BANDOKITITA
JF-Expert Member
- Oct 4, 2022
- 1,177
- 2,281
Kuna maswali mengi fikirishi juu ya uchipukaji huu wa kampuni za kitapeli (Scam companies) hapa Tanzania. Kampuni hizi ni pyramid/ponzi schemes na zimekuwa zikiwaumiza Watanzania sana, na pesa inayopatikana baada ya kukusanya kwa raia huenda kwenye mzunguko wa pesa nchini isivyo kihalali.
Kwa uchache zimekuwepo kampuni kama D9, SCATEC, KALYNDA, KIJIJI (tena hii imeanza juzi tu rarehe 29/09/2022 jijini Dar es Salaam) na nyinginezo nyingi. Hii ya KALYNDA ndio imezima juzi na kuwaacha watu na vilio.
Maswali ya kujiuliza:
1) Hivi serikali haijui uwepo wa uhuni huu hapa nchini? Nchi nyingi hasa Ulaya na Amerika walishapiga marufuku huu utapeli, maana unarudisha nyuma maendeleo ya watu wake.
2) Kama serikali inajua, je, imebariki Tanzania kuwa shamba la bibi? Yeyote toka nje au ndani anaweza kufanya atakavyo hata kuumiza raia kiuchumi pasipo kuguswa?
3) Kinachofanywa na hizi kampuni ni "ULAGHAI", je, serikali imeruhusu kitendo hiki ilihali ikijua kitendo cha utakatishaji fedha kinaua uchumi wa nchi?
4) Kama serikali haijaruhusu uhuni huu, je, hawa wenye kampuni wameizidi serikali akili na hivyo haina cha kuwafanya? Je, kati ya kampuni hizi na serikali nani ana mkono mrefu?
5) Je, serikali inapata mapato kutokana na kampuni hizi, kama inapata basi inajua kinachoendelea, kwa nini haichukui hatua?
6) Kampuni hizi zimekuwa zinatumia hadi vyombo vya habari vya humu ndani kama redio na TV mfano KALYNDA E-commerce imetumia redio nyingi tu na TV kama ITV. Je, serikali inaweza kusema haijui kinachoendelea?
7) Kwanini kampuni hizi zimeibuka kwa wingi wakati huu na wala sio hapo kabla? Huko nyuma zilikuja kadhaa na baadhi kuchukuliwa hatua na serikali. Mfano mzuri ni DESI. Kwanini sasa hatua hizo hatuzioni au ndio tuseme serikali haina taarifa?
NB:
a) Watu wamekuwa wakiwachukulia wanaoweka pesa kama wajinga na wapenda vya bure (mtelezo). Lakini ukweli ni kuwa wanaoingia katika mtego huu wa kitapeli wengine ni wasomi tena wenye elimu ya chuo kikuu. Hapa tukubali/tukatae tatizo hili linasabsishwa na hali ngumu ya maisha ya wananchi. Hivyo mtu anatafuta njia yoyote iwe halali/haramu kwa nia ya kujipatia kipato.
b) Tusiwanyooshee vidole wale wanaopigwa na hizi kampuni, kuna watu wengi wamelizwa kwenye biashara, ununuzi wa viwanja, nyumba, n.k, je hao nao ni wajinga?
c) Serikali ichukue hatua za haraka kunusuru watu wake na uchumi wa nchi. Iwakamate wamiliki wa kampuni hizi wasukumwe ndani na baadae mahakamani.
d) Kuwe na adhabu kali kwa wamiliki wa kampuni hizi za kitapeli, ikiwezekana adhabu iwe kunyongwa maana hata wao wamekuwa wanasababisha vifo ya mshituko wa moyo kwa ndugu zetu wanaowekeza pesa zao.
e) Serikali ikague kwa kina vibali vya wageni wanaokuja nchini kwa lengo la kufanya biashara, maana wengi wa watu wenye kampuni hizi watoka nje ya nchi hasa Nigeria na kwingineko.