Wakuu mlio Mwanza, Kagera na Mara, nitakuwa maeneo haya karibuni. Ningependa kuonana na walio tayari ili tubadilishane mawazo na kusikia kutoka kwenu. Baada ya safari hii nitaelekea Mbeya na Ruvuma.
Hii ni kuweza kuonana na wadau wa JF na kubadilishana nao mawazo, kuwasaidia wenye kuhitaji msaada (kiufundi) na zaidi kuweza kufahamiana na kushauriana namna ya kuipeleka JF kwenye hatua nyingine.
Maxence karibu saana... naamini nitakuepo moja ya maeneo ulotaja
and God Willing mambo/shughuli kama zitaruhusu inshallah tutaonana....
Nakuombea wepesi katika safari zako zoote...
Mkuu,
Kwa Dar hatujawahi kupanga kukutana. Tumekuwa tukikutana na wadau katika mazingira ya kawaida na kwenye events za kijamii, itabidi tuandae mkutano mmoja wa pamoja ambapo nasisitiza, ID za JF hazina umuhimu kusemwa labda mtu afanye hivyo kwa hiari yake.
All we need ni maoni ya wadau na kuyaweka kwny utekelezaji.
Nilipokutana na wadau huko Arusha tuliyoongelea asilimia kubwa (over 80%) yameshafanyiwa kazi na huenda ndiyo yametufikisha hapa
Kaka Maxence Melo huna ziara ya Lake Zone tena??? Miss you badly!!! :sad: