Kampuni zinazohusika na kutengeneza pesa

Kila nchi inautaratibu wake katika utengenezaji wa fedha zake mfano tuzungumzie Marekani coz ndo fedha yake utumika Kwa wingi duniani kule kuna taasisi inaitwa Bureau of Engravin printing (BEP) hii ni taasisi inayoshugulikia uchapishaji na usambazaji wa fedha ya Marekani kuna viwanda viwili ndani ya Marekani kimoja kipo fort Worth TEXAS na Kingine kipo nje kidogo ya jiji Washington karibu na yaliyokuwa makao makuu ya kampuni na viwanda vya kutengeneza ndege vya Boeing Everett Washington bt now Boeing makao makuu wameanishia north riverside illinois Chicago hapo ndo sehemu zinapochapishwa fedha za marekani na ulinzi wa hapo kiwandani ni mkubwa sana mfanyakazi aruhusiwi kutoka hata na kipande cha karatasi ingawa kipindi cha nyuma kuna mfanyakazi mmoja alishawahi kuiba fedha Kwa kujiwekea POP na alikuwa mjamzito so hakuwa anapita kwenye scanner kutokana na hali yake so akawa anafanyiwa ukaguzi wa kupapaswa kumbe alikuwa anazisokomeza ndani ya POP lililokuwa kwenye mguu wake

Bt duniani kuna makampuni yanayotengeneza fedha mengi yako nchi za ujerumani UK na Swiss bt yanakuwa controlled by Government so kama nchi inataka kutengeneza fedha zake wanatangaza tender za makampuni yana shindana ya mshindi anapata tenda ya kutengeneza malipo mnalipa Kwa dollars coz fedha nayo ni bidhaa inauzwa kama zilivyo bidhaa nyingine

Kwa Tanzania fedha zetu tunazitengenezea Germany na kusafiliswa kwenye containers mpaka kwenye port zetu then utaratibu wa custom ufanyika kuzitoa ni kama mizigo mengine inavyotolewa bt mzigo huu ni HVC high value cargo na ulinzi wake ni mkubwa sana kumbuka duniani kinacholindwa si fedha bt ni makaratasi ya kutengeneza fedha kwani tofauti ya fedha bandia na halali ni karatasi tu bt kila kitu vinaweza kufafana
Safi
 
Kila siku tunalalamika kuwa budget haitoshi si tuanzishe kiwanda cha kufyatua fedha na sisi..budget ikiyumba tunafyatua kadhaa kujazilia
Mkuu pamoja na US kuwa na viwanda viwili ndani ya US lakini hawawezi kufanya hvyo kwani ukifanya hvyo unakwenda kuzika thamani ya fedha yako kwani thamani ya fedha haipimwi kwa maitaji bali inapimwa kwa matumizi so kutotosha kwa Budget inaingia kwenye category ya mahitaji si matumizi, kwani mahitaji yanapokuwa makubwa automatically matumizi yanapungua kwani mahitaji yanaendana na kuadimika kwa kitu so US kama atafanya maamuzi ya kuchapisha tu fedha inamaana fedha yakeitatosa thamani ndio maana yuko radhi akakope China hili kumaintain thamani ya fedha yake

Note; China ndio nchi yenye kiwando kikubwa cha hifadhi ya dola za kimarekani Duniani
 
Mimi nina swali kidogo.....kama fedha zetu zinatengenezwa Ujerumani
Kwanini tusitoe oda zikatengenezwa fedha nyingiiii ili tuwe na fedha nyingi tuweze kutatua matatizo yetu ya kifedha???
 
Na mimi nasubiri jibu hapa
Mkuu kuna kitabu kinaitwa God's Banker Kinazungumzia undani wa haya mambo na jinsi Vatican tangu kipindi cha Byzantine Empire wamehusika na kutengeneza mifumo ambayo inaharibu mzunguko wa pesa hapa duniani.
Mwandishi Gerald Posner kafanya utafiti kwa miaka 9 na kukitoa mwaka 2015, humo ndani utasikitika sanaaa!
Utakuja kugundua ni Syndicate ndogo sana inatusababashia matatizo nchi nyingi hasa za Afrika.
 
Noti inachapishwa kama stationeries (document za kawaida) ila huchapwa na kampuni zilizobobea na zinaintergrity ya hali ya juu. Bei ya uchapaji wakuu haitifautiani, noti moja ya mia tano inaweza kuchapishwa kwa 2,000/ na noti ya elfu kumi nayo bei ni hyohyo 2000/.

Noti inaanza kuwa pesa inapotoka BOT kwa mara ya kwanza, kabla ya hapo linakua ni karatasi tu na ipo control ya kutosha kuhakikisha kwamba pesa haivuji kabla haijatolewa BOT. Na BOT wanazo nyingi tu ila hazijawa hela mpaka wazitoe. Pesa zina namba maalum (serial no) na kiasi kilichopo kwenye mzunguko kinafahamika na kinadhibitiwa na BoT na WB. Kwahyo hata BOT hawez ingiza noti/ chapisha noti kwa mahitaji ya serikali (seigniorage) kiholela.

Lkn pia huwa kuna dawa maalum ambayo pesa zikifungashwa kiwandani hazitafunguliaa na mtu mwingine yotote mpaka zifike BOT na akipatikana wa kukorokochoa masanduku pesa zinachujuka rangi na material. Hii ni hata zinaposafirishwa ndani ya nchi kwa kiasi kikubwa.
 
Mimi nina swali kidogo.....kama fedha zetu zinatengenezwa Ujerumani
Kwanini tusitoe oda zikatengenezwa fedha nyingiiii ili tuwe na fedha nyingi tuweze kutatua matatizo yetu ya kifedha???
Mkuu soma kitu kinaitwa inflation yani ikifanyika hiyo kitu unayotaka huta amini kitachotokea ni majanga zaidi ya awali.Alijalibu Mugabe kilichomkuta alijuta utakuwa unaenda sokoni na begi la hela kununua vitunguu na nyanya tu.
 
Kila nchi inautaratibu wake katika utengenezaji wa fedha zake mfano tuzungumzie Marekani coz ndo fedha yake utumika Kwa wingi duniani kule kuna taasisi inaitwa Bureau of Engravin printing (BEP) hii ni taasisi inayoshugulikia uchapishaji na usambazaji wa fedha ya Marekani kuna viwanda viwili ndani ya Marekani kimoja kipo fort Worth TEXAS na Kingine kipo nje kidogo ya jiji Washington karibu na yaliyokuwa makao makuu ya kampuni na viwanda vya kutengeneza ndege vya Boeing Everett Washington bt now Boeing makao makuu wameanishia north riverside illinois Chicago hapo ndo sehemu zinapochapishwa fedha za marekani na ulinzi wa hapo kiwandani ni mkubwa sana mfanyakazi aruhusiwi kutoka hata na kipande cha karatasi ingawa kipindi cha nyuma kuna mfanyakazi mmoja alishawahi kuiba fedha Kwa kujiwekea POP na alikuwa mjamzito so hakuwa anapita kwenye scanner kutokana na hali yake so akawa anafanyiwa ukaguzi wa kupapaswa kumbe alikuwa anazisokomeza ndani ya POP lililokuwa kwenye mguu wake

Bt duniani kuna makampuni yanayotengeneza fedha mengi yako nchi za ujerumani UK na Swiss bt yanakuwa controlled by Government so kama nchi inataka kutengeneza fedha zake wanatangaza tender za makampuni yana shindana ya mshindi anapata tenda ya kutengeneza malipo mnalipa Kwa dollars coz fedha nayo ni bidhaa inauzwa kama zilivyo bidhaa nyingine

Kwa Tanzania fedha zetu tunazitengenezea Germany na kusafiliswa kwenye containers mpaka kwenye port zetu then utaratibu wa custom ufanyika kuzitoa ni kama mizigo mengine inavyotolewa bt mzigo huu ni HVC high value cargo na ulinzi wake ni mkubwa sana kumbuka duniani kinacholindwa si fedha bt ni makaratasi ya kutengeneza fedha kwani tofauti ya fedha bandia na halali ni karatasi tu bt kila kitu vinaweza kufafana
Sasa kma kinacholindwa ni karatasi na sio pesa je mwisho wa cku ile pesa si inafika mikononi mwa mwananchi sasa huoni bado inaweza kuwa compromised na wakajua material inayotumika?? Hapo sijakuelewa kabisa mkuu
 
Mimi nina swali kidogo.....kama fedha zetu zinatengenezwa Ujerumani
Kwanini tusitoe oda zikatengenezwa fedha nyingiiii ili tuwe na fedha nyingi tuweze kutatua matatizo yetu ya kifedha???
Yeah kwa mtazamo wangu kuna matatizo ya kifedha sababu money supply itazidi money demand hivyo vitu vitapanda bei na thamani ya pesa itashuka kabisa pia inaweza sababisha pesa ikawa nyingi kwenye mzunguko ambayo nayo husababisha inflation pia
 
Zikiwa nyingi si tunafanya biashara ya kununua vitu nje ya nchi
Fedha zetu tunazibadili kwa hela ya kigeni mfano dollar au pound halafu tunaagiza bidhaa nje ya Nchi...
 
Mkuu pamoja na US kuwa na viwanda viwili ndani ya US lakini hawawezi kufanya hvyo kwani ukifanya hvyo unakwenda kuzika thamani ya fedha yako kwani thamani ya fedha haipimwi kwa maitaji bali inapimwa kwa matumizi so kutotosha kwa Budget inaingia kwenye category ya mahitaji si matumizi, kwani mahitaji yanapokuwa makubwa automatically matumizi yanapungua kwani mahitaji yanaendana na kuadimika kwa kitu so US kama atafanya maamuzi ya kuchapisha tu fedha inamaana fedha yakeitatosa thamani ndio maana yuko radhi akakope China hili kumaintain thamani ya fedha yake

Note; China ndio nchi yenye kiwando kikubwa cha hifadhi ya dola za kimarekani Duniani

Izzo nahisi wewe ni daudi balali si wanasema hakufaga yule...
Thumb up sana umetutoa tongotongo wengi
 
Mimi nina swali kidogo.....kama fedha zetu zinatengenezwa Ujerumani
Kwanini tusitoe oda zikatengenezwa fedha nyingiiii ili tuwe na fedha nyingi tuweze kutatua matatizo yetu ya kifedha???
Tanganyika hatuna matatizo ya kifedha bali kuna matatizo ya mifumo ya kuendesha uchumi wetu Duniani kuna vitu vitatu ambavyo vinachanganya watu vitu ambavyo kila kimoja kinajitegemea japo vyote vinamahusiano na fedha
1UCHUMI
2THAMANI YA FEDHA
3MAENDELEO
Vitu hv kila kimoja kinajitegemea na kusolve tatizo la kila kimoja si kuchapisha fedha kwan ukifanya hvyo ndio unakwenda kuharibu mifumo mizima ya upumuaji katika sector yote ya kiuchumi,maendeleo na mbaya zaidi sector ya thamani ya fedha yako dhidi ya fedha zngne
 
Sasa kma kinacholindwa ni karatasi na sio pesa je mwisho wa cku ile pesa si inafika mikononi mwa mwananchi sasa huoni bado inaweza kuwa compromised na wakajua material inayotumika?? Hapo sijakuelewa kabisa mkuu
Material yanayotumika kutengeneza fedha yanajulikana kabisa na ni
1 Cotton fiber 80-99%
2 Wood fiber 1-3%
3 Titanium white 2-3.5%
4 Polyamide epichlorohydrin 2-3.5%
5 Aluminum chloride
6 Melamine,formal dehyde resin , na animal grue
Kinacholindwa si fedha yani final product bali ni siri au jinsi ya kuchanganya hizo fomula ni top secret si kila mtu au mfanyakazi anaweza kuna na access ya kujua hilo mfano leo ni kama fomula ya kuchanganya soda ya Caca cola ilivyo kinacholindwa si material kama material ya coca hata Azam wanayo bali kuchanganya material hizo mpka zifanane na soda ya Coca Cola ndo tatizo ni sawa na fedha kinacholindwa ni formula ya kuchanganya hayo material na security features ambazo zinakuwa attached kwenye karatasi la kutengeneza fedha au kwa jina lingine wanaita makaratasi yenye thamani
 
Zikiwa nyingi si tunafanya biashara ya kununua vitu nje ya nchi
Fedha zetu tunazibadili kwa hela ya kigeni mfano dollar au pound halafu tunaagiza bidhaa nje ya Nchi...
Njia hyo nadhani kama ingekuwa inawezekana naamini Zimbabwe wangekuwa wameshaifanya siku nying kwani Unaitaji Zimbabwe dollar 35,000,000,000,000 kupata 1usd
 
Unajua hawa wanaotengeneza noti bandia wakiongezewa utaalam na ujuzi?wanaweza kutengeneza pesa iliyo bora

OvA
 
Kitu pekee watakachofanikiwa ni kuziingiza kwenye mzunguko lakini si kwenye system ya Banking yani Global financial system (GFS)
 
Kila nchi inautaratibu wake katika utengenezaji wa fedha zake mfano tuzungumzie Marekani coz ndo fedha yake utumika Kwa wingi duniani kule kuna taasisi inaitwa Bureau of Engravin printing (BEP) hii ni taasisi inayoshugulikia uchapishaji na usambazaji wa fedha ya Marekani kuna viwanda viwili ndani ya Marekani kimoja kipo fort Worth TEXAS na Kingine kipo nje kidogo ya jiji Washington karibu na yaliyokuwa makao makuu ya kampuni na viwanda vya kutengeneza ndege vya Boeing Everett Washington bt now Boeing makao makuu wameanishia north riverside illinois Chicago hapo ndo sehemu zinapochapishwa fedha za marekani na ulinzi wa hapo kiwandani ni mkubwa sana mfanyakazi aruhusiwi kutoka hata na kipande cha karatasi ingawa kipindi cha nyuma kuna mfanyakazi mmoja alishawahi kuiba fedha Kwa kujiwekea POP na alikuwa mjamzito so hakuwa anapita kwenye scanner kutokana na hali yake so akawa anafanyiwa ukaguzi wa kupapaswa kumbe alikuwa anazisokomeza ndani ya POP lililokuwa kwenye mguu wake

Bt duniani kuna makampuni yanayotengeneza fedha mengi yako nchi za ujerumani UK na Swiss bt yanakuwa controlled by Government so kama nchi inataka kutengeneza fedha zake wanatangaza tender za makampuni yana shindana ya mshindi anapata tenda ya kutengeneza malipo mnalipa Kwa dollars coz fedha nayo ni bidhaa inauzwa kama zilivyo bidhaa nyingine

Kwa Tanzania fedha zetu tunazitengenezea Germany na kusafiliswa kwenye containers mpaka kwenye port zetu then utaratibu wa custom ufanyika kuzitoa ni kama mizigo mengine inavyotolewa bt mzigo huu ni HVC high value cargo na ulinzi wake ni mkubwa sana kumbuka duniani kinacholindwa si fedha bt ni makaratasi ya kutengeneza fedha kwani tofauti ya fedha bandia na halali ni karatasi tu bt kila kitu vinaweza kufafana

Now macho yang meupe .
Ahsante kwa maelezo mazurii
 
Back
Top Bottom