Kuna vitu hapa tunachanganya, hapa kuna mipaka miwili, kuna mpaka wa kwanza uliowekwa na wakoloni ukionyesha ziwa lote ni la Malawi, lakini baada ya vita ya kwanza mpaka wakoloni wakachora mpaka mpya ambao uliligawa ziwa katikati, bongo tukapata na Malawi wakapata, ambao mkataba huu unaenda sambamba na sheria za umoja wa kimataifa kwamba mahali ambapo kuna ziwa na kuna nchi mbili mpaka unakuwa katikati ya ziwa lile. Lakini pia baada ya vita vya pili vya dunia,Tanzania iliendelea kuwa chini ya mkoloni (muingereza) kama mwangalizi ,sio mtawala,na sharia za kuwa mwangalizi huruhusiwi kuigawa nchi au kuhamisha mpaka wa nchi kwenda nchi nyingine,lakini waingereza ama kwa kupuuza au kulibeba koloni lake wakabadili mpaka wa ziwa na kulifanya ziwa lote kuwa ni mali ya Malawi. Pia kuna mkataba wa umoja wa nchi za Africa ,ambao unadai nchi za Africa wakubali mipaka iliyowekwa na wakoloni,nahisi mkataba huu ulikuja kuepusha migogoro baina ya nchi za Africa na tulisign hili dude, sasa swali ni kwamba mkataba huu wa Africa ambao tulisign kwa upande wa Tanzania tuheshimu mpaka upi? ule wa pili ( ambao unaeleza mpaka ni katikati) au ule wa tatu ambao waingereza walipeana ziwa lote kuwa mali ya Malawi pasifokufuata sheria? nadhani Tanzania wali sign mkataba wa Africa kwa tukijua mpaka ambao tunakubaliana nao ni ule wa pili ambao unaenda sambaba na sheria za umoja wa kimataifa, pia Malawi walisign mkataba ule wakijua wao wanafuata mpaka wa kwanza ambao walipewa na waingereza kuwa ziwa lote ni mali ya Malawi, hapa ndo sintafahamu inapoanzia. Sio sahihi kusema kuwa Tanzania walisign mkataba na nchi za Africa (OAU) kuwa tumekubali ziwa lote ni mali ya Malawi, hapa itabidi tuangalie mazingira yote na uhalali wa uingereza kurudia kwa mara ya tatu kugawa ziwa lile ambapo kisheria hakutakiwa kufanya vile, kwa hiyo pande zote zina sababu za kutosha kusema mpaka uwe katikati au laa.
Serikali ya Tanzania inatakiwa kuchangamka na kufuatilia suala hili na kumaliza tatizo hili kisheria once for all , kama nikutumia vyombo vya sheria vya ndani na nje, kama nikutumia wasuluhishi wa nchi pande zote mbili ,kama nikutafuta usuluhishi katika nchi wanachama wa SADC , AU,au UN basi tufanye hivyo, tusitegemee sana mambo ya utashi au busara za Maraisi walioko madarakani kwa pande zote mbili, utashi tu hautoshi maana unamaliza tatizo kwa muda mfupi linaibuka tena,hivyo hatusolve tatizo ila tunazuga zuga na kuvunga vunga tu, tutafute suluhu kisheria na tumalizane nalo.