Wananchi waliohudhuria mkutano wa BASHE Kisesa wamlilia Samia walipwe malipo yao

Stuka

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
272
869
WANANCHI kutoka Wilaya za Itilima, Maswa, Meatu, Bariadi, Busega, Kishapu na Ushetu waliohudhuria Mkutano wa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe uliofanyika Sep 13, 2024 Jimbo la Kisesa wamedai kutapeliwa fedha zao walizoahidiwa kulipwa Bashe.

Wananchi hao wengi wakiwa ni viongozi wa CCM ngazi ya mashina, matawi na Kata wamepaza sauti zao kuomba Rais Samia Suluhu aingilie kati walipwe kiasi walichoahidiwa cha shilingi 100,000 kwa kila mjumbe atakayefika kwenye mkutano huo na wao walifanikiwa kufika kama walivyokubaliana.

Wamesema waliratibiwa na ofisi za CCM wilaya na Ofisi za Wakuu wa wilaya kwa kupakiwa kwenye magari kwenda kwenye mkutano kwa maelezo kuwa wakimaliza mkutano watapewa shilingi laki moja za kurudi nazo nyumbani jambo ambalo wamesema halikutekelezwa na taarifa walizonazo ni kuwa BASHE hiyo fedha alishaitoa na imeliwa na wajanja wachache.

Wamesema walihamasishwa kwenda kwenye mkutano wa Waziri kwa lengo la kumpinga Mbunge Mpina kwamba matatizo ya wakulima anayoyasema ni ya kwake kwa chuki za kukosa uwaziri na wala sio matatizo yao kama wakulima na kwamba walipewa maelekezo kwamba Bashe akiwauliza wanyooshe mikono kumpinga Mbunge Mpina ili hiyo Video Clip atumiwe Mheshimiwa Rais kuona kumbe watu wa Kisesa hawamuungi mkono mbunge wao.

Kilichojificha nyuma zaidi ya mkutano huo wameahidi kuweka wazi kila kitu ikiwa hawatalipwa fedha yao kama walivyoahidiwa.
 
CCM haiwezi kupata watu bila kuwasomba na magari + pesa
 
Umaskini wa wananchi wa Tanzania unawafanya wazidi kuwa maskini, it’s so sad 😞.

Kwa tuhuma kama hizi TAKUKURU wako wapi kuchunguza hili?

Lakini pia mwananchi kwanini ushawishike kusema uongo kwa kitu kinachogusa maisha yako?

Haya sasa kiko wapi?
Mkono umenyoosha laki hujapata, umaskini unakutafuna BASHE anapokea per month wage and salary yake, we unakufa njaa.
 
WANANCHI kutoka Wilaya za Itilima, Maswa, Meatu, Bariadi, Busega, Kishapu na Ushetu waliohudhuria Mkutano wa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe uliofanyika Sep 13, 2024 Jimbo la Kisesa wamedai kutapeliwa fedha zao walizoahidiwa kulipwa Bashe.

Wananchi hao wengi wakiwa ni viongozi wa CCM ngazi ya mashina, matawi na Kata wamepaza sauti zao kuomba Rais Samia Suluhu aingilie kati walipwe kiasi walichoahidiwa cha shilingi 100,000 kwa kila mjumbe atakayefika kwenye mkutano huo na wao walifanikiwa kufika kama walivyokubaliana.

Wamesema waliratibiwa na ofisi za CCM wilaya na Ofisi za Wakuu wa wilaya kwa kupakiwa kwenye magari kwenda kwenye mkutano kwa maelezo kuwa wakimaliza mkutano watapewa shilingi laki moja za kurudi nazo nyumbani jambo ambalo wamesema halikutekelezwa na taarifa walizonazo ni kuwa BASHE hiyo fedha alishaitoa na imeliwa na wajanja wachache.

Wamesema walihamasishwa kwenda kwenye mkutano wa Waziri kwa lengo la kumpinga Mbunge Mpina kwamba matatizo ya wakulima anayoyasema ni ya kwake kwa chuki za kukosa uwaziri na wala sio matatizo yao kama wakulima na kwamba walipewa maelekezo kwamba Bashe akiwauliza wanyooshe mikono kumpinga Mbunge Mpina ili hiyo Video Clip atumiwe Mheshimiwa Rais kuona kumbe watu wa Kisesa hawamuungi mkono mbunge wao.

Kilichojificha nyuma zaidi ya mkutano huo wameahidi kuweka wazi kila kitu ikiwa hawatalipwa fedha yao kama walivyoahidiwa.
Aisee 😯
 
Back
Top Bottom