Hili kanisa linalotajwa kama kanisa katoliki takatifu la mitume linahitaji reforms ili kwenda sawa na amri ya upendo iliyoamriwa na Yesu Kristo. Viongozi wa kanisa wapunguze chuki dhidi ya kiongozi wa nchi ambaye wanaona haendi vile wanavyotaka wao.
Tunajua huu mwongozo wao wa kutaka viongozi wasipewe nafasi za kuongea ibadani umemlenga Mama yetu kipenzi ila sisi tumeamua kuwajibu RC kwa kuwataka waache unafiki. Kwenye awamu ya 5 tuliona mkatoliki mwenzao akiongea karibu kila jumapili kanisani ila kwa sasa sijui kuna kitu gani wamegundua zaidi ya chuki za kijinga.
Tunajua misiba ya matajiri wa kikatoliki huhudhuriwa na maaskofu ila akifa maskini hata katekista anaweza asiendeshe ibada na kuwekwa mizengwe kuwa marehemu alikuwa hahudhurii jumuiya na kutoa zaka. RC acheni ubaguzi. Onyesheni upendo kwa watu wote.Katoliki nüans za