Kamati ya Katiba na Sheria Bungeni yashauri Idara za Serikali kumtumia Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kwa kazi zote uchapishaji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria pamoja na mambo mengine mengi imeshauri ujenzi wa kiwanda cha nyaraka za Serikali ukamilike kwa wakati, Serikali itoe waraka maalum kuelekeza idara zake zote kutumia ofisi ya mpiga chapa Mkuu wa Serikali kwa kazi zote zinazohusu uchapishaji hususani nyaraka za siri, za kitaifa kama bendera, sheria mbalimbali na Kanuni n.k

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria, Dkt. Joseph Kizito Mhagama akiwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu kwa Mwaka wa Fedha 2022/ 23 pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Mpato na Matumizi ya ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2023/24.​
 
Back
Top Bottom