Kamari: Janga lingine lililofumbiwa macho

Kamari: Janga lingine lililofumbiwa macho

Unaitwa mchezo wa matumaini, kupata au kukosa, mchezo uliowafilisi wengi kuwafaidisha wachache na kuwanufaisha wamiliki. Zipo taratibu ngumu za kufanya hii biashara ya mashine za Kamari na michezo ya kubahatisha, lakini kwa kuchukulia mambo ya mazoea au vinginevyo taratibu zinakiukwa.

Hii biashara imekuwa kwa kasi mno miaka ya karibuni, kuna makasino karibia kila mahali sasa. Lakini kibaya na kwamba hii biashara sasa imetoka huko kwenye makasino na kuingia mitaani kwenye vibanda vya kubet sasa kuna vimashine vidogovidogo portable vinasambazwa mpaka sehemu zisizoruhusiwa kisheria kufanya hii biashara.

Kamari si mchezo mzuri unaleta wezi unaleta ujambazi, unalemaza vijana na kuacha kufanya kazi zenye tija, unahamasisha ulevi na umalaya kutelekeza familia na wengine kuleta magonjwa.Unasababisha mauaji mifarakano na migongano kati ya jamii.

China waliliona hili mapema wakapiga marufuku kuchezwa hovyo wakachagua maeneo maalum ya kufanya hii biashara walijua kwanini waliona mbali tulipaswa kujifunza kutoka kwao.Tunaliangamiza taifa na kulemaza kizazi.

Kuna mengi yakutazamwa upya vibali leseni maeneo ubora wa mashine nk, uzalendo ni dhana ngumu kuitekeleza kwa vitendo na uhujumu uchumi sio wizi wa fedha za Umma tuu.
Cha ajabu kuna mtanzania mmoja mzalendo mambo leo anawadanganya na kuwaminisha "wanaginingi " wezie kwamb ati mikutano ya vyama vya siasa ikiruhusiwa itafanya watu wasifanye kazi na bunge live pia.ati anataka pool table kuwa nalo limo na kwamba watu wakinywa pombe mchana utashuka? Iv hyu mzalendo wetu hajui kinachoendelea kule kwenye betting center! Na huko maofsini wanagining wanakosema nidhamu imerejeshwa si ndiko watu wana bet mpaka mabosi?
Vijana wanasema " bora kulala na mkeka kuliko jero"! Hatari sana lakini mpaka wakati wa uchaguzi watazuia
 
Addiction hii betting wengine kama wahindi iinafikia hatua mpka wanajiua sababu ya madeni waliko kopa.
 
Cha ajabu kuna mtanzania mmoja mzalendo mambo leo anawadanganya na kuwaminisha "wanaginingi " wezie kwamb ati mikutano ya vyama vya siasa ikiruhusiwa itafanya watu wasifanye kazi na bunge live pia.ati anataka pool table kuwa nalo limo na kwamba watu wakinywa pombe mchana utashuka? Iv hyu mzalendo wetu hajui kinachoendelea kule kwenye betting center! Na huko maofsini wanagining wanakosema nidhamu imerejeshwa si ndiko watu wana bet mpaka mabosi?
Vijana wanasema " bora kulala na mkeka kuliko jero"! Hatari sana lakini mpaka wakati wa uchaguzi watazuia
Umenikumbusha riwaya ya KISIWA CHA GININGI
 
Pambaneni na hali zenu! Kwani kuna mtu amelazimishwa kubeti? Kuna mtu kavunja sheria kwa kubeti? Acheni wivu wa KIKE acheni watu wabeti! Kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake

Millions dollars man and your genge, hii ni jamii forums,it is a place to discuss things and ideas concerning jamii yetu yote, from local, national or international perspectives.

It is a place to exchange different opinions without fear or favour, exchange views in mature fashion. It is forums which have members numbered in over 400,000 people. Adult, educated, most been there done it.

When we criticize North Korea, USA, France, British Israel or Iran, Tanzanian or Donald Trump policies it doesn't mean we are jealous, au kama tuna wivu, ni wachawi au kukatisha tamaa vijana wao wa hizo nchi.

Sasa kama ukiweka idea kama watu wengine wameifanya miaka mingi iliyopita halafu, hata wengine walikuwa brokers na wanakwambia experience yao na kuwaambia matokeo yake, halafu unawaita wachawi, wenye wivu, wenye fitna huo ni utoto.

Endeleeni kwenye thread zenu lakini achane zingine tuzungumze tunachotaka unless you told me you guys have bought JamiiForums.

You guys needs to discuss ideas truthful.

How many will make it out out 1000 may be 10 people.

What will be the cost to their lives? Many Lives will be be ruined.

Stress, depression, up and down, addictions, more criminals in our society and more suicidals rates. this will be the cost to us as a society, community, as citizens of Tanzania.

Kwa sababu most money they lost in Gambling it means they can't look out after their wife, their children and their mothers and fathers. Therefore we as society will have to do it, we have no choice.

You guys you put too much rubbish which makes genuine business, serious ideas, good business and ideas difficult to get look in.

Second mnawapotosha vijana sana. Yo are promising too much, while you know the truth is very different.

Third you will all be gone, when shit hit the fan or you will come with very good excuses. (Like guys you didn't follow the plan, you took too much risk etc) when we as society have to pick up the pieces.

Yaani genge lenu la vijana kumi mkiwa na different ID's kujiweka hata kuwa 50 siyo kitu cha muhimu to stop opinions of other Tanzanians and Africans.

Naona sasa mmeamua kuwa moderators wa JF, mna mkakati wa kudominate and not allow anybody else to speak, start a thread or advertise their business except your business and your genge.

You guys are not allowing anybody else to have a say. Even if they start different threads, you guys always interfering in very rude fashion thinking you know it all.

Guys, your tricks has been tried before in many countries, it is true, is good, and you will always get new people, you will make money. But it has done before in many countries, and some of us have seen it all before.

Lakini allow other people to express their view without your rudeness, silliness and stupidity. We are the Tanzanian public, we have been here longer before you guys and we will be here after you have gone, after you have taken people money from poor, impressionable young people and disappear with it.

I actually despair when you guys says want to spread this nonsense to the whole country to every place, colleges and University. Brothers why can you not teach others to make something better with their lives like Irrigation, farming using better seeds and fertilizers, ufugaji, kilimo, construction, kuanzisha biashara ndogo au kubwa sana pamoja. Kufanya kitu kitakaofaidisha vijana wetu,kuwapa ajira, to benefit our communities, our societies and our country for many years to come.

I think it very silly, cheap, silly immature to interfere with people discussing other issue with your juvenile posts.
 
Naona sasa hata kile kipingamizi cha umri sasa hakizingatiwi tena.
Mashine za kamari mpaka kwenye maduka ya vyakula.
Nadhani tunafanya uchaguzi mbaya wenye matokeo mabaya zaidi.
Marekani(Las Vegas) watu wanacheza kamari lakini vigezo na masharti vinazingatiwa, sio holela kama hapa kwetu kwa sasa.
Watu hawafanyi kazi wanashinda vijiweni wakisubiri kubet.....
Vijana wadogo waliopaswa kuzingatia masomo akili zote kwenye betting.
Mbaya zaidi tabaka la watu wa maisha ya chini wataathirika zaidi.
 
Bungua bongo.

Mara Biko!, mara mkeka beti, 3 mzuka! , sport pesa!

Vijana wanaamka asubuhi na karatasi za kamari sio majembe tena.

Mijadala ni kuchanika kwa mikeka yao au kupata fedha bila kuzalisha.

Viwanda vinahitaji mali ghafi lakini nguvu kazi ya taifa hili imezama kwenye kamari tu, inasikitisha sana.

Akili ya baadhi ya vijana wetu sasa kila asubuhi imejikita ktk kupata fedha kwa kamari. Hawafikiri tena kuanzisha biashara ndogo ndogo, viwanda vidogo, mashamba. Ni biko, 3 mzuka, mkeka beti. Ni kamari, kamari, kamari!

Vyombo vya habari navyo vimekazana kushadidia kamari ktk taifa hili lenye upungufu wa chakula. Wanavyotangaza kwa mbwembwe na ving'orimbo utadhani ni kampeni ya kuhamasisha Kilimo cha Kufa na Kupona au Kisomo cha Manufaa! Inasononesha kweli.

Viongozi nao (Wakuu wa Mikoa) wanavyoshuhudia mafanikio ya watu kutoka ktk mikoa yao kwa haraka utadhani wamefanya ushujaa wa kushinda vita vya kutetea nchi. Inasikitisha sana.

Kamari hii ya michezo imewagusa hadi watoto na wanafunzi wa shule za sekondari. Vyuo vikuu huko ndio usiseme. Wasomi wetu sasa hawafikri kuzalisha nadharia mpya au kizihakiki zilizopo, wao ni kubeti tu. Nguvu wanazozitumia ktk kufuatilia mipira na kubeti ni nyingi zaidi ya ile wanayotumia kufuatilia masomo yao.

Nchi inazama kwenye kamari kupitia michezo . Pamoja na ubaya wa kamari lakini kwa vile imewekwa kodi sasa, nchi haina habari.

Wana Dini na Wasomi Mahili ninataraji kukusikieni mkitoa neno ktk eneo hili hasa kwa uhai wa nguvu kazi ya taifa kufikia matarajio tunayoyatamani.

" Shauku bila mikakati ni kazi bure"
Je, tunawasemea na kuwawakilisha vijana wa taifa hili ipasavyo pindi yanapokuja haya ya Kifedhuli na ajabu kwa vijana ambao ndio taifa la LEO.
*Tafakari, Chukua Hatua.*
 
Mkuu nimekuelewa lakini kazi ya kustawisha viwanda ni ya kijana anayebeti au mtunga sera anayeshindwa kumwambia raisi kua kuhamia Dodoma siyo msingi wa viwanda?

Kosa ni la kijana mwenye mikeka mfukoni au kiongozi anayepewa ushauri wa ukweli na mwekezaji mkubwa kabisa Afrika kua sera zetu siyo rafiki halafu yeye akajibu kua huyu hajui asemacho?

Ngoja nikabeti narudi.
 
Unajua lazima uwaze nje ya box kwamba kushamiri kwa hizi unazoita kamari kwanini ni awamu hii? Unadhani kamari zimeanza Leo?
 
Back
Top Bottom