zake zimebaki chache.Ila kupoa sio TAG tu,ni makanisa yote ya Kipentekosti,sasa ni madhehebu tu kama Waroma,Wasabato,Presbyterian, African Inland Church,Baptist nk. Ila naomba nikurekebishe kidogo,TAG, yaani Tanzania Assemblies of God, ni dhehebu la Kipentekosti pia.
 
Tanzania Assemblies of God-T.A.G is even stronger than before:
1.Imekuwa na matawi nchi nzima, kila wilaya, kila kata.
2. T.A.G is the strongest Pentecostal denomination in the country. Askofu mkuu wa T.A.G ndiye Rais wa makanisa yote ya ki Assemblies ya Africa.
3.Ndiyo dhehebu pekee la kipentecost nchini lenye vyuo vya Biblia vinavyotoa diploma, degree hadi masters kwa kushirikiana na Global University ya USA
3.Ni dhehebu la kipentecost pekee nchini linalopeleka wamisionari nje ya Tanzania kama Rwanda, Burundi, Sudan kusini, DRC, na Magasca.
4.Linahubiri injili nchini kwa kasi zaidi kuliko huko nyuma.

Ukiangalia takwimu ya Nini T.A.G ilifanya huko nyuma na nini inafanya kwa sasa, na Neno linataka kanisa liweje utagundua kuwa ndiyo lina peak kwa viwango vikubwa.
Hayo mambo yote uliyoyataja hata mtu asiyekuwa na Roho Mtakatifu anaweza kuyafanya mkuu,in themselves haya prove that the denomination is "spiritually alive." Usikatae mkuu,na wala haikusaidii kukataa,mficha maradhi kifo humuumbua.Mkuu ni kweli kwamba TAG imepoa.Tena ukiingia kwenye matawi mengine hutamani kurudi,the Holy Spirit is absent na mahubiri yenyewe ni more hearthen than spiritual.Mkuu hata wachungaji wanakiri kwamba hali ni mbaya.
 
Kaka kanisa hili la TAG mbona lipo vyema mpaka sasa tena linampango mkakati kabambe wa kuivuna Tanzania yote kwa Yesu mpango huo upewa jina la miaka 10 ya mavuno.Pia wametengeneza mpango wa kujenga vyuo vya kufundisha Theologia kila jimbo la makanisa yao.
Hakika wanafanya vyema zaidi ni kuwaombea ili wafanye vyema na wawe na uamsho wa kiroho katka nguvu kubwa.
Ni kanisa pekee la Kipendecost lenye mipango na maono makubwa ya kumtangaza Yesu likifatiwa na EAGT,FPTC,KLPT,P Holiness etc
NAkushauri uokoke na wewe ili urudishe huo moto uliopotea ambao Mungu amekuonyesha.
Barikiwa sana
Theology ikishaingia kwenye dhehebu, ujue hilo dhehebu kiroho limekwisha.The devil penetrates his heresy through Theology because those are the teachings of man.Niwape pole TAG,mnaingiza Theology tena badala ya kumkumbatia Roho Mtakatifu,you are headed to Rome.Anyway,nendeni bwana, kwanza Vatican inawamezea mate sana.
 
TAG imekwisha, Baada ya kuimarika kwa EAGT. Hata hivyo kanisa kutoshirikiana na muungano wa makanisa ya kipentekoste (PCT) imelifanya hili kanisa kutoeleweka na jamii.
Mfumo wa TAG ni tofauti. Kama dhehebu si mshirika wa PCT, lakini ushiruka wa PCT uko katika ngazi ya kanisa LA mahali pamoja! Makanisa mengi ya mahali pamoja yako kwenye umoja huo wa makanisa ya kipentekoste!
 
Limejitenga mno na wenzake.Hii ni mpaka kuoa.Huoi pale kama si mshirika wake hata kama unanena kwa lugha.Wanaona wapentekoste wenzao si kitu na hawana imani
Hao unaowaita wapentekoste wenzao ni kina Nani? Maana ministry fake nyingi zinadai ni za kipentekoste na wanafanya biashara ya kuuza maji na mafuta ya upako! Hao nao kwako unawaita wapentekoste-no way!
 
ni kweli.AG zikatoka TAG na EAGT
Siyo kweli! AG ni Assemblies of God Mission, na ilikuwa inasimamiwa na wamishionari wa America. Kanisa lilipojitegemea likasajiliwa kama Tanzania Assemblies of God na askofu mkuu wa kwanza ni Emmanuel Lazaro.
Ulipotokea mgogoro wa kiuongozi, viongozi wakuu wawili yaani Askofu mkuu (Emmanuel Lazaro) na makamu wake ( Moses Kulola) walipishana mitazamo! Hatimaye Moses Kulola alisajili kanisa jipya LA EAGT na akaondoka na makanisa yote ya TAG yaliyojiweka upande wake na wakabadili ubao wenye jina LA TAG na kuandika EAGT. Lakini pia kwa kuwa mwanzilishi huyu alikuwa ni mwinjilisti aliendelea kufungua makanisa mapya ya EAGT. Kwa hiyo AG haikuuzaa TAG na EAGT Bali AG ilizaa TAG na kwa namna ya kutokuelewana, TAG ikazaa EAGT. Kuna kipindi cha mpito ambapo TAG ilikuwa na maaskofu wakuu wawili. Mmoja ni askofu mkuu halali aliyechaguliwa kikatiba Emmanuel Lazaro, na mwingine ni askofu mkuu asiyetambuliwa na katiba na hakuchaguliwa kikatiba lakini karibu nusu ya wachungaji wakakubali awe askofu mkuu wao japo hakuchaguliwa kikatiba. Baada ya kuanzishwa kwa EAGT huo utata ukaisha, na Leo ni ndugu haswa na kazi ya Mungu inasonga mbele na shetani ameshindwa!
 
pia kule UMPT nako kulitokea mafarakano ndiyo wakatokea hao kina FPCT na ndugu zake
Wewe mbona ni kama unafurahia mifarakano kwenye makanisa ya kiroho? Ni wakala nini? Samahani kama siyo na kama ndivyo na ushindwe kwa jina LA Yesu!
 
Point of correction (in green): Katunzi yuko EAGT siyo TAG! Mengine uliyoandika kwa kiwango kikubwa kuna ukweli fulani.
In red: Wachungaji wanaoanzisha makanisa kwa jina la TAG imepelekea makanisa hayo kuwa mali ya familia. Mwongozo au katiba ya TAG haifuatwi katika makanisa hayo. Idara ndani ya kanisa licha ya kuwa na uongozi, viongozi wa idara hawana mandate ya kuamua chochote pasipo mchungaji au mke wake kuridhia hata kama uamuzi wao uko ndani ya mipaka ya miongozo iliyoainishwa na TAG. Baraza la wazee limewekwa kama rubber stamp kupitisha mawazo ya mchungaji. Wazee wa kanisa ambao ni "ndiyo baba/mama mchungaji" yaani wasiopinga chochote hukumbatiwa sana. Mke wa mchungaji ambaye kimsingi siyo mmoja wa baraza la wazee huwa kiongozi wa baraza iwapo mume wake hayupo. Mke wa mchungaji huvuruga sana kanisa hasa kutokana na "sense of insecurity". Mama mchungaji huingilia kila kitu ili aonekane na kutambuliwa. Hiyo ni kwa sababu organization chart ya TAG kiuongozi haioneshi nafasi ya mke wa mchungaji, kwa hiyo lazima ajitutumue kuonesha kwamba yupo na ana nguvu.
Pia siku hizi hukumbatia idadi ya waumini (quantity) pasipo kusimamia maadili ya kiroho (spiritual quality)!
Mke wa mchungaji ana nafasi yake kikatiba. Ni mshauri wa idara ya wanawake yaani WWK.
Ila kuna wake za wachungaji ambao pia wana huduma na wito. Hivyo wamekuwa no wachungaji wasaidizi na hufanya huduma nzuri tu na hupewa heshima kubwa kanisani. Ni haki yao. Ila kwenye uongozi wa kanisa hawamo, nafasi yao ni ushauri, hawako juu ya wazee wa kanisa. Kama kuna kanisa LA TAG ambalo mama mchungaji anajiona kuwa na madaraka na mamlaka ya kikanisa zaidi ya wazee wa kanisa hilo ni kosa sawa na kosa lolote lingine maana katiba haielekezi hivyo. Japokuwa mama mchungaji kutokuwa sehemu ya uongozi wa kanisa kikatiba siyo tiketi ya wazee wa kanisa "kumkanyaga"! Aheshimiwe kama anavyoheshimiwa mchungaji!
 
Vp na haya makanisa yanayovuma kwa jina la mtu mmoja mmoja kwa mfano Lusekelo au Malisa, hayo makanisa yako chini ya mwamvuli gani? Wajuvi ufafanuzi tafadhali
Hayo makanisa ni Mali ya mtu mmoja! Huwezi kumwengua hata kama akitumia bapa!
 
Kwanza nikupongeze kwa kuileta mada hii hata hivyo niseme tu kwamba wewe hauabudu huko TAG hivyo basi hata ufahamu wako kuhusu TAG inavyojiendesha si mpana kivile. Niseme tu kwamba TAG ilianza kuyumba wakati ule wa mgogoro kati ya Askofu Lazaro na Mwinjilisti Moses kulola (Hayati) ambao hatimaye uliamuliwa na mahakama na kufanya TAG igawanyike kuzaa EAGT iliyokuwa chini ya Moses kulola. Kwa bahati mbaya sana TAG wameendeleza na ule ugomvi hadi leo kwa kuendelea kuwaita EAGT waasi (Roho mtakatifu hawezi kufanya kazi mahali pasipo na msamaha wa kweli). Jambo moja lipo wazi kwamba TAG wamekosa mbadala wa Moses kulola wa kusimamia ile idara ya uinjilisti kitaifa ingawa baadhi ya nyakati wamekuwa wakifanya kazi na Egon Folk na kumwalika Rev Reinhard Bonkey na Daniel Kolenda (wa Christ for all Nations) mwaka jana. Nadhani pia pia uendeshwaji wa TAG (Central Administration) ni changamoto ambapo kama sikosei watumishi/huduma wanawezeshwa kimaisha na Headquarter bila kujali idadi ya washirika mtumishi anaosimamia LAKINI pia Wachungaji wengi umri umesogea sana na hivyo kushindwa kuendana (Mahubiri + Ushuhudiaji) na hali ya kizazi cha sasa.

NB: Nipo tayari kukosolewa
Na wewe si mshirika wa TAG. Na kama ni mshirika basi hujihusishi kabisa kulifahamu kanisa lako. TAG ni kanisa lililojikita katika falsafa ya kanisa LA mahali pamoja linalojiongoza lenyewe na kujiendesha lenyewe na kujitegemeza lenyewe kwa kufuata miongozo, taratibu na sheria kutoka uongozi wa juu. Mchungaji hapewi posho wala msaada wowote toka makao makuu ya kanisa kama unavyodai! Wachungaji hawana mishahara wanayoweza kuidai! Kila kanisa humtegemeza mchungaji wao kwa kadri wanavyoweza kwa kufuata miongozo.
Wachungaji wa TAG acha Mungu awabariki! Wengi wanaona mafanikio yao ya leo lakini hawajui walikotoka! Wamelala njaa Mara nyingi! Watoto wao wamefukuzwa shule Mara nyingi huko nyuma! Leo wakijenga majumba ya kifahari ni ushahidi wa uaminifu wa Mungu kwa watu wake!
Miaka ile ya themanini na tisini wasichana wengi walikuwa hawakubali hata kuolewa na mchungaji! Wazazi wengi hawakupenda watoto wao wawe wachungaji! Leo mambo ni tofauti hasa kwa wachungaji wa mijini walioanza zamani. Ndiyo maana wachungaji vijana leo wanaobanana kuchunga mjini wito wao hutiliwa mashaka!
Wachungaji wa vijijini wengi bado wana changamoto lakini huko mbele ya safari lazima Mungu atawakumbuka tu!
 
Back
Top Bottom