Kamari: Janga lingine lililofumbiwa macho

Kamari: Janga lingine lililofumbiwa macho

Wamebadili jina wanaita betting, mama yangu kabla sijajua nilikuwa nikipita mtaaani nawaona vijana wengi wana karatasi na kalamu,, nikawa nashangaa nini kimetokea hapa mjini? mbona naona vijana wanapenda kujisomea siku hizi. kuja kugundua nini wanafanya niliishiwa nguvu. Kuna watu wanadesh hata chai ii aende aka bett. kwa kweli hili ni janga mkuu.
Kwa sasa ndio kama fasheni kila kona si kwa mkubwa wala mdogo, mfanyakazi na jobless
 
Unaitwa mchezo wa matumaini, kupata au kukosa, mchezo uliowafilisi wengi kuwafaidisha wachache na kuwanufaisha wamiliki. Zipo taratibu ngumu za kufanya hii biashara ya mashine za Kamari na michezo ya kubahatisha, lakini kwa kuchukulia mambo ya mazoea au vinginevyo taratibu zinakiukwa.

Hii biashara imekuwa kwa kasi mno miaka ya karibuni, kuna makasino karibia kila mahali sasa. Lakini kibaya na kwamba hii biashara sasa imetoka huko kwenye makasino na kuingia mitaani kwenye vibanda vya kubet sasa kuna vimashine vidogovidogo portable vinasambazwa mpaka sehemu zisizoruhusiwa kisheria kufanya hii biashara.

Kamari si mchezo mzuri unaleta wezi unaleta ujambazi, unalemaza vijana na kuacha kufanya kazi zenye tija, unahamasisha ulevi na umalaya kutelekeza familia na wengine kuleta magonjwa.Unasababisha mauaji mifarakano na migongano kati ya jamii.

China waliliona hili mapema wakapiga marufuku kuchezwa hovyo wakachagua maeneo maalum ya kufanya hii biashara walijua kwanini waliona mbali tulipaswa kujifunza kutoka kwao.Tunaliangamiza taifa na kulemaza kizazi.

Kuna mengi yakutazamwa upya vibali leseni maeneo ubora wa mashine nk, uzalendo ni dhana ngumu kuitekeleza kwa vitendo na uhujumu uchumi sio wizi wa fedha za Umma tuu.
 
wacha watu wajiajili huko, (wajipe matumaini)maana serikali imeshindwa wapa matumaini ya ajira wala nyenzo za wao kujiajiri (barabara, masoko, usimamizi).

tatu mzuka, biko, betting yaani kila siku unapoteza 10000+ kwa matumaini siku moja utapata m.80 duuu
 
wacha watu wajiajili huko, (wajipe matumaini)maana serikali imeshindwa wapa matumaini ya ajira wala nyenzo za wao kujiajiri (barabara, masoko, usimamizi).

tatu mzuka, biko, betting yaani kila siku unapoteza 10000+ kwa matumaini siku moja utapata m.80 duuu
Siha yote inachukuliwa na wachache [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144]
 
M nimuanga wa hii kitu ndani ya miaka 3 mwaka huu ndio nimegundua kamari si kitu kizuri bahada kufilisi off zangu nyingi baada ya kuacha tu nimeweze kuzifufua tena sitaki ata kuisikia ilitak kunitia umasikini
 
Back
Top Bottom