Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,733
- 40,846
Wiki chache zijazo, Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi itakutana katika kikao chake cha Kawaida huko Butiama. Kikao hicho ambacho kitatangulia kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM bila ya shaka kati ya mambo mengi ambayo itajikuta inakabiliwa nayo ni mgongano wa wazi ndani ya Chama hicho ambao umetokea baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa na malumbano kati ya baadhi ya viongozi wa chama hicho na chombo cha Bunge ambacho chama hicho hicho kinaongoza.
Kwa mujibu wa Katiba ya CCM Kamati Kuu ya CCM ina jukumu la "Kutoa uongozi wa siasa nchini" na hivyo bila ya shaka wajumbe wa Kamati hiyo wanaangalia kwa ukaribu maendeleo ya wanachama wake na hasa mpasuko wa wazi na ushindani wa wazi ambapo siyo tu unamuweka kwenye shabaha Rais (ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa) bali pia unagusa maslahi ya watu wengi ambao wana maslahi tofauti kupitia chama hicho.
Kwa kuangalia historia ya Kamati Kuu ni wazi kuwa chombo hicho bado kina nguvu ya kuweza kuingilia jambo lolote na wana uwezo wa kumchukulia hatua mwanachama wao yeyote yule ambaye siyo tu anatishia maslahi ya chama hicho bali pia anatishia hali ya mwelekeo wa kisiasa nchini.
Ni kwa sababu hiyo sitoshangaa kabisa endapo Mbunge wa Monduli Bw. Edward Lowassa akapewa karipio kali na akileta "zake" kuvuliwa uanachama kwa mujibu wa Ibara ya 110:7.
Historia ya CCM inaonesha kuwa hawakusita kuwachukulia hatua watu kama Aboud Jumbe, Seif Sharrif Hamad na wenzake, Horace Kolimba na viongozi kadha wa kadha pale inapobidi. Kwa mtu anafikiri kuwa ni popular kama Lowassa atafanya makosa makubwa sana kudhani kuwa mashabiki wake wa chini watasimama mbele ya Kamati hiyo. Kama nilivyosema miezi michache iliyopita, shoka limekwisha inuliwa; na Lowassa kwa makusudi amejilengesha kama shina la mti; Endapo Lowassa hatafyata mapema (sitarajii) kuna uwezekano mkubwa wa kuchukuliwa hatua kali na lile jinamizi liitwalo "nidhamu ya chama" na sitoshangaa akachukuliwa hata hatua ya kuvuliwa uanachama!!
You heard it first... !!
Lakini swali ambalo ni la kujibiwa kabla ya kufika huko ni je JK anaweza kuleta mizengwe ya kiCCM na kutumia fimbo yake ya Uenyekiti wa CCM kuvunja daima urafiki wake na Lowassa? Kwa upande wa Lowassa swali analohitaji kujibu kabla ya kugongana na KK ni je anakubalika kiasi gani kwa wananchi wa kawaida kiasi cha kuweza kumrudisha Bungeni kwa tiketi ya chama kingine chochote kile?
Ndugu zangu, naogopa yawezekana tunashuhudia kuanguka na kufutika kwa Lowassa katika uongozi wa Tanzania. Tunasubiri kuona nani ata mcheck mate mwenzie!!