Kanipa sharti la kugawana mshahara ili anioe

Kanipa sharti la kugawana mshahara ili anioe

nipo apa dilemma nipo kazini mwenzangu ajira bado, kanambia ili tufunge ndoa inabidi mshahara wangu tugawane pasu kwa pasu., ndo anioe... nipo tu nimebaki njia panda.
Mkubalie tu, wewe na yeye si mtakuwa mwili mmoja! Narrative ya kikiristo ambayo mi binafsi naona ni uongo.

Pili, mwanamke au mwanaume anayeingia kwenye ndoa akiwa amengalia maslahi si mwenza sahihi wa kuwa nae.

Nasisitiza, mkubalie maana huyo ndo chaguo lako mwenyewe
 
Feminists walisema 50/50 na nyie mkakubali kwasababu ya maslahi.

Ndio muonage jinsi ilivyo ngumu kwenye mali za mwanaume mgawane pasu kwa pasu kisa ndoa kuvunjika
N A K A Z I A [emoji419]

Feminist watamwambia aachane nae. Ila ndio hawa hawa mume akiwa na kazi wanampiga limbwata mpaka wanakaa na ATM ya mshahara wa mume.
 
Mpaka unaomba ushauri inaonekana karibia unakubaliana nae.

Nini hicho anakupa kitamu hivi hadi umelibeba hili wazo?... Kimbia utajuta!

Huyo hata umpe mshahara wako wote baadae atakusumbua tu
🤣🤣Huyo ni mikopo nyonya damu,kama Hana mbio aje nimwazime vile viatu vya kuslide,vimejaa huku Arusha🙏🤣
 
Run for what?

Kwenye mahusiano yaliyokolea upendo tumesikia makubwa hadi watu kuahidiana kumpa mwenza wake dunia.

Sasa kama ana upendo wa dhati basi kwenye case ya mdau mshahara ni kitu kidogo sana ukilinganisha na couples zilizokuwa tayari kutuuza ili kuwaridhisha wenzi wao.
Uyo mwanaume ni mdangaji bwana kama wadangaji wengine tu
 
Back
Top Bottom