Kanisa la Kristo Morroco na Magomeni

Kanisa la Kristo Morroco na Magomeni

Kwa kanisa la Kristo Magomeni, au popote pale, ni kufundishwa habari za Yesu Kristo(haijalishi muda gani), kuziamini na kubatizwa. Ukishwa batizwa, umefanyika kuwa mwanafunzi wa Kristo, hivyo unakuwa na fursa sawa na aliyekibatiza. Ila utahitaji kuendelea kujifunza siku zote ili kiwango cha kulijua neno kiwe kikubwa na cha kuridhisha.
Kama ulibatizwa kwa maji mengi, ukifika hapo unabatizwa pia?
 
Kwa kanisa la Kristo Magomeni, au popote pale, ni kufundishwa habari za Yesu Kristo(haijalishi muda gani), kuziamini na kubatizwa. Ukishwa batizwa, umefanyika kuwa mwanafunzi wa Kristo, hivyo unakuwa na fursa sawa na aliyekibatiza. Ila utahitaji kuendelea kujifunza siku zote ili kiwango cha kulijua neno kiwe kikubwa na cha kuridhisha.
Kama ulibatizwa kwa maji mengi, ukifika hapo unabatizwa pia ama?
 
Moja lipo Tanga mjini maeneo ya Donge kama unatokea Kwanjeka karibu na kanisa la Wasabato. Nimecheza pale volleyball na washkaji wa mtaani kwa miaka minne, ila sikuwahi kushuhudia ibada siku ya Jumapili au siku yoyote! Nikirud Tanga ntamuulizaga mshikaji wangu maana ndo anakaa pale
Si umpigie tu simu jamaa
 
Nashukuru kwa ufafanuzi mkuu. Ngoja tusubiri wa Morocco waje
Karibu sana tujifunze kwa pamoja. Kwa ufahamu tu, Yesu aliacha kanisa moja tu. Ndilo kanisa lake. Baada ya hapo, watu wakaanza kutunga vya kwao, ndiyo madhehebu yaliyopo leo. Na hilo lilionywa kupitia 1kor 1:9-13. Madhehebu ni upotofu, kanisa ni moja tu
 
Hao Wafuasi wa Mormon(Joseph Smith), Watakatifu wa siku za mwisho wanawapeleka vijana Marekani. Nafahamu mdogo wa rafiki yangu pamoja na rafiki yake walipelekwa Marekani miaka ile ya tisini.
Tena huyo rafiki yake alikuwa ni Muislamu, akatafuta cha uvunguni akainama huyooo na KLM .
 
Yawezakuwa ni Yale ya kuabudu Mara moja kwa mwaka kama lililoko kwenye shule ya st.Constantine arusha
 
Nimeona mdau mmoja akiuliza kuhusu Kanisa la Silom na Mimi nikapata wazo la kuuliza kuhusu makanisa mawili niliyotaja hapo juu. Hivi haya makanisa yana wahumini kweli maana sijawahi kuona watu wakiingia kuabudu wala kuona magari yamepaki nje pamoja na kuonekana kuwa ni makubwa sana.

Samahani kama nitakuwa nimemkwaza mtu
Ratiba ya ibada na vipindi vya kanisa, kwa wale walioko dsm, kanisa la Kristo Magomeni ratiba kwa wiki ni hii.

Magomeni CoC- Church of Christ

Ratiba ya Ibada zetu :
Jpili asbh saa tatu - sita mchana,

jioni saa kumi na moja mpaka saa kumi na mbili,

jtano saa kumi na moja mpaka saa kumi na mbili jioni. Mafundisho ya biblia(Bible school)

Karibuni tujifunze neno la Mungu kwa utukufu wake, hautojuta kujifunza neno, bali utajilaumu kwa kuchelewa.
 
lile la pale kinondoni morroco licha ya kwamba wakati fulani nilikuwa nafanya kazi maeneo yale,hata siku moja sikuwahi ona waumini mida ya mchana,iwe jumapili iwe jumamosi.

sijui huwa wanasali saa ngapi.
Wewe mnafiki acha uongo watu wanasali kama kawaida nenda pale utaona ratiba msiwe mnapotosha watu kama hamna kazi za kufanya mrudi vijijini kwenu kuliko kuwa unaandika uongo
 
Kama ulibatizwa kwa maji mengi, ukifika hapo unabatizwa pia?
Yeah, lazima ubatizwe. Kwa sababu kubwa moja. Ubatizo wa huko ulikotoka, haukuwa wa kukufanya kuwa mkristo, bali ilikuwa kukufanya kuwa mtu wa dhehebu husika.

Ukisha kuwa mtu wa dhehebu, utafanya mengi kwa kutumia jina la Yesu lkn yeye hakutambui.

Chukulia mfano huu wa Math 24:11 "....manabii wa uongo watatokea...". Hawa wanatumia maneno ya Kristo lkn kwa maslahi yao.

Hivyo ukianza kulitumia neno la Kristo kwa maslahi ya Kristo, kila kitu utaanza upya ili uliishi neno lake.

672258e253ffd79c9b99217cc5817cf7.jpg
 
hivi haya makanisa tata kati ya lile la kinondoni marroco na lile la barabara ya mandera-ubungo external hatua chache nyuma ya EPZA,yote yapo chini ya taasisi moja?.

na kwanini yanakuwa na ukimya wa kutisha namna ile?.
 
Back
Top Bottom