Kampuni inayosimamia wrong parking DSM inatumia sheria gani kutoza faini? Ni kigogo gani anayewakingia kifua wasitoe control number?Nani mmiliki?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Kuna kampuni imeanzishwa au kupewa tender inayokwamisha biashara nchini kwa kigezo cha wrong parking

Kampuni hii imekuwa chanzo cha wageni kugoma kutumia bandari yetu au kupeleka image mbaya nje ya nchi.

Kampuni haitoi control number ya malipo wanayodai wateja, haina risiti ya uthibitisho wa malipo na haifuati taratibu za kisheria katika kutekeleza wajibu wake.

Watendaji wa kampuni hii mara kwa mara wamekuwa wakitishia madereva kuwaweka ndani pale wanapokataa kutii amri zao, wamekuwa wakikamata magari bila kuandika kosa lililotendwa na mwenye gari, wamekuwa na tabia ya kuhamisha gari pale walipokutana kwa lengo la kufuta ushahidi wa dhulma wanayofanya.

Katika utaratibu wa natural justice unapokuta kosa limetendeka hakuna ulazima wakukokota gari kutoka kosa lililotendeka bali unapaswa kukusanya ushahidi wako na kisha kuandika faini unayodhani ipo kisheria kisha kuacha gari iendelee kufanya kazi na malipo yatalipwa na kampuni au muhusika kupitia mifumo ya kampuni.

Lakini kwa kuwa hawa watu wapo chini ya kiongozi mkubwa serikalini wao wamekuwa wepesi wakukokota magari bila kujali muda unaopotea au hasara inayoingia kwenye kampuni husika na kwa kiburi cha mkurugenzi wao.

Jeshi la polisi lingekuwa linakamata magari na kuyapeleka kituoni shughuli si zingesimama? Sumatra na wadau wengine wameacha kabisa kuangaika na ukamataji badala yake wanaandika kosa then taarifa zinatumwa kwenye mifumo na usipolipa fedha husika mifumo imewezeshwa kutoza penalty za ucheleweshaji.

Kampuni hii imeripotiwa mara kadhaa TAKUKURU temeke lakini hakuna hatua wanazochukua kudhibiti cash transaction na negotiation wanazofanya vijana wa kampuni hii. Kushindwa kuchukua hatua kwa TAKUKURU TEMEKE maana yake wanakubaliana na malipo ya cash lakini pia wanakubaliana na mfumo huu wa ukwamishaji biashara katika bandari yetu.

Mapendekezo
1. Wamiliki wa hii kampuni wawekwenwazi ifahamike wanalindwa na nani.

2. Serikali ielekeze wahusika wa kampuni hii kusitisha mara moja kupokea fedha cash badala yake malipo yote yafanyike kwa control number

3. TAKUKURU wachunguze kubaini wale wote wanaotumia kampuni hii kujipatia fedha kinyume cha sheria bila kutoa risiti.

4. Serikali ipige marufuku ukokotaji wa magari kupeleka ofisi za kampuni husika badala yake kila anayekamatwa aandikiwe kosa na faini ikiwemo kupewa control number akamilishe malipo

5. Sheria iliyotumika kuweka viwango wa tozo kwa kampuni zifahamike kwani hatuwezi kuwa na nchi ambayo mtoa huduma binafsi anajipangia tozo zilizotambuliwa kisheria....tozo ya laki nne kwa wrong packing na laki tatu kwa gari za kuvuta magari siyo himilivu na zinasababisha rushwa kukithiri eneo la temeke.

6. Wakurugenzi wa halmashauri wanaodaiwa kupata mgawo binafsi kutoka kwenye kampuni hii wachunguzwe na kuondolewa ofisini mara moja.

7. TAKUKURU wawaite madereva wazungumze nao kwa lengo la kupata taarifa za mfumo wa wizi unaotumiwa na watendaji wa kampuni hii kisha wale watakaotajwa wachukuliwe hatua.

Tunasema haya kunusuru mgomo uliopangwa kufanywa na madereva jambo ambalo linakwenda kuchafua taswira ya nchi yetu kwa ulafi wa vigogo wachache wanaonufaika na rushwa hizi.
 
Sababu kubwa ya msiba wa Magufuli kujaza watu Ilikua ni hiyo, watu walililia tumeisha
 
Mkurugenzi TEMEKE tunakupongeza kwa kuwafutilia mbali makanjanja waliokuwa wanasumbua watumiaji wa barabara......TAKUKURU mmeshindwa kuwakamata au mnawaogopa ?
 
siku hizi hata parking fees haisomi kwenye mtandao.
inapaswa unapopaki gari wakiwa wakusanya ushuru kupiga picha walau upate taarifa.
unaweza kutembea na gar mwaka mzima huku unadaiwa hukui
 
Back
Top Bottom