Kampuni za Kitapeli Tanzania (Scam companies)

Kampuni za Kitapeli Tanzania (Scam companies)

Nilichogundua Tanzania bado tuna safari ndefu sana ya kuchambua na kuelewa mambo kwa haraka na shida kubwa inakuja ni pale tunaposhindwa kutatua jambo bila kupata ushauri kwa rafiki.

Marafiki ndio tjnaingizana huko kwa sababu tunaamini ushauri ni bora kuliko kutumia akili yako.

Mdau anachosema ni muda sasa serikali kuokoa wananchi wake,maana wananchi wake uwelewa ni mdogo hivyo ni wazi wao kama serikali wabebe dhaman zote za kuwaokoa.

NILIVYOMUELEWA MM MTOA MADA NA SIO KWAMBA YEYE KACHEZA ILA ANATAKA SERIKAL KUWA MACHO DHIDI YA HAYA MAMBO.

"Maendeleo kwa wote,lakini maendeleo hayaji kwa kuwaibia kundi kubwa la watu.""
 
Changamoto ni umaskini unaotupelekea kudhani kuna kupata hela kwa urahisi bila ya kuvuja jasho!
 
Nchi hii jukumu LA kuijoambania Ni wewe mwenyewe. Kwa maslahi ya Umma huwezi kuina serikali.

Serikali utaiona ukigusa sharubu za Wanasiasa wenue madaraka au ukatae kulipa kodi.

Hayo makampuni yote ya kitapeli yanasajiliwa na serikali hiyo hiyo na kupewa vibali.

JATU iko mpaka soko LA his a, DSE.
 

Attachments

  • proxy.jpeg
    proxy.jpeg
    32.4 KB · Views: 16
  • download.png
    download.png
    122.3 KB · Views: 18
Nchi Kama Iran wamekamata wale promoter hapa bongo wapo kibao na wanawaangalia kama iyo kampuni Kuna jamaa kule twitter anaitangaza na kuingia kifua ni tapeli amejipa jina la mshauri serikali na kaweka bendera kabisa kumdanganya watu huyu ni WA kushughulikia kabisa.
Siku zote tapeli hutafuta fursa na kupanga karibu na TRA ndo fursa yenyewe
Hapo kwa mnaigeria ni msomi kuwatapeli wasomi wenzie,mbona unalalama sana ndugu,imejikuta kwenye 18za mnaigeria au mkenya ndugu
 
kuna watu serikalini watakuwa wanakula na matapeli. Ni jukumu la serikali kulinda raia wake. sasa mtu anaona kampuni imesajiliwa na inajitangaza, anajua kuwa ni halali na uwekezaji wake upo salama. kwenye hili huwezi kulamu ujinga wa watu bali serikali yenye kazi ya kuchunga masuala ya uwekezaji.
 
Kabla yakuingia kwenye haya mambo watu watafute ushauri wa kisheria. Tafuta wakili akushauri kitaalam kabisa lipa gharama z ushauri alafu kajilipue. Yakibumburuka wewe rudi kamalizane na wakili wako aliyekupa huo ushauri.

Ni rahisi ila ghali, ukija kwetu na sisi tutakupa gharama kubwa ya ushauri, alafu baadae hatutakushauri uingine kwenye.hio biashara, kama ukiingia uingie ukiwa unafahamu kuwa hatutahusika tena maana tulikupa.ushauri usiingie.

Kabla hujaingia kwenye hizo fursa jaribu kufuatilia yafuatayo:

1. Kama ni kampuni usajili wa BRELA hapa fanya Official search kabisa utalipa (20k)

2. Fuatilia TRA rekodi yao

3. Fuatilia TIC kama ni uwekezaji

4. Fuatilia BOT kama ni fedha

5. Angalia sheria zinazosimamia mambo wanayofanya hao watu, je wameendana na takwa la sheria husika?

6. Soma makubaliano yenu vizuri na uyaelewe

7. Kwa Apps soma terms, conditions na privacy policy vizuri na uielewe

8. Fuatilia, fuatilia, fuatilia

Mfano mdogo unaoendana na namba 5 hapo juu ni hii Kalynda, wanachofanya.ni jinai kwenye sheria ya makosa ya kimtandao Tz na bado watu wameingia kushiriki jinai, moja kwa moja unaona kabisa hii kampuni sio, sababu huwezi ruhusiwa kufanya jinai.

Jambo lingine ni vipi data za watu zinalindwa na hiyo Kalynda, sababu wanatumia data hizo.hizo kufanya watu.waamini bidhaa inauza (uongo/utapeli) wakati mtu ameweka tu comment na nyota tano kwenye bidhaa yaani na atakayenunua.hiyo bidhaa naye kaibiwa, kwa maana rahisi watu woote wanaofanya hiyo Kalynda nao ni waalifu maana wameshiriki ualifu.

Siku yakibumburuka wataambiwa wameshiriki uhalifu chini ya sheria ya makosa ya.kimtandao, sheria.ya utakatishaji fedha, kanuni ya adhabu na sheria ya kupambana na magenge ya uhujumu uchumi , alafu wataambiwa achaneni na hii mambo kabla hatujawashtaki. Watarudi makwao na vilio.
 
Kuna Salvation farm kwamba wanakulimia nchii hii
 
Back
Top Bottom