Kampeni ya kuikataa Vodacom

Kampeni ya kuikataa Vodacom

Yaani there's no time to wait. Washenzi kabisa hawa....
IMG_20190731_121216.jpeg
IMG_20190731_120421.jpeg
 
Hivi mfano uvamiwe na majambazi halafu huwezi kupiga simu polisi na huduma yako ya mawasiliano yamesitishwa kwa mda huo,kuna haja gani ya kutumia huo mtandao?hivi wale kina Membe na nape wanatumia mtandao gani
 
Mnaikataa leo tena kwa hayo tu?
Voda mwenyewe ni yule yule ..Mak..na imetumiwa kwa mengi tu...sasa hivi kategewa mumo mumo..kapatikana..ndio kelele mingi....

Utakatishaji fedha na mengineyo mengi ...ilikuwa kimya!
Hongera voda...mmebatiza kwa moto mbatizaji kwa maji!

Mwanzo wa mwisho huooo....pole pole!
Washamba wana ndabo kweli!
Wameshaharibu kote... kwa muundaji na muundwaji!
 
Habari zenu wana wa nchi na poleni kwa majukumu mbali mbali ya ujenzi wa taifa.
Baada ya tafakuli ya kina juu ya tukio la kukamatwa Mwandishi Erick Kabendera jana na Kufungiwa huduma ya mawasiliano ya simu yake na Vodacom nimeoma kuna mambo kadhaa yana tia simanzi sana juu ya Usalama wa raia yeyote kwa sasa hapa nchini.

Mwandishi Erick Kabendera anasema alipoona Mawasiliano yake yamefungwa aliwapigia vodacom na kuwauliza kulikoni? Vodacom wakamjibu kuwa wameagizwa na TCRA wafunge mawasiliano yake. Lakini baadae TCRA ambao ndio wenye jukumu la usimamizi wa Mawasiliano wakakanusha kuwa hawahusiki na tukio hilo na wala sio kazi yao kufungia watu mawasiliano.

Majibu ya TCRA yanatupa maswali magumu juu ya Mtandao wa Vodacom kama ifuatavyo.

1. Kwa nini Vodacom wanawaficha wahusika halisi waliotoa amri ambayo kama waliona ni halali?
2. Lengo halisi la kufunga mawasiliano ya mwandishi ni nini? Ili akitekwa asipatikane hewani na kuwasiliana na ndugu zake?

3. Kama mtuhumiwa anatafutwa na chombo cha usalama SIMU yake ikiwa hewani husaidia chombo cha usalama kujua mahali alipo na kumkamata kirahisi. Sasa Hawa Vodacom kumzimia Simu mtuhumiwa anaye tafutwa wana LENGO gani?

4.Makosa anayotuhumiwa Kabendera hayahusiani na mambo ya Mawasiliano kwa nini Vodacom wamfungie huduma mteja wao ambaye amelipia huduma?

Maswali haya yanatuonesha Vodacom sio Mtandao salama tena kwetu watanzania. Unashirikiana na wahalifu, watekaji, wauaji, na watesaji hapa mchini.

Pili Vodacom wameonesha dharau kubwa sana kwetu watanzania. Kama wanaweza kukufungia Mawasiliano mtu ambaye huna hatia ili udhurike na watekaji watashindwa kuvujisha habari zako?

Je, Pesa zetu tunazo ziweka huko M.PE.SA ni salama tena? Huwezi amka ukaambiwa akaunti yako imefungwa na pesa zako zimechukuliwa kwa maagizo toka juu?

Kitendo hiki hakipaswi kufurahiwa. Vodacom wanapaswa kuchukuliwa hatua na sisi wenyewe wananchi ili kulinda usalama wetu na kuwaonesha kuwa tumefedheheshwa sana na tukio hili.

Hatua za kuchukua ni hizi wana bodi.
1. Kuacha kutumia mtandao wa Vodacom na mitandao mingine kama hiyo inayo shirikiana na waharifu kutesa raia wema.

Vodacom wamejidhihirisha pasi na shaka kuwa ni hatari kwa usalama wetu hima hima tuchukue hatua haraka.
Asanteni.
chonde chonde, vunjeni laini zao, hamieni popote ili iwe funzo kwao, mimi sitaki kuwasikia kabisa hawa wapumbav
VODACOM ni sawa na SHETANI, DAMU YA AZORY, BEN SAA NANE, BOSI WA JUZI NA WALE WA VCIROBA WAO NDIO WALIKUWA WANAVUJISHA MAWASILIANO.
 
Habari zenu wana wa nchi na poleni kwa majukumu mbali mbali ya ujenzi wa taifa.
Baada ya tafakuli ya kina juu ya tukio la kukamatwa Mwandishi Erick Kabendera jana na Kufungiwa huduma ya mawasiliano ya simu yake na Vodacom nimeoma kuna mambo kadhaa yana tia simanzi sana juu ya Usalama wa raia yeyote kwa sasa hapa nchini.

Mwandishi Erick Kabendera anasema alipoona Mawasiliano yake yamefungwa aliwapigia vodacom na kuwauliza kulikoni? Vodacom wakamjibu kuwa wameagizwa na TCRA wafunge mawasiliano yake. Lakini baadae TCRA ambao ndio wenye jukumu la usimamizi wa Mawasiliano wakakanusha kuwa hawahusiki na tukio hilo na wala sio kazi yao kufungia watu mawasiliano.

Majibu ya TCRA yanatupa maswali magumu juu ya Mtandao wa Vodacom kama ifuatavyo.

1. Kwa nini Vodacom wanawaficha wahusika halisi waliotoa amri ambayo kama waliona ni halali?
2. Lengo halisi la kufunga mawasiliano ya mwandishi ni nini? Ili akitekwa asipatikane hewani na kuwasiliana na ndugu zake?

3. Kama mtuhumiwa anatafutwa na chombo cha usalama SIMU yake ikiwa hewani husaidia chombo cha usalama kujua mahali alipo na kumkamata kirahisi. Sasa Hawa Vodacom kumzimia Simu mtuhumiwa anaye tafutwa wana LENGO gani?

4.Makosa anayotuhumiwa Kabendera hayahusiani na mambo ya Mawasiliano kwa nini Vodacom wamfungie huduma mteja wao ambaye amelipia huduma?

Maswali haya yanatuonesha Vodacom sio Mtandao salama tena kwetu watanzania. Unashirikiana na wahalifu, watekaji, wauaji, na watesaji hapa mchini.

Pili Vodacom wameonesha dharau kubwa sana kwetu watanzania. Kama wanaweza kukufungia Mawasiliano mtu ambaye huna hatia ili udhurike na watekaji watashindwa kuvujisha habari zako?

Je, Pesa zetu tunazo ziweka huko M.PE.SA ni salama tena? Huwezi amka ukaambiwa akaunti yako imefungwa na pesa zako zimechukuliwa kwa maagizo toka juu?

Kitendo hiki hakipaswi kufurahiwa. Vodacom wanapaswa kuchukuliwa hatua na sisi wenyewe wananchi ili kulinda usalama wetu na kuwaonesha kuwa tumefedheheshwa sana na tukio hili.

Hatua za kuchukua ni hizi wana bodi.
1. Kuacha kutumia mtandao wa Vodacom na mitandao mingine kama hiyo inayo shirikiana na waharifu kutesa raia wema.

Vodacom wamejidhihirisha pasi na shaka kuwa ni hatari kwa usalama wetu hima hima tuchukue hatua haraka.
Asanteni.
Muda wa kulalamika umepita,. Washtakiwe ndio wataingia adabu
 
ungekuwa wewe Vodacom ukapewa amri kutoka huko zinakotoka ungekataa??

hebu acheni unafiki wakumnunia mnamjua voda mnamtwisha lawama bure tu.

haya mtoke voda muende wapi ttcl, Airtel, tigo, zantel Kati ya hao Kuna mwenye ubavu wakukataa maagizo kutoka huko yanapotaka
 
Kwa hiyo na wewe kwa akili yako unaona voda inaweza kufa sababu wateja watahama kwakuwa hawatunzi faragha zao?
. Zipi hasa?
1. Nimeongea kwa principle zaidi.

2. Vida inaweza kufa kwa sababu hiyo kama Watanzania wanajitambua.

3. Watanzania wengi hawajitambui, kwa hiyo Vida isipokufa sitashangaa.

4. Ni kawaida ya mtu asiyeelimika kujiona hana faragha.

5. Kila mtu ana faragha zake. Ni sehemu ya utu. Ndiyo maana tunavaa nguo na hatutembei uchi wa mnyama kama hayawani.
 
Back
Top Bottom