Kusema ukweli, vijana nchini wametengwa na wamechoka sana

Mtuflani Official

JF-Expert Member
Dec 31, 2019
1,938
4,354
Aisee kila ukizunguka nchini kote Tanzania. Vijana wana hali mbaya. Vijana wamesoma, ajira hakuna. Na sasa inasikitisha sana vijana wameingia kwenye shughuli za siasa. Wanatumika sana na wanasiasa kama “influencers” kujipatia umaarufu kwa pesa ndogo tu.

Kwanini serikali isiweke mikakati ya kuwakomboa vijana. Vijana wamekua wa hovyo, wanakimbilia kwenye siasa kisa wanadai kuna pesa “kitonga”. Hivi serikali inashindwa vipi kudhibiti wafanyakazi wa kigeni kwenye hizi kampuni hapa nchini. Tuwajengee waTanzania uwezo, wapate opportunity ya ku bargain mishahara, na mwisho wa pesa hizi zitatumika kuwekeza ndani.

Serikali inaruhusu hawa watu waje humu nchini na kufanya kazi ambazo zilitakiwa kufanywa na Watanzania. Pesa nyingi zinatoka nje ya nchi kwa sababu hawa raia wa kigeni wanalipwa kwa dola.

Watanzania wanaishia kulipwa vihela kidogo na wanashindwa kujengewa uwezo. Nawapongeza BOT kwa hatua ya kuamuru Microfinance zote nchini kutokutoa ajira kwa raia wa kigeni wasiozidi watano.

Hii ni hatua nzuri na serikali inapaswa kuweka sera ili kila kampuni ya kigeni ifuate huu muongozo. Hii itajengea uwezo waTanzania na itaipa pia serikali fursa ya kufahamu undani wa hizi kampuni na sio kama sasa mambo mengi yanafichwa.
 
Unaweza kumfikisha ng'ombe mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji!
Fursa za kupata hela ziko nyingi! Vijana hawazitaki wanataka wapate hela kwa mtelemko! Kubet, kamali kwa mashine za mchina, bodaboda! Hutoboi ng'o
 
Back
Top Bottom