Kampuni ya kukusanya madeni ya Marcas yatimuliwa kwa kuiba Mali za mteja katika hoteli ya Impala

nyamadoke75

Member
Apr 1, 2020
87
280
Mkurugenzi wa kampuni ya Marcas debt collectors, Richard Paul amekosa uaminifu na kutia aibu ya mwaka baada ya kampuni yake kufukuzwa kwenye tenda ya kuuza vifaa Mbalimbali katika jengo lililokuwa hotel ya Impala jijini Arusha baada ya kuiba vifaa vya mteja wake vya mamilioni ya fedha alivyokabidhiwa kupiga mnada.

Marcas ambaye amekuwa na sifa mbaya kupitia kampuni yake kwa kufanyakazi kitapeli na wakati mwingine kudhulumu watu na kujipatia Mali kwa njia ya udanganyifu, hivi karibuni alishinda tenda hiyo ya kuuza Mali za hoteli ya Impala na kufanikiwa kufanya mnada mmoja, lakini baada ya wahusika kukagua Mali zao na fedha zilizopatikana walibaini kwamba Mali nyingi hazipo eneo la mnada.

Walipofuatilia waligundua kwamba Marcas alihamisha Mali nyingi wakati wa kupakia kupeleka eneo la Mnada na kuzipitiliza kusikojulikana kupitia gari aina ya fuso.

Maboss baada ya kubaini hilo walimpiga chini na kumpatia tenda hiyo MTU mwingine na sasa wanatafuta ushahidi ili kumchukulia hatua.

Hotel ya Impala iliuzwa na benki ya NBC kutokana na Deni lililokuwapo, na kununuliwa na mfanyabiashara anayemiliki pia hoteli ya Morena iliyopo mjini Morogoro na sasa ameamua kuifanyia marekebisho kwa kubomoa baadhi ya majengo na kwamba baadhi ya thamani zilizokuwamo ndani ya hoteli hiyo ndio alizopewa kampuni ya Marcas kupiga mnada lakini kutokana na Tamaa ya fisi aliyonayo Richard Paul na bila aibu aliamua kuiba baadhi ya Mali hizo.
 
Hilo litakuwa dili la wafanyakazi pekee au mkurugenzi pia ana taarifa?
 
Back
Top Bottom