Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 11,827
- 20,414
Katika kuthibitisha kile ambacho wanasiasa wa upinzani na wananchi kwa ujumla wamekuwa wakikipigia kelele siku zote na serikali kujifanya kiziwi haitaki kusikia, makamu mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Bunge, Japhet Hasunga, ametoa tamko rasmi kwamba shirika la ndege la Tanzania ATCL liko mahututi na litakufa hivi karibuni.
Itakumbukwa kwamba suala la mkurupuko katika kulifufua shirika la ndege la Tanzania, ATCL, ni jambo lililosemwa sana na watu wa upinzani na Watanzania kwa ujumla, lakini CCM na serikali iliyopo madarakani siku zote hawakutaka kusikiliza na kukebehi ushauri na mapungufu yaliyokuwa yakitolewa na wadau hao.
Kwa kauli hii ya kamati ye fedha, inadhihirisha mtazamo kwamba sio kila ushauri unaotolewa na upande wa upinzani ni mbaya na unapaswa kubezwa kwamba ni harakati za upinzani kupinga kila kitu.
Nukuu ya maneno ya Makamu mwenyekiti wa kamati ya fedha PAC juu ya kuwa mahututi na kifo cha ATCL hivi karibuni iko hapa chini.
Tafsiri; "ukichukua madeni yote ya ATCL, yanayofikia 472.8bln/-, na mtaji wa mali za shirika ambazo ni 256.2bln, na ukatoa thamani ya madeni toka mtaji, wanabaki na mtaji ambao ni deni wa 216.6bln, alifafanua (Hasunga), akisisitiza kwamba hii ni dalili kwamba ATCL iko mahututi na itakufa hivi karibuni"
Jambo moja ambalo kamati ya fedha imeliongelea kwa namna ya kukosoa sana na kuonyesha kuwa ni mojawapo ya chanzo cha matatizo ya ATCL ni suala la kwamba ndege za ATCL sio zao ni za serikali kwa hiyo kwa namna fulani ATCL wanakuwa hawana mamlaka kamili kusimamia ATCL, bali mamlaka hayo yako Wizara ya Usafirishaji. Hii ni pamoja na matengenezo na matumizi ya ndege za ATCL. PAC imeeleza kuwa hawawezi kutoa maagizo moja kwa moja bali lazima wapitie kwa Katibu Mkuu Wizara ya Usafirishaji.
Angalia:
Kwa habari kamili fuatilia

Kwanini Rais Samia anatumia ndege za ATCL kwa safari zake hata fupi badala ya ndege ya Rais?
Kwa habari kamili fuatilia
PAC queries ATCL, TGFA planes’ lease
THE Public Accounts Committee (PAC) of the National Assembly has raised contentious issues in the contract between Air Tanzania Co. Ltd (ATCL) and the Tanzania Government Flight Agency (TGFA).
www.ippmedia.com