Kampeni Meneja wa Lowassa Ndani ya TAKUKURU

Kampeni Meneja wa Lowassa Ndani ya TAKUKURU

Nasubiri kwa hamu sana siku ndungai sita membe watakavyopanda kwa pilato h
 
Lowasa ameifilisi sana hii nchi kila ufisadi yumo hata lile jengo walilokodi SSRA wanaolipa kodi bilioni 600 ni lake..Angekuwa rais Taifa lingeangamia hili
Mkuu ni bilioni 600 au ni milioni 600? Je malipo hayo yalifanyika kwa kila baada ya muda gani?
 
Mbona Lowassa anacheleweshwa sana!! Au ndio kubwa la maadui kuuliwa mwisho wa muvi??
 
Eti efficient, huyo ni Kikwete, my foot!!
Hivi itatetea ujinga hadi lini, Faiza Fox???
 
Hongereni kwa propaganda mufilisi. Mnashtukia manyoya wakati kuku kesha liwa
 
Siyo Lowassa? Unafikiri dudu lilililomg'oa uwaziri mkuu ni moja tu? Ni mlolongo.

Kikwete alikuwa hapapariki katika maamuzi yake. Tartiibu lakini efficient.
Vipi na hii Kikwete alikuwa hapapaliki na maamuzi yake?

YAMEFICHUKA-- IKULU YA KIKWETE YANUFAIKA MIPESA YA ESCROW,NI ZILE ZA BENKI YA STANBIC,SOMA HAPA KUJUA
SELEMANI MAGARI

Jakaya-Kikwete1.jpg

Pichani ni Rais Jakaya Kikwete picha na Maktaba

MAJINA ya baadhi ya watu walionufaika na fedha za akaunti ya Escrow zilizowekwa katika akaunti ya Benki ya Stanbic jijini Dar es Salaam yameanza kutajwa,Chanzo changu kinafahamu.
Miongoni mwa majina ambayo vyanzo vyetu vimethibitisha kwamba yapo ni lile la mke wa mmoja wa vigogo wa ngazi za juu Ikulu (jina tunalihifadhi kwa sasa) ambaye anaelezwa kuchukua kiasi cha dola za Marekani milioni tatu (Sh. bilioni tano).
“ Tayari tunalo jina la mwanamke mmoja ambaye amefahamika kama mke wa mmoja wa watu wenye vyeo vikubwa Ikulu. Kwa sababu bado mapema kukupa jina kamili, vumilia kidogo hadi kila kitu kitakapokamilika,” kilisema chanzo cha kuaminika cha gazeti hili kinachoshiriki kwenye uchunguzi wa suala la namna fedha za akaunti ya Escrow zilivyolipwa kwa watu.
Chanzo chaetu linahifadhi jina la mwanamama huyo pamoja na mumewe kwa sasa kwa vile kuwataja majina kunaweza kuingilia upelelezi.
Wakati majina ya baadhi ya mawaziri, wanasiasa, majaji na viongozi wa dini yakionekana kulipwa fedha za mgao kutoka katika akaunti moja ya Benki ya Mkombozi, kumekuwa na kitendawili kuhusu ni akina nani hasa walilipwa fedha zilizokuwapo katika Benki ya Stanbic.
Wafaidikaji wengine wa akaunti hiyo ambao Chanzo chetu limefanikiwa kuwapata kwa sasa ni mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Rajiv Bharat Bhesania, anayetajwa kuwa mojawapo wa wasaidizi muhimu wa mmiliki wa kampuni ya Pan African Power (PAP), Harbinder Seth Singh.
Katika mojawapo ya miamala katika akaunti ya Stanbic iliyofunguliwa na PAP ambayo inaonekana katika ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Bhesania anaonekana kuchukua kiasi cha dola milioni moja (shilingi bilioni 1.6).
Mtu mwingine ambaye inaonyesha amefaidi fedha za akaunti ya PAP ni Mwanasheria wa PAP, Joseph Makandege, ambaye kampuni yake ya sheria ya Bulwark Associates imeonekana kupata malipo yakiwamo ya zaidi ya shilingi milioni 500 kwa nyakati tofauti.
Chanzo chetu kimefanya mawasiliano na mmoja wa wafanyakazi wa zamani wa IPTL aliyedai kwamba Rajiv pengine ndiye mtu anayefahamu vizuri zaidi mienendo na biashara nyingi zaidi za Sethi na kama Serikali inataka taarifa za mfanyabiashara huyo mtata; basi inapo pa kuanzia.
Ingawa PAC ilipendekeza Sethi akamatwe na kuhojiwa kutokana na tuhuma mbalimbali kama vile utakatishaji wa fedha, kukwepa kulipa kodi na udanganyifu, Raia Mwema limeambiwa kuwa mmiliki huyo wa PAP hayupo nchini kwa sasa.
“Kama Serikali inataka kupata chochote kutoka kwa Sethi inabidi wambane huyuhuyu Rajiv Bhesania. Yeye ndiye kila kitu kwa Sethi hapa Tanzania. Hata akitaka mambo yake yanyooke mahali huwa anamtumia huyu.
“Nafahamu si rahisi kusema kila kitu lakini nafahamu kwamba kama vyombo vya ulinzi vitambana kisawasawa, anaweza kutoa siri zote za Sethi na hatimaye Watanzania wakapata wanachokitaka,” alisema mfanyakazi huyo wa IPTL.
Malipo hayo yote yalifanyika katika kupitia katika akaunti namba 912 0000 12 52 94 ambayo ilifunguliwa tarehe 28 Novemba mwaka 2013 na kufungwa tarehe 14 Septemba 2014.
Ni katika benki hii ndiko ambako muamala wenye thamani ya shilingi bilioni 73.5 ulifanyika siku ya Januari 23 mwaka huu; muamala ambao sasa ndio unachunguzwa na vyombo vya ulinzi.
Ni katika siku hii ambapo ripoti za Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na ile ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), zilieleza kwamba kuna watu waliondoka katika ofisi za benki hiyo wakiwa na magunia yaliyojaa fedha.
“Kwa mujibu wa Takukuru baadhi ya watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa (Stanbic) wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, maboksi, magunia na lumbesa,” ilisema sehemu ya ripoti iliyowasilishwa bungeni na PAC.
Muamala huo unachunguzwa vikali na Takukuru pamoja na ule wa Februari, 2014 katika Benki ya Mkombozi jijini Dar es Salaam ambapo kiasi cha shilingi bilioni 3.3 zinadaiwa pia kuchukuliwa kwa siku moja.
Habari za mke wa mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa Ikulu kuhusishwa na uchotaji wa fedha za Escrow inakuja katika kipindi ambacho Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akidai bungeni kwamba ofisi hiyo ya juu nchini ina mkono katika utolewaji wa fedha hizo kutoka Benki Kuu ya Tanzania.
Wakati akizungumza bungeni, Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, alimtaja Prosper Mbena ambaye ni Katibu wa Ofisi ya Rais (Ikulu), kuwa ndiye aliyeandika barua ya kuruhusu fedha zilizokuwa zimehifadhiwa zitolewe katika akaunti hiyo.
Habari hizi za Stanbic kuhusishwa na fedha za Escrow zimesababisha benki hiyo kumpa uhamisho aliyekuwa Meneja wake, Paul Omara, ambaye sasa anadaiwa kurejeshwa nchini Uganda.
Omara anaelezwa kuitumikia benki hiyo kwa muda wa miaka zaidi ya 11 na Raia Mwema limeelezwa kwamba ofisa huyo tayari amehojiwa na Takukuru kuhusu suala hilo kabla hajaondoka.
Mmoja wa maofisa wa Takukuru aliyezungumza na Chanzo chetu kwa masharti ya kutotajwa jina kwa maelezo kwamba uchunguzi unaendelea, alisema wamepata ushirikiano mzuri kutoka Stanbic na kuna uwezekano kwamba “ watu watakula Krismasi wakati tayari Takukuru ikiwa imemaliza kazi”.

Suala la fedha za Escrow lililiteka Taifa wiki iliyopita na sasa wananchi wanasubiri kwa hamu hatua itakayochukuliwa na serikali kuhusu vigogo wanaotajwa kusaidia kutokea kwa kashfa hii.
Chanzo ni Gazeti la Raia Mwema
 
Magufuli lazima ainyooshe nchi.

Katika hili hapa chini Waziri aliyehusika na upotevu huu wa fedha alikuwa nani? je pilika zote za utumbuaji MAJIPU kwa nini Wizara ya Ujenzi na Miundombinu haijaguswa? ni wazi unashabikia ujinga huku yanayofanyika ni maigizo(Komedy)

Dodoma. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amewasilisha ripoti tano za ukaguzi wa fedha kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2014 akibainisha ufisadi wa zaidi ya Sh600 bilioni katika maeneo mbalimbali na matumizi ya fedha ambayo hayana maelezo ya kutosha.

Ukaguzi huo ulifanywa katika Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, mashirika ya umma, miradi ya maendeleo na ufanisi wa maeneo mbalimbali.

Ripoti hizo zinaonyesha jinsi watumishi hewa wa umma wanavyoendelea kulipwa mishahara, wakiwamo wa balozi za Tanzania waliostaafu, misamaha ya kodi na ukiukwaji wa ununuzi na matumizi yasiyoeleweka ya fedha katika Wizara ya Ujenzi na Kitengo cha Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Amina Mwidau na Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Rajab Mbaruk Mohamed walizichambua ripoti hizo na kueleza jinsi watumishi wa Serikali wanavyotafuna mabilioni ya fedha.

Akizungumzia ripoti hiyo katika mkutano wa pamoja na CAG, Mwidau alisema imeonyesha jinsi Sh285 bilioni za Kitengo cha Maafa zilivyotafunwa licha ya kuwa zilitengwa kwa ajili ya kufanya shughuli maalumu.

Kuhusu Wizara ya Ujenzi, alisema ililidanganya Bunge baada ya kueleza kuwa Sh262 bilioni zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara, kitu ambacho kimebainika kuwa siyo kweli.

“Ukaguzi unaonyesha kuwa fedha hizo zimetumika katika mambo mengine kabisa, yaani zimetumika tofauti na hakuna maelezo ya kuridhisha,” alisema Mwidau huku akifafanua kuwa wizara hiyo inadaiwa na makandarasi Sh800 bilioni.


Misamaha ya kodi


Profesa Assad alisema ofisi yake ilibaini kasoro katika mfumo wa ufuatiliaji wa misamaha ya kodi na kusababisha ukiukaji wa matumizi iliyotolewa kwa mafuta yanayotumika migodini.

Alisema mafuta yenye kodi ya Sh22.33 bilioni yaliyotakiwa kutumiwa na kampuni zilizosamehewa kodi, Geita Gold Mine na Resolute TZ Ltd, yalipelekwa kwa makandarasi wasiostahili msamaha na kusababisha hasara ya Sh22.33 bilioni,” alisema.

Alisema pia misamaha ya kodi kwa malengo tofauti na yaliyokusudiwa, ilitolewa na kusababisha upotevu wa Sh392.7 milioni katika Kampuni ya Kiliwarrior Expeditions Ltd ya Arusha iliyokuwa imesamehewa kodi Sh465.2 ili kuingiza magari 28.

Hata hivyo, alisema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kati ya hizo kukusanya Sh72.5 milioni.

Pia, alisema misamaha ya Sh53.4 milioni ilitolewa kwa Kampuni ya Kilemakyaro Mountain Lodge Limited kwa ajili ya mradi wa ujenzi na upanuzi hoteli katika Kijiji cha Changarawe wilayani Karatu, lakini kampuni iliagiza magari matatu kwa kutumia msamaha na mengine matano ‘kuchepushwa’.

“Hata hivyo, ukaguzi ulithibitisha ununuzi wa gari moja tu ya Hyundai Santa. Magari mengine matano aina ya BMW na Toyota Land Cruiser Prado hayakufahamika yalipo,” alisema. CAG aliishauri Serikali izibe mianya ya upotevu wa kodi kupitia misamaha ya kodi aliyobaini katika ukaguzi wa mwaka huu, ikiwa ni pamoja na kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa misamaha ya kodi iliyotolewa.
 
Siyo Lowassa? Unafikiri dudu lilililomg'oa uwaziri mkuu ni moja tu? Ni mlolongo.

Kikwete alikuwa hapapariki katika maamuzi yake. Tartiibu lakini efficient.
EL anaingiaje hapa? Skandali hii imetokea miaka 2 iliyopita wakati EL alishaachia ngazi miaka kadhaa iliyopita! Naona mzimu wa Lowassa utawatesa kwa miaka mingi ijayo.
 
Jamani lini LOWASSA ataanza kula ugali wa Bure huko KEKO. Waiting in vain.
 
Mimi yote tisa kumi nasubiri siku papa la ufisadi lenyewe Lowasa likishikwa na kupelekwa Kisutu halafu kupewa ndoo kupelekwa Mahabusu bila ya dhamana hiyo siku ikifika najua sasa haki itakuwa imetendeka TanZania, na kufunga ukurasa wa ufisadi rasmi na kuanza kujenga TZ yetu mpya ya bila mafisadi!!
Nakubaliana na wewe kabisa Maana Lowasa ndiyo mwalimu wa mafisadi tanzania.
 
Anayesubiri Lowassa Mahakamaani hajui seikali Magufuli anachopambana nacho !!
Watuhumiwa wa EPA ESCRO wako wazi kuliko lakini hana jeuri kwa sababu kila
Mbunge wa Ccm akiwemo.yeye Maguf aligawaiwa kwa ajili ya kampeni

sembuse Richmond amabayo hata Lowassa hajahusika wala hakutajwa na bunge !!

Mtasuburi sana !
We nyumbu muongo wa kutupwa kabisa.
 
Back
Top Bottom