Kamati ya Bunge yathibitisha ukweli wa Mtonyaji (alioutoa 2012) wa mikakati ya kuihujumu Chadema

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
Wakuu,
Takribani mwaka moja umepita tangu nilipowatonya kupitia uzi niliyounukuu hapa chini, kuwa kuna mtu serikalini amenitonya kuwa kuna mikakati mizito ya kuihujumu Chadema kabla ya 2015 ambayo pia imetengewa mafungu ya kutosha. Mmoja ya mikakati niliyoitaja wakati huo ni kuangalia uwezekano wa kutungwa kwa sheria inayoitwa 'Sheria ya kuonngoza Maandamano' au jina lingine lolote wakayoiita. Kwa mujibu wa mtonyaji wangu, ndani ya sheria hiyo kutawekwa mambo yatakayoonekana ni mazuri kwa nje lakini ikishaanza kutekelezwa ndo utaona ugumu wake.

Mfano michache ya vipengele vinavyotaka kuingizwa ni haya.

Mosi, Kiongozi wa Chadema wa eneo X (eg Ruvuma) atatakiwa apate kibali cha viongozi wa mkoa wa Y (Manyara) kama RC/DC au ye yote ili apate kibali cha kuhutubia mkutano au kushiriki operesheni ya ujenzi wa chama. Lengo hapa ni kuwathibiti wale viongozi maarufu wa Chadema hasa wabunge wasipeleke ushawishi wao nje ya maeneo yao waliyochaguliwa kwa kuwa vibali hivyo vitapatikana kwa tabu sana.

Pili, Mchakato au utaratibu wa kupata kibali cha mkutano utawekewa mlolongo na masharti au urasimu marefu na hivyo kupunguza kabisa mikutano ya Chadema kila kona ya nchi hii.

Tatu, kutakuwa na masharti mengi pia yatakayohusu nyakati za Chaguzi mbali mbali.

Baadhi ya magazeti jana yamenukuu kauli ya kamati mojawapo ya Bunge ( Ni Ulinzi na usalama kama sijasahau) ikipendekeza kutungwa kwa kanuni ya Bunge ya kuthibiti fujo Bungeni na wakati huo huo wakiitaka serikai pia ije na sheria ya kuthibiti maandamano sawa sawa na nukuu ya Mtonyaji wangu hapa chini. Msingi wa hoja yao ni fujo za Bungeni huku wakikwepa hoja ya vifo ktk maandamano ya Chadema maana hoja ya Chadema ya kudai kuundwa kwa tume ya kimahakama ya kuchunguza vifo (+ bomu la Arusha) ni mwiba mkubwa sana kwao.

Soma sehemu ya nukuu ya nilichokiandika hapa chini ili ujue kuwa huwa hatubatishi tunapofunua wazi hujuma zao.

Wakuu,

Jumatatu niliweka uzi hapa kuhusu nini hasa kinachoweza kuwa nyuma ya pazia la vifo vyenye utata ktk mikutano ya Chadema. Mtumishi wa idara muhimu ya serikali alniambia kuwa kuna mkakati wa kujaribu kudhoofisha chama chenu serikalini.
Kwamba mkakati wa serikali ni kutunga sheria ya kuthibiti vyama vya upinzani hususani Chadema mbele ya safari.
Kwamba hofu yao ni kama sheria hiyo itakukubalika kwa wananchi na wahisani. Na kwamba kuna maofisa wanaodhani kuwa sheria hiyo italeta vurugu.
Na hoja yake ni kwamba inawezekana vifo hivyo vimepangwa ili kuwalainisha wahisani, na kuwaandaa wananchi kuikubali sheria husika pamoja na kuwapa hoja wakubwa serikalini wanaoipigia chapuo sheria hiyo. Pili, sheria ikikwama basi mbinu za kuwachafua zinaweza kutumika. Utunzi wa sheria hii ulishadokezwa hadharani Bungeni na Mwanasheria mkuu.
mwisho wa kunukuu.

NB. Kuna tetesi nimepata ya kutaka viongozi wawili wa juu wa Chadema wasifike 2015 iwe kwa ajali, sumu kwenye chakula au njia yo yote itakayoepusha malalamiko kutoka kwa wananchi. Time will tell.

Nawasilisha.
Aweda, Mikael
.
 
jitu zima linaamka limebugia viroba linakuja kuleta hadithi hapa JF zisizokuwa na ushahidi ila uongo uongo, kauli ya JK kuwa TANZANIA kuna vijanani VIWANDA vya uongo naikubali kabisa
 
Aweda; usiwe na wasiwasi hawa Magamba wanajitungia sheria ya kuwabana wao wala sio CHADEMA,mwaka 2015 kwa vyovyote CHADEMA itaingia madarakana na hizi sheria za kipuuzi na kikandamizi wanazopitisha kwa sababu ya wingi wao zitawaumiza wao maana piga ua 2015 CCM will be oposition,waache watunge as many as they wish maana hali ilivyo kwa sasa CHADEMA ndio inayoongoza nchi 2015 tutakabidhiwa madaraka tuu na sisi ndio tutakao zisimamia hizi sheria na nijuavyo ustaarabu na utu wetu tutazibadilisha na kuwapa wapinzani wetu the then equal and fair political ground
 
jitu zima linaamka limebugia viroba linakuja kuleta hadithi hapa JF zisizokuwa na ushahidi ila uongo uongo, kauli ya JK kuwa TANZANIA kuna vijanani VIWANDA vya uongo naikubali kabisa

sasa kati yako na mleta mada nani ameamka na viroba??na je kwani mmeshatunga sheria inayozuia kuamka na viroba?washauri magamba wenzio na hii watunge kama inakuumiza maana kwa taarifa yako hao mnaowaita wanywa viroba ndio mtakaowapigia magoti 2015 mkiwaomba wasiwapeleke baba na mashost zenu The Haugue
 
Aweda; usiwe na wasiwasi hawa Magamba wanajitungia sheria ya kuwabana wao wala sio CHADEMA,mwaka 2015 kwa vyovyote CHADEMA itaingia madarakana na hizi sheria za kipuuzi na kikandamizi wanazopitisha kwa sababu ya wingi wao zitawaumiza wao maana piga ua 2015 CCM will be oposition,waache watunge as many as they wish maana hali ilivyo kwa sasa CHADEMA ndio inayoongoza nchi 2015 tutakabidhiwa madaraka tuu na sisi ndio tutakao zisimamia hizi sheria na nijuavyo ustaarabu na utu wetu tutazibadilisha na kuwapa wapinzani wetu the then equal and fair political ground

Sahau Chadema kuingia ikulu
 
Hivi Aweda uwezo wako wa kufikiri upoje? Yaani huwa napata sana shida kuelewa kile unachokiandika. Hakika wewe ni janga la CHADEMA
 
jitu zima linaamka limebugia viroba linakuja kuleta hadithi hapa JF zisizokuwa na ushahidi ila uongo uongo, kauli ya JK kuwa TANZANIA kuna vijanani VIWANDA vya uongo naikubali kabisa
Kama kweli unachoongea kinatoka moyoni basi Tanzania tuna kazi kubwa kukomboa fikra zetu hadi kupata uhuru wa kweli. Uwezi niambia kwamba yanayotokea ni mazuri wakati wananchi waliowengi tunaumia kwa viongozi wachache kujineemesha na kutunga sheria kandamizi. Leo hii unasema heti leta ushaidi ndiyo hayohayo tunayoambiwa kila siku tupeleke ushaidi serikalini wakati mambo yanaonekana bila chenga.

Tumezaliwa na tutakufa, Tanzania itaendelea hivyo vijana tufanye kazi yetu kama wazee wetu Mwalimu Nyerere, Mandela, Nkhuruma na wengine walivyopambana kutuletea uhuru. TUACHE UBINAFSI, HUU MFUMO HULIOPO UNAWANUFAISHA NINYI NDIYO MAANA HAMUONI TATIZO KUTULETEA SHERIA KANDAMIZI.
 
Aweda; usiwe na wasiwasi hawa Magamba wanajitungia sheria ya kuwabana wao wala sio CHADEMA,mwaka 2015 kwa vyovyote CHADEMA itaingia madarakana na hizi sheria za kipuuzi na kikandamizi wanazopitisha kwa sababu ya wingi wao zitawaumiza wao maana piga ua 2015 CCM will be oposition,waache watunge as many as they wish maana hali ilivyo kwa sasa CHADEMA ndio inayoongoza nchi 2015 tutakabidhiwa madaraka tuu na sisi ndio tutakao zisimamia hizi sheria na nijuavyo ustaarabu na utu wetu tutazibadilisha na kuwapa wapinzani wetu the then equal and fair political ground
Mkuu, hivi Ikulu mtaingia tu kwa kuendelea kufukuzana namkushinda humu JF? Hakika CHADEMA msahau kabisa suala la kwenda Ikulu labda mpaka mwaka 2080
 
Kama kweli unachoongea kinatoka moyoni basi Tanzania tuna kazi kubwa kukomboa fikra zetu hadi kupata uhuru wa kweli. Uwezi niambia kwamba yanayotokea ni mazuri wakati wananchi waliowengi tunaumia kwa viongozi wachache kujineemesha na kutunga sheria kandamizi. Leo hii unasema heti leta ushaidi ndiyo hayohayo tunayoambiwa kila siku tupeleke ushaidi serikalini wakati mambo yanaonekana bila chenga.

Tumezaliwa na tutakufa, Tanzania itaendelea hivyo vijana tufanye kazi yetu kama wazee wetu Mwalimu Nyerere, Mandela, Nkhuruma na wengine walivyopambana kutuletea uhuru. TUACHE UBINAFSI, HUU MFUMO HULIOPO UNAWANUFAISHA NINYI NDIYO MAANA HAMUONI TATIZO KUTULETEA SHERIA KANDAMIZI.
Mkuu, hakuna uhuru usio na mipaka. Kwani uhuru bila mipaka ni fujo. Maandamano yasipotungiwa sheria kali itatokea wajinga wachache watatumia mwanya huo kuhatarisha usalama wa taifa.
 
Aweda, wakati mwingine sikuelewi unachokiandika kwa nini usichukuwe muda wako akamshauri Dr.Slaa aache ubabe.
 
jitu zima linaamka limebugia viroba linakuja kuleta hadithi hapa JF zisizokuwa na ushahidi ila uongo uongo, kauli ya JK kuwa TANZANIA kuna vijanani VIWANDA vya uongo naikubali kabisa

Dawa yenu mastone tu!
 
Back
Top Bottom