Ukimpenda Utamjali na Kumlinda

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
21,247
36,300
Habari za muda huu,

Rejea kichwa cha uzi, kinaongea kwa mapana ila yaliyopo kwenye akili yangu yako kwenye nyanja tofauti tofauti.

1. Mwanaume kumjali jinsia ya kike yeyote yule aliyempenda.

Baba mzazi/mlezi kwa binti yake:
Kuna wababa asisikie au kujua binti yake ametendwa isivyo, yuko radhi ache kila kitu ila usalama wa binti yake kwanza.

Mume kwa mkewe:
Mwanaume akisikia au kujua kuna wanaotaka mdhuru mke wake huwa mbogo na hacheki na kima mbele ya mkewe wala kuleta matani. Achana na wivu kuna ile kumlinda bila kuwa na mtutu wa bunduki...

Kaka kwa dada wa damu (sibling):
Kaka wote wanaojielewa hawakotayari kuona dada yake/zake wanapata tabu. Awe mkubwa ama mdogo, atapambana kuhakikisha dada yake/zake wanakuwa salama.

Mtoto wa kiume kwa mama mzazi:
Hapa wanaume wenyewe mtaongea zaidi, ila iko asili sio tuu mapenzi makubwa yako kwa mama mzazi ila hata kuhakikisha mama hapati shuruba, hateseki yaani ile kumkingia kifua kwa namna yeyote ile...

Kiasili mwanaume ana mabavu kumzidi mwanamke, misuli na nguvu za ziada zipo kwa sababu maalum. Ukiacha kupigana na ubabe, kazi kubwa ni kutoa ulinzi.

Hakuna kitu mwanamke anapata tulizo la akili kama akijua ndani yuko ya mtu anaweza mkingia kifua kwenye jambo lolote lile hata kama sio la hatari...

Kale kahisia kuwa kuna sauti nene inakoromea shambulio lolote lile linaloelekezwa kwenye paa lenu bila ugomvi ila kwa hekima na umakini na msisitizo usio wa mchezomchezo.

Si wanawake wote ni wadau wa mambo za kuwa (protected), ila kuna raha yake... ni asili.

Ukiona hajali, hajisumbui nawe, hajihusishi na mambo yako, haimhusu uko salama ama hauko salama...

Tambua tuu kuwa haupo kwenye himaya yake ya anaowapenda.

Ngumu kukubaliana na uhalisia ila bora kuchukua njia mapema utabaki salama hadi pale atapotokea wa kukujali.

Hiyo ni upande mmoja, kurudisha majibu ya kuwa ulinzi wako umekubalika na unatambulika ni kukuheshimu.

Jinsia ya KE akikubali vile umempenda, umemjali na kumlinda, atakuheshimu na ATAKUTII.

Huu mjadala ni mpana sana ila akili yangu ililenga hapo kwa ME kumpenda, kumjali na kumlinda KE.

Wasalaam,

Kasinde Matata.
 
Hongera sana.

Unaishi sehemu ya asili ya maisha ya binadamu. Si jinsia ya kike wote wanakutqna na hii hali....

Kuna wataopita hapa na hawataelewa hisia iliyopo nyuma ya ulinzi kutoka jinsia ME.
Aliniambia “Nakulinda hata kabla hujajua unalindwa na mimi babe”
Nahitaji nini zaidi ktk haya maisha?

Mungu amenitendea mengi, hili ni zaidi.
 
Habari za muda huu,

Rejea kichwa cha uzi, kinaongea kwa mapana ila yaliyopo kwenye akili yangu yako kwenye nyanja tofauti tofauti.



Wasalaam,

Kasinde Matata.
Nimeishia hapo uliposema jinsia ke akikubali vile umempenda, umemjali na kumlinda atakutii,

Hapo inategemea, mwanamke anachojali ni hisia zake kwako, ke hajali kabisa kama umemnunulia gari, umempa Figo kuokoa maisha yake, umemaliza miezi 59 kumtongoza, umemsomesha chuo, ke hajali unampenda kiasi gani, ke hata umpende vipi na kusacrifice vipi kwa ajili yake, kama tangu mwanzo alikuwa anakuona nyani ataendelea kukuona nyani tu, kwanza ke wengi wa sahivi ukiwaambia unawapenda, hata kama ni ukweli, kichwani watakuona wewe ni muongo na mnafiki unaetaka kula papuchi halafu utembee, kumbe kiuhalisia unampenda kweli Kasie
 
Back
Top Bottom