Kanisa la Roma, sadaka na michango yake

Kanisa la Roma, sadaka na michango yake

mnampa zawadi bikira maria kwa kumzaa mtoto yesu ,ssa n yul aliemsaidia kubeba msalab mbn mmemsahau..
 
Jambo ambalo kisaikolojia huwatesa wengi na kufanya mtu alazimike kutafute kuanzia elfu moja kwenda juu hata kama ni mtu wa hali ya chini kabisa.
Kwa kauli hii tu, Ndipo watu wengi wanapotea katika maisha, kwa kuigana
Mkuu naomba nikwambie kitu, Iwe coin iwe noti, Anayetoa thamani ya Sadaka huwa ni MUNGU mwenyewe, Sio watu, sio mchungaji/Padri/Askofu, Sasa una shida gani kama ndiyo kitu Moyo wako umekusukuma Kumtolea Mungu????
Shida kubwa iliyopo mingoni mwa watu ni kwamba hawajui namna ya Kutoa, Sasa inakuharibu vipi kisaikolojia?
Unakumbuka habari ya mama mjane? Aliyesema ametoa nyingi ni Yesu Mwenyewe na si mwingine, Yawezekana watu wengine walishangaa maana wao walitoa manoti;

As long as Moyo wako umekusukuma kumtolea Mungu kwa uaminifu, haitakuwa shida; Yeye Mungu hachukui hela zetu, yeye anaangalia Moyo, then hiyo hela inayoachiliwa na Moyo itatumiwa na watumishi.
 
Write your reply...Sadaka sio lazima ,ukiwa nayo unatoa kama huna unaacha.
Mkuu watu hichi kitu hawakijui; Mungu anangalia Moyo kabla ya kitu;
Moyo ambao uko radhi kutoa na kiukweli hauna kitu cha kutoa, yaan Dhamiri yako ya ndani ndio inayodetermine utoaji wako na sivinginevyo;
Sasa mwingine hana sadaka, hata kwenda kwenye Kusanyiko la jumapili haendi;
Lakini pia ni mapokeo mabovu tu kutoka kwa watumish juu ya Utoaji, ndio yanaleta hofu miongoni mwa waamini.
 
Wakuu,

Napenda kwenda moja kwa moja kwenye maada. Ifuatayo ni orodha ya sadaka na michango mbali mbali iliyopo kanisani kwetu kanisani kwetu Roman Catholic.

ORODHA YA SADAKA
1. Huwa kunakuwa na sadaka ya kwanza -Jumapili
2. Sadaka ya pili - Jumapili
3. Sadaka ya tatu (hii ni sadaka ya inayotolewa kwa kanda ya parokia, kila kanda ina kikapu chake) - Jumapili
4. Sadaka ya kwanza (Jumamosi kwenye Jumuiya ambapo kila mkatoliki anatakiwa kuhudhuria mtaani kwake)
5. Sadaka ya pili (Jumamosi kwenye Jumuiya)

ORODHA YA MICHANGO
6. Mchango wa tegemeza parokia (kanisa)
7. Mchango wa tegemeza jimbo (kwa mfano, jimbo la dar es salaam)
8. Mchango kujenga kanisa (ujenzi wa makanisa huwa hauishi, kama sio lenu mtaambiwa kuna kanisa linajengwa sijui wapi na wao hawana uwezo hivyo mchangie)
9. Mchango wa kila mwezi kwenye Jumuiya ambapo huwa mnasali kila Jumamosi, unatoa ya mwaka mzima.
10. Mchango wa UWAKA (Umoja wa Wanaume Wakatoliki Tanzania)
11. Mchango wa WAWATA (Wanawake Wakatoliki Tanzania)
12. Mchango wa kununua viti vya jumuiya (kila mwaka)
13. Mchango wa kutimiza mwaka kwa Jumuiya (kila jumuiya ina tarehe yake kulingana na siku iliyoanza)
14. Mchango wa sherehe ya jimbo (kwa mwaka mara moja)
15. Zaka (hii unatoa kila mwezi, asilimia kumi ya pesa uliyoingiza mwezi mzima bahasha zinagawiwa kila nyumba)
16. Mchango wa kuhamia jumuiya - kila mtaa huonana jumamosi kwaajili ya kusali hivyo kama umetoka mtaa A umehamia mtaa B basi huko utatakiwa kulipia hiyo pesa
17. Mchango wa form kwaajili ya kipaimara
18. Mchango kwaajili ya watu wanaosomea upadrii
19. Mchango kwaajili ya wanaosafiri kwenda kutangaza neno la Mungu
20. Mchango kwaajili ya ujenzi wa shule/ hospitali ya kanisa.
21. Malimbikizo, hii unatoa kama kuna michango huko nyuma hukutoa. Labda ulikuwa huendi kanisani or so
22. Shukrani, hii ni pesa au chochote unatoa kama kumshukuru Mungu
23. Mchango wa bima ya mapadrii
24. Mchango wa tegemeza katekista (katekista ni msaidizi wa padri)
25. Mchango wa utatu mtakatifu (sherehe ziara makongamano ya taifa jimbo dekania parokia kanda)
26. Mchango wa Viwawa (vijana wa katoliki)
27. Michango ya vyama vya kitume (kwaya karsmatik yosefu maria nk)
28. Bahasha za mchango wa noeli, kwaresma nk
29. Mchango wa kumpa zawadi mama bikira maria kwa kujifungua mtoto Yesu Christmas
30. Sadaka ya mwisho wa mwaka, kutoa katika ulichopata mwaka mzima
31. Mchango wa radio Maria
32. Mchango wa radio Tumaini

:, Kama kuna mchango au sadaka nimeisahau naomba mnitajie au kama kuna kitu nimeongeza niambieni nipunguze. Mfano, jana (15/12/2018) tumeambiwa kila Jumuiya (mtaa) unatakiwa kupeleka watoto wa wili wakale na Padri hivyo tuchangie elfu 23,000 ya chakula

Makanisa ya Roma vifaa vyao vya kuwekea sadaka hutengeneza kwa zile mbao zenye kupiga makelele sana, afu hilo box la mbao huwa refu. Nini maana yake? Unapotoa sadaka ukitoa pesa ya sarafu kama mia tano au mia mbili ukiweka humo inapiga kelele sana kila mtu anajua umetoa sarafu. Jambo ambalo kisaikolojia huwatesa wengi na kufanya mtu alazimike kutafute kuanzia elfu moja kwenda juu hata kama ni mtu wa hali ya chini kabisa.

Kiukweli michango imekuwa miingi sana na ndiomana vijana wanaoanza maisha hawaji kanisani mpaka wakiona wanataka kuoa ndio wanakuja. Kanisani unakuta kumejaa wazee, mahouse girl na watoto kwasababu huku umri wa kati wakikimbia michango sababu ya wingi wa majukumu. Hata mimi nimechoka na hili kanisa langu, kama nina mapepo basi wenzangu mniombee yanitoke.

Note: Baadhi ya michango ipo katika maeneo fulani na maeneo mengine hamna.
Mkuu pole:

Mimi nikienda church natoa sadaka moja tu,Nyingine wala sisogei,Jumuia siendi,vyama vya kitume siende mtu akiniletea habari ya mchango nawaambia sina tu.Nikipeleka mtot kubatiza wakileta maneno mengi nawaambia tu nitampeleka kwenye ubatizo wa mwendo kasi.akikua ataamua kama atabatizwa tena au la.


Unajua kwa nini nimeamua hivo?NIMEACHA UNAFIKI so na wewe ka unaweza ACHA UNAFIKI na uache kulalamika hovyo.Kwani unafungwa usipitoa?
 
Hivi mlivyokuwa mnajengewa makanisa mazuri na misaada ya kanisa ulijua nani alikuwa anatoa? kuna watu walikuwa wanajitoa huko Ulaya, sas ni zamu yetu kujenga makanisa wenyewe, shule, hospitals na kuendesha taasisi zetu za kidini wenyewe! acha uvivu wa fikra TOA SADAKA NDUGU
 
2 Wakorintho 9:6-10
6 Kumbukeni kwamba, mtu anayepanda mbegu chache, atavuna mazao machache; na mtu anayepanda mbegu nyingi atavuna mazao mengi.7 Kila mtu atoe kama anavyokusudia moyoni mwake, si kwa kusita au kwa kulazimishwa, kwa maana Mungu anapenda mtu anayetoa kwa moyo. 8 Na Mungu anaweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili kila wakati muwe na kila kitu kwa kiasi cha kutosha na ziada kwa ajili ya kila kazi njema. 9 Kama Maandiko yanavyosema, “Yeye hutapanya kila mahali kuwapa maskini, haki yake hudumu milele.” 10 Na Mungu ambaye ndiye humpa mkulima mbegu za kupanda, na mkate kwa chakula, atawapa na kuzidisha mbegu mnazohitaji na kuziwezesha kukua zitoe mazao ya matendo mema ya haki.
 
Kwangu sadaka za kanisani hazijawahi nichosha kutoa kama ninazo na kwakweli kwangu kanisa huwa linanilipa na hasa kipindi cha masomo na mahubiri kwa kuwa wakati mwingine huwa napata majibu ya changomoto zangu kwa gharama nafuu.
lakini ifike wakati tuelewe hivi hizo fedha tunazotoa zina thamani gani ukilinganisha na unachopokea? kama upo kiimani na huchanganyi uganga huwezi kuona hasara kutoa sadaka.
tabu nyingi tumezitoa kwa waganga na hatuoni tabu
 
Huu ndio utumwa wa kisasa, unatumikishwa kisasa, ktk vitu sivitaki kusikia ni michango ya kanisa, RC wamekuwa kama wametumwa hela na Mungu kwetu, yaani wao siku hz ni helaaa helaaa helaaa helaaaaaaaaa, helaaaaaaaaa, kama yale makanisa mengine ya binafsi yanayofanya business..

Huu ni utumwa, mm siko huko kabisa, zaidi ya sadaka moja jpili, sitoi ng'oooooooo michango mingine, ujinga mtupu huu, michango mingiiiiiiii kukusanya tu hela kwa majina tofauti tofauti..

Yesu hakukusanya hela hivyooo..,ni wapi ktk biblia Yesu kakusanya mihela hivyo? Watu kila siku tunamtolea mfano Yesu makanisani ila hatuishi maisha kwa mfano wake..,hata mapadre hawaishi maisha hayo, hela zote za nn? Huu ni ujinga
 
Hama hilo kanisa mkuu, ndio suluhu inayokufaa.

Wengine hizo ni chache mno hata wangeambiwa watoe watoto wao kama Isaka wa Ibrahamu, wangekuwa tayari.
aslimia kubwa ya watu wanaotoa sana sadaka kwa haya makanisa wana hali duni maana hata wanatoa kiunafiki,angalia kama kuna padre au askofu mwenye njaa wote wana afya njema
 
Dada hakuna tofauti kati ya dini wote ni matapeli. Nimeshasema waafrika ni wajinga kuamini huu upuuzi unaitwa dini. Wanatishwa, makanisani na misikitini ati kuna moto. Watu wanaamini upuuzi vitabu vimeandikwa miaka 2000 iliyopita leo karne ya 21 bado tunaamini.

Jiulizeni huko nyuma waafrika walikua wanaamini nini? Hawakuwa na miungu yao? Biblia na Kuruani zote zilitumiwa kututapeli banadamu ili wafanye biashara. Ati imeshushwa kweli??????? imeshushwa??? Kuna tofauti gani na Chinua Achebe akiandika kitabu chake na Mtume akiandika hiyo Kuruani????

2018 jamani hakuna kitu kiitwacho dini na ninaamini kama hizi dini zisingekuwepo labda tungeishi salama.
Sasa uzi huu wa kidini umefata nini?
 
Sasa uzi huu wa kidini umefata nini?
Kwani ukichangia kujadili mambo ya ISIS unakua ni member wa ISIS siku hizi?
Mimi ni maoni yangu sina muda na huu uongo unaoitwa dini ila naheshimu wewe kuwa na dini ndiyo maana watoto wangu nimewaambia msimamo wangu kuwa siamini lolote kuhusu dini lakini wao ruksa kuabudu dini yeyote wanayoitaka iwatapeli na kwa bahati mbaya ninao wanne wote wameamua kutapeliwa na mapadre na masheikh na watu kama wewe. moja ni muislamu na wengine ni wakristu. Wanajua hilo kabisa kama sina muda na hiyo shughuli.

Kama nikiwaona nyie wafia dini mkishambuliana humu ninafurahi sana, maana mtu unafurahia na kujigamba mambo ya utapeli.
 
2 Wakorintho 9:6-10
6 Kumbukeni kwamba, mtu anayepanda mbegu chache, atavuna mazao machache; na mtu anayepanda mbegu nyingi atavuna mazao mengi.7 Kila mtu atoe kama anavyokusudia moyoni mwake, si kwa kusita au kwa kulazimishwa, kwa maana Mungu anapenda mtu anayetoa kwa moyo. 8 Na Mungu anaweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili kila wakati muwe na kila kitu kwa kiasi cha kutosha na ziada kwa ajili ya kila kazi njema. 9 Kama Maandiko yanavyosema, “Yeye hutapanya kila mahali kuwapa maskini, haki yake hudumu milele.” 10 Na Mungu ambaye ndiye humpa mkulima mbegu za kupanda, na mkate kwa chakula, atawapa na kuzidisha mbegu mnazohitaji na kuziwezesha kukua zitoe mazao ya matendo mema ya haki.

Mwandishi wa hii riwaya alikua muuaji mkubwa kama yule wa Kuruani. Ndiyo maana siamini hivi vitabu kwangu ni kama Riwaya tu.
 
Kwani ukichangia kujadili mambo ya ISIS unakua ni member wa ISIS siku hizi?
Mimi ni maoni yangu sina muda na huu uongo unaoitwa dini ila naheshimu wewe kuwa na dini ndiyo maana watoto wangu nimewaambia msimamo wangu kuwa siamini lolote kuhusu dini lakini wao ruksa kuabudu dini yeyote wanayoitaka iwatapeli na kwa bahati mbaya ninao wanne wote wameamua kutapeliwa na mapadre na masheikh na watu kama wewe. moja ni muislamu na wengine ni wakristu. Wanajua hilo kabisa kama sina muda na hiyo shughuli.

Kama nikiwaona nyie wafia dini mkishambuliana humu ninafurahi sana, maana mtu unafurahia na kujigamba mambo ya utapeli.
 

Hongera sana. Mimi nimeona kanisa limefanywa bar hicho cha mtoto mama yangu. Tena nilikua napenda sana kwenda kunywa hapo bar.

Mkifurahia hayo makanisa mjue pia kuwa mnalishwa sana vibudu huko. Machinjio yao hayana waislamu wa kuchinja
 
Back
Top Bottom