Kamati kuu CCM yamtosa Hussein Bashe, adaiwa si raia wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati kuu CCM yamtosa Hussein Bashe, adaiwa si raia wa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pilato, Aug 14, 2010.

 1. Pilato

  Pilato Member

  #1
  Aug 14, 2010
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 60
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kamati kuu ya chama cha mapinduzi imemtosa kijana mahili na chipukizi kwenye siasa Bwana Husein Bashe ambaye aligombea kura za maoni ccm kupitia jimbo la nzega na kumbwaga aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Bwana lukas selelii kwa jumla ya kura 14,200 za Bashe,dhidi ya 2700 za selelii,na sababu yao kubwa ni kwamba ni kutokana na utata wa uraia wake na si raia wa jamuhuri ya muungano wa tanzania

  Lakini tukirudi nyuma huyu bwana bashe ,NI MJUMBE WA BARAZA KUU UMOJA WA VIJANA TAIFA (UVCCM),NI MJUMBE MKUTANO MKUU WA CCM MKOA TABORA,AMEWAHI KUGOMBEA NAFASI YA NEC UVCCM TAIFA na AMEWAHI KUGOMBEA MAKAMO MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA.

  Kinachoshangaza sehemu zote hizi ni lazima wapitie na kuthibitisha kuwa yeye ni raia na baada ya kuridhika ndipo hupewa ruksa ya kugombea ama kuwa kiongozi .

  Swali gumu Ni kigezo kipi ambacho kilisahaulika leo ndio kimetumika?,kwa hisia za haraka hapa kuna mkono wa mtu

  ILa kwa mbali kuna fununu kwamba huyu Bwana Bashe hana mahusiano mazuri na mtoto wa MH.Rais Ridhwani Kikwete hasa baada ya uchaguzi wa makamo mwenyekiti wa UVCCM Taifa ambapo bwana Bashe alishiriki na Swahiba wa Ridhwani Bwana Beno Malisa..!!

  Je CCM inatufunza nini? na Tunakwenda wapi..?
   
 2. Pilato

  Pilato Member

  #2
  Aug 14, 2010
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 60
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kamati kuu ccm taifa yamtosa aliyemwangusha selelii
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwanza hujatupa chanzo cha story yako -- kama ni gazeti au la -- kwani sana sana umeonysha ushabiki wako tu kwa Bashe.

  Pili huyo Bashe ni mtu wa RA na alitumia pesa nyingi sana kuhonga katika kura za maoni. Jimbo la Nzega halikuingiliwa kabisa na maafisa wa Takukuru wakati wa kura za maoni na hailjulikani kwa nini -- wengine wanasema RA alihakikisha hawaingii. Kwa hivyo CCM wamefanya mnakusudi tu kutumia uraia wa Bashe na siyo rushwa aliyotoa -- na yote hii ni kwa sababu ya kumuokoa kutokana na rushwa, hela ambazo origin yake ni RA.
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Aug 14, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Ndugu wawili wanapogombana, wewe chukua jembe ukalime. Watakapopatana watakukuta wewe tayari unavuna wakati wao hawana cha kuvuna, ndipo watatambua ujinga wao.
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  ccm iko taabani........itakuja na kila aina ya sababu.
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  pAMOJA na mikwaruzo ya hapa na pale lakini CCM wapo strategic sana na mambo yao, kwa kifupi wameshaiona hali halisi ya kisiasa hapa nchini hasa baada ya Dk Slaa kuingia kwenye mchakato wa kugombea uraisi, wanachokijaribu sasa ni kukinusuru chama chao kwa njia yoyote ile, Bashe inawezekana amepata kura nyingi lakini labda hazikuwa za wapiga kura bali zile za kutengenezwa na CCM wameshaliona hilo kuwa jimbo litapotea kwa upinzani hivyo wakaamua kumrudisha yule mwenye kura za halali (probably Selelii)
   
 7. K

  Keil JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Zak Malang,

  Kama habari hiyo ina ukweli wowote, basi nitaanza kuamini maneno ya Pasco kwamba "wapiganaji" waliahidiwa kuachwa wabaki baada ya CCJ kuhusishwa nao. Lakini pia Kikwete anajua kwamba anapambana na Mkuu wa Vita ya Kupinga Ufisadi (Dr. Slaa), kwa hiyo ili CCM nao wajionyeshe wanapiga vita ufisadi, lazima "wapiganaji" waachwe ili watumike kama kete/mtaji kwenye kura za Rais, vinginevyo kura za JK zinaweza kupunguzwa sana.

  Hoja ya uraia is just an excuse ya kumtosa mtu ili asilalamike. Swala la rushwa ni gumu kulithibitisha kwa kuwa PCCB hawakumshika mtu yeyote kwa tuhuma hizo, japo Selelii alisema kulikuwa na rushwa kubwa sana.

  Mwisho, naona CC wana agenda ya kuendeleza mshikamano ili kupunguza exodus, maana wasipofanya hivyo inaweza kuwagharimu. Kijana bashe atapozwa kwa kupewa ukuu wa wilaya, ili asubiri 2015. Lakini je JK atawapoza wangapi kwa appointments?
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  itawezekanaje hii mkuu, kama tayari ameshapikiwa zengwe la uraia?
   
 9. K

  Keil JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hilo zengwe wamelipika tu ili kumtema, assumption yao ni kwamba the public will be in dark na kama wamesema "uraia wake una utata" maana yake ni kwamba anaweza kuchunguzwa na kuwa cleared na akapewa ulaji vile vile. CCM ni chama la wasanii na mambo yao wanaendesha kisanii tu.

  Wangekuwa wako serious na swala hilo wangeanza kwa kumvua nyadhifa zote alizo nazo ndani ya CCM na UVCCM, hapo ndio ningeamini kwamba kweli wako serious. Hawa jamaa huwa ni wazuri sana wa kutafuta excuse ya kutema mtu, halafu wanaangalia namna ya kumpoza. Masauni alipotemwa JK alisema tutampa nafasi nyingine ya uongozi.
   
 10. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Nakufagilia mkuu
  Imaelekea sasa CCM wameanza kuamka toka usingizini.
  Usingizi wa kulewa madaraka na uswahiba ulikuwa umekolea,but everybody can see the writimg on the wall.
  Bashe swahiba wa RA,RA mshika pochi chafu wa siasa za Tz.Huyu shetani aliingizwa ma CCM mdarakani na ni mzigo wao.
  Wananchi wanajua kivingine,sehemu nyingi hawadangayiki na rushwa.Pale wananchi watakapojiona wako helpless kura zao za chuki zitaenda CHADEMA.
  Uamuzi wa kumtosa Bashe ni dalili ya alarm ndani ya Chama tawala
   
 11. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #11
  Aug 14, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,856
  Likes Received: 11,977
  Trophy Points: 280
  Kwa kuwatosa walioshinda kura za maoni ndio kuendeleza mshikamano haiingii akilini. Halafu jamani hizo wilaya ziko ngapi maana kila anayetoswa mnatuambia atapewa u-DC kuna wagombea zaidi ya elfu tatu kama hiyo ndiyo njia mbadala CC watakuwa wanachemsha badala ya kupoza, afterall wilaya zote zina wakuu wake nao watatoswa na kupelekwa wapi sijui tusidanganyane CC inawasha moto iheshimu maamuzi ya wapiga kura.

  Kwa upande mwingine ni pigo kwa RA & co maana nasikia siku ya kura za maoni LA alikuwa Nzega physically.
   
 12. A

  August JF-Expert Member

  #12
  Aug 14, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  wenye kupewa udc. rc, ubalozi nk ni wale wenye mvuto wa kisiasa/ waliopigwa panga kwa ajili ya kitu flani, kwa hiyo uelewe sio wote wako kwenye kundi la kupozwa, kwani wengine sio wakwao.
  na hadithi hii ina nikumbusha Kinana alivyo kuwa mbunge Arusha, baadae likazuku kuhusu uraia , ingawa kwake hakuna tamko rasmi la serikali/chama kwamba si raia sasa sijui sirikali iliona aibu maana jama alikuwa kanali jeshini, naibu waziri wa ulinzi sasa naona ku-cover mambo na zaidi ya hapo kwa sababu ni wakwao, aliwekwa Red Cross, Bodi ya Muhimbili Hospitali, kwenye kamati za ccm, meneja wa kampeni, na biashara anazo fanya, iwe clearing and forwarding, shipping agency, dry cleaner, uwindaji nk,
   
 13. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #13
  Aug 14, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,856
  Likes Received: 11,977
  Trophy Points: 280
  Hapo ndipo CCM inapokosea kuzoa zoa hata watu wenye utata ilimradi ni mtu wao, ndiyo maana matatizo ya ndani huwa hayaishi unaona wanavyojuta kumkumbatia RA amekuwa mzigo na hawawezi kumtosa tena.
   
 14. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #14
  Aug 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,651
  Likes Received: 21,866
  Trophy Points: 280
  Atapewa ukuu wa wilaya na Dr Slaa? maana ndiye Rais ajaye au hapo sijaelewa vizuri.
   
 15. Pilato

  Pilato Member

  #15
  Aug 14, 2010
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 60
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii ni kashfa kwa mwenyekiti wa ccm na katibu wake na ni vuzuri wajiuzuru,kwa kudiliki kupitisha jina kwenye ngazi nyingine za mjumbe kamati kuu umoja wa vijana taifa n.k na wakati wakijua si raia
   
 16. K

  Keil JF-Expert Member

  #16
  Aug 14, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ninadhani Kituko amesema vyema kwamba, pamoja na mambo mengine inategemeana na huyo aliyeongoza huo ushindi wake ulipatikana kwa njia halali? Maana unaweza kuteua mpeperusha bendera ambaye si mwakilishi wa wanachama na matokeo yake chama kikauza jimbo kwa wapinzani kwa bei chee.

  Watakaopewa u-DC siyo wote watakaopigwa chini, ni wateule tu ambao ni washirika wa wenye chama chama. Pia wanaweza kuangalia nguvu ya mhusika na kama anaweza kuleta chokochoko ya kupunguza kura za chama.

  Kilichofanyika kwenye uteuzi wa Dr. Billal kuwa mgombea mwenza, ndio ambacho kinaangaliwa kama factor ya kuamua nani apozwe na nani aachwe.

  Pamoja na hayo lazima kutakuwa majeruhi wengi sana mwaka huu. Kama mtu alipata kura 14,000 then anaachwa halafu anapewa aliyepata kura 2,700 hiyo si dalili nzuri.
   
 17. K

  Keil JF-Expert Member

  #17
  Aug 14, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ninaombea sana hilo litokee, lakini kwa sasa bado ni mapema. Inshaa Allah tutampata kiongozi makini Dr. Slaa!
   
 18. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #18
  Aug 14, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,856
  Likes Received: 11,977
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo mnaona ni busara CC kumpitisha aliyepata kura 2,700 na kumwacha aliyepata 14,000, hiyo tofauti ya kura zaidi ya 10,000 mnataka ziende wapi CC waache mchezo wawe makini.
   
 19. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #19
  Aug 14, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Malecela nae arudi mjengoni
   
 20. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #20
  Aug 14, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Mzee Malecela kafedheheshwa sana iwapo kurudi mjengoni kwa njia hiyo kwani hata ile authority aliyokuwa nayo kwa wabunge wenzake wa CCM itakuwa haipo tena. Afterall hatujajua kama kweli atashinda uchaguzi mkuu, labda CCM ipeleke nguvu zote huko kwake kwani kama wapigaji wa CCM tu hawakumpenda, sioni namna ambayo wapigaji wasiokuwa wa CCM watampenda ukikumbushia ile tension iliyokuwapo kati yake na bwana Lusinde. Most likely wapigaji wa Lusinde hawatapiga kura, na kumwacha mzee wa CCM anaelea kama baloon.
   
Loading...