Kamwe usilazimishe mahusiano/ndoa

Kamwe usilazimishe mahusiano/ndoa

kwamba unamuacha polepole bila taarifa....kweli naona hupendagi ujinga
Ohoo shangaa unyonyolewe mjini hapa!

Yaani ukishaona mtu haeleweki, uchumba miaka mitano, saba, nawe mlize tu! Unajifanya uko nae kumbe uko busy na mambo yako na hakuna kumwambia sijui tuachane, na PAPUCHI humpi....

Atajiongeza tuu
 
Ilo nalo neno nina boyfriend ni mwaka Wa saba huu, hata nyumbani kwao hataki kunipeleka, najuana na marafiki zake tu..najipa moyo eti namsubiri akiwa tayari ila naona muda kwake haufiki..nazeeka buree...mambo haya magumu sana
Mmh... my dear chungulia na pembeni.
Nilikua na bf kwa miaka mitano.
Tangu nina 26 hadi 31yrs halafu hana mpango haeleweki na ananitumia bure! Nilikua nasimamia ujenzi wa nyumba zake, kufatilia madeni ya kampuni zake, kufukuzia nae tenda zake.
Bado nihangaike na mwanae issue za shule au hosp. Hakuwahi kuninyanyasa hata kidogo ila ana wanawake foleni.
Nikajichomoa tu mzimamzima bila ugomvi wala shari.
Wala hakushtuka
Nikaenda pengine...
Hadi leo hajaoa ananipongeza tu.
Na kanizidi 5yrs.
 
Yaani hiyo ndo akili shost!

Mi yalishanikuta Mara mbili hayo mauchumba sugua gaga!

Mwanzo nilikuwa nalia wee! Baadae nikaona najichosha nikawa ngangari,

Mwanaume ni wa kupambana nae ukilegea tu, utajuta maisha!
pole sana Wit naweza kuwa msaada kwako
 
Mmh... my dear chungulia na pembeni.
Nilikua na bf kwa miaka mitano.
Tangu nina 26 hadi 31yrs halafu hana mpango haeleweki na ananitumia bure! Nilikua nasimamia ujenzi wa nyumba zake, kufatilia madeni ya kampuni zake, kufukuzia nae tenda zake.
Bado nihangaike na mwanae issue za shule au hosp. Hakuwahi kuninyanyasa hata kidogo ila ana wanawake foleni.
Nikajichomoa tu mzimamzima bila ugomvi wala shari.
Wala hakushtuka
Nikaenda pengine...
Hadi leo hajaoa ananipongeza tu.
Na kanizidi 5yrs.
Haaa haaa haaa...nimecheka kama mazuri

Kuna wanaume wanawatumia wanawake kama mandondocha yao!

Bora ulishtuka mwingine angekomaa si anajua ana hela!?
 
Mapenzi hayaana formula vile sio lazima watu waish kama wengine wanaavotaka kila mahusiano ni vile walivojipangia na maisha yao ya kimahusiano. Kuna watu wamekaa miaka na miaka na wamekuja kuoana ...so msijaribu kuwakatisha tamaa wale waliokaa mda mrefu pamoja ndivo walivojiwekea na zaidi hatuez ishi maisha wote sawa. Kila wapenz wana utaratibu wao aka katiba yao. Tusiishi kwa mazoea.
Kaka vipi kwani yule wifi yetu hujamuoa au ndo umegoma kumsamehe...!!?
 
917ac30939667155c502f39d145c1f2a.jpg
tunapozungumzia hizi habari wengi wetu tutakimbilia kuwanyooshea vidole wanawake lakini kuna wanaume pia wana hizo tabia
Ndoa na mahusiano ni taasisi moja kubwa sana! Walioko kwenye mahusiano kwa sasa no matter mnapendanaje wengi wenu hamtaoana! Wakwenu wapo na wengine saa hii nao wakiota ndoto kama za kwenu
Ndoa bila kujali imani zetu ni kiunganishi cha kiroho kisihia na fikra za ndani kabisa, ndoa ni mwanzo wa msingi unaokuja kujengewa kuta imara
Kiroho ndoa yako ipo! Mtu wako yupo! Mahusiano yako yapo! Ambayo yatakuja kuwakutanisha bila kutumia nguvu na kulazimisha vitu au hata kutumia nguvu za giza
Mabinti msibebe mimba kama sababu ya ndoa, wazazi na walezi msipange fumanizi ili kuhalalisha ndoa za mkeka, wandugu msitumie ushawishi wenu nguvu ya fedha na ahadi za kazi nk ili ndoa ifungwe
Kufungwa kwa ndoa ni jambo la kwanza na wanandoa kudumu kwenye ndoa na kuishi maisha ya mafanikio ni kitu kingine kabisa
Wala hakuna haja ya kupoteza muda na fedha kwenda kwa wanajimu wa nyota na watabiri ati kuona kama mtaweza kuishi pamoja
Utabiri na unajibu hutoa majibu ya jumla tu kutokana na hesabu za nyota na majira ya nyakati, ni vitu vinavyobadilika kila wakati
Jipange na maisha huku ukijibidiisha na kazi, ukiwa na hakika kwamba wako sahihi uliyepangiwa atakuja katika muda sahihi uliopangwa na nguvu iliyo juu yetu sote
Ndoa nyingi zimevurugika na kuharibika kabisa kwa sababu ya kulazimisha mambo...!!!ndoa imeonekana ni taasisi ngumu kwa ajili ya kulazimisha mahusiano...! Kila jambo lina mahali pake Mtu wake na wakati wake!
Soon tutapata couples zilizokutana/kutanishwa na JF! Utashangaa na kujiuliza imekuwaje? Makutano ya mtandaoni! Ni kwa vile ndivyo ilivyopangwa iwe! Tuwaombee, nawe waombee pia! Wako pia hayuko mbali ni muda tu haujafika kama hayuko JF au pale kazini kwako, yuko mahali pengine kona ya mabibo! Vumilia yuaja...! Nakuombea
Hapa Mungu anahusika sana ili akujalie upate mke/mume mwema,kinyume cha hapo ni mauzauza tu.
 
Back
Top Bottom