Kanisa la Roma, sadaka na michango yake

Kanisa la Roma, sadaka na michango yake

Pole sana mkuu, Kwa yote hayo ila siku zote wanakusihi kwamba unapoitoa sadaka yako jitathmini mwenyew yakwamba ni mangapi mazuri na mema uliyotendewa na mungu na kile unachokitoa kinalingana na thamani halisi ambayo MUNGU kakutendea katika shughuri zako za kila Siku .? ( kama unaishi Kwa imani ya uwepo wa mungu) sadaka haulazimishwi kutoa ni hiali ya mtu kulingana na uwezo wako na kumbuka kila unapo toa huzidishiwa maradufu hayo ni maandiko katika bibilia takatifu. Na ili swala kama ilo lisiendelee kukutokea jaribu hata kila siku upatapo 5,000/= jiwekee 500/= kama shukurani (500×6 ni 3,000/=) inatosha sana
Endeleeni kutumia maneno mazuri na vitisho ili mpate sadaka na michango ila hamnipati tena
 
usipotoa inakuwaje??? iv michango hiyo ni lazima au ni mpaka ukijaaliwa kupata mfukoni mwako??
 
Pole sana mkuu, Kwa yote hayo ila siku zote wanakusihi kwamba unapoitoa sadaka yako jitathmini mwenyew yakwamba ni mangapi mazuri na mema uliyotendewa na mungu na kile unachokitoa kinalingana na thamani halisi ambayo MUNGU kakutendea katika shughuri zako za kila Siku .? ( kama unaishi Kwa imani ya uwepo wa mungu) sadaka haulazimishwi kutoa ni hiali ya mtu kulingana na uwezo wako na kumbuka kila unapo toa huzidishiwa maradufu hayo ni maandiko katika bibilia takatifu. Na ili swala kama ilo lisiendelee kukutokea jaribu hata kila siku upatapo 5,000/= jiwekee 500/= kama shukurani (500×6 ni 3,000/=) inatosha sana
Yani unatoa tu? Afu hamna mapato na matumizi
 
1 tegemeza jimbo
2 tegemeza parokia
3 mavuno jimbo
4 mavuno parokia
4 zaka
5 sadaka ya 1
6 sadaka ya 2
7 utoto mtakatifu (sherehe ziara makongamano ya taifa jimbo dekania parokia kanda)
8 vijana wakatoliki viwawa (semina ziara hija na majitoleo)
9 wanawake wakatoliki wawata( semina hija sare mafungo majitoleo hija)
10 wanaume wakatoliki uwaka( semina mafungo hija ziara majitoleo)
11 fomu mbali mbali (ubatizo ndoa)
12 tegemeza katekista
13 vyama vya kitume (kwaya karsmatik yosefu maria nk)
14 ujenzi wa kanisa ( bilioni 4)
15 jumuiyani sadaka sikukuu za somo wa jumuia kanda au kigango na parokia.
16 bahasha za noeli na kwaresma nk nk nk
Hio ni parokia yetu, samahani sana Mungu kwa coment hii kama nitakua nimefanya kosa.​
 
Haaa[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mbona husema wachungaji wa kilokole ni wapiga dili imekuwaje tena ? Hakuna namna wala kukimbia hakuna wakulijenga kanisa zaidi ya nyie hao hao waamini wake komalia humo humo
 
Lakini kanisa lina vitega uchumi kama vile shule, hospitali, kumbi za makutano sadaka
Bado hapo tunauhitaji wa michango titiri??
Kuna michango hutakaa usikie Inafanya nini...kama Zaka/Mavuno.
Huwa najiuliza kama zamani makanisa yalijengwa kwa misaada toke nje..Sisi tunajenga wapi? Manake tunakusanya kuliko huko Ulaya..
 
Mimi niliasha acha na jumuia kabisa,maana jumuia moto na kanisa moto,michango na sadaka za lazima utoe,parokia yetu furani mt p mwanzo sadaka ilikuwa nikwenye kikapu tena unatoa kwenye ukiwa kwenye bench,kwa sasa wameweka visanduku kama vibubu,ukiweka jero ndugu kanisa zima wanasikia,alafu mnapanga mstali kwenda kutoa sadaka,hapo mwanzo haikuwapo.
 
Yani unatoa tu? Afu hamna mapato na matumizi
Hapo nimepiga hesabu ya 5,000/= nikimaanisha ukiondoa mapato na matumizi kwamba katika kila 5,000/= unawekeza 4,500/=×6 almost saving ni 27,000/= kila wiki wakati sadaka yako in 3,000/= naamini ni ndogo sana hii pesa
 
Hivi mkuu huna Ndugu mwenye shida kwenye familia? Hizo sadaka/michango/zaka Kwanini tusiwasaidie hao wahitaji wa kweli? Na sio kanisa lenye Ukwasi wa kutosha?
Hapo nimepiga hesabu ya 5,000/= nikimaanisha ukiondoa mapato na matumizi kwamba katika kila 5,000/= unawekeza 4,500/=×6 almost saving ni 27,000/= kila wiki wakati sadaka yako in 3,000/= naamini ni ndogo sana hii pesa
 
Wakuu,

Napenda kwenda moja kwa moja kwenye maada. Ifuatayo ni orodha ya sadaka na michango mbali mbali iliyopo kanisani kwetu kanisani kwetu Roman Catholic.

ORODHA YA SADAKA
1. Huwa kunakuwa na sadaka ya kwanza -Jumapili
2. Sadaka ya pili - Jumapili
3. Sadaka ya tatu (hii ni sadaka ya inayotolewa kwa kanda ya parokia, kila kanda ina kikapu chake) - Jumapili
4. Sadaka ya kwanza (Jumamosi kwenye Jumuiya ambapo kila mkatoliki anatakiwa kuhudhuria mtaani kwake)
5. Sadaka ya pili (Jumamosi kwenye Jumuiya)

ORODHA YA MICHANGO
6. Mchango wa tegemeza parokia (kanisa)
7. Mchango wa tegemeza jimbo (kwa mfano, jimbo la dar es salaam)
8. Mchango kujenga kanisa (ujenzi wa makanisa huwa hauishi, kama sio lenu mtaambiwa kuna kanisa linajengwa sijui wapi na wao hawana uwezo hivyo mchangie)
9. Mchango wa kila mwezi kwenye Jumuiya ambapo huwa mnasali kila Jumamosi, unatoa ya mwaka mzima.
10. Mchango wa UWAKA (Umoja wa Wanaume Wakatoliki Tanzania)
11. Mchango wa WAWATA (Wanawake Wakatoliki Tanzania)
12. Mchango wa kununua viti vya jumuiya (kila mwaka)
13. Mchango wa kutimiza mwaka kwa Jumuiya (kila jumuiya ina tarehe yake kulingana na siku iliyoanza)
14. Mchango wa sherehe ya jimbo (kwa mwaka mara moja)
15. Zaka (hii unatoa kila mwezi, asilimia kumi ya pesa uliyoingiza mwezi mzima bahasha zinagawiwa kila nyumba)
16. Mchango wa kuhamia jumuiya - kila mtaa huonana jumamosi kwaajili ya kusali hivyo kama umetoka mtaa A umehamia mtaa B basi huko utatakiwa kulipia hiyo pesa
17. Mchango wa form kwaajili ya kipaimara
18. Mchango kwaajili ya watu wanaosomea upadrii
19. Mchango kwaajili ya wanaosafiri kwenda kutangaza neno la Mungu
20. Mchango kwaajili ya ujenzi wa shule/ hospitali ya kanisa.
21. Malimbikizo, hii unatoa kama kuna michango huko nyuma hukutoa. Labda ulikuwa huendi kanisani or so
22. Shukrani, hii ni pesa au chochote unatoa kama kumshukuru Mungu
23. Mchango wa bima ya mapadrii

:, Kama kuna mchango au sadaka nimeisahau naomba mnitajie au kama kuna kitu nimeongeza niambieni nipunguze. Mfano, jana (15/12/2018) tumeambiwa kila Jumuiya (mtaa) unatakiwa kupeleka watoto wa wili wakale na Padri hivyo tuchangie elfu 23,000 ya chakula

Makanisa ya Roma vifaa vyao vya kuwekea sadaka hutengeneza kwa zile mbao zenye kupiga makelele sana, afu hilo box la mbao huwa refu. Nini maana yake? Unapotoa sadaka ukitoa pesa ya sarafu kama mia tano au mia mbili ukiweka humo inapiga kelele sana kila mtu anajua umetoa sarafu. Jambo ambalo kisaikolojia huwatesa wengi na kufanya mtu alazimike kutafute kuanzia elfu moja kwenda juu hata kama ni mtu wa hali ya chini kabisa.

Kiukweli michango imekuwa miingi sana na ndiomana vijana wanaoanza maisha hawaji kanisani mpaka wakiona wanataka kuoa ndio wanakuja. Kanisani unakuta kumejaa wazee, mahouse girl na watoto kwasababu huku umri wa kati wakikimbia michango sababu ya wingi wa majukumu. Hata mimi nimechoka na hili kanisa langu, kama nina mapepo basi wenzangu mniombee yanitoke.

Note: Baadhi ya michango ipo katika maeneo fulani na maeneo mengine hamna.
Aisee, Abraham anatoa MTOTO kama sadaka wewe BUKU unaona shida????
 
Roman Catholic, wapi Tanzanian Catholic?
Nathani ni Kanisa Katoliki - Catholic church.
 
Hivi mkuu huna Ndugu mwenye shida kwenye familia? Hizo sadaka/michango/zaka Kwanini tusiwasaidie hao wahitaji wa kweli? Na sio kanisa lenye Ukwasi wa kutosha?
Mr Kiatu1 huwa Mimi naamini katika kanisa katoriki sadaka yangu ninapo itoa huenda kusaidia mamia ya watu nisio wajua nikitolea mfano kunakituo kimoja cha kulea watu wasio jiweza kilianzishwa na RC kipo mkoa mmoja ivi na naamini vipo vingi tu kama sampuli ile bado kuna hospitali zinajengwa na matibabu yake ni gharama nafuu zinazo milikiwa na RC na miradi mingineyo mingi tu inaonekana tofauti na dini zingine.

Si ivo tu unapo toa sadaka haikupingi kwamba hata siku ukipata mia miambili umeona kikongwe anaomba msaada apate hata chai ushindwe kumsaidia! Unatoa pale unapoona kwako panafaa kuna wakati nipo zangu Iringa niliona misikiti mikubwa sana imejengwa na ASAS na hii ndio maana anazidishiwa zaidi kutokana na kile anachokifanya mbele ya jamii
 
Back
Top Bottom