Kanisa la Roma, sadaka na michango yake

Kanisa la Roma, sadaka na michango yake

Mr Kiatu1 kuna wakati nipo zangu Iringa niliona misikiti mikubwa sana imejengwa na ASAS na hii ndio maana anazidishiwa zaidi kutokana na kile anachokifanya mbele ya jamii
ASAS na wengineo ambao hujawataja wanapata pesa kwa kufanya kazi kwa bidii na sio kwa kutoa makanisani au misikitini. Ingekuwa ni hivyo basi masikini wanaoshinda makanisani wanaombewa huku wanatoa hata kile kidogo walichonacho basi wangekuwa matajiri sana, wafundisheni watu kufanya kazi mana ndio msingi wa mafanikio na sio kuwaambia watoe ili wapate. Hicho kitu hakipo, tusaidie wasiojiweza sio wajanja wachache
 
Natumaini umekulia kwenye kanisa..Je unaona hali ya michango kwa sasa ni sawa na zamani? Je huoni malalamiko ya watu kuzidi kulingana na zamani?

Jumuiya zimekua kama Magereza ya kutubana...usipohudhuria/kutoa michango hubatizi mtoto,huzikwi na padre.Michango inasisitizwa kuliko Neno la Mungu.

Nimewahi kuwa Mlei niliyoyaona huko kuhusu sadaka/michango niliamua kukaa mbali na hayo mambo...amini Mkuu kwenye pesa isiyo na Ukaguzi kama ya kanisa kuna mengi ya kusikitisha yanaendelea...ukiwaambia watu wanakuambia wewe Toa tu mengine muachie Mungu.

Mr Kiatu1 huwa Mimi naamini katika kanisa katoriki sadaka yangu ninapo itoa huenda kusaidia mamia ya watu nisio wajua nikitolea mfano kunakituo kimoja cha kulea watu wasio jiweza kilianzishwa na RC kipo mkoa mmoja ivi na naamini vipo vingi tu kama sampuli ile bado kuna hospitali zinajengwa na matibabu yake ni gharama nafuu zinazo milikiwa na RC na miradi mingineyo mingi tu inaonekana tofauti na dini zingine.

Si ivo tu unapo toa sadaka haikupingi kwamba hata siku ukipata mia miambili umeona kikongwe anaomba msaada apate hata chai ushindwe kumsaidia! Unatoa pale unapoona kwako panafaa kuna wakati nipo zangu Iringa niliona misikiti mikubwa sana imejengwa na ASAS na hii ndio maana anazidishiwa zaidi kutokana na kile anachokifanya mbele ya jamii
 
Kweli kabisa mkuu, Jumuiya walileta kwaajili ya kukusanyia michango mana ni rahisi zaidi kuweza kuwajua watu na kuwatembelea nyumba kwa nyumba. Kwa mfano, hata kama hujawahi kwenda kanisani au kwenye jumuiya lakini michango huwa unaitoa kwa kuagiza mtu au wakija nyumbani kwako basi elewa kwamba ''huyu ni mwenzetu huwa anashiriki nasi'' kama sio mtoa michango na kanisani unaenda au jumuiya basi wataanza kuhoji ukatoliki wako. Kanisani unatambuliwa kwa michango na sio kwa imani
 
Harambeee umesahau kuku anauzwa kwa thamani laki 6 bado kanisa lingine linakuja au linaleta barua ili lichangiwe bado watoto kwenda ziara sehemu fulani tuchangie kwa kweli mi mwenyewe mzuka wa kwenda kanisani umenitoka.KARIBIA MASAA MENGI YA MISA YANAPOTEZWA KWENYE HARAMBEE NA MICHANGO MBALI MBALI BADALA YA NENO LA MUNGU.
KAMA MIMI NDO NILIKUWA KIHERE HERE WA KUCHANGIA KILA MCHANGO MPAKA MKE WANGU KANIKATAZA WAMEANZA KUNIPANGIA KIWANGO CHA KUTOA ETI WEWE NI WA KULIPA KUANZIA LAKI 2 NA KUENDELEA.
 
Mr Kiatu1 huwa Mimi naamini katika kanisa katoriki sadaka yangu ninapo itoa huenda kusaidia mamia ya watu nisio wajua nikitolea mfano kunakituo kimoja cha kulea watu wasio jiweza kilianzishwa na RC kipo mkoa mmoja ivi na naamini vipo vingi tu kama sampuli ile bado kuna hospitali zinajengwa na matibabu yake ni gharama nafuu zinazo milikiwa na RC na miradi mingineyo mingi tu inaonekana tofauti na dini zingine.

Si ivo tu unapo toa sadaka haikupingi kwamba hata siku ukipata mia miambili umeona kikongwe anaomba msaada apate hata chai ushindwe kumsaidia! Unatoa pale unapoona kwako panafaa kuna wakati nipo zangu Iringa niliona misikiti mikubwa sana imejengwa na ASAS na hii ndio maana anazidishiwa zaidi kutokana na kile anachokifanya mbele ya jamii

Utasaidiaje watu usiowajua ilhali kuna ndugu zako wengi wanaohitaji msaada wako?
 
Toka Vatican wajiondoe kujenga makanisa ya katoliki..michango imekuwa mingi mno.....
Binafsi sikuiamini hii habari. Nikaenda kwenye group letu la WhatsApp kuna baadhi yetu ni mapadre wakathibitisha. Nimewaambia bora waweke cash point kabisa. Nashukuru simo katika vyama iwe siasa ama dini. Sikiamini kitu kiitwacho dini. Kwangu mimi naona ni biashara dini zote
 
WAMEANZA KUNIPANGIA KIWANGO CHA KUTOA ETI WEWE NI WA KULIPA KUANZIA LAKI 2 NA KUENDELEA.
hahahah, eti wewe ni wa kulipa kuanzia laki mbili. Account yako wanajua ina sh ngapi? wanajua majukumu yako?
 
1 tegemeza jimbo
2 tegemeza parokia
3 mavuno jimbo
4 mavuno parokia
4 zaka
5 sadaka ya 1
6 sadaka ya 2
7 utoto mtakatifu (sherehe ziara makongamano ya taifa jimbo dekania parokia kanda)
8 vijana wakatoliki viwawa (semina ziara hija na majitoleo)
9 wanawake wakatoliki wawata( semina hija sare mafungo majitoleo hija)
10 wanaume wakatoliki uwaka( semina mafungo hija ziara majitoleo)
11 fomu mbali mbali (ubatizo ndoa)
12 tegemeza katekista
13 vyama vya kitume (kwaya karsmatik yosefu maria nk)
14 ujenzi wa kanisa ( bilioni 4)
15 jumuiyani sadaka sikukuu za somo wa jumuia kanda au kigango na parokia.
16 bahasha za noeli na kwaresma nk nk nk
Hio ni parokia yetu, samahani sana Mungu kwa coment hii kama nitakua nimefanya kosa.​
Mungu haijui hiyo sadaka nabpengine anakuonea huruma kama unatoa maana atakuona wewe ni zwazwa
 
Wafadhili walishastuka zamani maana mapadre wana vijumbs vidogo pesa zote wanajengea wanawake na familia zao wamesitisha. Mbona ulaya hilo kanisa halina michango kama hiyo
 
Wakuu,

Napenda kwenda moja kwa moja kwenye maada. Ifuatayo ni orodha ya sadaka na michango mbali mbali iliyopo kanisani kwetu kanisani kwetu Roman Catholic.

ORODHA YA SADAKA
1. Huwa kunakuwa na sadaka ya kwanza -Jumapili
2. Sadaka ya pili - Jumapili
3. Sadaka ya tatu (hii ni sadaka ya inayotolewa kwa kanda ya parokia, kila kanda ina kikapu chake) - Jumapili
4. Sadaka ya kwanza (Jumamosi kwenye Jumuiya ambapo kila mkatoliki anatakiwa kuhudhuria mtaani kwake)
5. Sadaka ya pili (Jumamosi kwenye Jumuiya)

ORODHA YA MICHANGO
6. Mchango wa tegemeza parokia (kanisa)
7. Mchango wa tegemeza jimbo (kwa mfano, jimbo la dar es salaam)
8. Mchango kujenga kanisa (ujenzi wa makanisa huwa hauishi, kama sio lenu mtaambiwa kuna kanisa linajengwa sijui wapi na wao hawana uwezo hivyo mchangie)
9. Mchango wa kila mwezi kwenye Jumuiya ambapo huwa mnasali kila Jumamosi, unatoa ya mwaka mzima.
10. Mchango wa UWAKA (Umoja wa Wanaume Wakatoliki Tanzania)
11. Mchango wa WAWATA (Wanawake Wakatoliki Tanzania)
12. Mchango wa kununua viti vya jumuiya (kila mwaka)
13. Mchango wa kutimiza mwaka kwa Jumuiya (kila jumuiya ina tarehe yake kulingana na siku iliyoanza)
14. Mchango wa sherehe ya jimbo (kwa mwaka mara moja)
15. Zaka (hii unatoa kila mwezi, asilimia kumi ya pesa uliyoingiza mwezi mzima bahasha zinagawiwa kila nyumba)
16. Mchango wa kuhamia jumuiya - kila mtaa huonana jumamosi kwaajili ya kusali hivyo kama umetoka mtaa A umehamia mtaa B basi huko utatakiwa kulipia hiyo pesa
17. Mchango wa form kwaajili ya kipaimara
18. Mchango kwaajili ya watu wanaosomea upadrii
19. Mchango kwaajili ya wanaosafiri kwenda kutangaza neno la Mungu
20. Mchango kwaajili ya ujenzi wa shule/ hospitali ya kanisa.
21. Malimbikizo, hii unatoa kama kuna michango huko nyuma hukutoa. Labda ulikuwa huendi kanisani or so
22. Shukrani, hii ni pesa au chochote unatoa kama kumshukuru Mungu
23. Mchango wa bima ya mapadrii
24. Mchango wa tegemeza katekista (katekista ni msaidizi wa padri)
25. Mchango wa utatu mtakatifu (sherehe ziara makongamano ya taifa jimbo dekania parokia kanda)
26. Mchango wa Viwawa (vijana wa katoliki)
27. Michango ya vyama vya kitume (kwaya karsmatik yosefu maria nk)
28. Bahasha za mchango wa noeli, kwaresma nk
29. Mchango wa kumpa zawadi mama bikira maria kwa kujifungua mtoto Yesu Christmas
30. Sadaka ya mwisho wa mwaka, kutoa katika ulichopata mwaka mzima

:, Kama kuna mchango au sadaka nimeisahau naomba mnitajie au kama kuna kitu nimeongeza niambieni nipunguze. Mfano, jana (15/12/2018) tumeambiwa kila Jumuiya (mtaa) unatakiwa kupeleka watoto wa wili wakale na Padri hivyo tuchangie elfu 23,000 ya chakula

Makanisa ya Roma vifaa vyao vya kuwekea sadaka hutengeneza kwa zile mbao zenye kupiga makelele sana, afu hilo box la mbao huwa refu. Nini maana yake? Unapotoa sadaka ukitoa pesa ya sarafu kama mia tano au mia mbili ukiweka humo inapiga kelele sana kila mtu anajua umetoa sarafu. Jambo ambalo kisaikolojia huwatesa wengi na kufanya mtu alazimike kutafute kuanzia elfu moja kwenda juu hata kama ni mtu wa hali ya chini kabisa.

Kiukweli michango imekuwa miingi sana na ndiomana vijana wanaoanza maisha hawaji kanisani mpaka wakiona wanataka kuoa ndio wanakuja. Kanisani unakuta kumejaa wazee, mahouse girl na watoto kwasababu huku umri wa kati wakikimbia michango sababu ya wingi wa majukumu. Hata mimi nimechoka na hili kanisa langu, kama nina mapepo basi wenzangu mniombee yanitoke.

Note: Baadhi ya michango ipo katika maeneo fulani na maeneo mengine hamna.
Mtatapeliwa sana kama hawa wenzenu
 
Hili ni kanisa linaloongoza kwa kufanya biashara ila faida itokanayo na biashara zao hairud kwa waumin.

Endeleeni kuwachangia, mim ntatoa kwa wasiojiweza kimaisha.
 
Duniani huko Makanisa yanafanywa misikiti nyie bado tu:
 
ASAS na wengineo ambao hujawataja wanapata pesa kwa kufanya kazi kwa bidii na sio kwa kutoa makanisani au misikitini. Ingekuwa ni hivyo basi masikini wanaoshinda makanisani wanaombewa huku wanatoa hata kile kidogo walichonacho basi wangekuwa matajiri sana, wafundisheni watu kufanya kazi mana ndio msingi wa mafanikio na sio kuwaambia watoe ili wapate. Hicho kitu hakipo, tusaidie wasiojiweza sio wajanja wachache
Na hicho hicho mkuu BABA TUPAC ndicho ninacho sistizia yakwamba Fanya kazi Kwa bidii na ukumbuke kutoa sadaka ama kusaidia watu wasio jiweza, kunaandiko moja katika biblia linasema asie Fanya kazi na asile na Mwenye nacho ataongezewa na asie nacho atanyang'anywa pia wanasema umaskini ni dhambi kwa sababu kila binadamu aliumbwa na macho,miguu,mikono,utashi, akili na haikuishia hapo pia Mungu akaumba mbingu na ardhi na akampa binadam mamlaka yakutawala kila kiumbe kilichopo ardhini na ukijaribu kutafsiri swala hili kwa mapana unaweza pata jibu la uwepo wa fursa nyingi sana ambazo zinao uwezo wakumkomboa mwanadam kujikwamua kiuchumi. Jaribu kufikiria ilo na naamini utanielewa kwanini naongelea hili (ila kama unaimani na uwepo wa mungu)
 
Hivi mkuu huna Ndugu mwenye shida kwenye familia? Hizo sadaka/michango/zaka Kwanini tusiwasaidie hao wahitaji wa kweli? Na sio kanisa lenye Ukwasi wa kutosha?
Kwa mujibu wa mafundisho ya Kimungu

" Mpe kaisari yaliyo yake kaisari na Mpe Mungu yaliyo yake Mungu"

Unatakiwa kutoa sadaka, zaka na michango mbalimbali ya kanisa na vilevile unapaswa kufanya Matendo saba ya huruma kwa Roho na Matendo saba ya Huruma kwa Mwili.

Hivyi usiache kuchangia Huduma za Kanisa kwa kisingizio cha kusaidia ndugu maana imekupasa kutenda yote.

Tena Kanisa Katoliki linatufundisha kutoa kwa Moyo wa Ukarimu wala si kwa kulazimishwa wala manung'uniko. Maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa Ukarimu. Kadiri ya Maandiko Matakatifu.
 
Duniani huko Makanisa yanafanywa misikiti nyie bado tu:

Mungu Mwana Yesu Kristo Masihi ambaye waarabu wanamuita Isa Al Masih alitabiri hayo. Alitutia Moyo kuwa yajapo hayo tusifadhaishwe.

"Watawafanyia ubaya wakidhani wanamtumikia mungu"
 
Natumaini umekulia kwenye kanisa..Je unaona hali ya michango kwa sasa ni sawa na zamani? Je huoni malalamiko ya watu kuzidi kulingana na zamani?

Jumuiya zimekua kama Magereza ya kutubana...usipohudhuria/kutoa michango hubatizi mtoto,huzikwi na padre.Michango inasisitizwa kuliko Neno la Mungu.

Nimewahi kuwa Mlei niliyoyaona huko kuhusu sadaka/michango niliamua kukaa mbali na hayo mambo...amini Mkuu kwenye pesa isiyo na Ukaguzi kama ya kanisa kuna mengi ya kusikitisha yanaendelea...ukiwaambia watu wanakuambia wewe Toa tu mengine muachie Mungu.
Hapo na Mimi nakuunga mkono ila nakusistiza utoe pale unapoona pana faa kama haipo katika uwezo wako iache tu na kama unafanyiwa hivo basi hao viongozi niwatu ambao hawajitambui bado ila pole kwa yote aise
 
Back
Top Bottom