Uzinduzi wa Mama Samia Legal Aid Kampeni - Singida Januari 10, 2024

Venus Star

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
19,696
59,852
UZINDUZI WA MAMA SAMIA LEGAL AID KAMPENI - SINGIDA

Kampeni hii ni mahususi kwaajili ya kuwafikia na kutoa msaadabwa kisheria kwa Wananchi wote buree

Kampeni hii itahusisha utoaji wa Elimu ya kisheria na kusikiliza migogoro yote ya kisheria ikiwa ni pampja na mirathi, ardhi, ndoa na usajili pamoja na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa na mengineyo kwa Wananchi wote pasipo gharama yoyote.

Mgeni Rasmi;
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana
Waziri wa Katiba na Sheria

🗓️ 10 Januari, 2024
📍Viwanja vya Stendi ya zamani - Mkoani Singida
🕗 Saa 1 Asubuhi

Wananchi wote mnakaribishwa !

Tangazo hili limetolewa na Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.

#MSLAC
#SamiaLegalAid
#KatibaNaSheria
#MsaadaWaKisheria
#WizaraYaKatibaNaSheria
 
IMG-20240107-WA0003.jpg
IMG-20240107-WA0004.jpg
IMG-20240107-WA0006.jpg
IMG-20240107-WA0005.jpg
 
Ni kampuni ndiyo, imeanzishwa na serikali au private? Je Jina lenyewe haitakuwa chanzo cha uvunjifu wa sheria? Walioianzisha walikubaliwa kweli kutumia Jina la Mama Samia kama Rais na mkuu wa Serikali kweli? Kwamba Mama Samia anakwenda kupambana kisheria na wale polisi na vyombo vingine wanaovunja sheria?
Je, hakutakuwa na uoga kwenye kutoa maamuzi kule ustawi wa jamaii kwa vile Jina la Mama Samia imeshaingilia kati?
Itapendeza tukijua hiyo kampuni imeanzishwa na serikali au watu nje ya serikali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom