Kamari: Janga lingine lililofumbiwa macho

Kamari: Janga lingine lililofumbiwa macho

Lakini wenye kuendesha michezo hii ndio wananufaika zaidi. Chukua mfano, Asilimia tano ya watu 20,000,000 wenye simu wanacheza hizo kamari. Hiyo ni idadi ya watu 1,000,000. Tuseme kila mmoja anatumia sh 500 tu. Jumla ya fedha yote ipatikanayo ni sh.500,000,000 yaani nusu bilioni. Jumla ya zawadi zote na matumizi mengine ni kama milioni 200. Hivyo basi faida ipatikanayo ni sh. milioni 300 hivi. Na huu ni mchezo mmoja tu.
Mchezo unaendelea na kila siku wengine wapya wanajiunga. Na kama kawaida hii michezo hujenga tabia ya kuendelea nao kila uchao (uraibu). Ni aina ya mtego ambao ni rahisi kuingia lakini vigumu kutoka. Fikiri kwanza kabla hujatumbukia huko.
Ni mchezo ambao hauna hasara na faida yake ni faida kufuru..... Ila ni pesa isiyo na baraka kabisa
 
6a3db5ac980c88bfe982b1d7a059abd2.jpg



Mkuu usikate tamaa
Bet tena mkeka kuvunjika sio mwisho wa kubet[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mu hali gani wana JF. Nashangazwa na wimbi la kamali nchini hasa kwa kipindi hiki. Zamani tulizoea kukuta sehemu za kamali kuwepo mafichoni sana lkn siku hizi kamali zinatangazwa hadi maredioni na kwenye TVs.

Mara utasikia BIKO, TATU MZUKA, M-BET etc. ... Hizo zote ukiziangalia na kuzichambua kiundani zaidi utaona ni kamali tupu.

Nawasilisha hoja kwenu wana JF.

Alamsiki.
 
Kamari halali siku nyingi.

Unafikiri Magufuli kapataje urais?

Watu wamepiga kura kwa kamari.
 
Kweli asee, wana hadaa watu tuu
Kweli kabisa watu wanadanganywa sana. Kama leo nmeona tangazo la tatu mzuka eti kuna droo ya million 100 kwa kila mshindi kwa washindi watatu. Eti kweli kwa hali hii ya uchumi mtu kweli yuko ready kutoa milion 300 kisa umechezesha namba tatu. Is it serious?????
 
Unaitwa mchezo wa matumaini, kupata au kukosa, mchezo uliowafilisi wengi kuwafaidisha wachache na kuwanufaisha wamiliki. Zipo taratibu ngumu za kufanya hii biashara ya mashine za Kamari na michezo ya kubahatisha, lakini kwa kuchukulia mambo ya mazoea au vinginevyo taratibu zinakiukwa.

Hii biashara imekuwa kwa kasi mno miaka ya karibuni, kuna makasino karibia kila mahali sasa. Lakini kibaya na kwamba hii biashara sasa imetoka huko kwenye makasino na kuingia mitaani kwenye vibanda vya kubet sasa kuna vimashine vidogovidogo portable vinasambazwa mpaka sehemu zisizoruhusiwa kisheria kufanya hii biashara.

Kamari si mchezo mzuri unaleta wezi unaleta ujambazi, unalemaza vijana na kuacha kufanya kazi zenye tija, unahamasisha ulevi na umalaya kutelekeza familia na wengine kuleta magonjwa.Unasababisha mauaji mifarakano na migongano kati ya jamii.

China waliliona hili mapema wakapiga marufuku kuchezwa hovyo wakachagua maeneo maalum ya kufanya hii biashara walijua kwanini waliona mbali tulipaswa kujifunza kutoka kwao.Tunaliangamiza taifa na kulemaza kizazi.

Kuna mengi yakutazamwa upya vibali leseni maeneo ubora wa mashine nk, uzalendo ni dhana ngumu kuitekeleza kwa vitendo na uhujumu uchumi sio wizi wa fedha za Umma tuu.
.
Kuna mtu mmoja alitonya kuwa pamoja na ukweli kwamba kamari ni mchezo unaoweza kuharibu uchumi wa nchi lakini bado umeruhusika na serikali ya awamu ya tano kuchezwa mfululizo.
Aliendelea kutonyesha kuwa ni kama serikali yenyewe ndio inacheza maana inachukua asilimia sabini ya pesa inayokusanywa kutoka kwa wachezaji.
Hii ni sawa na kusema TRA wamerasimisha rasmi kamari kuwa chanzo chao cha mapato baada ya hali ya uchumi kuwa tete.
 
Sijajua Nini kinatokea kwa nchi yetu kwa kuwa na michezo Mingi ya BAHATI nasibu maana kila ukipitia au ukiingia huku unakutana na matangazo ya BAHATI nasibu sijajua Nini mtazamo wa hii michezo maana miaka Mingi iliyopita nchi yetu haikuwa na hii michezo kama sasa imezidi ...
AISE MIMI BADO NAPATA SHIDA JUU YA HII MICHEZO MAANA SI VIJANA WALA WAZEEE WOTE WANACHEZA.
 
hali ngumu na namba zinasomeka vilivyo kwa hiyo watu wanaamua wajilipue kwenye michezo ya kubahatisha
 
Back
Top Bottom