Kampeni Kupinga 'chenji' ya fedha za Radar wasipewe tena Serikali

Kampeni Kupinga 'chenji' ya fedha za Radar wasipewe tena Serikali

WanaJF tuache kulalamika tuchukue hatua! Fedha za radar serikali inazotaka irudishiwe ni dhuluma tupu! Tuandike emails, sms , piga simu hata kwa kiswahili kupinga serikali isipewe fedha ilizoitoa kwa ufisadi. Hapa nimeweka anwani za BAE wanashughulikia namna fedha hizo zinaweza kurejeshwa kwa wananchi wa Tanzania ili ziwanufaishe. Andika kwa mfano: Mimi ni mtanzania napinga sina imani na serikali kufanya matumizi bora tafadhali fedha hizi zirudishiwe umma kupitia NGOs

Leonie Foster, BAE Systems
Tel: +44 (0)1252 383777 Mob: +44 (0)7540 630168
Leonie.foster@baesystems.com

jamani lets think twice
hivi naomba mnijuze ni NGO gani safi hapa bongo inayotumikia vizuri wananchi? maana naona ni kama mtu anaruka mkojo na kukanyaga m...........i
labda mniambie kuwa mnataka hela hiyo ibaki Uingereza. au wapewe CDM
 
Haki Elimu, TAMWA, TGNP niambie serikali ilitumiaje fedha zilizorudishwa za EPA au Stimulus Package!
 
Nna uhakika wanao i support hii nyuzi wote ni Chadema. Na walifanyalo hawalijui.
 
WanaJF tuache kulalamika tuchukue hatua! Fedha za radar serikali inazotaka irudishiwe ni dhuluma tupu! Tuandike emails, sms , piga simu hata kwa kiswahili kupinga serikali isipewe fedha ilizoitoa kwa ufisadi. Hapa nimeweka anwani za BAE wanashughulikia namna fedha hizo zinaweza kurejeshwa kwa wananchi wa Tanzania ili ziwanufaishe. Andika kwa mfano: Mimi ni mtanzania napinga sina imani na serikali kufanya matumizi bora tafadhali fedha hizi zirudishiwe umma kupitia NGOs

Leonie Foster, BAE Systems
Tel: +44 (0)1252 383777 Mob: +44 (0)7540 630168
Leonie.foster@baesystems.com

K
ama hujaona hii thread tafadhali bofya hii link hapo chini. Lengo letu ni mmoja:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-not-return-radar-money-to-tz-government.html

nadani tufike wakati na kujadili ni NGO gani zinatakiwa zipewe fedha hizi au fedha hizi ziende wapi tusije fika wakati tukapewa fedha hizi lakini zikaelekezwa kwenye NGO za ususi wa wanawake au zikapelekwa kwenye NGO ambazo wafanyakazi wake wengi ni wageni kwahiyo zikarudi mikononi mwa wageni. pia kwa mifumo yetu ya NGO ni mibovu sana kwani zimekuwa ni sehemu za wachache kuchuma.

mimi nashauri fedha hizi ziende moja kwa moja kwenye barabara au kujenga ili kupunguza hadha ya usafiri
 
Nna uhakika wanao i support hii nyuzi wote ni Chadema. Na walifanyalo hawalijui.

FF sio wote wanaounga mkono ni Chadema. Hapa Watanzania tuliibiwa kwa kuuziwa radar mbovu na ambayo hatukuhitaji in the first place. Hapa kinacholipwa ni fidia ya £29.5 million kwa wananchi wa Tanzania. Sio kwa wananchi wanaounga mkono chama cha Chadema. Kama kweli serikali ina uchungu na hili suala kwanza kabisa ingewashughulikia wale wote waliohusika. So far hakuna hata mmoja aliyeshughulikiwa. Kama Mh membe ana uchungu na hili suala angedai full repayment ya £40 million tulizolipia ile radar. Badala yake anang'ang'ania reparations. Wapi na wapi.
 
nadani tufike wakati na kujadili ni NGO gani zinatakiwa zipewe fedha hizi au fedha hizi ziende wapi tusije fika wakati tukapewa fedha hizi lakini zikaelekezwa kwenye NGO za ususi wa wanawake au zikapelekwa kwenye NGO ambazo wafanyakazi wake wengi ni wageni kwahiyo zikarudi mikononi mwa wageni. pia kwa mifumo yetu ya NGO ni mibovu sana kwani zimekuwa ni sehemu za wachache kuchuma.

mimi nashauri fedha hizi ziende moja kwa moja kwenye barabara au kujenga ili kupunguza hadha ya usafiri

wazo lako ni sahihi kabisa, NGO za bongo ni mali banafsi za watu
kama nia ni kwamba ziwafikie wananchi kupitia NGO, inamaana tunaongelea NGO zinazotoa mikopo kama PRIDE au BAYPOT nk. nyingine kama HAKIELIMU ni za kiutafiti zaidi. sasa je zikipelekwa PRIDE au BAYPOT si ndiyo itakuwa shida zaidi? hatutaisha kulalamika
 
WanaJF tuache kulalamika tuchukue hatua! Fedha za radar serikali inazotaka irudishiwe ni dhuluma tupu! Tuandike emails, sms , piga simu hata kwa kiswahili kupinga serikali isipewe fedha ilizoitoa kwa ufisadi. Hapa nimeweka anwani za BAE wanashughulikia namna fedha hizo zinaweza kurejeshwa kwa wananchi wa Tanzania ili ziwanufaishe. Andika kwa mfano: Mimi ni mtanzania napinga sina imani na serikali kufanya matumizi bora tafadhali fedha hizi zirudishiwe umma kupitia NGOs

Leonie Foster, BAE Systems
Tel: +44 (0)1252 383777 Mob: +44 (0)7540 630168
Leonie.foster@baesystems.com

K
ama hujaona hii thread tafadhali bofya hii link hapo chini. Lengo letu ni mmoja:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-not-return-radar-money-to-tz-government.html

Mkuu nimekusoma, I AM IN.
 
Nna uhakika wanao i support hii nyuzi wote ni Chadema. Na walifanyalo hawalijui.

Wewe mawazo yako yatakupotosha sana. Tofautisha ushabiki wa chama, na upiganiaji wa maslai ya wananchi. Umewahi ona wapi fisi akipewa kazi kuchunga Butcher?. Hizi fedha si sahihi kupewa selikari ya kisadi.
 
Nna uhakika wanao i support hii nyuzi wote ni Chadema. Na walifanyalo hawalijui.

Waliotumwa na CCM kuchafua mijadala hapa jamvini. Haanzishi mada, huchafua za wenzake! Shame on you
 
Nna uhakika wanao i support hii nyuzi wote ni Chadema. Na walifanyalo hawalijui.
Natumaini haujachakachuliwa akili! Hili halihitaji kuwa CDM kuliona, linahitaji upeo fulani na uzalendo na utanzania tu. Kupinga kila hoja nikukosa maono au nikuchakachuliwa kiakili au wazanzibari husema umenyweshwa maji ya bendera!

Miaka 50 uhuru maisha ya umaskini usiokifani bado hatujiulizi maswali magumu tu! Bado tunashabikia ufisadi? Naomba nikulize, da Faiza kwa faida ipi? U-CCM, Ushabiki Udini, Unazi, kukosa uelewa au nini au basi tu? Nenda hospitali ya Mwananyamala wajawazito wanalala chini serikali inatoa misamaha ya kodi kwa makampuni ya madini amabayo ni tajiri mara kumi ya serikali tena kwa miaka 10! Sipendi kusema neno baya juu yako lakini ningefurahia kusikia mantiki yako? "unchain your mind from slavery" = "kata minyororo ya utumwa wa fikra" aliimba Bob Marley
 
BAE nao pia ni wezi tuu kama our tainted tz gov.
Mi nadhani kama wanataka kuwapa NGO then fedha wapewe serikali ya uingereza halafu wao ndio waratibu huo ugawaji.
La sivyo kwa hiyo E-mail BAE systems wanaenda Bar kunywa vodka kazi ishaisha.. mkono huu unatoa halafu unapokea na mwingine.

Basi
 
Serikali imeumbuliwa bungeni ikidaiwa kuwasilisha taarifa za uongo kupitia Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu ugawaji wa madawati yaliyonunuliwa kwa ‘chenji ya rada'.
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu alitoa tuhuma hizo jana, wakati akichangia mjadala wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/2014, akisema Serikali imewadanganya wabunge kwa kuwa hakuna kitu kilichofanyika.

Alisema katika majibu ya Serikali kumekuwa na mkanganyiko mkubwa kwa kuwa imetangaza kununua madawati 93,740 na kuyagawa katika halmashauri mbalimbali nchini wakati siyo kweli.

Alisema kwa mtindo huo, Serikali imelidanganya Bunge pamoja na Watanzania kwa kuwa imetangaza madawati hewa ambayo hayapo.

"Wabunge kama kweli mnatimiza majukumu yenu na hampo hapa kwa masilahi yenu tu, hebu hojini halmashauri zetu zimepelekewa haya madawati 93,000 yanayozungumzwa humu au mnapiga makofi tu? Serikali inadanganya tunatakiwa tuihoji tuiwajibishe," alisema.

Lissu ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alitoa mfano wa mgawo huo kwenye Halmashauri ya Ikungi, Singida kwamba ilitangazwa kupelekewa madawati 508 lakini amekwenda jimboni na hakukuta dawati hata moja.

Alisema uchunguzi wake umebaini kuwa hata katika wilaya mbalimbali ikiwamo ya Iringa, hakuna kitu kama hicho.

"Jana sikuwa hapa bungeni nilikwenda kwenye halmashauri yangu, hakuna dawati hata moja. Hata Halmashauri ya Iringa kwa Mchungaji Msigwa (Peter) hapa ananiambia hakuna dawati hata moja, mnatudanganya ili iweje?" Aliwashauri wabunge wengine kufanya utafiti katika maeneo yao iwapo kuna madawati ambayo yamepelekwa kutokana na fedha zilizorejeshwa na Serikali kama chenji ya rada.

Lissu alisema ni maneno matupu ambayo yamekuwa yakiwahadaa wabunge na kuwafanya wasahau wajibu wao wa kuisimamia Serikali na kujikuta ni washangiliaji wakati wote. Lissu alisema kinyume na taarifa hizo za Waziri Mkuu, Bunge jana lilikuwa limeelezwa na Naibu Waziri (hakumtaja) kuwa madawati hayo hayajagawanywa.

Katika kipindi cha maswali na majibu, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Kassim Majaliwa akijibu swali la nyongeza la Ibrahim Sanya (Mji Mkongwe - CUF), kuhusu madawati hayo, alisema kwa kuwa madawati hayo bado yanagawanywa, watakaa na kuangalia utaratibu mzuri wa kuyafikisha Zanzibar.

Lissu pia alisema fedha ambazo zilitajwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospter Muhongo kuwa ni pato la Watanzania ni uongo kwa kuwa ni mali ya wamiliki wa migodi.

Alisema takwimu za waziri zimesababisha Watanzania kuamini kuwa wameingiza fedha nyingi ilihali kiasi kilichoingia hakifikii hata asilimia 10 ya pato la wawekezaji
Awali, akichangia mjadala huo, Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhanga Mpina alielezea hofu yake kuhusu maendeleo ya mifuko ya hifadhi ya jamii kwamba inaweza kufa kutokana na Serikali kutokuilipa madeni yake.

"Mifuko ya hifadhi ya jamii itakufa kutokana na kuidai Serikali madeni mengi makubwa. Kuna haja ya kuangalia jinsi ambavyo tunaweza kuishauri Serikali kwa suala hili," alisema Mpina.

Mbunge huyo alielezea kukerwa kwake na matumizi ya Dola ya Marekani badala ya Shilingi katika malipo mbalimbali, jambo ambalo linazidi kushusha thamani ya Shilingi.

"Watu wanakuja na Dola wanatumia na wanaondoka nazo bila hata kuzibadilisha, basi ni vyema kama tunaona fedha yetu haifai tuiondoe tutumie hizo Dola," alisema Mpina.

Aliikosoa Serikali akisema haijawahi kufanya mdahalo wa kina kujadili jinsi matumizi ya Dola yanavyoiathiri Shilingi ya Tanzania.

Majaliwa

Hata hivyo, Majaliwa akizungumza na gazeti hili jana jioni alisema inawezekana Lissu hakumwelewa au amefanya makusudi kupotosha kile ambacho yeye alikizungumza ili kujipatia sifa kwa umma.

"Nilichokisema hakitofautiani na kile kilichomo kwenye jedwali la hotuba ya Waziri Mkuu, nimesema kwamba hadi sasa tunaendelea kugawa madawati ya plastiki katika halmashauri za wilaya 41 na hivi ninavyozungumza halmashauri ya mwisho inayopelekewa madawati leo (jana) ni Temeke," alisema Majaliwa na kuongeza:

"Kwa upande wa madawati ya mbao, ambayo yeye (Lissu) ameyaita ya chuma, nayo yanaanza kusambazwa katika halmashauri zilizobaki 123, na kazi hiyo itaendelea na ifikapo Agosti 15 mwaka huu kila halmashauri itakuwa imepata mgawo wake."

Alisema tayari Serikali imetangaza zabuni ya utengenezaji wa madawati awamu ya pili ambayo itafunguliwa Jumatatu ijayo na kwamba baada ya taratibu kukamilika utengenezaji huo utaanza na kukamilika katika muda wa miezi miwili.

Alisema katika awamu ya kwanza, kila halmashauri inatarajiwa kupata madawati 756, sawa na madawati 123, 984.

"Kama unakumbuka awali tulipanga madawati haya yapelekwe kwenye wilaya kama sita nadhani, lakini wabunge walishauri kwamba kila wilaya inufaike na ndicho tulichokifanya," alisema.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom