Kanisa la Kristo Morroco na Magomeni

Kanisa la Kristo Morroco na Magomeni

Naskia huwa wanasali usiku wa manane,af nlskia pia kuwa wanaabudu bila kuvaa nguo, Mara y kwanza nlkuw siamin ,bt kwa maswal haya ya wadau naanza kuamin taratib ,itakuw n kwel
Lipi? La magomeni au la morocco? Magomeni ibada zao ni za wazi sana. Jumapili nenda saa tatu asubuhi, utajifunza mengi
 
Mnapewa utajiri jipange ujr kwa Yesu kuna kila kitu utakipata karibu tujumuike
 
Kwa lile la Morocco sijalifahamu vizuri, ila hili la Kristo kwa ninavyolielewa halina shida yeyote na ni moja kati ya makanisa kongwe sana hapa nchini...lipo karibia mikoa yote ni maarufu kama " KANISA LA KRISTO". Tofauti ni kwamba hawa sio watu wa tikadi kali kama makanisa mengine ya kilokole. Wamebase sana katika kufundisha biblia na ibada zao huwa ni fupi, pia halina waumini wengi. (Utaratibu wao hautofautiani sana na wale Mashahidi wa Yehova).
Ni tofauti na mashahidi. Mashahidi wanaamini kurithi ulimwengu huu, kanisa la kristo huamini ufufuo na uzima wa milele.

Ila ni kweli tunajikita katika mafundisho ya biblia tu, na kufanya kama inavyoelekeza.

Karibu tujifunze neno la Mungu kwa usahihi
 
Moja liko Chang'ombe, majani mpaka mlangoni, hata usafi kwa nje imekuwa shiida.
Pale Morroco nimewahi pita asubuhi na jioni ndani ya mwezi mmoja hivi sijaona wakiabudu. Nasikia ni kanisa ambalo ukienda masikini baada ya kutoa sadaka, wewe ndo unapewa sadaka.
Hata me nilisikia hivyo kuwa ukienda kusali kama wewe maskini basi unapewa pesa ila wanaojua ukweli waje watuambie ukweli
 
Moja lipo Tanga mjini maeneo ya Donge kama unatokea Kwanjeka karibu na kanisa la Wasabato. Nimecheza pale volleyball na washkaji wa mtaani kwa miaka minne, ila sikuwahi kushuhudia ibada siku ya Jumapili au siku yoyote! Nikirud Tanga ntamuulizaga mshikaji wangu maana ndo anakaa pale
Miaka minne hiyo hukuwahi kuuliza! mi hata isingechukua mwezi na nusu, zikipita tu wiki 3 kavu za siku za ibada, nahoji.
 
Mkuu Mshana sidhani kama ni kweli; nilipokua nafanya mtihani wa form 6 mwaka 1996 nili opt pia kufanya somo la Divinity na mafundisho ya mtihani huo niliyapatia hapo Mwembe Chai, kulikuaga na mchungaji wao mzungu hivi na anaongea Kiswahili kizuri tu; nilikuja gundua wana tofauti kadhaa za Kikristo na wengine but kwakua sio sehemu yake hapa sitazisema hizo tofauti zao.
Hata mie nimelifahamu kupitia somo la divinity, na leo ni muumini. Ziseme tu, ndo watu watafunguka. Ibada za kanisa la Kristo siyo siri, ni wazi na kama biblia ilivyoagiza.

Ni kweli liko tofauti sana, maana halina kiongozi mkuu. Baraza la wazee lipo, na hakuna anayelipwa mshahara kwa kuwa kiongozi wa kanisa. Ni wito kama Paulo, hakuna kumwelemea mtu labda kama wewe ni missionary, utalipwa posho
 
Mimi sikua naenda kusali pale, tulikua tunafundishwa tu mambo ya divinity baaasi; kwa ujumla mwalimu yule (nadhani alikua Mmarekani) alikua vizuri kwenye kuifundisha divinity but again niligundua wana vitu Fulani hivi vya tofauti wanavyo viamini.
Viseme
 
ukiingia kanisa hilo ni sawa na kuingia masonic temple ,hata ibada zao zina uelekeano-kwa mujibu wa literature review.linaitwa kanisa la kristo la watakatifu wa siku za mwisho kwa kiingereza church of Christ of letter days saints ,
Duuuh. Ebu ongeza kachumbari na pilipili kidogo mkuu
 
Ili kuwa muumini wao inabidi ufanye nini?
Nadhani wana ibada siku za kazi hizi na jumapili karibia pale utapata maelezo. Kanisani full mufindi watu wananukia tuu. Ukijibidiisha safari za amerika kiulaini sana pale.
 
Mimi nalifahamu kanisa la Kristo Magomeni karibu na sheli yenye sanamu la Michelin.

Nililifahamu kupitia kwa rafiki zangu wakati tunasoma high school, baada ya kuonesha nia ya kufanya mtihani wa divinity. Walimu wengi waliokuwa wanafundisha shuleni, walikuja kufundisha madhehebu yao, hivyo tukaona hatari ya kushindwa mtihani, hivyo tukalazimika kutafta mwalimu aliyekuwa anafundisha syllabus ya divinity, tukampata Mwl. James Mhenga wa kanisa la Kristo magomeni. Huyu alitusaidia sana wanafunzi wa divinity japo hakuwahi kutualika kuingia kanisani kwao, nadhani mambo ya professional ethics, alitaka uelewa wetu ndo uamue kujiunga nao au tuendelee kusoma tukimakiza tusepe. Hatukuwa tunalipa chochote, ila tulipomaliza walitupa zawadi ya biblia english version.

Kwa sasa na mimi ni mkristo, muumini wa kanisa la Kristo.

Kujibu maswali yako ni kuwa:-

1. Kanisa la Kristo magomeni, ni tofauti na lile la Morocco. Morocco sijawahi fika kuabudu hivyo siwajui kabisa. Ila wao hawaitwi kanisa la Kristo, bali wanaitwa kanisa la Yesu Kristo(Jesus Christ Church) nadhani wakati la Magoneni linaitwa Kanisa la Kristo(Church of Christ)

2. Kuhusu waumini, Kanisa la Kristo magomeni wapo waumini na kwa kipindi kile zilikuwa misa mbili. Ya kizungu asubuhi saa 06:00hrs hadi 09:00hrs, hafu inaanza ya kiswahili 09:00-12:00hrs. Hivyo kuna waumini, lkn ni wanaojielewa kwa nini ni waumini ndio maana ni wachache sana.

Maana ukiwa muumini wa kanisa, maana yake lazima umebatizwa. Ukisha batizwa, nawe unakuwa kuhani. Utarndesha ibada, utahubiri, utabatiza, utaomba n.k.

Ukiwa kanisa la Kristo, ngumu kumpata mtu anayeitwa Askofu au mchungaji, maana sifa za daraja hilo, ni Mungu mwenyewe anayejua nani ni askofu.

Pia hakuna kiongozi wa kanisa anayelipwa, labda kama umepewa kazi mfano ya kufundisha wanafunzi, michango ya kanisani(sadaka) utapewa posho kwa kazi hiyo, siyo kama madhehebu yafanyavyo ambapo wamejitengenezea ajira
Sikuwahi kufikiria kama haya ni makanisa mawili tofauti
 
Nipo hapa Mkristo wa kanisa la Kristo, moja ya tawi lake ni Magomeni. La Morocco siyo Kanisa la Kristo, linaitwa Jesus Christ Church(Kanisa la Yesu Kristo) hawa siwajui, lakini la Magomeni ni Kanisa la Kristo (Church of Christ) nawajua na ni muumini pia.

Hivyo waumini tupo, na tunajielewa kwelekweli, hakuna mafundisho ya upotofu kama kwenye madhehebu, kanisani tunajifunza na kufanya neno yaani Kristo alivyo agiza.

Ukitaka kuja kushiriki nasi unakaribishwa, jumapili ni kuanzia saa tatu hadi saa sita.

Pia kwa magoneni dsm, kuna mafundisho ya biblia kila siku ya jumatano. Namtafta muumini wa pale ntawapa ratiba ya wiki nzima.

Kwa sasa mimi niko Magu mwanza, ila nakusanyika kanisa la Kristo Kishiri Igoma, au kanisa la Kristo michungwani kilimahewa mwanza. Ni mshazali na kwa malisa
Nashukuru kwa ufafanuzi mkuu. Ngoja tusubiri wa Morocco waje
 
Kanisa lipi? La magomeni au la morocco? Maana ni vitu viwili tofauti.

Lugha inayotumika kanisa la kristo popote, ni lugha rahisi na ya kueleweka. Hivyo, hata magomeni ni kiswahili cha kawaida tu
Morocco mkuu
 
Back
Top Bottom