Kamati kuu CCM yamtosa Hussein Bashe, adaiwa si raia wa Tanzania

Uraia wa Bashe wazidi kukoroga





husseinbashe.jpg

Hussein Bashe


*UHAMIAJI WAKIRI KUTUMA BARUA YA KUMTHIBITISHA CCM, MAKAMBA ASEMA HAWAKUBALIANI NA BARUA YA HIYO


Boniface Meena
SAKATA la uraia wa Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Hussein Bashe aliyeamriwa arejeshe kadi na kumvua mamlaka yote aliyokuwa nayo ndani ya chama hicho tawala, limeibua maswali mengi, huku kukiwa na maelezo kuwa ni raia na chama chake kung'ang'ania kuwa si raia hata kama nyaraka zipo.

Baadhi ya nyaraka ambazo zimetolewa na Idara ya Uhamiaji nchini na kuonwa na Mwananchi zilionyesha kuwa Bashe aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika Jimbo la Nzega, ni raia wa Tanzania.

Waraka uliothibitisha uraia wake na kutumwa kwa Katibu Mkuu wa CCM, makao makuu Dodoma ambayo gazeti hili imeuona unaeleza kuwa Bashe alikabidhiwa hati ya uthibitisho wa kuwa raia yenye Na. S/N 312 ya Agosti 10 mwaka 2009 na kivuli cha nakala hiyo kiliambatanishwa kwenye barua hiyo ya uthibitisho.

Maelezo ndani ya waraka huo yalieleza kuwa idara ya Uhamiaji inapenda kujulisha kuwa Hussein Mohamed Bashe Ibrahim alithibitishwa kuwa raia wa Tanzania kwa kuzaliwa chini ya kifungu Na.5(1) au 7(8) cha sheria ya Uraia Na. 6 ya mwaka 1995.

Waraka huo ambao nakala yake ilitumwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo imetiwa saini na P. W. Nombo kwa niaba ya Kaimu Kamishna Mkuu wa Uhamiaji.


Ingawa alipozungumzia uthibitisho ulioelezewa kwenye waraka huo Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba alisema kuwa ni kweli ameiupata,lakini akasisitiza kuwa Bashe si raia japokuwa chama kinampenda.


"Nimeipata barua, nimeusoma, lakini nasema Bashe si raia, tunampenda na ana uwezo wa kupigiwa kura na kushinda, lakini si raia,"alisema Makamba.


Alisema kuwa uhamiaji huwa wanaangalia vitu vichache tu kumthibitisha mtu hivyo hakubaliani na uthibitisho wa uhamiaji.


"Uhamiaji wanaangalia kitu kimoja tu kama ni raia labda cheti cha kuzaliwa, mimi nasema si raia, hatuwezi kumpitisha na hatukubali kwa kuwa masuala ya uraia yana mambo mengi,"alisema Makamba.
Makamba anavunja sheria makusudi kabisa hapa. Kama una viongozi wa kitaifa wanaovunja sheria kirahisirahis hivi, kweli tuaelekea pabaya. Hivi kati ya Makamba na wale Wataalamu wa Uhamiaji, ni nani ana jukumu la kuthibitisha uraia wa mtu? Ni nani anayejua zaidi sheria za uraia na uhamiaji? Kama Makamba ndiye anayejua mambo ya uraia zaidi yao, kwa nini asifanye kazi hiyo ya uhamiaji?
Gazeti hili lilimtafuta Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha ili azungumzia waraka huo ambao nakala yake imetumwa kwake, lakini simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa.

Alipotafutwa Naibu waziri wa wizara hiyo, Balozi Khamis Kagasheki alisema kuwa yuko katika ofisi za CCM akiomba wanachama wa chama hicho wamdhamini hivyo hawezi kuzungumza.

"Niko katika ofisi za CCM ninaomba udhamini kwa wanachama hivyo 'please' siwezi kuzungumza,"alisema Kagasheki.

Kwa upande wa Idara ya uhamiaji msemaji wa idara hiyo, Abdi Ijimbo alisema kuwa waraka huo ameuona hivyo atautolea ufafanuzi pamoja na mambo mengine baada ya kuupitia vizuri.

"Nimeuona waraka huo baada ya kuutafuta kwa kuwa nilitaka nijiridhishe kwanza na si kuongea tu, hivyo njoo kesho saa tatu asubuhi (leo) nitakupa taarifa kamili pamoja na mambo mengine,"alisema Ijimbo kwa njia ya simu.

Uamuzi wa kumvua madaraka na tamko la kutokuwa kwake raia lilitolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati baada ya kumalizika kwa kikao hicho cha NEC, Bashe alitakiwa pia kuanza mara moja mchakato wa kutafuta uraia wa Tanzania.

Chiligati alisema kwamba Bashe si raia kwa kuwa wazazi wake walivyomzaa walikuwa ni raia wa Somalia.

Kwa upande wake, Bashe alisema kwamba yeye ni raia wa Tanzania na kwamba alikwisha ukana uraia wa baba yeke, kupitia Mahakama ya Kivukoni jijini Dar es Salaam.
"Kesho (leo) nitaongea na waandishi wa habari na kuweka kila kitu wazi ili wananchi wajue ukweli," alisema Bashe alipotakiwa kuongelea suala hilo.

Alisema kwamba baada ya kuongea na wanahabari atakwenda Nzege kuwashukuru wananchi walioonyesha imani kubwa kwake kwa kupata kura zaidi ya kura 14,000.

Tayari wanasheria wa Bashe wameshachukua hatua ya kufuatilia sakata zima la mteja wao kwenye ofisi za Idara ya Uhamiaji. Bashe aliongoza kura za maoni Jimbo la Nzega kwa kupata kura 14, 466, Lucas Selelii 2,706 na Khamis Kigwangala aliyepata kura 1,566. Kigwangala ndiye aliyepishwa kupeperusha bendera ya CCM.
 
Mkuu
Kwanini akosane na mtoto wa rais? Huoni huo ni utovu mkubwa wa nidhamu? Mtoto wa rais ni mtu mkubwa sana. Kwa usalama wa taifa lolote inafaa aheshimiwe. Kila anachotaka kufanya hairuhusiwi kumpinga. Wana JF tusipokuwa makini itafikia mahali watu watatulisha maneno ya uchonganishi kiasi siku ukimkuta mke wako akanavinjari na mtoto wa rais uanze kumkasirikia. Hii itakuwa ni mbaya sana kwa mustakabadhi wa taifa letu. Mtoto wa rais popote duani anaruhusiwa kufanya lolote bila kuhojiwa na wala watu kukasirika. Mfano mzuri ni Libya au Iraq kabla ya USA kuingia. Hizo ndio heshima wanazotakiwa kupewa watoto wa marais. Nashukuru kuona Watanzania na sisi tumeanza kuamka kwani nimesikia hata uchaguzi wa Yanga alikuwepo. Hii inatupa matumaini kwni tunaanza konyesha heshima anayostahili kupewa.

What a tongue in cheek...!!
 
Hapo mgosi Makamba anavunja sheria kwa kujadili suala ambalo halijui kwani yeye si idara ya uhamiaji wala msemaji wake.

Hapa anakuwa kama wale wabwanga wengine ambao husemasema kwamba fulani hawena uwezo wa "kuabua gai" bila kwanza kufanya utafiti kama mtu huyo kweli anazo fwedha..

Hata Hussein Bashe nae anatakiwa akae kimya na kuibuka siku ambayo itathibitishwa na idara hiyo kupitia hao wanasheria wake kwamba yeye ni raia wa Tanzania.

Ila kwa ujumla hapa mambo hayajekaa sawa kuna kasoro kubwa sana.
 
Nimeviona ktk T Daima ya leo vivuli vya hati za Bashe vya kuukana uraia wa Somalia. Makamba could be right, at least this time, kwani inaonekana kama vile hati hizi ni feki tu. Jamaa yangu mmoja ambaye ni very conversant ktk masuala ya Uhamiaji na uraia kaniambia hii ni feki moja kwa moja. Nafikiri hapa kuna bomu jingine litakalolipuka -- dhidi ya utawala wa CCM -- kwamba kuna milungula iliotembea kupata hati hii pamoja na ile barua ya Uhamiaji.

Tusubiri.

Tatizo la ufeki basi ni la Uhamijai maana ndio walotowa hizo nyaraka na wamekubali kuwa ni raia..
 
Wakuu zangu,
kuhusiana na Bashe ni za kimafia tu hakuna jingine. Tanzania yetu imejaa washombe kibao ambao baba zao ni wazungu ila mama zao ni watanzania wanaishi nchini kama Watanzania pasipo shida ya kuulizwa ati baba yako ni mwenye asili gani?.

Kama kweli Makamba anataka kuanzisha sheria hiyo mpya basi woote wenye asili ya Ushombe itabidi wapitiwe upya Uraia wao na kama kweli baba zao walikana kule walikotoka..
Nijuavyo mimi kama umezaliwa Tanzania na mmoja wa wazazi wako ni Mtanzania na umelelewa Tanzania hadi kufikia umri wa kupata Masi yako, wewe ni Mtanzania pasipo kujali una rangi au asili gani.

Nnakumbuka wala sii muda mrefu ulopita, Karume pia alitaka kuwafanyia hivyo hivyo Wangazija huko Unguja lakini amekwama kutokana na kwamba hiyo serikali yenyewe ya Unguja imeshikwa na Wangazija (Comorians).
 
Kijana amewashangaza sana kwani kupata kura za maoni zaidi ya 14,000 si jambo dogo ni tishio kubwa.
 
Kazi aliyotakiwa kufanya Bashe ni kuhakikisha Lucas Seleli hapiti kura za maoni, hilo amelifanya kwa ufanisi wa hali ya juu hivyo kazi yake imeisha. Maana kama CCM ni watu wa haki hawawezi kusema mtu aliyepata kura 2000 hakubaliki ila aliyepata kura 1500 ndiye anayekubalika hivyo kupitishwa kuchukua nafasi ya mtu aliyepata kura 14,000!!!!!.
 
Wakuu zangu,
Mtasema mnavyotaka kusema lakini Mtu yeyote anayezaliwa Tanzania, akalelewa na kukulia Tanzania akiwa na mzazi wake hata mmoja Mtanzania, huyu mtu ni MTANZANIA. Maadam pasi yake ya kwanza kaipata tanzania huwezi kumtoa Utanzania ati kwa sababu baba yake hakuukana Usomali.

Na kama sivyo, basi serikali inatakiwa kuwapitia mashombe (hao point five) nchini waliozaliwa baba zao wakiwa Wazungu, Wahindi, Waarabu na watu wa mataifa ya nje waliokuja hapa nchini na kuzaa na wanawake zetu, tena basi hao baba zao hawaishi tena Tanzania wamerudi makwao na kuwaacha watoto wakilelewa na mama zao. Tuwanyang'anye pia Uraia na kuwahukumu kama tunavyomkuhumu huyu Bashe.

Maadam imesadikika kwamba Bashe sii Mtanzania basi ifikishwe mahakamani kwani hakuna sheria ya Uhamiaji ya CCM na sheria ya uhamiaji ya Taifa. na laukama hivyo ndivyo vigezo basi woote wwaliozaliwa nchini na wazazi (Baba) wenye asili ya nje ni lazima wathibitishe baba zao waliukana uraia wa nje kama inavyotakiwa kwa Bashe. Akili za Idd Amin Dada!

Kinyume cha hapo - MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO
 
Kufuatia Sakata la uraia wa bashe nimesoma katika gaziti la Mwananchi majibu ya Makamba na kutaka hata KUTAPIKA... Hivi hawa wazee sijui wanazeeka vipi??? (Makamba na Msekwa). Yaani baada ya uhamiaji kukubali kuwa Bashe ni raia kwa kupatikana kwa nyaraka zinazoonyesha kuwa jamaa ni raia yeye anajibu hivi..."Nimeipata barua, nimeusoma, lakini nasema Bashe si raia, tunampenda na ana uwezo wa kupigiwa kura na kushinda, lakini si raia,"alisema Makamba.

Alisema kuwa uhamiaji huwa wanaangalia vitu vichache tu kumthibitisha mtu hivyo hakubaliani na uthibitisho wa uhamiaji.

"Uhamiaji wanaangalia kitu kimoja tu kama ni raia labda cheti cha kuzaliwa, mimi nasema si raia, hatuwezi kumpitisha na hatukubali kwa kuwa masuala ya uraia yana mambo mengi,"alisema Makamba"


Sidhani kama kulikua na sababu ya kuongea upuuzi kama huu zaidi ya kutueleza kuwa hawamtaki BASHE ndani ya CCM....

My take...

Kwa kura 14000 ulizopata kati ya 19000 ni ushahidi tosha kuwa unakubalika na unaweza kufichua michezo michafu mingi koz i can feel the pain u gat....nenda chama cha upinzani kagombee (CHADEMA) will be better...... U are the future SLAA......
 
Mkuu
Kwanini akosane na mtoto wa rais? Huoni huo ni utovu mkubwa wa nidhamu? Mtoto wa rais ni mtu mkubwa sana. Kwa usalama wa taifa lolote inafaa aheshimiwe. Kila anachotaka kufanya hairuhusiwi kumpinga. Wana JF tusipokuwa makini itafikia mahali watu watatulisha maneno ya uchonganishi kiasi siku ukimkuta mke wako akanavinjari na mtoto wa rais uanze kumkasirikia. Hii itakuwa ni mbaya sana kwa mustakabadhi wa taifa letu. Mtoto wa rais popote duani anaruhusiwa kufanya lolote bila kuhojiwa na wala watu kukasirika. Mfano mzuri ni Libya au Iraq kabla ya USA kuingia. Hizo ndio heshima wanazotakiwa kupewa watoto wa marais. Nashukuru kuona Watanzania na sisi tumeanza kuamka kwani nimesikia hata uchaguzi wa Yanga alikuwepo. Hii inatupa matumaini kwni tunaanza konyesha heshima anayostahili kupewa.

Hivi watu wengine huwa mna akili zenu au mmeshavuta vya kuvuta. Yaani wewe kwa akili yako mtoto wa Rais ana nguvu/heshima ama hadhi yoyote kama kiongozi wa serikali ama vinginevyo? Yaani watu wengine kama hamna vya kuongea embu chukua pipi umng'unye uwaache watu wenye hoja waandike mambo ya maana. Ati kwa kuwa ni mtoto wa Rais basi afanye atakalo? EBO!. Nyamaza na tulia kabisa, usilete tena upuuzi kama huu jamvini, just shut the hell up.
 
Bashe hana professional nyingine ? Naona siasa za CCM hazina tija kwake


Kaka hili sio suala la ajira. Ni lazima kuliangalia suala hili kwa mapana yake. Hili ni suala la haki ya mtu, maoni ya wanaccm wa nzega, uhalali wa CCM kuingilia majukumu ya idara ya uhamiaji lakini, siasa za makundi ndani ya MTANDAO kuelekea 2015 na zaidi ni suala zima la siasa za uraia katika nchi yetu na bara letu la Afrika. Hili ni suala kubwa sana ambalo Bashe anapaswa kuliangalia katika ktazamo mpana kwa maslahi ya taifa letu.

omarilyas
 
Mwenye kujua SHERIA naomba anijuze: Mfano nimezaliwa Tanzania maisha yangu yote ni hapo hapo TZ kuanzia kielimu hadi kikazi nikaowa TZ na mwenzi wangu ni mtu wa TZ nikizaa watoto watakuwa ni raia wa wapi? nami ni raia wa wapi ikiwa baba yangu ni MGHANA mama yangu ni Mtanzania??
Nitafuata uraia wa kuzaliwa au wa Baba au wa Mama??


KWANZA tuanzie na uraia wako na pia tuangalie uraia wa baba maana ndiye mwenye haki ya kumpa mtoto uraia hadi hapo mtoto akiwa 21 ili achague mwenyewe... Mtoto siku zote huchukua uraia wa baba yake kwa sheria za Tanzania kwa sasa hata kama mtoto huyo kazaliwa tanzania na mama yake ni mtanzania... haijalishi... siku zote inategemea na baba yake...pia kwamba uraia wa tanzania haupasishwi na baba mtoto kama baba huyo aliupata utanzania kwa any means of registration au naturalisation...

Hivyo kama baba Bashe ni Msomali.. watoto wake watachukua uraia wa somalia hadi hapo watakapo ukana uraia wa baba yao..

Bashe alete ushahidi kwamba aliukana uraia wa baba yake kwanza na si vinginevyo maana kuzaliwa tu na mama mtanzania kwa sheria za Tanzania haitoshi...

Mwisho.. baba mtanzania wa kuzaliwa ndiye pekee ana haki ya kumpasia mtoto wake uraia na hata baba huyo akiwa na uraia wa nchi nyingine..ili mradi hajaukana/renounce Utanzania basi atakuwa na uwezo wa kumpa mtoto wake uraia...maana sheria ya 1995 citizenship act section 13 inasema ni mpaka aukane ...

Tunahitaji mabadiliko ya sheria hii ya ura maana haikidhi mahitaji ya wakati huu + including dual nationality...

Act inapatikana hapa http://www.bunge.go.tz/Polis/PAMS/Docs/6-1995.pdf
 
Back
Top Bottom