Kampuni zinazohusika na kutengeneza pesa

Kampuni zinazohusika na kutengeneza pesa

Mkuu umeeleza vyema sana lakini vipi kuhusu uaminifu wa makampuni hayo?
Hayawezi kufanya janja janja ya kutengeneza pesa za ziada na kuziingiza kwenye mzunguko kiaina?!

Najua kuna namba za fedha na ugumu kidogo wa hili ila wanaaminiwa vipi? na kwa nini kusiwe na jinsi ya kutengeneza fedha zetu hapa?
Pesa haziingi kwenye mzunguko bila kuwa registered na kuwa halali.... baada ya kutengenezwa lazima BOT wafanye mambo then ziwe halali kutumika....
Kwamfano, wanaziingiza kwenye mfumo wa computer, and thus y, ukienda benk huwez kuweka pesa fake lazima wakukamate..... kuzitatambua kwa BOT, kuna zipa thaman pesa.... ukiliteka gar la pesa likitoka airport, huwez zitumia pesa hizo kwan sio halali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hi wana JF,

Nimekuwa nikisikia kuwa pesa ya nchi yoyote ile utengenezwa katika nchi ya Uswisi, lakini katika kujua huko nimekuwa nabaki na maswali mbalimbali juu ya hilo. Maswali hayo ni pamoja na;

(i) Je katika nchi hiyo ni kampuni binafsi au za serikali ndiyo zinahusika kutengeneza?
(ii) Je kampuni hizo zinafanya kazi hiyo kama msaada au ni ki biashara?
(iii) Kama ni ki biashara?, wao wanalipwa nini? pesa hiyo hiyo wanayotengeneza au kitu kingine? kwa maana kama ni pesa hiyo sioni kama wana fanya biashara, nitoe mfano mdogo, chukulia umpe mtu order ya kukutengenenezea mikate, na baada ya kukutengenezea umlipe kiasi fulani cha mikate hiyo, hapo si ni sawa sawa mikate hiyo kakupa bure? n.k

Kwa kutambua JF ni jukwaa lililojaa wataalamu katka nyanja mbalimbali natumaini nitapata majibu kulingana na duku duku hizo.

Nawasilisha.
Gusa hapa Vatican Inamiliki Dunia - JamiiForums
 
Mkuu umeeleza vyema sana lakini vipi kuhusu uaminifu wa makampuni hayo?
Hayawezi kufanya janja janja ya kutengeneza pesa za ziada na kuziingiza kwenye mzunguko kiaina?!

Najua kuna namba za fedha na ugumu kidogo wa hili ila wanaaminiwa vipi? na kwa nini kusiwe na jinsi ya kutengeneza fedha zetu hapa?
Lazima kuwe na taasisi zinazo wacontrol sivyo michezo ingekuwa mingi na habari za mapichapicha
 
Kujibu swali lako Dr. Duniani kuna taasisi mbili zinazohusika na maswala ya kifedha na uchumi taasisi hzo ni International Monetary Fund (IMF) na World Bank (WB) taasisi hzi zinaongozwa na money policy act (MPA) ndani ya MPA kuna mfumo unaoitwa Global financial system (GFS) mfumo huu unamilikiwa na Rothschild family kumekuwa na fikra ya kuwa Rothschild family ndio wamiliki wa Bank kubwa kubwa ikiwamo WB , IMF na Federal Reserve System japo wengi wanajua ni Federal Reserve bank lakini ukweli ni Federal Reserve System huku bank ikiwa ni Bank of America (FRS ) ni mfumo tu unaoendesha bank hzo ambapo unaendeshwa na sheria ya federal reserve system act ya mwaka 1913
Rothschild si wamiliki wa banks hzo bali wanamiliki mfumo wa GFS unaotumika kwenye banks nying duniani kuelewa vizuri ni kama leo MAX malipo wanamfumo wao wa maxcom mfumo unaotumika kufanya malipo kwa huduma mbalimbali so ndio mfumo wa GFS unavyofanya kazi


Money policy act (MPA) ndio mwongozo wa centro banks zote duniani na kazi ya centro bank duniani ni

1 print money
2 control supply of money
3 Set the Reserve Requirement
4 Influence Interest Rates
5 Engage in Open Market Operations
6 Control inflation

Hii ndio kazi ya CB zote duniani kuhusu kushuka kwa thamani ya fedha au uchumi

Kwanza unatakiwa kujua hakuna mahusiano ya thamani ya fedha na uchumi japo wengi wanajua kuna mahusiano ya vtu hv lakini ukweli ni kwamba hakuna wakati formula ya uchumi wa ndani ni

MV=PY
M=Money suppy
V=Velocity of circulation
P=price level
Y=National income


Wakati formula ya kushusha au kupandisha thamani ya fedha ni vitu hv
1 INFLATION
2 INTREST RATES
3 Current-Account Deficits
4 Public Debt
5 . Terms of Trade
6 . Political Stability and Economic Performance

Kutokana na kutokuwa na mahusiano hayo ndio unaona dola ya US kuna fedha duniani zimeizidi thamani kama Euro,paund,dinar ya oman pia ukiangalia uchumi wa US na uchumi ya Omani ni vichekesho leo kama kungekuwa na mahusiano ya uchumi na thamani ya fedha basi leo fedha ya Japani ,China zingekuwa ni moja ya sarafu zenye nguvu kubwa duniani na USD ndio ingekuwa fedha yenye thamani kuliko zote

Kuna kitu kinaitwa Balance of trade na ambayo mfumo wake ndio unakwenda kwenye mfumo wa uchumi mkuu moja kwa moja yani GDP

GDP = C + I + G (Ex - Im)

C = Consumer spendng
I= Investment spendng
G= Govement spendng
Ex= Export
Im=Import

Sasa kuhusu uchumi wetu Tanganyika na thamani yetu ya fedha kushuka au kuteteleka aidha kuna vitu viwili

1 Wataalamu wetu wameshindwa kutumia maarifa (Ufahamu) wao vizuri (kwani kwa binadamu tuna vitu vitatu

(A) Utashi (B) Akili ( C) Ufahamu

Sasa Akili ni matumizi mazuri ya ufahamu ambao mara nying unapatikana kwa uzoefu au kwa kwenda shule

2 Labda wataalamu wetu hawajui kupigana vita hii ya kiuchumi na kifedha

Duniani kuna vita tatu
1 Vita vya silaha na majeshi

2 Cyber war(Vita vya mifumo ya technologia ya habari na mawasiliano)

3Economic war (Vita vya kiuchumi)

Vita vya kiuchumi ndio vita inayopiganwa sasa duniani kuliko vita vingine vyote unavijua zipo mpaka mbinu za kimafia za kupigana vta hii ya kiuchumi
ambazo zipo njia 6 za kupadisha uchumi na fedha

Matola jibu lako ni wanapokuchejia dola iliyoexpire kwanza unachenjiwa chini ya exchange rate ya siku hyo kama ni dola mia ni sh 200,000 ww kwa fedha yako ya zamani utachengiwa chini ya laki mbili then wanazipeleka Zanzibar fedha za zamani huko wanapewa wageni au wazungu wanaorudi makwao wanarudi nazo US
mwenye swali anaweza uliza kwani JF ndio sehemu pekee ambapo hakuna bodi ya mikopo hapa unapata elimu bure

Mkuu MALCOM LUMUMBA unaweza kujazia nilichosahau kuweka hapa

brazuca Paprika k_dizle Juma chief MNANSO mtimkav Dux_1234 LIKE Niku ADD Kalamu Yangu

Molaro
Nimekubali jamaa uko vizuri👏👏👏👏
 
Je wanatumia kipimo gani kujua kuwa tulete kiasi flani ndicho kitatosha mahitaji yetu?
 
kila nchi ina kitu kinaitwa money policy act MPA huu ndo mwongozo wa central bank zote duniani ikiongozwa na WB mfumo huu ndo unawaongoza katika ku supply and monitoring currently so kuhusu ni kiasi gani wanachapisha inategemea na maitaji ya nchi husika kuna msemo wa kibiashara unasema ukitaka kukipandisha kitu thamani kifanye kuwa adimu pia ukitaka kukishusha kitu thamani basi kifanye kipatikane kwa wepesi so chaguo ni lako kuchapisha tuuuuu au kuchapisha pale inapoitajika

kwa wenzetu yani federal reserve bank and bank of England pia na bank of Canada hawa ndo wanacontrol karibu institutions zote za fedha ikiwamo WB na IMF so ni kama money policy act wanazizibiti wao

lakini thamani ya fedha hawapangi wao kama ingekuwa hvyo basi dollar ndo ingekuwa na thamani kuliko zote bt kuna fedha za nchi zingine zimeizd thaman usd mfano Swiss fanc pound na dinar ya Oman

pia wenzetu wana mfumo mzuri mfano marekani kiwanda cha kutengeneza fedha cha fort Worth cha TX na cha Washington cha tour and visitor centre kwa pamoja vinauwezo wa kutengeneza kiasi cha dollar million 28 par hour na pia wameweka expire date ya ela yao ili kuweza kujua ni kiasi gani cha fedha kipo katika mzunguko duniani na pia kudhibiti mijitu inayoficha ela kwenye masandarusi na ndoo coz ikifika mda fedha inaexpire so ikiexpire mkononi mwako itakuwa ni taratasi tu coz huwezi kufanya manunuz yeyote popote pale kwani itakuwa imeondolewa kwenye mzunguko nadhani ni miaka 10 wao hawasuhili mpaka ela ichanike au kuchakaa kama tunavyofanya ss
Hawa mabeberu kumbe hawakwepeki, bado ndio wanatutengenezea hizi pesa zetu za madafu halafu kila siku tunawananga??
 
duuuh kumbe inamaana pesa mfano za kwetu sisi tunaweza tukacontroll thamani yake ipande au ishuke kwa kuiadimisha mitaani na nchi zingne? au cjamwelewa vizur #izzo!
Ninavyoelewa sio hivyo! Huwezi kuipandisha dhamani fedha kwa kuificha, kinachopandisha dhamani fedha ni jinsi inavyohitajika(demand for money), ili fedha yetu iwe na dhamani, kinachotakiwa ni kuwa na bidhaa nyingi sana zinazouzwa kwa Shilingi, mfano, watalii wakija wengi sana, na tukalazimisha watumie shilingi, au tukiuza sana madini yetu kwa shilingi, mazao yetu kwa shilingi, kwa hivyo vichache tu, utakuta kila mtu anatafuta shilingi, so dhamani yake inaenda juu, fedha ni bidhaa, ikihitajika sana dhamani hupanda
 
Mkuu umeeleza vyema sana lakini vipi kuhusu uaminifu wa makampuni hayo?
Hayawezi kufanya janja janja ya kutengeneza pesa za ziada na kuziingiza kwenye mzunguko kiaina?!

Najua kuna namba za fedha na ugumu kidogo wa hili ila wanaaminiwa vipi? na kwa nini kusiwe na jinsi ya kutengeneza fedha zetu hapa?

ukiwa unachapisha noti mpya unatakiwa uwe makini sana: maaana hapo unaweza rudisha uchumi wako mpaka 0, ukichapisha nyingi kuna kinaitwa inflation yaani pesa zmekua nyingi sana na kila mtu anaweza kuafford hapo ndo heshima ya pesa inashuka na wafanya biashara wanapandisha bei ya huduma zao mfano chakula: nchi pekee ambao wanaweza kuchapisha kiasi chochote wanachotaaka ni kwa trump peke yake kwa sababu uchumi wao uko stablized already but they are moving to digital cash instead of physical papers: they can print hata trilion moja na wakawapa nchi za afrika misaada and many more but yet pesa yao ikabaki an thaman kubwa pale pale: infact USA wana federal institution kwa ajili ya kuprint pesa: rumours has it that USA dollar is printed by different institutions at the same time:

ni nchi tatu tu kama sio nne hawatumii USA dollar kwenye money reserve zao including rumours za china and russia, but sisi wengine wote tunatumia USA dollar as global money exchange:
rejea inflation ya zimbabwe amabapo walichapisha pesa nyingi sana ikafika hatua unatoroli la pesa kwenda kununua mkate, lazima pesa iwe limited and less

2) ukitaka kuchapisha pesa haulipi chochote bali unakopa: ni terminology ndefu kidogo kuelezea ila kuna kitabu kinaitwa CREATURE FROM JEKYLAND kinaelezea vizuri zaidi jinsi pesa zilianza rasmi maaana sehem yenyewe zilipoanza panaitwa jekyland

3) kwa mfumo wa dunia ya sasahv pesa zilizopo kwenye papers ni 5% tu: pesa zingine zote zipo in digital form
 
Mkuu kumbuka hata majangili wanatengeneza fedha na kujaribu kuziingiza kwenye mzunguko hata marekani mpaka Leo wanapambana na kuzuia fedha bandia kuingizwa katika mzunguko wao kazi nyingine ya kikosi cha secret service si kumlinda rais wa marekani peke yake pia na kuhakikisha federal reserved system FRS ya marekani inakuwa safe and secure secret service walisha wai kukamata mabilion ya fedha bandia katika godawn huko Colombia

kama nilivyo sema hapo mwanzo kampuni hizi zote zinakuwa controlled by the government pia kila kampuni inakuwa na material ya utengenezaji wa zile karatasi inakuwa ni top secret au classified kwa kampuni husika na ndo kitu kinachofanya kampuni kupewa tenda kwani isingekuwa hvyo kumbuka kuwa kuna watu wanatengeneza fedha bandia pia utakiwa kujua kinacholindwa si fedha bali makaratasi ya kutengeneza fedha

kuhusu ss kutengeneza fedha zetu hapa tunaweza bt kuna vitu unatakiwa kujiuliza kama tunaweza? ?
1 je thamani ya fedha yetu nani atakuwa anaicontrol kulinganisha na fedha za wenzetu kwani tunaweza kuwa tunaprint tuuuuu mifedha mfano Zimbabwe kuna mpaka noti ya laki moja


2 je tuna technology ya kutengeneza fedha zetu ili watu wasiweze kucopy na kutengeneza zao na kuziingiza kwenye mzunguko

3 maswala ya kifedha duniani yanakuwa controlled by IMF na WB bt kuna nchi hazipo kwenye mfumo wa kinyonyaji wa IMF mfano Iran na china tatizo lake linakuja pale unapotaka kufanya international transaction kwani bank zako zinakuwa hazipo kwenye mifumo ya kibenk zingine mfano ilifikia kipindi ukitaka biashara Iran itakulazimu uende na fedha kwani bank zao zilikuwa hazipo katika mfumo wa mabanki mengine so huwezi kufanya wire transaction

mkuu naomba nkurekebishe: kampuni zinazochapisha fedha hazipo chini ya serikali, mfano hakuna institution yoyote duniani including CIA inaruhusiwa kufanya uchunguzi wowote katika federal reserve even the government of united states of America haina ruhusa yoyote kufanya uchunguzi wowote hapo: hili swali alishaulizwa Alan Greenspan (Former manager wa FEDERAL RESERVE) na akasema kabisa hakuna shirika lolote linaloruhusiwa kufanya uchunguzi kwenye federal reserve hio interview ipo youtube:

na pia maswala ya fedha duniani hayako controlled by WB or IMF, money is controlled by the central bank wao ndo wanamaamuzi ya pesa katika hio nchi, wanaweza kuongeza kiasi ama kupunguza:mfano sisi tumeamua noti zetu ziishie 10K ila kuna zimbambwe wana noti ya trillion moja

na pia fedha za tanzania znachapishwa na yeyote anaweza kuendana na matakwa ya benki kuu, kuna baadhi ya benki Tanzania hua yanachapisha noti mpya kwa sababu wanazo negative assets nyingi ambazo zpo typed tu kwenye computer: na pia lazima ujue benki pia znatengeneza pesa mpya kila sku ingawa sio kwa noti ila kwa digits lakini bado ni pesa na unaweza kuziweka katika noti mwisho wa siku


swala la mwisho: duniani pesa zinamilikiwa na wenye hisa katika federal reserve, rumours has it, the rothchild family: kwakua federal reserve ina hisa na wametaja kabisa katika website yao inamaanisha yoyote atakaenunua hisa kubwa ndo atakua mmiliki wa federal reserve: mfano major banks in the world, barclays, bank of england ni baadhi ya waliotajwa kua na hisa katika federal reserve, hakuna anaejua ukwel kwa sababu hisa zao ni siri zote hua ni rumours nan mmiliki halali wa federal reserve
 
Asante kwa Elimu hii nzuri, lakini iweje nchi zetu zinauwa maskini wakati uchumi unapimwa kwa kiwango cga fedha?? Mfano Rais Magufuli anataka kununua ndege ya bilioni 500 za kitanzania sawa na Usd 20Milioni, kwanini ahangaike kukopa huko nje badala ya kuagiza kampuni yetu ya Ujerumani ikatengeneza bilio 500 za kitanzania tuka exchange into usd tukaagiza ndege yetu kanada bila kukopa kopa na kupiga watu marisasi?

nchi pekee inaoweza kufanya ivo ni united states of america peke yake: kwa sababu pesa yao ndo global exchange, hauwezi kwenda kununua ndege kwa kutumia tsh kwa sababu hakuna anetaka kuskia tsh nje ya tz: utaenda BOT utawapa tsh watakupa $$ kutokana na reserve walionao: kila nchi duniani kote kasoro north korea, cuba and afghanistan ndo hawatumii usd kama exchange: they use gold and other valuable assets, simply one reason: they never loose value, US dollar looses value each end of the year. china + russia walianza kuuuza reserve zao za USD kitambo ili kununua gold:

sasa wengine tuliobaki lazima ufanye exchange, kwa kutumia USD:
jibu la swali lako: kwakua usd ndo global exchange they can print as much as they want, kuna kiwanda cha watu binafsi pia kinaprint pesa marekani, wengine wote tukiprint pesa inakua useless

imagine una pesa nyingi sana mpaka zimezidi expenses zako, means hautakua na kazi nazo na wafanya biashara watapandisha bei, na kutakua na makaratasi mengi mtaani ambayo ni fedha halali, hiki ndicho kiliitokea zimbabwe, na pia ndicho kinaendelea tanzania, mfno tsh 1, tsh 10, tsh 20, tsh 50: hizo zote sasa hivi they are considered gone kwa sababu wafanya biashara bei zao zipo juu ya hapo
 
Umeuliza: Kampuni gani inahusika na kutengeneza pesa?

Jibu ni Benki Kuu ya kila nchi. Benki Kuu ya kila nchi ndo inahusika na kutengeneza pesa. Kwa hiyo sio kampuni, bali ni taasisi.

Ila kama msingi wa swali lako ni kutaka kujua kuwa ni kampuni au taasisi zipi zinatengeneza noti na sarafu, majibu ndo kama hayo uliyopewa na wadau huko juu.

Hata hivyo inatakiwa ujue kuwa anayehusika na utengenezaji wa noti na sarafu ni Benki Kuu ya nchi husika. Yeye Benki Kuu ndo ataamua kuwa tenda ya kuchapisha noti au sarafu ampe nani, lakini anayehusika ni Benki Kuu.

Na pia utambue kuwa noti na sarafu ni sehemu tu ya pesa. Lakini pesa yenyewe ni hisabati za kiuchumi. Ni namba inayotengenezwa kwenye computer. Unapoona namba mahali popote pale ujue kuna hisabati imetumika. Kwa hiyo unapoona ile 10,000/- kwenye noti, ni matokeo ya hisabati hayo.

Kwa hiyo kuna hela zinatengenezwa na Benki Kuu, au chini ya usimamizi wa Benki Kuu, lakini haziwekwi katika mfumo wa noti na sarafu. Zinaishia katika mfumo wa kidigitali. Lakini ni pesa halali na zinatumika kununua mali kama nyumba, magari, n.k.
 
Umeuliza: Kampuni gani inahusika na kutengeneza pesa?

Jibu ni Benki Kuu ya kila nchi. Benki Kuu ya kila nchi ndo inahusika na kutengeneza pesa. Kwa hiyo sio kampuni, bali ni taasisi.

Ila kama msingi wa swali lako ni kutaka kujua kuwa ni kampuni au taasisi zipi zinatengeneza noti na sarafu, majibu ndo kama hayo uliyopewa na wadau huko juu.

Hata hivyo inatakiwa ujue kuwa anayehusika na utengenezaji wa noti na sarafu ni Benki Kuu ya nchi husika. Yeye Benki Kuu ndo ataamua kuwa tenda ya kuchapisha noti au sarafu ampe nani, lakini anayehusika ni Benki Kuu.

Na pia utambue kuwa noti na sarafu ni sehemu tu ya pesa. Lakini pesa yenyewe ni hisabati za kiuchumi. Ni namba inayotengenezwa kwenye computer. Unapoona namba mahali popote pale ujue kuna hisabati imetumika. Kwa hiyo unapoona ile 10,000/- kwenye noti, ni matokeo ya hisabati hayo.

Kwa hiyo kuna hela zinatengenezwa na Benki Kuu, au chini ya usimamizi wa Benki Kuu, lakini haziwekwi katika mfumo wa noti na sarafu. Zinaishia katika mfumo wa kidigitali. Lakini ni pesa halali na zinatumika kununua mali kama nyumba, magari, n.k.

well explained
 
Pesa ya Tanzania inatengenezwa Ujerumani, kama Sikosei na huwa inatangazwa zabuni na mshindi ndiye anayechukua tenda na malipo ni kama tenda nyingine tu mkuu!!
Ila nasikia pesa ya Marekani inatengenezwa na freemason ingawa sina uhakika sana!!
Ninavyojua angola zimbabwe wana mitambo ya kutengeneza hela mizuri tu. Hata tz tunaweza kua na yetu. Ila kutengeneza hela ya nchi kuna mambo makubwa ya viwango na kuaminiana.

Ila ni biashara ambayo nchi isipokua na usimamizi mzuri vigogo wa mamlaka nchini mwenu wanaweza kuwapiga sana. Kwanza bei kubwa na wanaweza kuchapisha hela ovyo kwa motisha ya kupiga hela tu.

Wakati fulani ilisemekana BOT wali outsource hiyo shughuli kwa mwananchi mmoja wakapiga hela sana. Ni shughuli lazima ifanywe na benki yenyrwe kwani watengenezaji wa fedha wanajulikana ni ulaji tu kumpa mtu hana kiwanda.
 
Hapana hazisafirishwi kwa meli.
Husafirishwa kwa ndege za mizigo
Na zinapokuja zile noti Huwa ktk mtindo kama mkanda mmoja mrefu.

Zikifika hutolewa na magari maalumu zikiwa kwenye makasha na hupelekwa bank kuu moja kwa moja
Huko huanza kugongwa namba kwasababu zinapokuja Huwa hazina namba. Kwahiyo kama Kuna noti zilirudishwa BOT Kwaajili ya kuteketezwa kutokana na uchakavu namba zake kupewa noti nyingine.

Kisha hupelekwa kitengo Cha kuweka alama za Siri.
Kisha hupelekwa kitengo Cha kukata kata noti Kwa saizi yake halisi.. ndipo huanza kuingizwa kwenye mizunguko ya matumizi kwa kupitia mabank

Kwahiyo huwezi kuiba noti zikiwa mpya toka kiwandani. Zinakuwa hazijakamilika na zinakuwa ni kama taili kubwa.. labda kama taili ya coaster.

Noti zinapokuja zikifika airport huondoshwa muda huohuo yaani zikishuka kwenye ndege utakuta magari ya BoT tayari yanasubiri nje ya custom

Kitengo ch clearing agent hupewa makalatasi na kwenda ku process na mpaka wanapata release basi wanaondoka kwa sababu mzigo inakuwa ulishachukuliwa.
 
Back
Top Bottom