Kampuni za Kitapeli Tanzania (Scam companies)

ANAYEJUA NAMNA YA KUTENGENEZA PLATFOM KAMA HIYO ANIFUNDISHE NICHUKUE ELA ZA WAJINGA .
 
Zipo microfinance zinazo sema uwatumie 10% ya kiasi unachotaka kukopa ndio ukope.
Ziogopeni Kama kaswende.
Kuna moja inajiifanya ni TAWI maana Kuna neno tawi tatika tangazo lao.
 
Kuna maswali mengi fikirishi juu ya uchipukaji huu wa kampuni za kitapeli (Scam companies) hapa Tanzania. Kampuni hizi ni pyramid/ponzi schemes na zimekuwa zikiwaumiza Watanzania sana, na pesa inayopatikana baada ya kukusanya kwa raia huenda kwenye mzunguko wa pesa nchini isivyo kihalali.

Kwa uchache zimekuwepo kampuni kama D9, SCATEC, KALYNDA, KIJIJI (tena hii imeanza juzi tu rarehe 29/09/2022 jijini Dar es Salaam) na nyinginezo nyingi. Hii ya KALYNDA ndio imezima juzi na kuwaacha watu na vilio.

Maswali ya kujiuliza:
1) Hivi serikali haijui uwepo wa uhuni huu hapa nchini? Nchi nyingi hasa Ulaya na Amerika walishapiga marufuku huu utapeli, maana unarudisha nyuma maendeleo ya watu wake.

2) Kama serikali inajua, je, imebariki Tanzania kuwa shamba la bibi? Yeyote toka nje au ndani anaweza kufanya atakavyo hata kuumiza raia kiuchumi pasipo kuguswa?

3) Kinachofanywa na hizi kampuni ni "ULAGHAI", je, serikali imeruhusu kitendo hiki ilihali ikijua kitendo cha utakatishaji fedha kinaua uchumi wa nchi?

4) Kama serikali haijaruhusu uhuni huu, je, hawa wenye kampuni wameizidi serikali akili na hivyo haina cha kuwafanya? Je, kati ya kampuni hizi na serikali nani ana mkono mrefu?

5) Je, serikali inapata mapato kutokana na kampuni hizi, kama inapata basi inajua kinachoendelea, kwa nini haichukui hatua?

6) Kampuni hizi zimekuwa zinatumia hadi vyombo vya habari vya humu ndani kama redio na TV mfano KALYNDA E-commerce imetumia redio nyingi tu na TV kama ITV. Je, serikali inaweza kusema haijui kinachoendelea?

7) Kwanini kampuni hizi zimeibuka kwa wingi wakati huu na wala sio hapo kabla? Huko nyuma zilikuja kadhaa na baadhi kuchukuliwa hatua na serikali. Mfano mzuri ni DESI. Kwanini sasa hatua hizo hatuzioni au ndio tuseme serikali haina taarifa?

NB:
a) Watu wamekuwa wakiwachukulia wanaoweka pesa kama wajinga na wapenda vya bure (mtelezo). Lakini ukweli ni kuwa wanaoingia katika mtego huu wa kitapeli wengine ni wasomi tena wenye elimu ya chuo kikuu. Hapa tukubali/tukatae tatizo hili linasabsishwa na hali ngumu ya maisha ya wananchi. Hivyo mtu anatafuta njia yoyote iwe halali/haramu kwa nia ya kujipatia kipato.

b) Tusiwanyooshee vidole wale wanaopigwa na hizi kampuni, kuna watu wengi wamelizwa kwenye biashara, ununuzi wa viwanja, nyumba, n.k, je hao nao ni wajinga?

c) Serikali ichukue hatua za haraka kunusuru watu wake na uchumi wa nchi. Iwakamate wamiliki wa kampuni hizi wasukumwe ndani na baadae mahakamani.

d) Kuwe na adhabu kali kwa wamiliki wa kampuni hizi za kitapeli, ikiwezekana adhabu iwe kunyongwa maana hata wao wamekuwa wanasababisha vifo ya mshituko wa moyo kwa ndugu zetu wanaowekeza pesa zao.

e) Serikali ikague kwa kina vibali vya wageni wanaokuja nchini kwa lengo la kufanya biashara, maana wengi wa watu wenye kampuni hizi watoka nje ya nchi hasa Nigeria na kwingineko.
Hapo kwa mnaigeria ni msomi kuwatapeli wasomi wenzie,mbona unalalama sana ndugu,imejikuta kwenye 18za mnaigeria au mkenya ndugu🏃🏃
 
Zipo microfinance zinazo sema uwatumie 10% ya kiasi unachotaka kukopa ndio ukope.
Ziogopeni Kama kaswende.
Kuna moja inajiifanya ni TAWI maana Kuna neno tawi tatika tangazo lao.
Sasa unaogopa kutoa tawi upewe mti🥱
 
Kumekucha
Rais Bado anapiga misele akijashtuka kila mtu ni taperi anapokelewa airport na vibaka wanampora hadi vile vihereni vyake..😅😅😅😅
 
BOT walishasema zamani sana kuhusu aina hii ya biashara ya utapeli mtandaoni. Yaani mnajiunga uchochoro ni huko halafu mnakuja kulalamika hadharani baada ya kuigwa. Who to blame zaidi ya udhaifu wenu wa kutaka pesa za miujiza?
Zinasajiliwa na serikali
 
Screenshot_20221009-125227.png
Screenshot_20221009-125341.png

Yaan hii site ukiingia tu ukaiangalia unagundua ni Scam sasa unaibiwa vipi

Alafu mbaya wamesajiri na mitandao ya kuweka Pesa TIGO TANZANIA na HALOTEL TANZANIA

Waanzie hapo na wafanywe km alichofanywa Mr Kuku
 
Pole sana, wakati mwingine utumie akili.
Nonsense to the highest level. Tunaongea kuliokoa Taifa mtu ananipa pole. Are you a great thinker.

Mtu anasema Serikali haijawatuma. Are you serious. Unajua majukumu na kazi ya serikali. Wewe unavyopigwa Kariakoo, kuuziana viwanja, nyumba na nk na ukakimbilia polisi Huwa umetumwa na polisi? Si Huwa unaenda mwenyewe na mapesa Yako.

Ulishajiuliza kwa nini ukifanya jaribio la kujiua ukanusurika unashitakiwa na Jamhuri wakati uhai ni wako mwenyewe. Kwani huwa unatumwa na serikali kujiua.
Kwanini ukimuua mtoto wako wakuzaa unashitakiwa na Jamhuri kwani ni Serikali imemzaa.

Great thinker must be open minded, sio kuropoka.
 
Kuna maswali mengi fikirishi juu ya uchipukaji huu wa kampuni za kitapeli (Scam companies) hapa Tanzania. Kampuni hizi ni pyramid/ponzi schemes na zimekuwa zikiwaumiza Watanzania sana, na pesa inayopatikana baada ya kukusanya kwa raia huenda kwenye mzunguko wa pesa nchini isivyo kihalali.

Kwa uchache zimekuwepo kampuni kama D9, SCATEC, KALYNDA, KIJIJI (tena hii imeanza juzi tu rarehe 29/09/2022 jijini Dar es Salaam) na nyinginezo nyingi. Hii ya KALYNDA ndio imezima juzi na kuwaacha watu na vilio.

Maswali ya kujiuliza:
1) Hivi serikali haijui uwepo wa uhuni huu hapa nchini? Nchi nyingi hasa Ulaya na Amerika walishapiga marufuku huu utapeli, maana unarudisha nyuma maendeleo ya watu wake.

2) Kama serikali inajua, je, imebariki Tanzania kuwa shamba la bibi? Yeyote toka nje au ndani anaweza kufanya atakavyo hata kuumiza raia kiuchumi pasipo kuguswa?

3) Kinachofanywa na hizi kampuni ni "ULAGHAI", je, serikali imeruhusu kitendo hiki ilihali ikijua kitendo cha utakatishaji fedha kinaua uchumi wa nchi?

4) Kama serikali haijaruhusu uhuni huu, je, hawa wenye kampuni wameizidi serikali akili na hivyo haina cha kuwafanya? Je, kati ya kampuni hizi na serikali nani ana mkono mrefu?

5) Je, serikali inapata mapato kutokana na kampuni hizi, kama inapata basi inajua kinachoendelea, kwa nini haichukui hatua?

6) Kampuni hizi zimekuwa zinatumia hadi vyombo vya habari vya humu ndani kama redio na TV mfano KALYNDA E-commerce imetumia redio nyingi tu na TV kama ITV. Je, serikali inaweza kusema haijui kinachoendelea?

7) Kwanini kampuni hizi zimeibuka kwa wingi wakati huu na wala sio hapo kabla? Huko nyuma zilikuja kadhaa na baadhi kuchukuliwa hatua na serikali. Mfano mzuri ni DESI. Kwanini sasa hatua hizo hatuzioni au ndio tuseme serikali haina taarifa?

NB:
a) Watu wamekuwa wakiwachukulia wanaoweka pesa kama wajinga na wapenda vya bure (mtelezo). Lakini ukweli ni kuwa wanaoingia katika mtego huu wa kitapeli wengine ni wasomi tena wenye elimu ya chuo kikuu. Hapa tukubali/tukatae tatizo hili linasabsishwa na hali ngumu ya maisha ya wananchi. Hivyo mtu anatafuta njia yoyote iwe halali/haramu kwa nia ya kujipatia kipato.

b) Tusiwanyooshee vidole wale wanaopigwa na hizi kampuni, kuna watu wengi wamelizwa kwenye biashara, ununuzi wa viwanja, nyumba, n.k, je hao nao ni wajinga?

c) Serikali ichukue hatua za haraka kunusuru watu wake na uchumi wa nchi. Iwakamate wamiliki wa kampuni hizi wasukumwe ndani na baadae mahakamani.

d) Kuwe na adhabu kali kwa wamiliki wa kampuni hizi za kitapeli, ikiwezekana adhabu iwe kunyongwa maana hata wao wamekuwa wanasababisha vifo ya mshituko wa moyo kwa ndugu zetu wanaowekeza pesa zao.

e) Serikali ikague kwa kina vibali vya wageni wanaokuja nchini kwa lengo la kufanya biashara, maana wengi wa watu wenye kampuni hizi watoka nje ya nchi hasa Nigeria na kwingineko.
Sijajuwa sheria zake,ila nasi wananchi ulimbukeni na uvivu vinatuponza kwa kutaka mafanikio ktk njia rahisi.Na yale madude ya kichina vipi?Na kwanini wanao miliki ni wachina tu?
 
Serikali ikachukua kodi yake nyie wengine mtajuana wenyewe,.! Kama hawa tatu mzuka na biko si matapeli watupu wanaopigiwa chapuo kwenye radio kubwa na tv.

Note. Wajinga huwa hawaishagi siku zote.
 
Mwwnye account Kalynda yenye kuanzia laki moja aje nimpe msaada buree apate pesa zake
 
BOT walishasema zamani sana kuhusu aina hii ya biashara ya utapeli mtandaoni. Yaani mnajiunga uchochoro ni huko halafu mnakuja kulalamika hadharani baada ya kuigwa. Who to blame zaidi ya udhaifu wenu wa kutaka pesa za miujiza?
Mnakosea sana mnapoiondoa serikali kulinda haki za watu eti sababu wakati wakijiunga hawakuihusisha!

Unataka kunieleza watu wanapoaminiana kisha kudhulumiana, kwanini huwa wanashitakiana kutaka haki ambayo serikali haikuwepo kwenye mwanzo wake?

Kama walivyokwisha sema wadau, kazi ya serikali ni kulinda haki za raia iwe imehusishwa ama haikuhusishwa.
 
Back
Top Bottom