Kanisa la Roma, sadaka na michango yake

Kanisa la Roma, sadaka na michango yake

Hivi mlivyokuwa mnajengewa makanisa mazuri na misaada ya kanisa ulijua nani alikuwa anatoa? kuna watu walikuwa wanajitoa huko Ulaya, sas ni zamu yetu kujenga makanisa wenyewe, shule, hospitals na kuendesha taasisi zetu za kidini wenyewe! acha uvivu wa fikra TOA SADAKA NDUGU
Makanisa tunajenga kila siku!!!?
Dini ni Biashara.
 
Sadaka ya kweli ni Kuwasaidia Wahitaji (Masikini, Wagonjwa, Yatima na Wajane)
Hizo sadaka zenu nyingi huko Makanisani ni Ubatili.
Jifunzeni kuwasaidia Wahitaji na matunda yake mtayaona.
 
hahahah, eti wewe ni wa kulipa kuanzia laki mbili. Account yako wanajua ina sh ngapi? wanajua majukumu yako?
Kilichoniponza nilikuwa najitoa sana kwenye kutoa michango na mbaya zaidi jumuiya ikifeli kitu fulani nilikuwa naokoa jahazi kumbe wenzangu wakanitafsiri kuwa nina mpunga mwingi.
 
Swali zuri ,ambalo hata mm nimelitafakar sana, utasaidiaje usiowajua wakat nyumba ya jiran kuna mtu analala njaa, au kuna kijana kakosa ada ya shule


Hapo ndipo msingi wa mashaka unapoanzia. Ila kila mtu afanye ajuavyo
 
Nina mashaka kama we ni mkatoliki. Maana umoja wa wanaume wakatoliki hauitwi WAWAKA wala umoja wa wanawake hauitwi UWATA.

Rudi kwa aliyekutuma akuelekeze vizuri ndo uje na andiko hili tena.
Hiyo michango ipo au haipo,unakosoa spelling badala ya kukosoa andiko zima
 
Wakuu,

Napenda kwenda moja kwa moja kwenye maada. Ifuatayo ni orodha ya sadaka na michango mbali mbali iliyopo kanisani kwetu kanisani kwetu Roman Catholic.

ORODHA YA SADAKA
1. Huwa kunakuwa na sadaka ya kwanza -Jumapili
2. Sadaka ya pili - Jumapili
3. Sadaka ya tatu (hii ni sadaka ya inayotolewa kwa kanda ya parokia, kila kanda ina kikapu chake) - Jumapili
4. Sadaka ya kwanza (Jumamosi kwenye Jumuiya ambapo kila mkatoliki anatakiwa kuhudhuria mtaani kwake)
5. Sadaka ya pili (Jumamosi kwenye Jumuiya)

ORODHA YA MICHANGO
6. Mchango wa tegemeza parokia (kanisa)
7. Mchango wa tegemeza jimbo (kwa mfano, jimbo la dar es salaam)
8. Mchango kujenga kanisa (ujenzi wa makanisa huwa hauishi, kama sio lenu mtaambiwa kuna kanisa linajengwa sijui wapi na wao hawana uwezo hivyo mchangie)
9. Mchango wa kila mwezi kwenye Jumuiya ambapo huwa mnasali kila Jumamosi, unatoa ya mwaka mzima.
10. Mchango wa UWAKA (Umoja wa Wanaume Wakatoliki Tanzania)
11. Mchango wa WAWATA (Wanawake Wakatoliki Tanzania)
12. Mchango wa kununua viti vya jumuiya (kila mwaka)
13. Mchango wa kutimiza mwaka kwa Jumuiya (kila jumuiya ina tarehe yake kulingana na siku iliyoanza)
14. Mchango wa sherehe ya jimbo (kwa mwaka mara moja)
15. Zaka (hii unatoa kila mwezi, asilimia kumi ya pesa uliyoingiza mwezi mzima bahasha zinagawiwa kila nyumba)
16. Mchango wa kuhamia jumuiya - kila mtaa huonana jumamosi kwaajili ya kusali hivyo kama umetoka mtaa A umehamia mtaa B basi huko utatakiwa kulipia hiyo pesa
17. Mchango wa form kwaajili ya kipaimara
18. Mchango kwaajili ya watu wanaosomea upadrii
19. Mchango kwaajili ya wanaosafiri kwenda kutangaza neno la Mungu
20. Mchango kwaajili ya ujenzi wa shule/ hospitali ya kanisa.
21. Malimbikizo, hii unatoa kama kuna michango huko nyuma hukutoa. Labda ulikuwa huendi kanisani or so
22. Shukrani, hii ni pesa au chochote unatoa kama kumshukuru Mungu
23. Mchango wa bima ya mapadrii
24. Mchango wa tegemeza katekista (katekista ni msaidizi wa padri)
25. Mchango wa utatu mtakatifu (sherehe ziara makongamano ya taifa jimbo dekania parokia kanda)
26. Mchango wa Viwawa (vijana wa katoliki)
27. Michango ya vyama vya kitume (kwaya karsmatik yosefu maria nk)
28. Bahasha za mchango wa noeli, kwaresma nk
29. Mchango wa kumpa zawadi mama bikira maria kwa kujifungua mtoto Yesu Christmas
30. Sadaka ya mwisho wa mwaka, kutoa katika ulichopata mwaka mzima
31. Mchango wa radio Maria
32. Mchango wa radio Tumaini

:, Kama kuna mchango au sadaka nimeisahau naomba mnitajie au kama kuna kitu nimeongeza niambieni nipunguze. Mfano, jana (15/12/2018) tumeambiwa kila Jumuiya (mtaa) unatakiwa kupeleka watoto wa wili wakale na Padri hivyo tuchangie elfu 23,000 ya chakula

Makanisa ya Roma vifaa vyao vya kuwekea sadaka hutengeneza kwa zile mbao zenye kupiga makelele sana, afu hilo box la mbao huwa refu. Nini maana yake? Unapotoa sadaka ukitoa pesa ya sarafu kama mia tano au mia mbili ukiweka humo inapiga kelele sana kila mtu anajua umetoa sarafu. Jambo ambalo kisaikolojia huwatesa wengi na kufanya mtu alazimike kutafute kuanzia elfu moja kwenda juu hata kama ni mtu wa hali ya chini kabisa.

Kiukweli michango imekuwa miingi sana na ndiomana vijana wanaoanza maisha hawaji kanisani mpaka wakiona wanataka kuoa ndio wanakuja. Kanisani unakuta kumejaa wazee, mahouse girl na watoto kwasababu huku umri wa kati wakikimbia michango sababu ya wingi wa majukumu. Hata mimi nimechoka na hili kanisa langu, kama nina mapepo basi wenzangu mniombee yanitoke.

Note: Baadhi ya michango ipo katika maeneo fulani na maeneo mengine hamna.
basi hizo pesa peleka bar kapige watu ofa,ili moyo wako ufurahi..
 
Pole sana mkuu, Kwa yote hayo ila siku zote wanakusihi kwamba unapoitoa sadaka yako jitathmini mwenyew yakwamba ni mangapi mazuri na mema uliyotendewa na mungu na kile unachokitoa kinalingana na thamani halisi ambayo MUNGU kakutendea katika shughuri zako za kila Siku .? ( kama unaishi Kwa imani ya uwepo wa mungu) sadaka haulazimishwi kutoa ni hiali ya mtu kulingana na uwezo wako na kumbuka kila unapo toa huzidishiwa maradufu hayo ni maandiko katika bibilia takatifu. Na ili swala kama ilo lisiendelee kukutokea jaribu hata kila siku upatapo 5,000/= jiwekee 500/= kama shukurani (500×6 ni 3,000/=) inatosha sana
5000 matumizi ni kiasi gani mpaka nitoe 500 ya sadaka
 
Wakuu,

Napenda kwenda moja kwa moja kwenye maada. Ifuatayo ni orodha ya sadaka na michango mbali mbali iliyopo kanisani kwetu kanisani kwetu Roman Catholic.

ORODHA YA SADAKA
1. Huwa kunakuwa na sadaka ya kwanza -Jumapili
2. Sadaka ya pili - Jumapili
3. Sadaka ya tatu (hii ni sadaka ya inayotolewa kwa kanda ya parokia, kila kanda ina kikapu chake) - Jumapili
4. Sadaka ya kwanza (Jumamosi kwenye Jumuiya ambapo kila mkatoliki anatakiwa kuhudhuria mtaani kwake)
5. Sadaka ya pili (Jumamosi kwenye Jumuiya)

ORODHA YA MICHANGO
6. Mchango wa tegemeza parokia (kanisa)
7. Mchango wa tegemeza jimbo (kwa mfano, jimbo la dar es salaam)
8. Mchango kujenga kanisa (ujenzi wa makanisa huwa hauishi, kama sio lenu mtaambiwa kuna kanisa linajengwa sijui wapi na wao hawana uwezo hivyo mchangie)
9. Mchango wa kila mwezi kwenye Jumuiya ambapo huwa mnasali kila Jumamosi, unatoa ya mwaka mzima.
10. Mchango wa UWAKA (Umoja wa Wanaume Wakatoliki Tanzania)
11. Mchango wa WAWATA (Wanawake Wakatoliki Tanzania)
12. Mchango wa kununua viti vya jumuiya (kila mwaka)
13. Mchango wa kutimiza mwaka kwa Jumuiya (kila jumuiya ina tarehe yake kulingana na siku iliyoanza)
14. Mchango wa sherehe ya jimbo (kwa mwaka mara moja)
15. Zaka (hii unatoa kila mwezi, asilimia kumi ya pesa uliyoingiza mwezi mzima bahasha zinagawiwa kila nyumba)
16. Mchango wa kuhamia jumuiya - kila mtaa huonana jumamosi kwaajili ya kusali hivyo kama umetoka mtaa A umehamia mtaa B basi huko utatakiwa kulipia hiyo pesa
17. Mchango wa form kwaajili ya kipaimara
18. Mchango kwaajili ya watu wanaosomea upadrii
19. Mchango kwaajili ya wanaosafiri kwenda kutangaza neno la Mungu
20. Mchango kwaajili ya ujenzi wa shule/ hospitali ya kanisa.
21. Malimbikizo, hii unatoa kama kuna michango huko nyuma hukutoa. Labda ulikuwa huendi kanisani or so
22. Shukrani, hii ni pesa au chochote unatoa kama kumshukuru Mungu
23. Mchango wa bima ya mapadrii
24. Mchango wa tegemeza katekista (katekista ni msaidizi wa padri)
25. Mchango wa utatu mtakatifu (sherehe ziara makongamano ya taifa jimbo dekania parokia kanda)
26. Mchango wa Viwawa (vijana wa katoliki)
27. Michango ya vyama vya kitume (kwaya karsmatik yosefu maria nk)
28. Bahasha za mchango wa noeli, kwaresma nk
29. Mchango wa kumpa zawadi mama bikira maria kwa kujifungua mtoto Yesu Christmas
30. Sadaka ya mwisho wa mwaka, kutoa katika ulichopata mwaka mzima
31. Mchango wa radio Maria
32. Mchango wa radio Tumaini

:, Kama kuna mchango au sadaka nimeisahau naomba mnitajie au kama kuna kitu nimeongeza niambieni nipunguze. Mfano, jana (15/12/2018) tumeambiwa kila Jumuiya (mtaa) unatakiwa kupeleka watoto wa wili wakale na Padri hivyo tuchangie elfu 23,000 ya chakula

Makanisa ya Roma vifaa vyao vya kuwekea sadaka hutengeneza kwa zile mbao zenye kupiga makelele sana, afu hilo box la mbao huwa refu. Nini maana yake? Unapotoa sadaka ukitoa pesa ya sarafu kama mia tano au mia mbili ukiweka humo inapiga kelele sana kila mtu anajua umetoa sarafu. Jambo ambalo kisaikolojia huwatesa wengi na kufanya mtu alazimike kutafute kuanzia elfu moja kwenda juu hata kama ni mtu wa hali ya chini kabisa.

Kiukweli michango imekuwa miingi sana na ndiomana vijana wanaoanza maisha hawaji kanisani mpaka wakiona wanataka kuoa ndio wanakuja. Kanisani unakuta kumejaa wazee, mahouse girl na watoto kwasababu huku umri wa kati wakikimbia michango sababu ya wingi wa majukumu. Hata mimi nimechoka na hili kanisa langu, kama nina mapepo basi wenzangu mniombee yanitoke.

Note: Baadhi ya michango ipo katika maeneo fulani na maeneo mengine hamna.
Kati ya hiyo michango yote,kuna mchango wowote ambao mkatoliki analazimishwa kuutoa?
Nendeni kanisani mkasali mumjue Mwenyenzi Mungu vema,
Toa sadaka kama unayo kama huna basi huna,kelele ya nini?
Ni wangapi wanakwenda kanisani na kurudi bila kutoa sadaka?
Majaribu hayana budi kuwepo lakini ole wake yule atakayesababisha.
 
Aende wapi ndugu?
unapoambiwa toka kwenye nyumba inayoungua usiulize niende nyumba gani, kwanza toka halafu utaona nyumba ya kuingia.
Kiufupi,akishatoka huko ngiposa atajua aende wapi.
 
Back
Top Bottom