Kamati ya Bunge ya PAC yaridhika na kazi za Serikali Mtandao

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
942
Dodoma, Dodoma

Kamati ya Bunge ya kudumu ya Mahesabu ya Serikali yaani PAC imeeleza kuridhishwa na kazi zinazofanywa na menejimenti ya Serikali Mtandao wakati walipodhuru kituo cha Ubunifu na Uendelezaji Vipaji jijini Dodoma. Wakizungumza baada ya kukagua kazi zinazofanywa na kituo hicho, Wajumbe hao wa kamati wamepongeza jitihada zinazofanywa na serikali kuhakikisha kuwa serikali inatoka kwenye karatasi na kuingia kwenye Digitali.

Akizungumza kwa niaba ya kamati Mwenyekiti wa kamati hiyo Ndg. Japhet Hasunga , alimpongeza kwa kazi na kumuahidi Naibu Waziri Utumishi na Utawala Bora kuwa watafanya jitihada kama kamati kuhakikisha kuwa kazi nzuri zinazofanywa na ofisi hiyo inapigiwa mfano pamoja na kusimamia upatikanaji wa Bajeti ili kufiki malengo ya kutoa huduma zilizobora kwa wananchi wetu.

Akizungumza katika Kikao hicho Naibu Waziri Kikwete , aliishukuru Kamati kwa miongozo iliyowezesha kufanikishwa kwa mafanikio yanayoonekana. Pamoja na hayo, Naibu Waziri huyo ameishukuru Serikali kwa kuendelea kupeleka fedha nyingi zinazowezesha kazi za ubunifu na uwezeshaji mifumo zifanikiwe kwa kiasi kikubwa.

Kituo hiki kimekuwa kinafanya kazi nyingi zikiwemo za ubunifu mbalimbali wa mifumo ya TEHAMA iliyowezesha serikali kufanya kazi ya kutoa huduma kwa wananchi, kuwasiliana na kushauri juu ya hali ya usalama na huduma za TEHAMA serikalini.

#KaziInaendelea

WhatsApp Image 2024-02-10 at 17.14.29.jpeg
WhatsApp Image 2024-02-10 at 17.14.30.jpeg
WhatsApp Image 2024-02-10 at 17.14.32.jpeg
WhatsApp Image 2024-02-10 at 17.14.34.jpeg
 
Back
Top Bottom