Mikael Aweda
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 2,973
- 3,901
Wakuu,
Takribani mwaka moja umepita tangu nilipowatonya kupitia uzi niliyounukuu hapa chini, kuwa kuna mtu serikalini amenitonya kuwa kuna mikakati mizito ya kuihujumu Chadema kabla ya 2015 ambayo pia imetengewa mafungu ya kutosha. Mmoja ya mikakati niliyoitaja wakati huo ni kuangalia uwezekano wa kutungwa kwa sheria inayoitwa 'Sheria ya kuonngoza Maandamano' au jina lingine lolote wakayoiita. Kwa mujibu wa mtonyaji wangu, ndani ya sheria hiyo kutawekwa mambo yatakayoonekana ni mazuri kwa nje lakini ikishaanza kutekelezwa ndo utaona ugumu wake.
Mfano michache ya vipengele vinavyotaka kuingizwa ni haya.
Mosi, Kiongozi wa Chadema wa eneo X (eg Ruvuma) atatakiwa apate kibali cha viongozi wa mkoa wa Y (Manyara) kama RC/DC au ye yote ili apate kibali cha kuhutubia mkutano au kushiriki operesheni ya ujenzi wa chama. Lengo hapa ni kuwathibiti wale viongozi maarufu wa Chadema hasa wabunge wasipeleke ushawishi wao nje ya maeneo yao waliyochaguliwa kwa kuwa vibali hivyo vitapatikana kwa tabu sana.
Pili, Mchakato au utaratibu wa kupata kibali cha mkutano utawekewa mlolongo na masharti au urasimu marefu na hivyo kupunguza kabisa mikutano ya Chadema kila kona ya nchi hii.
Tatu, kutakuwa na masharti mengi pia yatakayohusu nyakati za Chaguzi mbali mbali.
Baadhi ya magazeti jana yamenukuu kauli ya kamati mojawapo ya Bunge ( Ni Ulinzi na usalama kama sijasahau) ikipendekeza kutungwa kwa kanuni ya Bunge ya kuthibiti fujo Bungeni na wakati huo huo wakiitaka serikai pia ije na sheria ya kuthibiti maandamano sawa sawa na nukuu ya Mtonyaji wangu hapa chini. Msingi wa hoja yao ni fujo za Bungeni huku wakikwepa hoja ya vifo ktk maandamano ya Chadema maana hoja ya Chadema ya kudai kuundwa kwa tume ya kimahakama ya kuchunguza vifo (+ bomu la Arusha) ni mwiba mkubwa sana kwao.
Soma sehemu ya nukuu ya nilichokiandika hapa chini ili ujue kuwa huwa hatubatishi tunapofunua wazi hujuma zao.
Wakuu,
Jumatatu niliweka uzi hapa kuhusu nini hasa kinachoweza kuwa nyuma ya pazia la vifo vyenye utata ktk mikutano ya Chadema. Mtumishi wa idara muhimu ya serikali alniambia kuwa kuna mkakati wa kujaribu kudhoofisha chama chenu serikalini.
Kwamba mkakati wa serikali ni kutunga sheria ya kuthibiti vyama vya upinzani hususani Chadema mbele ya safari.
Kwamba hofu yao ni kama sheria hiyo itakukubalika kwa wananchi na wahisani. Na kwamba kuna maofisa wanaodhani kuwa sheria hiyo italeta vurugu.
Na hoja yake ni kwamba inawezekana vifo hivyo vimepangwa ili kuwalainisha wahisani, na kuwaandaa wananchi kuikubali sheria husika pamoja na kuwapa hoja wakubwa serikalini wanaoipigia chapuo sheria hiyo. Pili, sheria ikikwama basi mbinu za kuwachafua zinaweza kutumika. Utunzi wa sheria hii ulishadokezwa hadharani Bungeni na Mwanasheria mkuu. mwisho wa kunukuu.
NB. Kuna tetesi nimepata ya kutaka viongozi wawili wa juu wa Chadema wasifike 2015 iwe kwa ajali, sumu kwenye chakula au njia yo yote itakayoepusha malalamiko kutoka kwa wananchi. Time will tell.
Nawasilisha.
Aweda, Mikael.