Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Jamaa kaja juu kwa sababu mke wake kamwambia ati anamuonea na kumfuatafuata kama "ana wivu wa kike". jamaa akamzaba kibao mkewe maskini.. baada ya kutulizana nikataka kujua kwanini jamaa kakasirika sana kuambiwa ana "wivu wa kike" kwani kuna tofauti gani kati ya 'wivu wa kike' na 'wivu wa kiume'? Kuna mtu anaweza kutusaidia kutufafanulia wivu wa kike uko je hasa kiasi kwamba uonekane ni kama tusi la aina fulani hivi?