Wakuu,
Napenda kwenda moja kwa moja kwenye maada. Ifuatayo ni orodha ya sadaka na michango mbali mbali iliyopo kanisani kwetu kanisani kwetu Roman Catholic.
ORODHA YA SADAKA
1. Huwa kunakuwa na sadaka ya kwanza -Jumapili
2. Sadaka ya pili - Jumapili
3. Sadaka ya tatu (hii ni sadaka ya inayotolewa kwa kanda ya parokia, kila kanda ina kikapu chake) - Jumapili
4. Sadaka ya kwanza (Jumamosi kwenye Jumuiya ambapo kila mkatoliki anatakiwa kuhudhuria mtaani kwake)
5. Sadaka ya pili (Jumamosi kwenye Jumuiya)
ORODHA YA MICHANGO
6. Mchango wa tegemeza parokia (kanisa)
7. Mchango wa tegemeza jimbo (kwa mfano, jimbo la dar es salaam)
8. Mchango kujenga kanisa (ujenzi wa makanisa huwa hauishi, kama sio lenu mtaambiwa kuna kanisa linajengwa sijui wapi na wao hawana uwezo hivyo mchangie)
9. Mchango wa kila mwezi kwenye Jumuiya ambapo huwa mnasali kila Jumamosi, unatoa ya mwaka mzima.
10. Mchango wa UWAKA (Umoja wa Wanaume Wakatoliki Tanzania)
11. Mchango wa WAWATA (Wanawake Wakatoliki Tanzania)
12. Mchango wa kununua viti vya jumuiya (kila mwaka)
13. Mchango wa kutimiza mwaka kwa Jumuiya (kila jumuiya ina tarehe yake kulingana na siku iliyoanza)
14. Mchango wa sherehe ya jimbo (kwa mwaka mara moja)
15. Zaka (hii unatoa kila mwezi, asilimia kumi ya pesa uliyoingiza mwezi mzima bahasha zinagawiwa kila nyumba)
16. Mchango wa kuhamia jumuiya - kila mtaa huonana jumamosi kwaajili ya kusali hivyo kama umetoka mtaa A umehamia mtaa B basi huko utatakiwa kulipia hiyo pesa
17. Mchango wa form kwaajili ya kipaimara
18. Mchango kwaajili ya watu wanaosomea upadrii
19. Mchango kwaajili ya wanaosafiri kwenda kutangaza neno la Mungu
20. Mchango kwaajili ya ujenzi wa shule/ hospitali ya kanisa.
21. Malimbikizo, hii unatoa kama kuna michango huko nyuma hukutoa. Labda ulikuwa huendi kanisani or so
22. Shukrani, hii ni pesa au chochote unatoa kama kumshukuru Mungu
23. Mchango wa bima ya mapadrii
24. Mchango wa tegemeza katekista (katekista ni msaidizi wa padri)
25. Mchango wa utatu mtakatifu (sherehe ziara makongamano ya taifa jimbo dekania parokia kanda)
26. Mchango wa Viwawa (vijana wa katoliki)
27. Michango ya vyama vya kitume (kwaya karsmatik yosefu maria nk)
28. Bahasha za mchango wa noeli, kwaresma nk
29. Mchango wa kumpa zawadi mama bikira maria kwa kujifungua mtoto Yesu Christmas
30. Sadaka ya mwisho wa mwaka, kutoa katika ulichopata mwaka mzima
:, Kama kuna mchango au sadaka nimeisahau naomba mnitajie au kama kuna kitu nimeongeza niambieni nipunguze. Mfano, jana (15/12/2018) tumeambiwa kila Jumuiya (mtaa) unatakiwa kupeleka watoto wa wili wakale na Padri hivyo tuchangie elfu 23,000 ya chakula
Makanisa ya Roma vifaa vyao vya kuwekea sadaka hutengeneza kwa zile mbao zenye kupiga makelele sana, afu hilo box la mbao huwa refu. Nini maana yake? Unapotoa sadaka ukitoa pesa ya sarafu kama mia tano au mia mbili ukiweka humo inapiga kelele sana kila mtu anajua umetoa sarafu. Jambo ambalo kisaikolojia huwatesa wengi na kufanya mtu alazimike kutafute kuanzia elfu moja kwenda juu hata kama ni mtu wa hali ya chini kabisa.
Kiukweli michango imekuwa miingi sana na ndiomana vijana wanaoanza maisha hawaji kanisani mpaka wakiona wanataka kuoa ndio wanakuja. Kanisani unakuta kumejaa wazee, mahouse girl na watoto kwasababu huku umri wa kati wakikimbia michango sababu ya wingi wa majukumu. Hata mimi nimechoka na hili kanisa langu, kama nina mapepo basi wenzangu mniombee yanitoke.
Note: Baadhi ya michango ipo katika maeneo fulani na maeneo mengine hamna.