Kamati kuu CHADEMA kufunika Arusha Alhamisi

Kamati kuu CHADEMA kufunika Arusha Alhamisi

acheni uongo mbona shibuda hamkumfukuza, madiwani wa chadema bado ni madiwani halali wanaenda mahakamani kupinga kuvuliwa udiwani.
chadema hajawavua udiwani na haina uwezo huo..wamevuliwa uwanachama wa chadema na biashara ikaishia hapo
 
Hapana sijalazimishwa isipokuwa wizi na uvunjifu wa amani.Hatutaki mabomu,majeruhi,vifo.

Hivi wewe ulifikiri waliopigania Uhuru wa nchi zao walikuwa na mawazo ya woga kama wewe? Hivi Watanzania tuko je? we unaona sawa tu nchi hii iendelee na maisha haya mpaka lini? hebu fungua akili yako na ufikiri kwanza kabla ya kutoa maoni yako hapa. Kila siku amani amani wakati hata amani yenyewe hakuna.

Badilika mtanzania nchi hii inahitaji ushujaa wa kweli kuiokoa katika maisha haya.
 
Kichwa kimoja kinapambana na zaidi ya vichwa mia tano. Hivi siku mkimfukuza Shibuda si mtabeba na Billcanas casino muende nayo kwa wasukuma maana kwa madiwani imebidi muende na chama chote.
billcan ni chombogani bona unafikiri kwa kutumia makalio..nyie kuwavua magamba watu 3 mmezunguka nchi nzima bado magamba hayavuki je mmepaga kutumia nini zaidi maana siku 90 zilishaisha..
 
Karibuni sana cc ya cdm Arusha. Natumaini mtajibu maswali mengi tuliyonayo wana cdm Arusha.
 
Ni heri tupoteze hizo kata nne kuliko tukavunja kanuni, katiba na misimamo ya Chadema ambayo tuliyanadi kwa watanzania wakati wa uchaguzi tukaamniwa na kupigiwa kura na watz kutokana na katiba, kanuni na msimimo hiyo tuliyoyasimamia.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Ni heri tupoteze hizo kata nne kuliko tukavunja kanuni, katiba na misimamo ya Chadema ambayo tuliyanadi kwa watanzania wakati wa uchaguzi tukaamniwa na kupigiwa kura na watz kutokana na katiba, kanuni na msimimo hiyo tuliyoyasimamia.

mkuu ..... bravo sana

nimefurahia na kupata faraja knatinka bandiko lanko hili ..... hiii inaashiria umaknini kwenye dhana nzima ya uongozi na dhamana ya uwakilishi wa wananchi

safi sana mkuu
 
Viongozi makini wa chama makini ni wale wenye kutoa maamuazi magumu. Chadema wameonyesha mfano na sio vinaya na vyama vingine ikiwemo chama tawala waige Mfano huo. Kila la kheri kwa mkutano wa alhamisi jijini ARUSHA.
 
Iko haja ya kuwa na wagombea huru wasio na vyama. Kamati Kuu ya CHADEMA ilipaswa kuwasikiliza wapiga kura waliowachagua madiwani hawa kabla ya kuwafukuza.
 
Chadema kimeandaa mkutano mkubwa wa hadhara mjini Arusha Alhamisi wiki hii utakao ongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Freeman Mbowe Kwa kushirikiana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibroad Slaa, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na wajumbe wa CC.

Wajumbe wa CC watakaokwenda kuhutubia mkutano huo ni Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa; Mbunge wa Viti Maalum, Regia Mtema; Mwenyekiti wa baraza la Vijana Taifa wa chama hicho, Heche Suguta; Mbunge wa Viti Maalum, Chiku Abwao na Mbunge wa Nyamagana Ezekia Wenje.

Wengine ni Mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu wa kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu; Meya wa Manispaa ya Musoma, Kasululu Malima; Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu, Lazaro Masai, na Mwenyekiti Manispaa ya Moshi, Jaffar Maiko. Pia atakuwapo Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na madiwani wengine wa Jiji la Arusha.

Madiwani waliofukuzwa

attachment.php


Kutoka kushoto: Estomih Mallah wa Kata ya Kimandolu, John Bayo wa Kata ya Elerai, Ruben Ngowi wa Kata ya Themi, Rehema Mohamed wa Viti Maalum na Charles Mpanda wa Kata ya kaloleni.

Source: Nipashe

He he heeee mtatafunana kama panzi safari hii, na wao wamesema mkitoka nyie tu na wao wanaitisha maandamano!
 
He he heeee mtatafunana kama panzi safari hii, na wao wamesema mkitoka nyie tu na wao wanaitisha maandamano !
Unawasema wepi wale wahuni 17 tena wa kukodi hawana chama wala ofisi labda wakafanyie Garden Bar.
 
Iko haja ya kuwa na wagombea huru wasio na vyama. Kamati Kuu ya CHADEMA ilipaswa kuwasikiliza wapiga kura waliowachagua madiwani hawa kabla ya kuwafukuza.

Una maana kila wakati kunapotokea viongozi kukosea Kamati kuu lazima iende kuonana na wapiga kura wao, kwa hiyo kazi ya kamati mwaka mzima itakuwa ni kutembelea wananchi wenye migogoro nafikiri hapa huna point.

Madiwani waliitwa wakasikilizwa si mara moja zaidi ya mara mbili unataka Kamati ifanyenini zaidi, angalia ushahidi huu wa picha unawasuta ndio maana wanajiuliza kwenda mahakamani ukitolewa ushahidi kama huu hawawezi kupinga.

Waliokuwa Madiwani wa Chadema wakisubiri kuhojiwa na kamati kuu Dodoma trh 6/8/2011

Kutoka kushoto: Estomih Mallah wa Kata ya Kimandolu, John Bayo wa Kata ya Elerai, Ruben Ngowi wa Kata ya Themi, Rehema Mohamed wa Viti Maalum na Charles Mpanda wa Kata ya kaloleni.
 
Wabunge wa chadema kesho j5 watatembelea kata za Kimandolu, Kaloleni na Elerai kufungua matawi na mashina na cdm katika wilaya ya Arusha.

Kwa mujibu wa kiongozi wa task force wilayani Arusha ambaye pia ni diwani wa Levolosi, mh. Nanyaro Ephata, baada ya kufanya kazi hiyo, mh. Lema atahutubia mkutano kwenye kata ya Kimandolu, mh Wenje, Tundu Lissu na Mh Henche watahutubia kata ya Kaloleni, Mh. Regia Mtema na wabunge wengine wakuteuliwa watahutubia mkutano utakaofanyika majengo kwenye kata ya Elerai.

Kata zote zinazofanyika mikutano hiyo ni kata ambazo madiwani wake wametimuliwa uanachama na CDM mwishoni mwa wiki.

Baada ya mikutano hiyo kutakuwa na mkutano mkubwa kwa wakazi wote wa jiji la Arusha siku ya Alhamisi utakaohutubiwa na Mh. Mbowe, Mh. Slaa na wabunge mbalimbali wa chama.
 
Barua kwa Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Wananchi wa Tanzania kuwaomba waibane Serikali juu ya kadhia ya Mwembechai

Utangulizi
Mara baada ya mauaji ya kinyama yaliyofanywa na polisi katika eneo la Mwembechai tarehe 13 Februari, 1998, Kamati yetu iliitisha mkutano na waandishi wa habari kueleza ukweli wa mambo yalivyotokea. Tulifanya hivyo kwa sababu hadi wakati huo, taarifa zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya viongozi wa mamlaka mbalimbali za nchi zilikuwa hazielezi ukweli wote. Na kwa bahati mbaya taarifa hizo zikawa zinafikishwa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari na hivyo kupotosha ukweli wa mambo.

Ndio maana katika mkutano ule tuliiomba serikali yetu, ili kuondosha utata uliokuwepo, iunde tume huru ya kuchunguza tukio la Mwembechai na yale yaliyopelekea kutokea kwa tukio hilo.

Kwa bahati mbaya hadi leo tume hiyo bado haijaundwa. Mbali ya kutoundwa kwa tume, taarifa zilizotolewa na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu serikalini, viongozi ambao awali walidai kuujua ukweli wa mambo na hivyo kuikataa haja ya kuundwa tume, ziliendelea kuwakanganya wananchi. Kwa kipindi kisichozidi mwezi na nusu, viongozi hao waliodai kuujua ukweli wa mambo walitoa sababu nne tofauti, na zenye kupingana.

Hali hiyo ilitosha kuwa ni ushahidi wa haja na umuhimu wa kuundwa tume ya kuchunguza ukweli wa tukio na hasa yale yaliyopelekea kuzuka kwake.

Waheshimiwa wabunge, hiyo ndio hali iliyopelekea Kamati yetu kutoa waraka wa kurasa 13 ambao ulieleza kwa kina chanzo cha tukio lile na yale yaliyotokea. Waraka huo uliosainiwa na Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu wa Kamati yetu, ulisambazwa kwenu waheshimiwa wabunge, wanasheria, wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na taasisi mbalimbali za nchi ikiwemo inayoshughulikia usalama wa taifa letu.

Tulikuleteeni waraka ule Waheshimiwa wabunge ili kukujulisheni ukweli wa mambo na hivyo kukupeni fursa ya kuuchambua ukweli wa tukio hilo kwa kupima maelezo ya pande zote.

Hatuna budi Waheshimiwa wabunge kutanguliza shukrani zetu kwenu na hususan Mheshimiwa Kitwana Kondo, Mheshimiwa Ibrahim Msabaha, na Mheshimiwa Spika wa Bunge aliyewaruhusu kuzungumza juu ya kadhia ya Mwembechai, na ukatili wa polisi uliowadhalilisha akina mama na uliomtia kilema kijana Chuki Athumani.

Aidha Waheshimiwa wabunge tunaomba kutoa shukrani za dhati kwa mbunge na waziri, Mheshimiwa Kingunge Ngombale Mwiru pamoja na baadhi ya wabunge kwa jinsi alivyojitokeza na kumtembelea mtoto Chuki Athumani alipokuwa mahabusu Hospitali ya Muhimbili alikofungwa pingu kitandani licha ya kilema cha kupooza mwili, alichopewa na polisi waliompiga risasi.

Waheshimiwa wabunge, Kamati yetu na wanachi wote waliolaani mauaji yaliyofanywa na polisi Mwembechai tulifarijika sana kuona Jumuiya ya wanafunzi wa taaluma ya siasa, Utawala na Sayansi ya Jamii wakishirikiana na jopo la wasomi maarufu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliona umuhimu wa kukutana ili kujadili kadhia ya Mwembechai, ukatili wa polisi na uvunjwaji wa haki za binadamu ulioandamana na kadhia hiyo.

Tunakiri kufarijika vilevile na juhudi za Mwislamu mmoja aitwae Abu Aziz aliyempelekea Mwanasheria Mkuu wa Serikali yetu waraka wa kurasa 53 kuhusu suala la Mwembechai. Waraka huo ambao nakala yake pia ulitumwa kwenu, ofisi ya Rais, mabalozi na kwenye taasisi na jumuiya mbalimbali nchini, ulituongezea tamaa kuwa huenda wahusika na wenye majukumu ya kusimamia haki nchini watauona ukweli wa mambo kutokana na uchambuzi wa kina uliofafanua dhulma iliyotendwa na polisi Mwembechai dhidi ya haki za raia zilizoainishwa katika katiba ya nchi yetu.

Matumizi Mabaya ya Bajeti, Waheshimiwa wabunge, wananchi tunafahamu kuwa moja ya majukumu yenu ni kuchambua na kuidhinisha kasma ya bajeti kwa ajili ya matumizi ya wizara na taasisi mbalimbali za serikali, na mnafanya kwa niaba yetu. Na kwa sababu ya idhini mliyoipata kutoka kwa wananchi, mnayo haki na wajibu wa kuhoji matumizi mabaya au yale yanayokwenda kinyume na makusudio ya idhini yenu.

Ni dhahiri, Waheshimiwa wabunge, kuwa kitendo cha wizara ya Mambo ya Ndani kuwaacha polisi wawapige risasi raia na kuwauwa kwa makusudi ni matumizi mabaya ya idhini yenu katika kupitisha bajeti ya wizara hiyo mwaka uliopita (1997/98). Hatuamini kwamba mliipa idhini serikali kutumia kodi za wananchi kununulia risasi jeshi la polisi ili liwauwe raia kwa kuwalenga shabaha kama wanyama.

Na hivyo ndivyo walivyofanya pale Mwembechai tarehe 13 Februari, 1998. Mbali ya mauaji hayo wizara ya Mambo ya Ndani ilitumia pesa mlizoidhinisha mwaka jana kuwalipa posho askari ili wauzingire na waugeuze msikiti wa Mwembechai kuwa ni lindo la polisi, na wakadiriki hata kuzifuja pesa za wananchi kwa kuzungukazunguka na helikopta eneo la msikiti huo.

Ilizitumia pesa hizo pia kwa kuwatesa raia waliovamiwa na kukamatwa kwa nguvu pasipo na kosa lolote, wengine wakiwa wamelala majumbani kwao, bila hata kufuata taratibu za kisheria kama vile kuwa na "Arrest Warrant" au "search warrant." Wananchi zaidi ya 200 walikumbwa na ukamatwaji huo wa kinyama ndiyo maana wengi kati ya hao wameachiwa na Mkurugenzi wa Mashtaka kwa kutokuwepo na shitaka la kujibu.

Wengi wa watuhumiwa, wake kwa waume, watoto na vikongwe waliwekwa mahabusu kwa zaidi ya miezi minne na kupewa mateso ya kila aina. Waliwekwa katika hali mbaya na kupatwa na magonjwa, walinyimwa matibabu wanayostahili, kisha walinyanyaswa kwa matusi na masimango kinyume na haki zao za Kibinadamu.

Waheshimiwa wabunge, mahabusu mmoja Mohamed Omari alifia mikononi mwao. Wengi wengine wametoka wakiwa katika hali mbaya kiafya. Mtoto Chuki Athumani aliendelea kufungwa pingu kiasi cha kuwa taabu kumhudumia huku akiwa katika hali mbaya kiafya baada ya kupigwa risasi na polisi.

Familia za mahabusu hao zimeteseka pia kwa kukosa huduma na msaada wa wale ambao walikuwa wasimamizi na viongozi wa familia hizo, kutokana na kuwekwa mahabusu kinyume cha sheria.

Ni mateso makubwa kwa binadamu kuona binadamu mwenziwe anaonewa kwa kunyimwa haki yake ya kimsingi kama Mwanadamu. Ni jambo la mateso na huzuni kubwa vile vile kwa wananchi waliohuru katika nchi yao kuona wananchi wenzao wakinyanyaswa na kudhulumiwa haki zao kama raia.

Kulaani na Kudhibiti Madhalimu, Waheshimiwa wabunge, tumewaandikieni barua hii kwa kuzingatia mambo mengi likiwemo hili la kuidhinisha na kusimamia matumizi ya serikali na kutetea haki za raia. Mkiwa wananchi mlio Bungeni, mnalo jukumu la kitaifa la kuona kuwa taifa letu katika masuala tuliyoyataja haliwi taifa la madhalim na wabaguzi wa haki za binadamu kwa kisingizio chochote kile kama ilivyokuwa katika nchi ya Afrika Kusini zama za utawala wa makaburu.

Ndiyo maana mnapo tunga na kuzipitisha sheria mbalimbali huzingatia yale yaliyotamkwa kwenye Katiba yetu ya nchi ambayo inalinda ubinadamu wetu na kusimamia haki za raia, pasipo ubaguzi.

Hivyo mnayo haki na uwezo wa kulaani na kudhibiti madhalim wa haki za binadamu na raia nchini.

Hadi leo, Wizara ya Mambo ya Ndani haijawakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya Sheria wale polisi waliouwa wananchi kwa kuwapiga risasi tarehe 13/2/98 Mwembechai. Bado haijawakamata na kuwafikisha mbele ya Sheria wale waliotoa amri kwa polisi kuwauwa wananchi wale. Bado haijachukua hatua yoyote dhidi ya malamiko ya wananchi waliopata mateso wakati wakiwa mahabusu.

Haijawachukulia hatua yoyote wale polisi waliompiga risasi mtoto Chuki Athumani na kumsababishia kilema cha kupooza mwili. Hawajachukua hatua yoyote ya kuchunguza kifo cha mtuhumiwa Mohamed Omari aliyefia mahabusu

Maombi Yetu
Kutokana na haya, Waheshimiwa wabunge tunakuombeni
(i) Mchukue hatua za kulaani utendaji mbovu uliojitokeza Wizara ya Mambo ya Ndani kuhusu suala la Mwembechai kwa kushindwa hadi sasa kuchukua hatua dhidi ya wauaji na waliodhulumu haki za raia kwa kuwatesa, kuwatia kilema na kuwaweka ndani kinyume cha Sheria.

(ii) Tunakuombeni muibane Serikali iwaondoshe watendaji wabovu katika Wizara hiyo hususan viongozi wa Wizara na watendaji wake wakuu kwa kuachia polisi wauwaji na watesaji kuwa huru hadi leo.

(iii) Tunawaomba muibane serikali ihakikishe kuwa polisi waliouwa Mwembechai na wale waliowatesa watuhumiwa wanafikishwa mbele ya Sheria.

(iv) Tunakuombeni Waheshimiwa wabunge muibane Serikali mpaka tume ya kuchunguza kifo cha mtuhumiwa Mohamed Omari aliyefia Mahabusu inaundwa kama taratibu za kisheria (Inquest) zinzvyotaka.

(v) Waheshimiwa tunawaomba muiambie Serikali iunde tume huru ya kuchunguza sababu zinazopelekea Waislamu kupuuzwa na kunyimwa haki zao za kimsingi kama binadamu na raia katika nchi yao.

Tupo tayari kushirikiana na tume hiyo kupata ukweli wote ili nchi yetu iepukane na dhulma zinazotaka kuota mizizi dhidi ya wananchi kwa misingi ya kibaguzi.

Tunakuombeni Msiidhinishe bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya mwaka huu (1998/99) mpaka Serikali ikupeni majibu sahihi.

Vinginevyo itakuwa mmeshirikishwa katika kuwapa nyenzo wauwaji na kuhalalisha dhulma kwa kwa raia nchini. Tuanakutakieni heri, (Abdul Sattar
KAIMU Katibu
Kamati ya Kupigania Haki za Waislamu Tanzania.
Dar es Salaam, 9 Julai, 1998.
 
&
Wabunge wa chadema kesho j5 watatembelea kata za Kimandolu, Kaloleni na Elerai kufungua matawi na mashina na cdm katika wilaya ya Arusha. <br />
<br />
Kwa mujibu wa kiongozi wa task force wilayani Arusha ambaye pia ni diwani wa Levolosi, mh. Nanyaro Ephata, baada ya kufanya kazi hiyo, mh. Lema atahutubia mkutano kwenye kata ya Kimandolu, mh Wenje, Tundu Lissu na Mh Henche watahutubia kata ya Kaloleni, Mh. Regia Mtema na wabunge wengine wakuteuliwa watahutubia mkutano utakaofanyika majengo kwenye kata ya Elerai. <br />
<br />
Kata zote zinazofanyika mikutano hiyo ni kata ambazo madiwani wake wametimuliwa uanachama na CDM mwishoni mwa wiki. <br />
;br />
Baada ya mikutano hiyo kutakuwa na mkutano mkubwa kwa wakazi wote wa jiji la Arusha siku ya Alhamisi utakaohutubiwa na Mh. Mbowe, Mh. Slaa na wabunge mbalimbali wa chama.
<br />
<br />
Safi sana viongozi wa chadema kwa kwenda kusafisha hali ya hewa na kuwaeleza wananchi ukweli. Hao jamaa hawajafungua kesi na kuzuia mikutano ya chadema?kuna mdau mmoja toka huko arusha alisema jamaa watazuia mikutano ya chadema.
 
chadema kimeandaa mkutano mkubwa wa hadhara mjini arusha alhamisi wiki hii utakao ongozwa na mwenyekiti wake mhe. Freeman mbowe kwa kushirikiana na katibu mkuu wa chama hicho, dk. Willibroad slaa, naibu katibu mkuu, zitto kabwe na wajumbe wa cc.

Wajumbe wa cc watakaokwenda kuhutubia mkutano huo ni mbunge wa iringa mjini, mchungaji peter msigwa; mbunge wa viti maalum, regia mtema; mwenyekiti wa baraza la vijana taifa wa chama hicho, heche suguta; mbunge wa viti maalum, chiku abwao na mbunge wa nyamagana ezekia wenje.

Wengine ni mbunge wa singida mashariki na mnadhimu wa kambi ya upinzani bungeni, tundu lissu; meya wa manispaa ya musoma, kasululu malima; mwenyekiti wa halmashauri ya karatu, lazaro masai, na mwenyekiti manispaa ya moshi, jaffar maiko. Pia atakuwapo mbunge wa arusha mjini, godbless lema na madiwani wengine wa jiji la arusha.

Madiwani waliofukuzwa

attachment.php


kutoka kushoto: Estomih mallah wa kata ya kimandolu, john bayo wa kata ya elerai, ruben ngowi wa kata ya themi, rehema mohamed wa viti maalum na charles mpanda wa kata ya kaloleni.

Source: Nipashe
kwani jamii forum = chadema? Maana 95% ya threads za humu ndani zinazungumzia chadema na kumtukana rais wetu jk ambaye ni kipenzi cha watu! Why? Not fair!
 
Natamani niwepo ila niko mbali najua siku hiyo asiye na mwana aeleke jiwe!!!!
 
Back
Top Bottom