Kamari: Janga lingine lililofumbiwa macho

Kamari: Janga lingine lililofumbiwa macho

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
374,205
Reaction score
866,461
Unaitwa mchezo wa matumaini, kupata au kukosa, mchezo uliowafilisi wengi kuwafaidisha wachache na kuwanufaisha wamiliki. Zipo taratibu ngumu za kufanya hii biashara ya mashine za Kamari na michezo ya kubahatisha, lakini kwa kuchukulia mambo ya mazoea au vinginevyo taratibu zinakiukwa.

Hii biashara imekuwa kwa kasi mno miaka ya karibuni, kuna makasino karibia kila mahali sasa. Lakini kibaya na kwamba hii biashara sasa imetoka huko kwenye makasino na kuingia mitaani kwenye vibanda vya kubet sasa kuna vimashine vidogovidogo portable vinasambazwa mpaka sehemu zisizoruhusiwa kisheria kufanya hii biashara.

Kamari si mchezo mzuri unaleta wezi unaleta ujambazi, unalemaza vijana na kuacha kufanya kazi zenye tija, unahamasisha ulevi na umalaya kutelekeza familia na wengine kuleta magonjwa.Unasababisha mauaji mifarakano na migongano kati ya jamii.

China waliliona hili mapema wakapiga marufuku kuchezwa hovyo wakachagua maeneo maalum ya kufanya hii biashara walijua kwanini waliona mbali tulipaswa kujifunza kutoka kwao.Tunaliangamiza taifa na kulemaza kizazi.

Kuna mengi yakutazamwa upya vibali leseni maeneo ubora wa mashine nk, uzalendo ni dhana ngumu kuitekeleza kwa vitendo na uhujumu uchumi sio wizi wa fedha za Umma tuu.
 
Mkuu pitia huku, hawa waandishi wetu naona wametusaidia kunyambua hili suala lako aisee

Ubungo-2-copy-798x350.jpg


JESHI la Polisi nchini, hasa katika jiji la Dar es Salaam, limeendelea kufumbia macho vitendo vya kihalifu, hata vile vinavyofanyika katika maeneo yanayozunguka vituo vya Polisi.

Duru za uchunguzi wa FikraPevu, zimebaini kwamba pamoja na matukio hayo ya kiharifu kufanyika mita chache kutoka vilipo vituo vya Polisi, baadhi ya askari polisi wanatuhumiwa kushirikiana na wahalifu hao kuvunja sheria za nchi kwa kulipwa fungu maalum kwa siku, wiki au wiki mbili.

Michezo ya kamari ya kitapeli

Wageni wengi wanaoingia Jijini Dar es Salaam kila siku, wameendelea kutapeliwa na makundi ya kihalifu ya vijana, yanayochezesha mchezo wa kamari ambao umeonekana kuwa ni vigumu kukomeshwa kutokana na baadhi ya askari polisi kufika maeneo ambayo vijana hao wanachezesha mchezo huo na kupatiwa fedha kama kinga ya kuchukuliwa hatua.

Mbinu nyingine zinazotumiwa na wahalifu hao, ni kutafuta kibali bandia kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, ambapo pia taarifa zimeeleza kuwa vibali hivyo hutolewa kinyemela na baadhi ya watumishi wa bodi hiyo kwa kulipwa kiasi cha 40,000. Kwa kawaida kibali hicho huwa ni cha miezi mitatu.

Katika uhalifu huo, mwananchi anapobaini kwamba ametapeliwa na kisha kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi kilichopo karibu na eneo la tukio, anadaiwa kufukuzwa na walinzi hao wa usalama wa raia na mali zao.

Athumani Rajabu, Marry Kileo na Titus Julius ni miongoni mwa mashuhuda waliowahi kutapeliwa kabla ya kutoa taarifa katika vituo vya polisi Magomeni, Urafiki na Buguruni, lakini wakaishia kufukuzwa na polisi wa zamu wa vituo hivyo.

Kwa takriban miezi miwili sasa, FikraPevu imekuwa ikifuatilia suala hili la michezo ya kamari ya kitapeli. Maeneo maarufu yaliyobainika kukithiri michezo hiyo, ni pamoja na Ubungo-mbele ya mitambo ya kuzalisha umeme ya Songas, Manzese, Mwenge na mitaa mbalimbali ya Kariakoo.


Wananchi walio wengi wamekuwa wakitapeliwa kila siku kutokana na mchezo huo kana kwamba vyombo vya dola havioni ili kuchukua hatua za kisheria.

Mara nyingi, wanaofanyiwa utapeli huo huangua kilio na kufanya baadhi ya wananchi wanaokuwa katika eneo hilo kuingilia kati, kwa kuwataka wanaoendesha michezo hiyo kuwarudishia fedha zao waathirika hao, ambao baadhi yao hujikuta wakitapeliwa hata simu zao za mkononi, kwa matarajio ya kurejesha fedha zao zilizokwishatapeliwa.

Hata hivyo, pamoja na wasamaria wema hao kuingilia kati, wachezeshaji wa kamari hiyo ya utapeli huwa wakali, huku wakiwataka wasamaria hao na hao waliotapeliwa kwenda kokote, kwa madai kwamba wao hawawezi kufanywa chochote na vyombo vya dola.

Taarifa zinaeleza kuwa jeuri na viburi hivyo vya vijana hao hutokana na kulindwa na baadhi ya polisi wanaodaiwa kufaidika kwa namna moja au nyingine na utapeli huo.

Hata timu ya waandishi wetu wamepata vitisho vikali kutoka kwa vijana hao wakati wakifuatilia uhalali wa vitendo hivyo ya kihalifu pamoja na kubaini ni nani walioko nyuma yao, kiasi cha kujaa jeuri na viburi kiasi hicho.

Uchunguzi zaidi umebaini kwamba vijana wanaoendesha michezo hiyo hutumia mbinu nyingi kujihami, ikiwa ni pamoja na kutembea kwa makundi ya watu wasiopungua 20 hadi 40, ambapo inadaiwa kuwa wengi wao wamebainika kuwa ni wapambe maarufu kwa jina la ‘wavungavaku' wanaojifanya kuwa ni wateja kwa lengo la kuvuta wananchi ili nao washiriki katika mchezo huo.

Madanguro ya ‘Madada poa'

Ukiacha michezo hiyo ya kitapeli ya kamari inayofanyika maeneo ya wazi barabarani huku polisi wa doria wakishuhudia, lipo tatizo jingine la wanawake ‘madada poa' wanaouza miili yao katika madanguro yaliyopo karibu kabisa na vituo vya polisi katika jiji la Dar es Salaam.

Uchunguzi wa kina uliofanyika, umebaini kuwepo kwa aina mbili za makundi ya wanawake wanaouza miili yao. Kundi la kwanza ni lile linaloendesha vitendo hivyo kama biashara katika vyumba maalum wanavyomiliki kwa kupanga, na kundi la pili ni la wale ambao ni wazururuaji ambao huonekana wakirandaranda katika maeneo mbalimbali ya barabara za jiji la Dar es Salaam, hususan wakati wa usiku, ‘wakitega' wateja barabarani, katika vilabu vya pombe na katika nyumba za wageni, maarufu kama ‘gesti bubu.'

Wengi wa wanawake wanaojihusisha na biashara hiyo ya kuuza miili yao, maarufu kwa jina la machangudoa au madada poa, katika mazungumzo yao na timu ya waandishi wetu walikuwa na maoni tofauti juu ya sababu zilizowatumbukiza katika biashara hiyo hatari...........

Soma zaidi ==>Magenge ya uhalifu yashamiri mbele ya vituo vya Polisi Dar
 
Mkuu pitia huku, hawaaandishi wetu nao wametusaidia kunyambua hili suala lako aisee

Tena hii ni Kama imehalalishwa kabisa na ukishadhulumiwa usijaribu kwenda polisi utakutana na vikwazo na wakati mwingine vitisho mpaka hiyo ishu utaachana nayo
 
Wamebadili jina wanaita betting, mama yangu kabla sijajua nilikuwa nikipita mtaaani nawaona vijana wengi wana karatasi na kalamu,, nikawa nashangaa nini kimetokea hapa mjini? mbona naona vijana wanapenda kujisomea siku hizi. kuja kugundua nini wanafanya niliishiwa nguvu. Kuna watu wanadesh hata chai ii aende aka bett. kwa kweli hili ni janga mkuu.
 
Wamebadili jina wanaita betting, mama yangu kabla sijajua nilikuwa nikipita mtaaani nawaona vijana wengi wana karatasi na kalamu,, nikawa nashangaa nini kimetokea hapa mjini? mbona naona vijana wanapenda kujisomea siku hizi. kuja kugundua nini wanafanya niliishiwa nguvu. Kuna watu wanadesh hata chai ii aende aka bett. kwa kweli hili ni janga mkuu.

weka buku tano..ule 75 elfu..faida 70 elfu...uwe na bahati yako lakinii
 
Kadiri muda unavyosonga, vijana wengi zaidi wanazidi kuwekeza ktk michezo mbalimbali ya kamari (bahatinasibu). Kwa mwenendo huu zidhani kama tutaifikia Tanzania mpya ya viwanda.

Kinachoniogopesha zaidi ni vitendo vya wateuliwa wa Rais (wakuu wa wilaya) kujitokeza waziwazi kuwasihi wananchi kucheza kamari badala ya kuwaongoza ktk Tanzania ya viwanda.

Naiona Tanzania ya kubet na kamari nyingine ikichanua.
 
Back
Top Bottom