Ruhusa ya mikutano ni mtego kwa CHADEMA

Ruhusa ya mikutano ni mtego kwa CHADEMA

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
23,942
Reaction score
29,299
Ruhusa hii imetolewa na jeshi la polisi ambao hawakukataza mikutano! Mikutano ilikatazwa na waziri wa mambo ya ndani.

Hivi sasa kuna ukamataji ambao huenda umelengwa kwa wafuasi wa Chadema, kinachokosekana ni viongozi wake na njia ya kuwapata ni kupitia majukwaa ya mikutano, hali ya kisiasa kwa hivi sasa ni tete kwani kila neno jukwaani linaweza kukutia matatani hata kama si kosa, ila dhamana haipo kwa utashi tu wa wakamataji!
 
Waziri ndo anaakiiwa kutoa tamko japo alivunja katiba hakuna kifungu kinaruhusu waziri kuzuia mikutano ya kisiasa kwa sababu zake binafsi au Katambi kaona aibu kutoka kuruhusu mikutano angeoneka homnanzo japokua yote yanawezekana anatumia police kutengua kauli ya ovyo je kuna barua kutoka kwa IGP wa police Wambura kuruhusu mikutano?
 
Pumbavu, ccm hawataki kusikia ukweli, ukisema ukweli ni ugaidi
1+1=2, Ukisema hivyo ni kosa, inabidi useme ni 11.
.
Na kwa elimu yangu, ni kiumbe mmoja tuu ambaye yeye na uongo ni damu damu mpaka akaitwa baba wa uongo.

Kwa kiumbe kisichotaka ukweli, maana yake kinataka na kinapenda uongo.

Baba wa uongo ni shetani, hivyo kama CCM ni baba wa uongo, maana yake CCM ni .....
 
4. MASHARTI NA MUDA MAALUMU KUTOKA COMMONWEALTH CMAG(The Ultimatum)

Kutokana na mapendekezo ya Mjumbe Maalum, CMAG imetoa maelekezo yenye ukomo wa muda (Time-bound actions) kwa Tanzania:

Ndani ya Siku 30: Kutatua suala la kushikiliwa kwa Tundu Lissu kupitia njia za kisiasa au kisheria, na kuwaachia wengine wote wanaoshikiliwa kwa kutumia haki zao kwa amani.

Ndani ya Siku 60: Kurejesha upatikanaji kamili wa mitandao ya kijamii na kuacha vitisho dhidi ya vyombo vya habari na watetezi wa uhuru wa kujieleza.

Ndani ya Siku 90: Kuitisha jukwaa shirikishi na la kuaminika la vyama vya siasa (likiongozwa na mwezeshaji huru) kujadili mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi, ushindani wa kisiasa, wafungwa, na uwajibikaji.

Bila Kuchelewa: Kuanza uchunguzi huru wa makosa ya jinai uliopendekezwa na Tume ya Uchunguzi, pamoja na fidia kwa wahanga.

MWISHO WA UBAYA NI AIBU.
 
Selikali imefyata mkia mashart ya Jumuia ya madola.

HAMTASIKIA TENA.
1. Utekaji.
2. Mauaji.
3. Ukiukwaji wa katiba.
4. Kubambikizwa kesi za Ugaidi, Uchochezi, uhaini
5. Zuio la mikutano ya kisiasa
6. Wafungwa wa kisiasa.
 
Selikali imefyata mkia mashart ya Jumuia ya madola.

HAMTASIKIA TENA.
1. Utekaji.
2. Mauaji.
3. Ukiukwaji wa katiba.
4. Kubambikizwa kesi za Ugaidi, Uchochezi, uhaini
5. Zuio la mikutano ya kisiasa
6. Wafungwa wa kisiasa.
Waanze na kumwachia yule Simba aliyeanza kupewa jina la simba wa kizimkazi na baadae kweli wamemzuia ndani ya fensi halafu maisha mengine yaendelee.
 
Hivi hakuna namna ukawa jukwaani ukasema maneno ya upinzani bila kuzua utata, yaani bila lugha za kichochezi wala matusi?
Kama lugha ipi? Weka mfano. Jukwaani ni sehemu ya vyama kushambuliana, bahati mbaya chama kimojawapo kishambuliwapo polisi hukikingia kifua na kulifanya shambulizi hilo ni dhidi ya serikali! Hali hii ndiyo imeifanya Tanzania kuwa nchi ya hovyo kwenye siasa ambayo sasa ni kazi hatarishi licha ya kupungua kwa ukamataji, utekaji na mauaji ya kifahari yaliyokuwa yakifanyika kila siku, wameshiba.
 
Selikali imefyata mkia mashart ya Jumuia ya madola.

HAMTASIKIA TENA.
1. Utekaji.
2. Mauaji.
3. Ukiukwaji wa katiba.
4. Kubambikizwa kesi za Ugaidi, Uchochezi, uhaini
5. Zuio la mikutano ya kisiasa
6. Wafungwa wa kisiasa.
Zuio bado lipo palepale kwani lilitolewa na waziri mambo ya ndani, halikutolewa na polisi ambaye yuko chini ya waziri kiutendaji.
 
Mmeona hamna cha kuongea mnaanza kutafuta sababu.
 
Back
Top Bottom