Kampeni ya Ubunge Arusha Mjini - Batilda Burian Vs Lema

Kampeni ya Ubunge Arusha Mjini - Batilda Burian Vs Lema

KATI YA BATILDA NA LEMA YUPI ATIBUKA KIDEDEA?


  • Total voters
    52
Dawa/Mawe/AK47 na kila aina ya silaha ya kujikinga na KIJANI ni KURA yako 31/OCT/2010 tuu basi.
" Value your VOTE, Vote for Change "
 

Heshima kwako Nyumbu,

Mkuu hizi taarifa nilizisikia jana saa moja usiku nilikuwa maeneo ya Soweto napata kinywaji mleta habari alisema aliyepigwa ni kada wa CCM [mwanamke] kwakuwa aliyejeruiwa hakuwa Mama Dr Batilda sikufuatilia sana.Nasikia viongozi wa CCM na CHADEMA walikuwa kituo cha polisi jana usiku kushughulikia dhamana za wapenzi wao waliohusika moja kwa moja na sakata lenyewe.

Naambiwa kada wa CCM alivunjwa meno kadhaa kapelekwa Mt Meru kwa matibabu zaidi na utaratibu wa kupachika meno bandia unaandaliwa baada ya kupona majeraha.


Nimecheka sana!
Halafu ukute alilipwa Sh. 10,000/- tu!
 

Heshima kwako Gerad2008,

Mkuu tafuta sehemu niliposema Lema hana uhungwaji mkono wewe umesema 85 % sina tatizo hata kidogo tena ungeweza kuongeza 95%,hoja yangu imezungumzia ushiriki wa Lema kwenye tukio la ujambazi uliofanyika mwaka 1998.Mkuu Gerad2008 Mramba kaitia hasara serekali mabilioni ya fedha,serekali hii hii ya Kikwete imempeleka mahakamani usijekushangaa Mramba akashinda ubunge uko Rombo au asiposhinda utashangaa kapata kura nyingi tu.Mambo ya hovyo hovyo sana yanafanyika Tanzania wananchi wanaona ni mambo ya kawaida.

Mkuu Ngongo,

Mbona unatuchanganya sana na upenzi wako kwa Dk Batilda?
Kama kuna ushahidi kiasi hicho kuhusu Lema, ni kwanini hajapelekwa polisi mpaka sasa?
Mie ninavyojua angeshaswekwa rumande haraka ili apishe Dk Batilda awe mbunge. Kuna nguvu kubwa ya Lowasa na JK katika kampeni za Dk Batilda, hivyo wasingeshindwa kusweka rumande Lema ili kipenzi chao apite. Leo hii tunashuhudia matiumizi makubwa ya pesa hapo Arusha ili tu Batilda apite, kwanini wasimkamate Lema na kumweka ndani mchezo uishe?
Jibu ni moja: Tuhuma hizo ni za kupikwa na hazina msingi wowote. Baada ya uchaguzi hutazisikia tena!
 
Chonde chonde jihadharini na vurugu ili wasipate kisingizio
 
Mkuu Ngongo,

Mbona unatuchanganya sana na upenzi wako kwa Dk Batilda?
Kama kuna ushahidi kiasi hicho kuhusu Lema, ni kwanini hajapelekwa polisi mpaka sasa?
Mie ninavyojua angeshaswekwa rumande haraka ili apishe Dk Batilda awe mbunge. Kuna nguvu kubwa ya Lowasa na JK katika kampeni za Dk Batilda, hivyo wasingeshindwa kusweka rumande Lema ili kipenzi chao apite. Leo hii tunashuhudia matiumizi makubwa ya pesa hapo Arusha ili tu Batilda apite, kwanini wasimkamate Lema na kumweka ndani mchezo uishe?
Jibu ni moja: Tuhuma hizo ni za kupikwa na hazina msingi wowote. Baada ya uchaguzi hutazisikia tena!
Usihangae na Ngongo anachuki binafsi na Lema angalia post zake zote hakuna jema kwa Lema ana jaribu kumnadi Lyimo wa TLP lakini Ngongo amengudua jamaa hauziki hata kwenye ukweli unaomhusu Lema anaupindisha mfano Arusha Lema anakubalika kuliko mgobea yoyote kwa nafasi ya ubunge lakini Ngongo atakwambia Lyimo ndiyo anaekubalika hasa sombetini ambako kuna wapinga kura wapatao 30,000 lakini cha ajabu Lyimo akifanya mkutano watu 60 ni mbinde kuwapata na subiri siku lema akitangazwa kuwa mbunge wa Arusha mjini sijui atakuja na pumba gani?
 
Kama ni kweli hiyo ndiyo dawa yao. Ukiwapeleka polisi wataachiwa wale. Sasa unaniletea fedha ya kununua utashi wangu na hekima niliyo nayo unifanye zuzu nitakufanyaje? Mimi nakudunda tu na 31.10.2010 nakunyima kura pia. Unakuwa na fimbo ya kwanza ya kumwonyesha mume wako na familia wakuuguze majeraha ya pili kuwaonyesha watanzania kwamba tumechoka na CCM na mambo yao yote

Hapana hii siyo njia sahihi ya kuwaadhibu wanasiasa. Kumdunda mtu hata kama hukubaliani naye kimtazamo ni kosa la jinai na inabidi wananchi waelimishwe hivyo. Wakiendelea na utaratibu huu ile dhana inayoenezwa na CCM kuwa wapinzani wanapanga kumwaga damu itapata mshiko na itakuwa siyo kwa maslahi ya wapinzani na wapenda mabadiliko wote nchini.
 
Chonde chonde jihadharini na vurugu ili wasipate kisingizio

Kweli. Kipigo wanachotakiwa kupata hawa watoa rushwa ni kunyimwa kura za wananchi itakapofika tarehe 31/10/2010. Vitendo vingine vyovyote vya kuwapiga watu wenye mrengo tofauti wa kisiasa ni makosa ya jinai. Na wakiendelea wataipa nguvu ile hoja ya CCM ambayo tumekuwa tukiisikia miaka yote (tangu 1995) kuwa wapinzani wakipewa nchi watamwaga damu. Tumeshamsikia kinara wa CCM akitoa hoja hii bila kutoa ushahidi wowote. Sasa hizi vurugu zikiendelea zitawapa CCM ushahidi wa kuhalalisha kwa haya madai ya kinara wao ambayo mpaka sasa wananchi wameyachukulia kuwa ni uzushi tu.
 
hii inaonyeha ni jinsi gan watu wamechoshwa na utawala uliopo kwa kumbatia ufisadi na rushwa,mwisho wa ccm umekaribiakwan dalili ndo hizo zinajionyesha mapema.
 
Tumedanganywa vya kutosha, tumeonewa vya kutosha. Tumeibiwa vya kutosha.Sasa tunawaomba waondoke watuachie nchi yetu. Hizo walizotuibia nadhani zinawatosha.


Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha.
 
Chonde chonde jihadharini na vurugu ili wasipate kisingizio


Lakini hawa CCM wanatuchokonoa sana -- tena kimakusudi tu, wakijua vyombo vyao vya usalama -- kama vile polisi -- wakikaa kimya bila kuchukua hatua yoyote.
 

Heshima kwako Acid,

Mkuu mwendo wa kampeni Arusha ukiachiwa uendelee hakika Tarime nyingine itazaliwa Tanzania kwasababu ya upuuzi wa watu wachache sana.
nilijionea mwenyewe ushabiki usio na staha... arusha imekua kama kempu mbaya kweli!!! Jazba imeanza kutawala na hicho ndicho hasa ccm wanakitaka, very unfortunately wapinzani wameshindwa kusoma alama za nyakati

(Being a conspiracy theorist as i am, unaweza kukuta hata hayo mawe huyo mama kajitandika na vijana wake kutaka kuharibu mambo... joke)

eniwei, tusifike huko kwani njimbo la arusha kwa mbinu safi ni la wapinzani
 
Heshima kwenu,

Gari iliyokamatwa inasadikiwa ni usalama wa taifa [ikulu/ofisi ya waziri mkuu] wahusika walikuwa wanagawa khanga,tshirt,kofia na vipeperushi kwaniaba ya Dr Batilda.CHADEMA wakapigiwa simu walipofika eneo la tukio [Matevesi] wakalizingira gari na kuanza kutoa kichapo cha hatari polisi [FFU]walipofika eneo la tukio walikuta watuhumiwa katika hali mbaya sana.

Kwakuwa gari iliyokamatwa ni mali ya serekali [UWT] nina mashaka sana kama polisi watatenda haki au watakuwa na ubavu wa kuwashitaki wafanyakazi wenzao.Inashangaza sana role ya UWT badala ya kuangalia usalama wa taifa wanafanyakazi ya usalama wa CCM !.
 
ukweli lazima ubaki kuwa ukweli . lema hawezi kupata ubunge wa arusha . sababu ya kwanza ni skendo ile kupokea rushwa kutoka kwa felex mrema ili afute kesi ya uchaguzi na hile ya ujambazi wa ndugu zake na marafiki zake walio uwawa na polisi . kila mtuu arusha anajua skendo za lema . ingawa anapigiwa kura na mjomba wake (kileo wa ccm ) lakini haisaidii . tunajua wote ni thugs.
 
nakumbuka kuna wakati taarifa ya rushwa ilipelekwa au kuripotiwa, lakini hakuna hatua zilizo chukuliwa na huyo akida wa takukuru, sasa inawezekana watu wameona yatakuwa yale yale
 
kuna taarifa kwamba mgombea ubunge kwa tiketi ya ccm jimbo la arusha mjini amepigwa na wananci wenye hasira baada ya kuonekana akifanya vitendo vinavyoashiria rushwa maqeneo ya fire arusaha, ambako kimsingi ndiko alikozaliwa. Taarifa hii imepatikana kwa kupigiwa simu na mdau aliyepo arusha na ambaye pia ni kada wa ccm.
Tunaomba akina ngongo na paka jimmy watutaarifu zaid kuhusu tukio zima, maana nasikia hata gari yake imeharinbiwa na tayari taarifa ziko polisi......

Poleni wote mlioathiriwa na tukio zima

uzushi mwingine huo!!!! Yaani kwanza unadai kuna taarifa kwamba,,, halafu pili ili kusisitizia uwongo wako unapakazia ati kada wa ccm wa arusha ndie aliekupigia simu na kukupasha hizi!!!

Haya wewe kada wa chadema unashirikiana vipi na kada wa ccm? Tena kupashana habari za kumwaga damu za watu?
Jamani sasa na huu uchaguzi heri uishe tu! Maana kila siku tutapashwa uzushi tu, mara utasikia masanduku ya kura yameingizwa toka zambia, mara fulani kafa kumbe yuko hai, mara ccm wameshaiba kura kumbe hata uchaguzi haujafanyika!!!

Sasa chadema mukiambiwa kuwa munataka kuleta machafuko nchini kweli munasababu ya kukanusha? Mbona dalili zote zinajitokeza kuwa kila penye fujo na umwagaji damu chadema wanahusika mwaka huu!!!

Mbona hatusikii vyama vingine vikidai kumwaga damu isipokuwa chadema!!! Nani aliewaroga chadema uchaguzi huu!!! Mimi sitashangaa kusikia hivi karibuni kuwa kontena za silaha zimekamatwa bandarini zikiwa na stakabadhi za chama cha siasa!!!
 
Mshirazi unashangaza kweli ndugu. Nomba utisaidia aliyemwaga damu tarime, musoma, iringa na songea ni chadema au ni ccm? Wenye nia ya kumwaga damu ni yupi au huyu anayetumia serikali na halafu anashindwa kujitetea bila hoja za maana?
 
Back
Top Bottom