Kanisa la Roma, sadaka na michango yake

Kanisa la Roma, sadaka na michango yake

Message yako haieleweki ndiyo matatizo ya kufuata dini hayo. Soma vizuri ulichokiandika mkuu.
Ukiwa na akili ndogo kamwe huwezi kunielewa nilichoandika.

Ukristo siyo dini bali imelazimishwa tu kuwemo kwenye orodha ya dini.

Kristu ni kwa ajili ya watu wote, ni nini usichokielewa hapa?

Waulize watu wenye dini zao tofauti tofauti wanamjuwa Masiha? Ukipata jibu la Masiha ni nani ndio utaelewa hakuna dini.
 
wa-katoliki wote mikono juu mwendo wa mateka.!
Siyo mwendo wa mateka,itakuwa mwendo wa mateka kama muumini mwenyewe hajajitambua.

Tuanze hivi;
Zaka,simuelewi mtu anajiita Mkatoliki au Mkristo halafu analalamikia yeye kutoa zaka wakati zaka ni amri kwamba lazima 10% ya kipato chako umtolee Mungu ambaye sina shaka anaamini ndiye aliyemwezesha kupata riziki,kwa maneno mengine kutokutoa zaka ni dhambi kama zilivyo dhambi nyengine.

Sijajua anacholalamika hapa huyu ikiwa anajua kabisa hapana sehemu Kanisa Katoliki limemlazimisha mtu kutoa sadaka,na asije mtu akajidanganya eti haendi Kanisani kwa sababu anaogopa michango hiko ni kiburi tu tunachojijengea wanadamu.

Kingine,kutoa sadaka siyo mpaka uwe na cha ziada,kwenye Bible kuna mfano Bibi alitoa mpaka cent yake ya mwisho akiwa hajui hata baada yakutoka pale atakula nini leo kijana unalalamika kutoa sadaka,kutoa zaka?umepewa nguvu, akili na maarifa unakuwa mchoyo hata kwa yule aliyekupa?toa ukiamini Mungu atakupa kingine cha kula mara ngapi tunalala tunaamka ila wale tuliolala nao wakiamka hali wamekufa?hivi ktk situation kama hii unamshukuruje Mungu kama siyo kwa kupitia kujitoa kama ni kujenga Kanisa mahali hata kama unajua hutokaa usali pale we toa alimradi ni kazi ya Mungu.

Mimi sijui ila Kanisani mchango wowote kama nina hela mfukoni nitatoa wala sitotafuta excuses,siijui hata sekunde moja ya maisha yangu mbele ning'ang'anie hela za kazi gani?ila pia Kanisa Katoliki lina mfumo mzuri wa uwazi,kama muumini una wasiwasi na matumizi unaweza kwenda kuhoji kama ukikosa majibu ya kuridhisha nenda jimboni utasikilizwa vizuri.
 
U
Unajua mkuu Jokajeusi kwamba sisi tunaoamini katika kristu, aliteswa msalabani kwaajili yetu sisi na kwaajili yawote Kwa maondoleo ya dhambi zetu. Sinaimani kama alikuwa ananifaham Mimi au wewe kwamba ipo karne tutaja kuzaliwa

Nyerere alilipigania taiga letu ikiwemo kutaifisha hospitali na shule mbali mbali ambazo hata wewe yawezekena ndipo ulipo patia elimu lakini chaajabu sinaiman kama alikuwa anatufaham Mimi na wewe

1 Timotheo 5:
8 Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.
 
Unajua mkuu jokajeusi


Huwezi msaidia mtu usiyemjua ilhali unayemjua anataabika, huwezi mpenda mtu usiyemjua na ambaye hujawahi muona wakati unaowajua huwapendi. Ukifanya haya ujue haupo mbali na unafiki
 
Wakuu,

Napenda kwenda moja kwa moja kwenye maada. Ifuatayo ni orodha ya sadaka na michango mbali mbali iliyopo kanisani kwetu kanisani kwetu Roman Catholic.

ORODHA YA SADAKA
1. Huwa kunakuwa na sadaka ya kwanza -Jumapili
2. Sadaka ya pili - Jumapili
3. Sadaka ya tatu (hii ni sadaka ya inayotolewa kwa kanda ya parokia, kila kanda ina kikapu chake) - Jumapili
4. Sadaka ya kwanza (Jumamosi kwenye Jumuiya ambapo kila mkatoliki anatakiwa kuhudhuria mtaani kwake)
5. Sadaka ya pili (Jumamosi kwenye Jumuiya)

ORODHA YA MICHANGO
6. Mchango wa tegemeza parokia (kanisa)
7. Mchango wa tegemeza jimbo (kwa mfano, jimbo la dar es salaam)
8. Mchango kujenga kanisa (ujenzi wa makanisa huwa hauishi, kama sio lenu mtaambiwa kuna kanisa linajengwa sijui wapi na wao hawana uwezo hivyo mchangie)
9. Mchango wa kila mwezi kwenye Jumuiya ambapo huwa mnasali kila Jumamosi, unatoa ya mwaka mzima.
10. Mchango wa UWAKA (Umoja wa Wanaume Wakatoliki Tanzania)
11. Mchango wa WAWATA (Wanawake Wakatoliki Tanzania)
12. Mchango wa kununua viti vya jumuiya (kila mwaka)
13. Mchango wa kutimiza mwaka kwa Jumuiya (kila jumuiya ina tarehe yake kulingana na siku iliyoanza)
14. Mchango wa sherehe ya jimbo (kwa mwaka mara moja)
15. Zaka (hii unatoa kila mwezi, asilimia kumi ya pesa uliyoingiza mwezi mzima bahasha zinagawiwa kila nyumba)
16. Mchango wa kuhamia jumuiya - kila mtaa huonana jumamosi kwaajili ya kusali hivyo kama umetoka mtaa A umehamia mtaa B basi huko utatakiwa kulipia hiyo pesa
17. Mchango wa form kwaajili ya kipaimara
18. Mchango kwaajili ya watu wanaosomea upadrii
19. Mchango kwaajili ya wanaosafiri kwenda kutangaza neno la Mungu
20. Mchango kwaajili ya ujenzi wa shule/ hospitali ya kanisa.
21. Malimbikizo, hii unatoa kama kuna michango huko nyuma hukutoa. Labda ulikuwa huendi kanisani or so
22. Shukrani, hii ni pesa au chochote unatoa kama kumshukuru Mungu
23. Mchango wa bima ya mapadrii
24. Mchango wa tegemeza katekista (katekista ni msaidizi wa padri)
25. Mchango wa utatu mtakatifu (sherehe ziara makongamano ya taifa jimbo dekania parokia kanda)
26. Mchango wa Viwawa (vijana wa katoliki)
27. Michango ya vyama vya kitume (kwaya karsmatik yosefu maria nk)
28. Bahasha za mchango wa noeli, kwaresma nk
29. Mchango wa kumpa zawadi mama bikira maria kwa kujifungua mtoto Yesu Christmas
30. Sadaka ya mwisho wa mwaka, kutoa katika ulichopata mwaka mzima
31. Mchango wa radio Maria
32. Mchango wa radio Tumaini

:, Kama kuna mchango au sadaka nimeisahau naomba mnitajie au kama kuna kitu nimeongeza niambieni nipunguze. Mfano, jana (15/12/2018) tumeambiwa kila Jumuiya (mtaa) unatakiwa kupeleka watoto wa wili wakale na Padri hivyo tuchangie elfu 23,000 ya chakula

Makanisa ya Roma vifaa vyao vya kuwekea sadaka hutengeneza kwa zile mbao zenye kupiga makelele sana, afu hilo box la mbao huwa refu. Nini maana yake? Unapotoa sadaka ukitoa pesa ya sarafu kama mia tano au mia mbili ukiweka humo inapiga kelele sana kila mtu anajua umetoa sarafu. Jambo ambalo kisaikolojia huwatesa wengi na kufanya mtu alazimike kutafute kuanzia elfu moja kwenda juu hata kama ni mtu wa hali ya chini kabisa.

Kiukweli michango imekuwa miingi sana na ndiomana vijana wanaoanza maisha hawaji kanisani mpaka wakiona wanataka kuoa ndio wanakuja. Kanisani unakuta kumejaa wazee, mahouse girl na watoto kwasababu huku umri wa kati wakikimbia michango sababu ya wingi wa majukumu. Hata mimi nimechoka na hili kanisa langu, kama nina mapepo basi wenzangu mniombee yanitoke.

Note: Baadhi ya michango ipo katika maeneo fulani na maeneo mengine hamna.
[emoji121]
KWA HIYO TUKUSAIDIE NINI LABDA MKUU?
 
Kanisani kwetu ss kuna sanduku la mbao lisilopenya salafu.unatakiwa kutoa noti tu.kw hiyo km uko na mke wako na watoto 4 na mfanyakaz mmoja inabidi utumie 7000.hii ni pesa nyingi sn.na imeandikwa utoapo sadaka mkono wako wa kushoto usijue.kw kweli haya makanisa ndimo shetani amehamia na kuishi.cjui yesu akija atayakubali kweli haya makanisa.
 
Nina uhakika 97% ya sadaka ulizotaja ni machukizo mbele za Mungu.
Huu ni
Wizi
Ukora
Utapeli.
 
Kanisani kwetu ss kuna sanduku la mbao lisilopenya salafu.unatakiwa kutoa noti tu.kw hiyo km uko na mke wako na watoto 4 na mfanyakaz mmoja inabidi utumie 7000.hii ni pesa nyingi sn.na imeandikwa utoapo sadaka mkono wako wa kushoto usijue.kw kweli haya makanisa ndimo shetani amehamia na kuishi.cjui yesu akija atayakubali kweli haya makanisa.
Unasubiri nini hapo Ndugu?
 
Harambeee umesahau kuku anauzwa kwa thamani laki 6 bado kanisa lingine linakuja au linaleta barua ili lichangiwe bado watoto kwenda ziara sehemu fulani tuchangie kwa kweli mi mwenyewe mzuka wa kwenda kanisani umenitoka.KARIBIA MASAA MENGI YA MISA YANAPOTEZWA KWENYE HARAMBEE NA MICHANGO MBALI MBALI BADALA YA NENO LA MUNGU.
KAMA MIMI NDO NILIKUWA KIHERE HERE WA KUCHANGIA KILA MCHANGO MPAKA MKE WANGU KANIKATAZA WAMEANZA KUNIPANGIA KIWANGO CHA KUTOA ETI WEWE NI WA KULIPA KUANZIA LAKI 2 NA KUENDELEA.
Hahaaaa ,wakaona wewe ni wao ,wakabid wakupangie na kiwango kabisa
 
KUNA JAMAA MMOJA ALIPEWA NAFASI YA KUHAMASISHA MICHANGO KANISANI KWETU, KATIKA KAULI ZAKE MOJAWAPO ALISEMA ANASHANGAA SANA MWANAUME MZIMA MKATOLIKI ETI ANATOA SADAKA YA SHILINGI 1000 !!!!
ILIBIDI NIJIULIZE HIVI HUYU JAMAA ANAHISI WAUMINI WOTE WAKATOLIKI NI MAMILIONEA NINI?
 
Kwangu sadaka za kanisani hazijawahi nichosha kutoa kama ninazo na kwakweli kwangu kanisa huwa linanilipa na hasa kipindi cha masomo na mahubiri kwa kuwa wakati mwingine huwa napata majibu ya changomoto zangu kwa gharama nafuu.
lakini ifike wakati tuelewe hivi hizo fedha tunazotoa zina thamani gani ukilinganisha na unachopokea? kama upo kiimani na huchanganyi uganga huwezi kuona hasara kutoa sadaka.
tabu nyingi tumezitoa kwa waganga na hatuoni tabu
Wewe ushakuwa brainwashed ,
 
aslimia kubwa ya watu wanaotoa sana sadaka kwa haya makanisa wana hali duni maana hata wanatoa kiunafiki,angalia kama kuna padre au askofu mwenye njaa wote wana afya njema
Hao maaskofu na mapadri wana afya njema maana wananenepa bila kufanya kazi kwa hela za maskini
 
Lakini kanisa lina vitega uchumi kama vile shule, hospitali, kumbi za makutano sadaka
Bado hapo tunauhitaji wa michango titiri??

Hapa ndio huwa hata mie sielewi! Kanisa tajiri sana hili, lina vitega uchumi vingi tu kama mashule, vyuo vikuu, kumbi, hostels lakini ni tegemezi kupindukia. Hivi mapato ya hivyo vitega uchumi huwa yanatumika vipi?!

Shule zao ukipungukiwa hata laki kwenye ada mtoto hapokelewi hadi umekamilisha!!
 
Wewe sio Padri? Waite hao wenzako ambao ni mapadri waje wajibu hoja huku!

Binafsi sikuiamini hii habari. Nikaenda kwenye group letu la WhatsApp kuna baadhi yetu ni mapadre wakathibitisha. Nimewaambia bora waweke cash point kabisa. Nashukuru simo katika vyama iwe siasa ama dini. Sikiamini kitu kiitwacho dini. Kwangu mimi naona ni biashara dini zote
 
Back
Top Bottom