Kamati kuu CHADEMA kufunika Arusha Alhamisi

Madiwani wale hawana hatia wakubwa wataumbuka sana kwa hili. I wise man changes his mind but a full will never.kwenye hili haikutakiwa kuonesha ubabe wa kutafasiri kanuni bali ilitakiwa kuonesha hekima. Madiwani sio watendaji bali ni watu wakuchaguliwa. Ukishika mpini lazima ujue namna ya kuyatumia makali
 
Hivi hiyo Alhamisi ni siku ya kazi au ni mapumziko? Utaandaaje mkutano siku ya kazi? Mi naona hawa CDM wanaleta vurugu tu hapa nchini na kuwanyima wananchi fursa ya kufanya kazi na kujikwamua kiuchumi!
 
Hivi hiyo Alhamisi ni siku ya kazi au ni mapumziko? Utaandaaje mkutano siku ya kazi? Mi naona hawa CDM wanaleta vurugu tu hapa nchini na kuwanyima wananchi fursa ya kufanya kazi na kujikwamua kiuchumi!
1 kwenye mikutano ya chadema hulazimishi kwenda kama wanavyofanya ccm Kufunga ofisi zetu kwa lazima na vitisho kwa wenye majengo, 2. tumefanyakazi kwa miaka 50 mbona hatuoni mabadiliko..
 
Hivi hiyo Alhamisi ni siku ya kazi au ni mapumziko? Utaandaaje mkutano siku ya kazi? Mi naona hawa CDM wanaleta vurugu tu hapa nchini na kuwanyima wananchi fursa ya kufanya kazi na kujikwamua kiuchumi!

Mikutano ya kisiasa ndio kazi rasmi kwa vyama vya siasa.

Kama tumefanya kazi kwa muda wa miaka 50 chini ya magamba na hakuna maendeleo ya maana yaliyopatikana, ni vizuri sasa watu wote tukajielekeza kufanya kazi za siasa ili tujikwamue.

magamba na serikali yake ndo wanaleta vurugu na kudidimiza uchumi kwa kuwekwa mfukoni na wauza mafuta.
 
Kazi ipo si rahisi hata kidogo kuwa rubuni wakazi wa Arusha, kwani suala kubwa na kiu chai ni maendeleo na si malumbano. sasa ni lipi watajisafisha kwao.
 
Kazi ipo si rahisi hata kidogo kuwa rubuni wakazi wa Arusha, kwani suala kubwa na kiu chai ni maendeleo na si malumbano. sasa ni lipi watajisafisha kwao.
Unavyopenda kuwafanya wanaarusha mandondocha ndio ninapochoka kabisa hawahitaji kurubuniwa na mtu kwani wamejiandaa kwa mabadiliko
 
Dah! Ebwana kwa hali hii Arusha ishapoteza umaarufu wake, coz utalii na mikutano ya mara kwa mara iliyokuwa ikifanyika katika Hotel zetu sasa hv umepungua. Wageni huofia maandamano na vurugu zitokanazo na maandamano hayo.
Mungu baba tutangulie watanzania...................................
 
Jamani niko hapa Mianzini Arusha nimekutana na msafara wa makamanda wa CHADEMA, wakiwa na gari la matangazo wanahamasisha watu hahudhulie kwenye mkutano.

Kiukweli magari ni mengi, pikipiki na hata daladala nazo zimefunga bendera za CHADEMA kwa mbele. Naona hapo kwenye mkutano patachimbika. Kwa haraka nimewaona Mh. Lema, Msigwa, Wenje na wengine sijawatambua vizuri.

Nasikia maoni ya watu huku mitaani wanalaani kitendo cha madiwani kukubali mwafaka feki. Kwa mimi navyoona huku Arusha hata uchaguzi ukirudiwa cdm inachukua kata zote. Wenye habari zaidi watujuze.
Chama cha demokrasia na Maendeleo kimefunika Arusha ni kwenye ufunguzi wa matawi 16…nimebahatika kuhudhulia ufunguzi wa tawi moja la Soko kuu hakika CHADEMA hapendwi mtu kinapendwa chama….sipati picha kesho
attachment.php


attachment.php


attachment.php


attachment.php


attachment.php


attachment.php


attachment.php


Nilichelewa kufika hivyo sikuweza kuwakalibia makamanda..ila alikuwepo meya wa musoma, Peter msigwa, Lema...
 
Nimepita hapa kituo cha Tax Baracuda karibu na manispaa Arusha namwona Rasta yaani aliyekuwa diwani wa Kaloleni kwa tikiti ya CDM akiwa amevalia suti nyeusi then akaingia kwenye gari yake Escudo huku akivuta sigara kwa hisia na haongei na mtu.

Na pale headquarters ya wakereketwa Philips nimekuta watu wakiwa wameshika bendera za CDM na kuna uwezekano wa maandamano ya CDM kwa upande mmoja na waliofukuzwa wanajaribu ku fight back kwa upande mwingine. Tusubiri jioni sijajua kitakachotokea ila kuna kila dalili hata wananchi wamefurahi hao jamaa kufukuzwa.
 
Kwa watu wenye akili na maono ya mbali ni lazima watakubali kwamba CHADEMA walifanya maamuzi magumu na ya busara sana ambayo ni nadra kufanyika na chama chochote cha siasa. Si mnawaona CCM wanavyoongezeana muda ili angalau 2015 isogee?

Si kazi rahisi kumnyang'anya mwanachama wako kadi. Viva CHADEMA.
 
Mpaka sasa maandamano sehemu inayoweza kufanya mabadiliko ya kweli ya taifa hili ni Arusha.

Dar watoto wakiswahili wengi mno na masharoharo wa kijinga mno, Dar inakera sana, tumetumia mbinu mbalimbali kuiamsha dar ila hawataki kuamka tukafanikiwa wabunge wawili tu.

Wakati Dar ingepaswa kuwa mfano wa kuigwa kwakufanya mabadiliko makubwa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, mwisho wa siku unawakuta watu jioni wapo bar wanacheka wakati taifa lina msiba mkubwa.
 
Mpaka niwasikilize hawa viongozi wangu wasiopenda unafki ndio nitaendelea na ujenzi wa taifa.
Kwa sasa naelekea kwenye msafara.
BADAE.
 
Viongozi wa kitaifa wa Chadema tayari wapo mitaani Arusha ambapo wanafungua matawi na kuzungumza na wananchi kwenye kata nne ambazo madiwaninwake wametimuliwa uanachama. Wanawaeleza wananchi kwa nini wakafikia maamuzi hayo magumu.

Mji umeamka na watu wamewapoke vizuri sana tofauti hata mm binafsi nilivyokuwa nategemea. Msafara umeanzia Soweto Kaloleni kuelekea Elerai. Daladala, gari binafsi na pikipiki zote zimefunga bendera za cahdema. Baadae jioni watagawanyika na kufanya mikutano ya hadhara minne kwenye kata nne.

Waliopo Arusha ambao nimewaona kwa macho yangu ni Mbowe, Lema, msigwa, Wenje, Joyce, Heche, Nassari, meya wa Musoma. Na nimeambiwa leo jioni anaingia Dr. Slaa, Zitto, Rachel, Esther ila Lissu amekwama Jimboni kwake Singida kwa sababu ya crisis ya mafuta.

Kesho mkutano mkubwa wa hadhara uwanja wa NMC.

Nitawajuza zaidi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom