Kamanda wa Malawi aapa kulinda Ziwa Malawi

Kamanda wa Malawi aapa kulinda Ziwa Malawi

hivi hili ziwa si limeingia mpaka Mozambique kwann sis tu na si mozambiq wanatafuta nin kwetu?????
Wakoloni ndio walichora hivyo na tumesaini mkataba kuheshimu mipaka iliyochorwa na wakoloni Nyerere amesaini kwa niaba yetu.
 
Huyu jamaa naona huko kwenye Supu kumemchosha makomandoo wetu watamtoa humo kwenye Supu si anajiita Supu-ni! Shauri yake!
 
Huyo kamanda ni sawa na chui wa makaratasi tu.Halafu hawa wanatakiwa wawe pre emptied kidogo.Kuzamisha boti yao ya kijeshi, halafu tunajifanya kuwaomba radhi kuwa boti ilizamishwa kimakosa.ki nchi hakina hata helicopter, watu wanaleta dharau
 
Wakuu hawa wamalawi walidai wamekamata maspy wa Tz mwenye taarifa juu ya hili jambo maana liko kimya.
 
Kuna vitu hapa tunachanganya, hapa kuna mipaka miwili, kuna mpaka wa kwanza uliowekwa na wakoloni ukionyesha ziwa lote ni la Malawi, lakini baada ya vita ya kwanza mpaka wakoloni wakachora mpaka mpya ambao uliligawa ziwa katikati, bongo tukapata na Malawi wakapata, ambao mkataba huu unaenda sambamba na sheria za umoja wa kimataifa kwamba mahali ambapo kuna ziwa na kuna nchi mbili mpaka unakuwa katikati ya ziwa lile. Lakini pia baada ya vita vya pili vya dunia,Tanzania iliendelea kuwa chini ya mkoloni (muingereza) kama mwangalizi ,sio mtawala,na sharia za kuwa mwangalizi huruhusiwi kuigawa nchi au kuhamisha mpaka wa nchi kwenda nchi nyingine,lakini waingereza ama kwa kupuuza au kulibeba koloni lake wakabadili mpaka wa ziwa na kulifanya ziwa lote kuwa ni mali ya Malawi. Pia kuna mkataba wa umoja wa nchi za Africa ,ambao unadai nchi za Africa wakubali mipaka iliyowekwa na wakoloni,nahisi mkataba huu ulikuja kuepusha migogoro baina ya nchi za Africa na tulisign hili dude, sasa swali ni kwamba mkataba huu wa Africa ambao tulisign kwa upande wa Tanzania tuheshimu mpaka upi? ule wa pili ( ambao unaeleza mpaka ni katikati) au ule wa tatu ambao waingereza walipeana ziwa lote kuwa mali ya Malawi pasifokufuata sheria? nadhani Tanzania wali sign mkataba wa Africa kwa tukijua mpaka ambao tunakubaliana nao ni ule wa pili ambao unaenda sambaba na sheria za umoja wa kimataifa, pia Malawi walisign mkataba ule wakijua wao wanafuata mpaka wa kwanza ambao walipewa na waingereza kuwa ziwa lote ni mali ya Malawi, hapa ndo sintafahamu inapoanzia. Sio sahihi kusema kuwa Tanzania walisign mkataba na nchi za Africa (OAU) kuwa tumekubali ziwa lote ni mali ya Malawi, hapa itabidi tuangalie mazingira yote na uhalali wa uingereza kurudia kwa mara ya tatu kugawa ziwa lile ambapo kisheria hakutakiwa kufanya vile, kwa hiyo pande zote zina sababu za kutosha kusema mpaka uwe katikati au laa.

Serikali ya Tanzania inatakiwa kuchangamka na kufuatilia suala hili na kumaliza tatizo hili kisheria once for all , kama nikutumia vyombo vya sheria vya ndani na nje, kama nikutumia wasuluhishi wa nchi pande zote mbili ,kama nikutafuta usuluhishi katika nchi wanachama wa SADC , AU,au UN basi tufanye hivyo, tusitegemee sana mambo ya utashi au busara za Maraisi walioko madarakani kwa pande zote mbili, utashi tu hautoshi maana unamaliza tatizo kwa muda mfupi linaibuka tena,hivyo hatusolve tatizo ila tunazuga zuga na kuvunga vunga tu, tutafute suluhu kisheria na tumalizane nalo.
Uko sahihi bali nikurekebishe kidogo kuwa mkataba wa mwisho unaokubalika unasema malawi wanacontain ziwa lote. Makubaliano ya OAU hayaongelei mpk wa nchi moja moja bali yanazitaka nchi zote ziheshimu mipaka inayotambulika iliyochorwa na wakoloni hivyo tunajifunga kutumia mikataba mingine yoyote labda kwa ridhaa ya nchi husika. Tanzania tunafanya majadiliano tokea enzi za mkapa kwa sab tunaamini tukienda mahakamani tutashindwa tunajaribu kuishawishi malawi kwa kutumia haki za urithi wa mali za asili n.k kitu ambacho malawi wamekuwa wanasuasua japo utawala wa bakili muluzi ulielekea kukubaliana na tanzania. Ni kweli mikataba ya maridhiano ya viongozi huwa inaleta migogoro wakati mwingine lkn inatambulika kimataifa na inaheshimika kuivunja itakuwa ni ukorofi ambao unaweza kutumika kuvunja hata mikataba ya kimahakama au mingine kama alivyofanya idd amin ndio maana dunia ya leo imeweka adhabu za vikwazo vingi ili kuzifanya nchi ziache ubabe dhidi ya nchi nyingine. Hivyo kwa kuwa tunaweza kushindwa mahakamani na bado tuna haki ya kuyatumia maji yale hata kwa urithi tu ni vizuri tuongee nao wakubali tutumie mkataba wa UN kwani ni kitu kisichoingia akilini wananchi washindwe kuvua kuoga au kuchota maji ziwani mpk waende upande wa pili kuomba kibali!!!
 
Upo na ndio unaowapa kiburi malawi. Mpaka wa mwisho unaoheshimika na OAU ni ule uliochorwa na wakoloni ambao unaonyesha ziwa lote ni malawi (sijui walikula maharagwe gani) na marais wote wa Africa wakati huo walisaini makubaliano ya kuheshimu mkataba huo wakiwemo Nyerere na Banda lkn kuna mkataba mwingine wa UN unazitaka nchi zinazopakana na maji zigawane maji hayo nusu kwa nusu. Mkataba wa OAU umetufunga tusiende kwenye ule wa UN sasa suluisho kwa sasa ni mahakama ya kimataifa au maridhiano ya kibinaadam ambayo ni hiyari na ridhaa inayotawala. Tanzania haitaki kwenda mahakamani inahofia kushindwa kutokana na kujifunga kimkataba badala yake inataka maridhiano kwa upande wa malawi wanasuasua kukubali maridhiano sab wanajua kuna haki nyingi za kimsingi za binadamu aliyezaliwa eneo lenye maji zinavunjwa na mchoro wa wakoloni lkn wanasisitiza kwamba wakoloni walikuwa na sab za msingi kuwapa ziwa lote hasa ukizingatia Tanzania tuna maziwa na mito mingi vilevile bahari kubwa tu.
Ninaomba MOLA aingilie kati. ..na ninaomba AMANI. ..Mwenye Enzi Mungu ashike hivyo vichwa vya wamalawi na kila tunalosema watusikilize.. kama yule babu wa kikombe alivyo fanya MIUJIZA watu wakanywa vitu wasivyo vijua. ...upepo huo huo wakapuliziwe wamalawi wote na wawe watulivu kama maji ya mtungi. ..
Amen RA
 
Uko sahihi bali nikurekebishe kidogo kuwa mkataba wa mwisho unaokubalika unasema malawi wanacontain ziwa lote. Makubaliano ya OAU hayaongelei mpk wa nchi moja moja bali yanazitaka nchi zote ziheshimu mipaka inayotambulika iliyochorwa na wakoloni hivyo tunajifunga kutumia mikataba mingine yoyote labda kwa ridhaa ya nchi husika. Tanzania tunafanya majadiliano tokea enzi za mkapa kwa sab tunaamini tukienda mahakamani tutashindwa tunajaribu kuishawishi malawi kwa kutumia haki za urithi wa mali za asili n.k kitu ambacho malawi wamekuwa wanasuasua japo utawala wa bakili muluzi ulielekea kukubaliana na tanzania. Ni kweli mikataba ya maridhiano ya viongozi huwa inaleta migogoro wakati mwingine lkn inatambulika kimataifa na inaheshimika kuivunja itakuwa ni ukorofi ambao unaweza kutumika kuvunja hata mikataba ya kimahakama au mingine kama alivyofanya idd amin ndio maana dunia ya leo imeweka adhabu za vikwazo vingi ili kuzifanya nchi ziache ubabe dhidi ya nchi nyingine. Hivyo kwa kuwa tunaweza kushindwa mahakamani na bado tuna haki ya kuyatumia maji yale hata kwa urithi tu ni vizuri tuongee nao wakubali tutumie mkataba wa UN kwani ni kitu kisichoingia akilini wananchi washindwe kuvua kuoga au kuchota maji ziwani mpk waende upande wa pili kuomba kibali!!!

Sio kweli mkuu,
Hilo ziwa limepitia stage mbalimbali za umiliki ulio na unaozichanganya Malawi na pia Tanzania, kifupi Malawi wanajua hawana haki ya ziwa lote kutokana na mikataba na pia maamuzi ya mtawala wetu wa Mwisho Muingereza
Kama Wamalawi wanajua wana haki ya Ziwa lote na pia Waingereza wanataka mali asili (Gas na Mafuta) basi zamani wangeshalichukua
 
Wewe vyombo vya ulinzi vikuchunguze kauli hii inanifanya niamini kuwa wewe si Mtanzania....

Watch your way linapokuja suala la maslahi mapana ya Mama Tanzania.........[emoji109] [emoji109][/QUOTE
Maslahi mapana ya mama Tanzania ni kufuata katiba ambayo ni mwongozo wetu...Ziwa Malawi sio letu
 
Kama amekwisha jifananisha na "humming bird" haina shida wala!
 
JK alilegeza kimtindo japokuwa vikosi vilishasogea pande hizo. Huyu hana baadae aisee. Watapigwa na hilo ziwa tutamiliki sisi na Mozambique
 
Wanafuata makubaliano ya OAU kuwa mipaka ya wakoloni iheshimiwa kwa sab ya kuondoa migogoro ya mipaka iliyokuwa inajitokeza mara kwa mara mkataba ambao Nyerere aliusaini kikamilifu hivyo according to that mkataba ziwa ni lao lkn kuna mkataba mwingine wa umoja wa mataifa unaosema nchi zinazopakana na eneo la maji basi maji hayo yagawanywe nusu kwa nusu. Sasa ugomvi upo mkataba gani utumike kwenye mzozo wetu kati ya ule wa OAU au UN
Utumike wa UN Kwasababu ndiyo wa kimataifa.
 
Ni mpaka gani huo unaopita pembezoni mwa maji? Unajua kitu kinachoitwa mmonyoko wa ardhi wewe,, kwa umoja wetu watanzania tutalinda nchi yetu hata inchi moja haitaondoka,, isije ikawa mnaona watu wakipingana humu ndani kwa mambo yetu ya ndani yanayotuhusu mfikiri kwamba mkileta chokochoko tutatengana.

Tutasimama kidete kutetea ardhi yetu. Msitujaribu.
Asante sana kiongozi, una roho nzuri sana.
 
Waachwe watulindia Ziwa letu For Free maana sie hatutoacha kulitumia...
 
Back
Top Bottom