Kampuni zinazohusika na kutengeneza pesa

Kampuni zinazohusika na kutengeneza pesa

Asante mkuu izzo kwa elimu nzuri. Kwenye post za mwanzoni ulisema kuna njia sita za kupandisha ama kushusha thamani ya pesa. Ningependa uniambie njia hizo sita na kwanini nchi yetu isizitumie kupandisha thamani ya shilingi yetu kuwa kama zamani miaka ya 1960s-1980s?
Mkuu swali lako ni zuri sana na majibu yake ni marefu sana nitakuja na jibu lako kwa urefu coz inabidi tuanze kuchambua kuanzia tulipo potea kuanzia miaka ya 1985 na mbaya zaidi 2014 kumekuwa na tatizo juu ya watalamu wetu wa maswala ya kifedha na uchumi tumeacha soko ndio liamue thamani ya huduma au bidhaa baada ya mahitaji ndio yaamue thamani ya bidhaa au huduma
 
Asante mkuu,nalisubiri jibu lako kwa hamu.
 
Halafu haya mambo hatufundishwi darasani, acha niendelee kuisoma thread nkiwa darasani maana huku darasani tunachoshana tu.

Izzo brother big up sana nimeupenda uchambuzi wako.
 
32bbfd3df9f3996c8ebd66b1e4ba8d69.jpg
 
mimi sitaki kuamini kwamba mia tano ya noti ilitengenezwa ujerumani mana haina tofauti na majani ya kisamvu
Wewe acha kuhidhihaki pesa ya Tanzania nyie ndio watu mnaoidhihaki nchi, kukejeli na kudharau viongozi. Mkishikwa eti oh oh oh mara viongozi wanawaonea wanatumia mabavu kumbe sijui dikteta uchwara kumbe ni nyinyi wenyewe sasa kwa mfano wewe uongozi ukija kukuchukua kwa mahojiano kuhusu hiki ulichoandika utasema umeonewa em fanya haraka ufute hii comment haraka haraka. Maxence Melo alitiwa nguvuni sababu ya wapumbavu wachache kama ninyi. Futa hii comment chap chap ukaanzishe uzi jukwaa la Kilimo, Ufugaji na Uvuvi. Si unafahamu kwamba KAZA ROHO. HAPA KAZI TU.
 
mkuu cwez kuingia ndani sana ktk security details za fedha yetu coz is highly classified pia ni HVCs cargo bt kukujibu swali lako kiufupi tu ni kama vle vocha zinapotoka kiwandani kwenda kwa makampuni ya simu kwa ajili ya kusambazwa kwetu zinakuwa hazina number? ?? kumbuka kiwanda cha vocha kipo hapa hapa Tanzania na pia ni njia gani utumika kuzi install kwenye system mpaka ukikwangua na kuweka zinakubali majibu yake ndo njia hizo hutumika pia ktk fedha .........
Daah mkuu izzo hakuna hata siku moja umeniangusha huwa napendezwa sana na majibu yako na mi nafikiri tunahitaji watu kama wewe, elimu yako tuitumie watanzania na taifa likanufaike nakuheshimu sana kaka God bless you.
 
Wewe acha kuhidhihaki pesa ya Tanzania nyie ndio watu mnaoidhihaki nchi, kukejeli na kudharau viongozi. Mkishikwa eti oh oh oh mara viongozi wanawaonea wanatumia mabavu kumbe sijui dikteta uchwara kumbe ni nyinyi wenyewe sasa kwa mfano wewe uongozi ukija kukuchukua kwa mahojiano kuhusu hiki ulichoandika utasema umeonewa em fanya haraka ufute hii comment haraka haraka. Maxence Melo alitiwa nguvuni sababu ya wapumbavu wachache kama ninyi. Futa hii comment chap chap ukaanzishe uzi jukwaa la Kilimo, Ufugaji na Uvuvi. Si unafahamu kwamba KAZA ROHO. HAPA KAZI TU.
🙂🙂🙂🙂🙂🙂 Na we mkuu bwana!
 
hizi sh 500 zinachakaa haraka sana nahisi wajerumani wanatuibia kwenye kuzichakata si bure
 
Ni nchi ya USA ndio wameweka mfumo wa fedha yao kuexpire kila baada ya miaka 10 yani dola iliyotengenezwa mwaka 2007 mpaka leo ndio inatumika lakini iliyotengenezwa nyuma ya 2006 haitumiki kama unayo uwezi kwenda kubadilisha kwenye maduka ya fedha kwni inahesabiwa kama imeshaexpire na inakuwa imeshatolewa kwenye mzunguko

Kiwanda cha Washington cha( tour and visitor centre) chenye uwezo wa kutengeneza kiasi cha dollar million 28 par hour na ndio fedha zinazotoka pale nying ndo zinaingia wenye nzunguko dunian na pia wameweka expire date ya ela yao ili kuweza kujua ni kiasi gani cha fedha kipo katika mzunguko duniani na pia kudhibiti mijitu inayoficha ela kwenye masandarusi na ndoo coz ikifika mda fedha inaexpire so ikiexpire mkononi mwako itakuwa ni taratasi tu coz huwezi kufanya manunuz yeyote popote pale kwani itakuwa imeondolewa kwenye mzunguko nadhani ni miaka 10 so ela iliyotengenezwa juu ya miaka 10 yani inayokubalika sasa sokoni ni yakuanzia 2007 wao hawasubili mpaka fedha kuchanika au kuchakaa kama tunavyofanya ss
NOTE: Matumizi ya miaka kumi kwa fedha ya dola yamewekwa kwa nje ya US lakini ndani ya US inatumika na inaondolewa kwenye mzunguko kama ilivyo huku ndio maana dola ya 2006 inatumika US lakni nje ya US inaonekana kama imekwisha mda wake wa matumizi

Kazi nyingine ya kikosi cha secret service si kumlinda rais wa marekani peke yake pia na kuhakikisha federal reserved system FRS ya marekani inakuwa safe and secure kumbuka hata majangili wanatengeneza fedha na kujaribu kuziingiza kwenye mzunguko hata marekani mpaka Leo wanapambana na kuzuia fedha bandia kuingizwa katika mzunguko wao pia dola ni fedha inayotumika dunia nzima ktk maswala ya manunuzi, malipo na mikopo so mahitaji ya dola ni makubwa sana duniani nia ya kuweka expire date ni kwa ajili ya kuweza kulinda na kujua mzunguko wa fedha yao duniani
Hapa sibanduki ngoja nisogeze kigoda kabisa..
Mkuu izzo tumekuwa tukisikia pesa ya nchi flani inagumvu hili swala limekaaje maana nimejaribu kufatilia kwa mwaka 2013 Kuwait dinar ndiyo ilikuwa pesa yenye nguvu kuliko zote kwa ambapo ukiwa nayo moja ni sawa na hii yetu(Tsh 5509)..ya pili ni Bahrain dinar ambayo moja ni sawa na TSH 4169..Ya tatu ni Oman rial ambayo moja ni sawa na Tsh 4067 ya nne ni latvia lats ambayo moja ni Tsh 2921 na ya tano ni Uk Pound ambayo moja ni Tsh 2409 japokuwa zina badilikabadilika mpaka sasa lakini hizi ndio pesa zenye nguvu sana,kwa mpangilio huu dola ilikuwa ya kumi na tatu katika pesa zenye nguvu,kuna bwana mmoja aliniambia pesa ya mwarabu ina nguvu kwa ajiri ya mafuta inawezakuwa kweli lakini ni kwanini Nigeria ambayo ni ya sita duniani kwa uzalishaji wa mafuta pesa yao (Naira)haina nguvu??maana pesa ya kenya ina nguvu kuliko ya nigeria..ni vitu gani vinavyofanya pesa ya nchi iwe na thamani???niliambiwa kuna kipindi cha nyuma 1960s pesa yetu ya tanzania ilikuwa na nguvu sana tsh moja ilikuwa kama dola 5 na ilikuwa na nguvu kuliko ile ya kenya,kwa afrika pesa nne zilizo na nguvu ni cedi ya ghana..pound ya sudan..botswana pula..na rand ya SA...au ufisadi pia unachangia pesa kushuka??maana nigeria kama nilivyosema ni ya sita duniani katika kuzalisha mafuta..inazalisha mafuta mara kumi zaidi ya nchi ya UAE lakini pesa yake naira haina nguvu sana..kwa nini??? Vitu gani huzingatiwa zaidi kwenye uthamani wa pesa na kuwa na nguvu?
 
Hi wana JF,

Nimekuwa nikisikia kuwa pesa ya nchi yoyote ile utengenezwa katika nchi ya Uswisi, lakini katika kujua huko nimekuwa nabaki na maswali mbalimbali juu ya hilo. Maswali hayo ni pamoja na;

(i) Je katika nchi hiyo ni kampuni binafsi au za serikali ndiyo zinahusika kutengeneza?
(ii) Je kampuni hizo zinafanya kazi hiyo kama msaada au ni ki biashara?
(iii) Kama ni ki biashara?, wao wanalipwa nini? pesa hiyo hiyo wanayotengeneza au kitu kingine? kwa maana kama ni pesa hiyo sioni kama wana fanya biashara, nitoe mfano mdogo, chukulia umpe mtu order ya kukutengenenezea mikate, na baada ya kukutengenezea umlipe kiasi fulani cha mikate hiyo, hapo si ni sawa sawa mikate hiyo kakupa bure? n.k

Kwa kutambua JF ni jukwaa lililojaa wataalamu katka nyanja mbalimbali natumaini nitapata majibu kulingana na duku duku hizo.

Nawasilisha.
We jamaa una akili sana.....japo wachangiaji wengi wamempongeza bwana izzo kama mkufunzi wetu hapa lakini amini nawaambia bila ya wewe bwana izzo tusingemjua....hongera sana bwana kwa kuja na swali lenye kutufungua wengine ufahamu wetu wa mambo.

Pia kwa heshima na taadhima nichukue nafasi hii kukushukuru bwana izzo kwa darasa maridhiwa unalotupatia. Nadhani wazazi wako waliokupeleka huko shuleni must be proud of you. Sio wazazi tu bali wanao, wanajf na watz wote kwa ujumla we are proud of you.

Mungu akubariki sana mkuu kwa moyo wako wa kuelimisha umma pasipo kudai malipo.
 
Kilichonifurahisha,,,... hakuna kejeli za "nenda google" hii inadhihirisha jinsi muuliza swali ambaye ni mtoa mada kauliza wengi tulichotaka kujua..

Asante kwa aliyejibu na wauliza maswali wengine na waliojibu.
 
Ni nchi ya USA ndio wameweka mfumo wa fedha yao kuexpire kila baada ya miaka 10 yani dola iliyotengenezwa mwaka 2007 mpaka leo ndio inatumika lakini iliyotengenezwa nyuma ya 2006 haitumiki kama unayo uwezi kwenda kubadilisha kwenye maduka ya fedha kwni inahesabiwa kama imeshaexpire na inakuwa imeshatolewa kwenye mzunguko

Kiwanda cha Washington cha( tour and visitor centre) chenye uwezo wa kutengeneza kiasi cha dollar million 28 par hour na ndio fedha zinazotoka pale nying ndo zinaingia wenye nzunguko dunian na pia wameweka expire date ya ela yao ili kuweza kujua ni kiasi gani cha fedha kipo katika mzunguko duniani na pia kudhibiti mijitu inayoficha ela kwenye masandarusi na ndoo coz ikifika mda fedha inaexpire so ikiexpire mkononi mwako itakuwa ni taratasi tu coz huwezi kufanya manunuz yeyote popote pale kwani itakuwa imeondolewa kwenye mzunguko nadhani ni miaka 10 so ela iliyotengenezwa juu ya miaka 10 yani inayokubalika sasa sokoni ni yakuanzia 2007 wao hawasubili mpaka fedha kuchanika au kuchakaa kama tunavyofanya ss
NOTE: Matumizi ya miaka kumi kwa fedha ya dola yamewekwa kwa nje ya US lakini ndani ya US inatumika na inaondolewa kwenye mzunguko kama ilivyo huku ndio maana dola ya 2006 inatumika US lakni nje ya US inaonekana kama imekwisha mda wake wa matumizi

Kazi nyingine ya kikosi cha secret service si kumlinda rais wa marekani peke yake pia na kuhakikisha federal reserved system FRS ya marekani inakuwa safe and secure kumbuka hata majangili wanatengeneza fedha na kujaribu kuziingiza kwenye mzunguko hata marekani mpaka Leo wanapambana na kuzuia fedha bandia kuingizwa katika mzunguko wao pia dola ni fedha inayotumika dunia nzima ktk maswala ya manunuzi, malipo na mikopo so mahitaji ya dola ni makubwa sana duniani nia ya kuweka expire date ni kwa ajili ya kuweza kulinda na kujua mzunguko wa fedha yao duniani
Ubarikiwe sana mkuu, leo nimejifunza kitu muhimu sana kutoka kwako na nitakuwa makini sana kwa hilo.

Mimi nimefanyakazi tours kuna kipindi nilipewa tip na Wamarekani ya some dollars ambazo zimepita miaka 10 nadhani hata wao nina uhakika wengi hawana elimu hii kwamba pesa yao nje ya nchi yao ina expire date, basi nilipata shida sana kuzichange zile dollar na wale Wamarekani tulikuwa tumeshaagana kwa kweli haikuniingia akilini hata kidogo noti ni mpya kabisa na siyo fake halafu bereu de change wananiambia pesa ya mwaka flani hawachenji kwakweli iliniuma sana mpaka kuna mtu mmoja BOT akaniambia nenda bereu de change flani naomba nisiitaje jina basi nikaenda hapo wakanichenjia.

Sasa swali langu ile bereu de change wanaokubali expired usd mmiliki wake anasafari za Marekani mara kwa mara ndio maana anazipokea kwamba anazitumie dollar zile akifika Marekani?

Pia nimalize kwa kukushukuru kuanzia sasa nami nitaanza kuzikaguwa dollar kujuwa zimetengezwa mwaka gani, maana binafsi mpaka leo nilikuwa naamini ni ukiritimba tu Watanzania kuzikaguwa miaka usd. Nimeelimika leo.
 
Kila nchi inautaratibu wake katika utengenezaji wa fedha zake mfano tuzungumzie Marekani coz ndo fedha yake utumika Kwa wingi duniani kule kuna taasisi inaitwa Bureau of Engravin printing (BEP) hii ni taasisi inayoshugulikia uchapishaji na usambazaji wa fedha ya Marekani kuna viwanda viwili ndani ya Marekani kimoja kipo fort Worth TEXAS na Kingine kipo nje kidogo ya jiji Washington karibu na yaliyokuwa makao makuu ya kampuni na viwanda vya kutengeneza ndege vya Boeing Everett Washington bt now Boeing makao makuu wameanishia north riverside illinois Chicago hapo ndo sehemu zinapochapishwa fedha za marekani na ulinzi wa hapo kiwandani ni mkubwa sana mfanyakazi aruhusiwi kutoka hata na kipande cha karatasi ingawa kipindi cha nyuma kuna mfanyakazi mmoja alishawahi kuiba fedha Kwa kujiwekea POP na alikuwa mjamzito so hakuwa anapita kwenye scanner kutokana na hali yake so akawa anafanyiwa ukaguzi wa kupapaswa kumbe alikuwa anazisokomeza ndani ya POP lililokuwa kwenye mguu wake

Bt duniani kuna makampuni yanayotengeneza fedha mengi yako nchi za ujerumani UK na Swiss bt yanakuwa controlled by Government so kama nchi inataka kutengeneza fedha zake wanatangaza tender za makampuni yana shindana ya mshindi anapata tenda ya kutengeneza malipo mnalipa Kwa dollars coz fedha nayo ni bidhaa inauzwa kama zilivyo bidhaa nyingine

Kwa Tanzania fedha zetu tunazitengenezea Germany na kusafiliswa kwenye containers mpaka kwenye port zetu then utaratibu wa custom ufanyika kuzitoa ni kama mizigo mengine inavyotolewa bt mzigo huu ni HVC high value cargo na ulinzi wake ni mkubwa sana kumbuka duniani kinacholindwa si fedha bt ni makaratasi ya kutengeneza fedha kwani tofauti ya fedha bandia na halali ni karatasi tu bt kila kitu vinaweza kufafana
Asante mkuu
 
Samahani kwa nini picha ya hela haibadiliki ni ileile ya mwl nyerere kwani wengini hawaruhusiwi na mantiki ya picha nini
Inaweza badirika ndo maana kuna Pesa zenye Picha ya nyerere, mwingi , karume...ila raid mkapa kikwete, rais karume (karume mdogo) walikataa Picha zao kuwekwa kwa Pesa tunazotumia.
 
Nina maswali machache ya kizushi:
1. Je kwanini serikali isichape Pesa nyingine kwaajili ya miradi mikubwa itayofanywa na makampuni ya ng'ambo (ulaya & marekani) maana hao tukiwalipa Pesa wanazipeleka kwa nchi zako ila na Wazo wanakuwa wametuachia tangible dvp .

Mfano: tukajenga barabara za lami mjini na vijijini,
: tukasambaza umeme nchi nzima kwa kampuni za kimataifa maana Pesa zote wanapeleka nchini kwao, ila sis wanatuachia maendeleo.
Tukatengeneza madawati na kuchapa vitabu vya kutosha nchi nzima.
Tukanunua madawa hospital...

Yako.mengi ninawaza kwa sauti kubwa "thinking out loudly" kuwa mambo ya kiuchumi Haya kuna watu wanatupangia tu kwa kadri wanavyotaka Wao na madhumuni yao wenyewe.

Maana Nina amini kama Pesa ukiingiza nyingine kwenye mzunguko wa kununua nyanya, mchele, nk inaleta mfumuko wa Bei maana wananchi wanakuwa na Pesa nyingi sana, ila Mimi logic yangu ni kuwa Je ikitokea tukaingia mkataba na makampuni ya kimataifa yakafanya kazi za maana tukayalipa Pesa zao (automatic yatapeleka nchini mwao ulaya) na hivyo kutoathiri sana uchumi Wetu kwa kuwa na mapesa mengi.

FYI: I'm declaring interest that, am neither economist nor financial planner.

Hivyo nielimishwe kwa kina.
 
Hapa sibanduki ngoja nisogeze kigoda kabisa..
Mkuu izzo tumekuwa tukisikia pesa ya nchi flani inagumvu hili swala limekaaje maana nimejaribu kufatilia kwa mwaka 2013 Kuwait dinar ndiyo ilikuwa pesa yenye nguvu kuliko zote kwa ambapo ukiwa nayo moja ni sawa na hii yetu(Tsh 5509)..ya pili ni Bahrain dinar ambayo moja ni sawa na TSH 4169..Ya tatu ni Oman rial ambayo moja ni sawa na Tsh 4067 ya nne ni latvia lats ambayo moja ni Tsh 2921 na ya tano ni Uk Pound ambayo moja ni Tsh 2409 japokuwa zina badilikabadilika mpaka sasa lakini hizi ndio pesa zenye nguvu sana,kwa mpangilio huu dola ilikuwa ya kumi na tatu katika pesa zenye nguvu,kuna bwana mmoja aliniambia pesa ya mwarabu ina nguvu kwa ajiri ya mafuta inawezakuwa kweli lakini ni kwanini Nigeria ambayo ni ya sita duniani kwa uzalishaji wa mafuta pesa yao (Naira)haina nguvu??maana pesa ya kenya ina nguvu kuliko ya nigeria..ni vitu gani vinavyofanya pesa ya nchi iwe na thamani???niliambiwa kuna kipindi cha nyuma 1960s pesa yetu ya tanzania ilikuwa na nguvu sana tsh moja ilikuwa kama dola 5 na ilikuwa na nguvu kuliko ile ya kenya,kwa afrika pesa nne zilizo na nguvu ni cedi ya ghana..pound ya sudan..botswana pula..na rand ya SA...au ufisadi pia unachangia pesa kushuka??maana nigeria kama nilivyosema ni ya sita duniani katika kuzalisha mafuta..inazalisha mafuta mara kumi zaidi ya nchi ya UAE lakini pesa yake naira haina nguvu sana..kwa nini??? Vitu gani huzingatiwa zaidi kwenye uthamani wa pesa na kuwa na nguvu?
Kujibu swali lako Dr. Duniani kuna taasisi mbili zinazohusika na maswala ya kifedha na uchumi taasisi hzo ni International Monetary Fund (IMF) na World Bank (WB) taasisi hzi zinaongozwa na money policy act (MPA) ndani ya MPA kuna mfumo unaoitwa Global financial system (GFS) mfumo huu unamilikiwa na Rothschild family kumekuwa na fikra ya kuwa Rothschild family ndio wamiliki wa Bank kubwa kubwa ikiwamo WB , IMF na Federal Reserve System japo wengi wanajua ni Federal Reserve bank lakini ukweli ni Federal Reserve System huku bank ikiwa ni Bank of America (FRS ) ni mfumo tu unaoendesha bank hzo ambapo unaendeshwa na sheria ya federal reserve system act ya mwaka 1913
Rothschild si wamiliki wa banks hzo bali wanamiliki mfumo wa GFS unaotumika kwenye banks nying duniani kuelewa vizuri ni kama leo MAX malipo wanamfumo wao wa maxcom mfumo unaotumika kufanya malipo kwa huduma mbalimbali so ndio mfumo wa GFS unavyofanya kazi

Money policy act (MPA) ndio mwongozo wa centro banks zote duniani na kazi ya centro bank duniani ni

1 print money
2 control supply of money
3 Set the Reserve Requirement
4 Influence Interest Rates
5 Engage in Open Market Operations
6 Control inflation

Hii ndio kazi ya CB zote duniani kuhusu kushuka kwa thamani ya fedha au uchumi

Kwanza unatakiwa kujua hakuna mahusiano ya thamani ya fedha na uchumi japo wengi wanajua kuna mahusiano ya vtu hv lakini ukweli ni kwamba hakuna wakati formula ya uchumi wa ndani ni

MV=PY
M=Money suppy
V=Velocity of circulation
P=price level
Y=National income

Wakati formula ya kushusha au kupandisha thamani ya fedha ni vitu hv
1 INFLATION
2 INTREST RATES
3 Current-Account Deficits
4 Public Debt
5 . Terms of Trade
6 . Political Stability and Economic Performance

Kutokana na kutokuwa na mahusiano hayo ndio unaona dola ya US kuna fedha duniani zimeizidi thamani kama Euro,paund,dinar ya oman pia ukiangalia uchumi wa US na uchumi ya Omani ni vichekesho leo kama kungekuwa na mahusiano ya uchumi na thamani ya fedha basi leo fedha ya Japani ,China zingekuwa ni moja ya sarafu zenye nguvu kubwa duniani na USD ndio ingekuwa fedha yenye thamani kuliko zote

Kuna kitu kinaitwa Balance of trade na ambayo mfumo wake ndio unakwenda kwenye mfumo wa uchumi mkuu moja kwa moja yani GDP

GDP = C + I + G (Ex - Im)

C = Consumer spendng
I= Investment spendng
G= Govement spendng
Ex= Export
Im=Import

Sasa kuhusu uchumi wetu Tanganyika na thamani yetu ya fedha kushuka au kuteteleka aidha kuna vitu viwili

1 Wataalamu wetu wameshindwa kutumia maarifa (Ufahamu) wao vizuri (kwani kwa binadamu tuna vitu vitatu

(A) Utashi (B) Akili ( C) Ufahamu

Sasa Akili ni matumizi mazuri ya ufahamu ambao mara nying unapatikana kwa uzoefu au kwa kwenda shule

2 Labda wataalamu wetu hawajui kupigana vita hii ya kiuchumi na kifedha

Duniani kuna vita tatu
1 Vita vya silaha na majeshi

2 Cyber war(Vita vya mifumo ya technologia ya habari na mawasiliano)

3Economic war (Vita vya kiuchumi)

Vita vya kiuchumi ndio vita inayopiganwa sasa duniani kuliko vita vingine vyote unavijua zipo mpaka mbinu za kimafia za kupigana vta hii ya kiuchumi
ambazo zipo njia 6 za kupadisha uchumi na fedha

Matola jibu lako ni wanapokuchejia dola iliyoexpire kwanza unachenjiwa chini ya exchange rate ya siku hyo kama ni dola mia ni sh 200,000 ww kwa fedha yako ya zamani utachengiwa chini ya laki mbili then wanazipeleka Zanzibar fedha za zamani huko wanapewa wageni au wazungu wanaorudi makwao wanarudi nazo US
mwenye swali anaweza uliza kwani JF ndio sehemu pekee ambapo hakuna bodi ya mikopo hapa unapata elimu bure

Mkuu MALCOM LUMUMBA unaweza kujazia nilichosahau kuweka hapa

brazuca Paprika k_dizle Juma chief MNANSO mtimkav Dux_1234 LIKE Niku ADD Kalamu Yangu

Molaro
 
Back
Top Bottom