Kampuni gani bora za mabasi Dar kwenda Mwanza?

Zamani super najmunisa ya mwanza tulidandia hapo kati shy-igunga sa tatu asb scania sa tisa tuko kibaha na jamaa anaomba site. Tukapigwa poo na dereva akawekwa ndani mpk sa tatu usiku.kisa hakutakiwa kuwepo pale mda ule, so ye yuko ndani si tunapiga miayo tu ndani ya basi.
Ila yule commando alipiga moto ile gari mpk harufu ya matairi unaskia nafkiri aliambiwa mchepuko unapigwa kule alipouacha.
 
Kama unataka bus roho mkononi panda Ally's.(zinakimbia hovyo) Kama unataka usafiri wa kistarabu,DarLux( Tanzanite) is the best.
 
Panda frester ndugu chuma inaingia 5 kasoro
Kumbe wanawahi Mkuu, Asee niliwahi panda super Sammy, tulitoka wa mwisho mwisho ubungo lakini yule dere alikuwa ni mjuba hatari yaani alikuwa analaza mshale ki professional huwezi amin tuliwapita wote japo kisbo alionekana kichwa ngumu lakin hakutia dafu asee tulifika saa 5 Mwanza.
 
Yale malori ya kisbo na kibo yameshindwa ligi ya mwanza?? Maana 2019 walikimbiza sana
Kisbo wamepunguzwa kasi na ujio wa vidhibiti mwendo...VTS. Na kuchelewa kwao kuhamia kwenye gari za kichina pia kumewashusha kidogo, zamani kwa bodi zao local wali rely on speed and time keeping. Now, speed imeshikwa na VTS, na ana local body, so hawana soko sana.

Plus ubovu wa magari...mengi ulikuwa unayakuta Nyegezi pale yameharibika..muda mrefu tu.
 
Anaweza kulala njiani kiutani utani tu...maan ni juzi tu hapa natoka mwanza nakutana nayo njian imeharbika ikiwa ni saa tano asubuhi na sio mbali kutoka ofisi zao za Mwanza so wakashidwa hata kuwaletea abiria gari nyingine...waza sasa saa tano bado wako mwanza Dar waliingia lini
 
Back
Top Bottom