Kamati Kuu ya CHADEMA, mkiteua wabunge wa Viti Maalumu kuingia Bungeni, mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana

Sizungumzii yaani isahaulike kabisa Tanzania, namaanisha watapoteza wapiga kura kwasababu wengi watakata tamaa kwa yaliyotokea this year.

They need to be very clever on this, lazima wajue namna ya kukabiliana na adui yao kwa akili, sio kususa.
Mkuu ucleva gani na chama kinachotumia nguvu badala ya democracy na kuacha sanduku la kura liseme.
 
Niwajuavyo wanasiasa ningumu kutokwenda,maana ndiyo ajira yao kubwa,hawana chanzo kingine cha mapato.....viti maalum wataenda tu......mtaani hali mbaya
 
Maswali gani? Siko hapa kujibu maswali yako. Hayo yote unayoyapendekeza yaamefanyika tangu 1995 mpaka leo. CCM inaendelea hivyo hivyo. Chama cha siasa serious kinawaza kushika dola, siyo kuwepo kuwepo. NGOs ndio zinakuwepo kuwepo.

Ingekuwa kutokuingia bungeni ni kukata tamaa, unafikiri kwa nini wazo la Aida kutokuingia Bungeni linaihuzunisha sana CCM? Au unafikiri baada ya uchaguzi wamepata mapenzi ya ghafla kwa CHADEMA?
Mkuu ungekua tunaonana ana kwa ana ningekupa bia 3. Yaani Watanzania wote tungekua na vichwa kama hivi, huu ujinga tuliofanyiwa haungetokea. Huyu jamaa simuelewi nini nia ya kuwasukumia CHADEMA Bungeni.
 
Maswali yako ni ya kitoto kabisa (sorry). Endelea kuamini kuwa Aida anaweza kupata Tume huru yeye mwenyewe Bungeni. Sana sana anakwenda kuhalalisha udhalimu uliofanyika. Ndio maana CCM wanataka aende.
Huyu jamaa hovyo kabisa.
 
Kwanza nianze kwa kusema kuwa, Katika vitu ambavyo CCM kwa sasa wanatamani vitokee, ni kupata wabunge wa upinzani japo wachache ili kuondoa dhana ya Bunge kuitwa Bunge la CCM-Bunge la chama kimoja...
HAPANA , nawashauri wawateue na waende bungeni.
Wanaenda bungeni kwa madhumuni mbalimbali.
.Hela watayopata itachangia kipato kwenye chama, kitu ambacho ni muhimu.
.Kaa na adui yako ili umsome madhaifu yake.
.Chanzo cha kipato cha hao wateuliwa.

.Wanannchi bado wanapata uwakilishi bungeni angalau kwa uchache.
.Awepo mtu/watu wa kuwakosoa ccm live pale bungeni.
Wataendelea kupata airtime.
 
Ingawa naelewa unakotokea lakini kwenye hili natofautiana na wewe. Mimi nadhani kuwa kuna umuhimu wa Chadema kuwepo Bungeni kwa sababu zifuatazo:
1. Ingawa tutaliita kuwa ni Bunge la CCM lakini ukweli ni kuwa ni Bunge la taifa la Tanzania lenye wajumbe wengi kutoka CCM. Kwa sababu hiyo kuna haja ya uwepo wa wajumbe wataowatetea wananchi na kusimamia taifa lao...
Kumbe mnaumia kukosekana kwa wabunge wa upinzani. Kumbuka lengo la yote yaliyofanyika ni kuua upinzani. Hakuna haja ya upinzani Bungeni, endeleeni mkiwa chama kimoja ili msicheleweshwe maendeleo.
 
Kumbe mnaumia kukosekana kwa wabunge wa upinzani. Kumbuka lengo la yote yaliyofanyika ni kuua upinzani. Hakuna haja ya upinzani Bungeni, endeleeni mkiwa chama kimoja ili msicheleweshwe maendeleo.
Tatizo ni kuwa mkishaitwa Expert Member na JF basi mnaamini kuwa kweli nyie ni maexpert.

Amandla...
 
N
Kwanza nianze kwa kusema kuwa, Katika vitu ambavyo CCM kwa sasa wanatamani vitokee, ni kupata wabunge wa upinzani japo wachache ili kuondoa dhana ya Bunge kuitwa Bunge la CCM-Bunge la chama kimoja...
Yie ndo.mnashiriki kukiua hicho chama, endeleeni kutoa ushauri usio kuwa na maana.
Chama chenu kitabaki kama cha Dovutwa hapa tanzania.
 
Walioshinda ubunge kama yule dada wa Nkasi aende bungeni (japo namtilia shaka nyendo zake), viti maalum nao waende bungeni, na wale wanaoona wameonewa kwenye majimbo yao hawakushindwa kihalali waende mahakamani...

Sishauri viti maalum waende bungeni, huyo dada aliyechaguliwa aende maana ameshaonyesha hajali sana yaliyotokea kwenye uchaguzi huu, bali anajali zaidi ubunge wake. Ili asipewe airtime negative, aachwe aende.

Kusikika sio lazima bungeni, mbona Lisu hakuwa bungeni zaidi ya miaka mitatu, na bado karudi na mvuto hadi imebidi uchaguzi unajisiwe?

Hawa chadema hata sasa hawakupata mvuto huu kupitia bunge hili maana halikuwa live, na walitangazwa zaidi kwa mambo negative kuliko positive. Siamini kama bunge hili ndio linaweza kuwajenga Chadema zaidi ya kuhalalisha uhayawani.
 
Mie nilishapendekeza kwamba CCM na Magufuli need to learn their lesson. Wapinzani wasijishughulishe kabisa na hili BUnge, hata wale wapinzani walioshinda ubunge nilipendekeza wajiuzulu...
2015 Zanzibar ilienda bila upinzani mpaka 2020...Kuna faida au hasara?
 
WANAWAKE CHADEMA WAKOMALIA VITI MAALUM UBUNGE: WASEMA WAKO TAYARI KUVULIWA UANACHAMA WAKIWA BUNGENI

- Ni katika kikao kinachoendelea muda huu bahari beach Hotel

- Wanaume wawataka wanawake wa Viti Maalum kukataa Ubunge huo

- Halima Mdee na Esther Bulaya waongoza mgomo wa BAWACHA kutaka waingie bungeni

- Lissu acharuka, ataka wanawake hao wafutiwe uanachama, Mbowe asema michango yao ya fedha ni muhimu kusaidia kuimarisha Chama

- Hadi sasa mvutano ni mkubwa na kikao kinaendelea

- Ikumbukwe orodha ya Viti maalum vya ubunge ilipelekwa tume ya Uchaguzi siku 30 kabla ya Uchaguzi Mkuu.

- Orodha hiyo inaongozwa na Halima Mdee, Joyce Mukya na Esther Bulaya

- Nitaendelea kuwajuza hatima ta kikao


Wako,

Deo Meck, toka Bahari Beach, Dar es Salaam.
 
WANAWAKE CHADEMA WAKOMALIA VITI MAALUM UBUNGE: WASEMA WAKO TAYARI KUVULIWA UANACHAMA WAKIWA BUNGENI

- Ni katika kikao kinachoendelea muda huu bahari beach Hotel

- Wanaume wawataka wanawake wa Viti Maalum kukataa Ubunge huo...
Kuwazuia Wabunge wa CHADEMA kutokuwa Wabunge au Kushiriki shughuli za Bunge si tu ni Uwendazimu bali pia ni Upumbavu uliovuka Kiwango.
 
Back
Top Bottom